CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

Mheshimiwa Mbowe,

Kwenye siasa, kama kuna migongano ya viongozi wa juu, wenye mamlaka ya kujua nani yuko sahihi ni wanachama.

Mulichotakiwa ni kuitisha mkutano mkuu wa wanachama wenu na kuomba kura zao. Wale
ambao wamepoteza dira wasingelichaguliwa tena.

Lakini kuanza kufukuzana, mnaturudisha kwenye ukiritimba wa CCM na marafiki zake mbalimbali hapo Afrika na kwenye nchi za Kikomunisti zamani.

Kwa mwendo kama huu Watanzania hatuwezi kutegemea makubwa kwenye hicho chama chenu. Labda wakati umefika kwa wanachama wengine makini wa CHADEMA kuamua kugombea uenyekiti na kukinusuru chama.

Sikutegemea CHADEMA na nyie mnaona mtasolve matatizo yenu kwa kufukuza viongozi wenzenu. Yaani kweli ndio tulivyo! nakubaliani na Nyani.

Ulitaka chama kiendeshwe bila kuangalia katiba na taratibu walizojiwekea?

Huo mkutano mkuu unaoutaka unaitishwa kwa mujibu wa katiba ,sasa wewe unataka chama kiendeshwe kwenye utaratibu gani?

Kamati kuu ni chombo cha utendaji cha Baraza Kuu na mkutano mkuu .

Hakuna demokrasia isiyokuwa na mipaka wala taratibu ...haijawahi kutokea pakawepo na loose democracy.....
 
Kuweka rekodi sahihi ni kuwa hajafukuzwa uanachama ila kasimamishwa kukaimu nafasi ya umakamu mwenyekiti tuu.

Sasa watu siwaelewi mtu akichukua hatua mnalalamika ,akikaa kimya mnalalamika.

Kwanza aliyeleta hoja ya kumsimamisha ni Mzee Makani na Balozi Ngaiza hawa ni wazee ambao walikaa naye na kumshauri bila mafanikio,sasa ungekuwa wewe ungechukua hatua gani?
 
mnatukatisha tamaa kweli kweli sisi wapiga kura, haya mwageni siri zenu zote hapa tujue hamuwezi kuendesha nchi.
 
Kamati ya wazee wa CHADEMA imejaa wazee wenye utaalamu mbalimbali na busara za hali ya juu.
Prof.Baregu ni mtaalamu wa conflict management sasa kashidwa ...

Balozi Ngaiza ni Balozi wa kwanza mweusi kuiwakilisha nchi UN naye pamoja na diplomasia yake kashindwa.

Mzee Makani ni mwanasheria aliyebobea naye kashindwa .

ungekuwa wewe ungefanaya nini baada ya jitihada zote kushindwa ?
 
Ulitaka chama kiendeshwe bila kuangalia katiba na taratibu walizojiwekea?

Huo mkutano mkuu unaoutaka unaitishwa kwa mujibu wa katiba ,sasa wewe unataka chama kiendeshwe kwenye utaratibu gani?

Kamati kuu ni chombo cha utendaji cha Baraza Kuu na mkutano mkuu .

Hakuna demokrasia isiyokuwa na mipaka wala taratibu ...haijawahi kutokea pakawepo na loose democracy.....
Mbowe,

Chama kimekushinda, itisha uchaguzi ili wana CHADEMA waamue wanataka kuongozwa na nani. Haya mambo ya kufukuzana uongozi wa siasa yamepitwa na wakati.

Sababu zote mlizotoa zinaonyesha ni ugomvi wa mafahari wawili, hapo hakuna cha maadili au katiba. Ni mafahari wawili ambao kwasababu zao wameamua kulimana na sasa wanataka kuonyeshana umwamba.

Kama unaungwa mkono na CHADEMA basi itisha uchaguzi, vinginevyo kaa kimya.

Pia usitupotoshe kwamba Wangwe alichaguliwa na kamati kuu, hata kama sijui katiba ya CHADEMA na wala sina hata muda wa kupoteza kusoma katiba inayoruhusu mambo mliyofanya jana, lakini nakumbuka kabisa ilijadiliwa hapa JF. Wangwe hakuchaguliwa na kamati kuu ya CHADEMA, alichaguliwa na chombo kikubwa kuliko kamati kuu. Kwenye kamati kuu naamini Wangwe asingeshinda. Kama nimekosea nisahihishe.
 
mnatukatisha tamaa kweli kweli sisi wapiga kura, haya mwageni siri zenu zote hapa tujue hamuwezi kuendesha nchi.

Kitendo cha kuweza kumwambia mtu ukweli na kumkabili sio mara ya kwanza kufanyika kwa CHADEMA kumbukeni Kabourou naye alijiuzulu ukatibu mkuu baada ya kutofautiana na Mzee Makani 2003.
 
Ndugu zangu,

Mimi sii mkali katika maswala kama haya isipokuwa kusema kweli naliona swala halikukaa vizuri kabisa...Uamuzi uliopitishwa kidogo una mushkheri yaani ni ktk maamuzi yale ambayo sikuyategemea..
Binafsi nilitegemea baada ya maamuzi ya Kikao basi Uongozi wa Chadema wangewakilisha swala hili kwa wananchi wake waliompigia kura na kuwapa taarifa yote hii ili wapate kupiga tena kura za kumsimamisha Wangwe..
Chadema kama chama hawahitaji kufanya kama CCM ambao tumewaona siku nyingi wakiondoa watu wapinzani na kuwabeba wanaounga mkono Ubabe na Ufisadi..Hii ni hatari sana kama mtu hakubaliani na baadhi ya vitu ama viongozi fulani basi aondolewe na kuwekwa yule mwenye utiifu kwa mtu ama kundi la watu...
Binafsi naamini kuwa kinachotupanga nyuma ya chama ni Mrengo, sera na ilani za chama sio upinzani kati ya watu na kama kweli Chacha Wangwe amekuwa akijaribu kupotosha mwelekeo wa Chama nadhani hilo ni jukumu la wananchama wote kulisikia na pengine kusikia Utetezi wa Wangwe mwenyewe sawa kabisa na utaratibu uliofuatwa alipochaguliwa...
Nadhani hapa kumetumika zaidi hisia za watu na upinzani ama chuki baina ya watu badala ya haki kutumika, hata kama Wangwe ni mkodefu kweli.. Utaratibu uliotakiwa ungekuwa na UWAZI zaidi kwa wanachama kuliko taarifa ya kamati kuu kwani hadi sasa hivi sidhani kama wananchi waliomchagua wanafahamu utetezi wa Chacha Wangwe kuhusiana na tuhuma zilizowakilishwa..
ChaCha Wangwe pamoja na makosa yote ambao alionyesha hata kabla ya Uchaguzi alikuwa pendekezo la wananchi na ikaleta matatizo kwa baadhi viongozi na kama nakumbuka ilibidi tu hao viongozi waheshimu uchaguzi wa wananchi waliokuwa wengi (demokrasia) lakini hayakuwa matakwa yao hata kidogo.. leo hii baada ya kukaa muda kamati (viongozi hao) inachukua madaraka ya kile walichokusudia toka ama kabla ya Uchaguzi!.. Hiki ndicho kinachonekana kwa wananchi ...hii inatisha!
 
mnatukatisha Tamaa Kweli Kweli Sisi Wapiga Kura, Haya Mwageni Siri Zenu Zote Hapa Tujue Hamuwezi Kuendesha Nchi.

Gombaneni Kukicha Itakuwa Si Bao La Kisigino Tena Ila bao La Mkono La Maradona[/b]
 
Kitendo cha kuweza kumwambia mtu ukweli na kumkabili sio mara ya kwanza kufanyika kwa CHADEMA kumbukeni Kabourou naye alijiuzulu ukatibu mkuu baada ya kutofautiana na Mzee Makani 2003.

Mfano Mbowe angekuwa Rais wa nchi na Wangwe makamu wa Rais halafu wakatofautiana ingekuwaje kwa sifa hizi za chadema za kutiamuana na kujiuzulu, inaonyesha mna siasa za bifu na kususa.
 
Kamati ya wazee wa CHADEMA imejaa wazee wenye utaalamu mbalimbali na busara za hali ya juu.
Prof.Baregu ni mtaalamu wa conflict management sasa kashidwa ...

Balozi Ngaiza ni Balozi wa kwanza mweusi kuiwakilisha nchi UN naye pamoja na diplomasia yake kashindwa.

Mzee Makani ni mwanasheria aliyebobea naye kashindwa .

ungekuwa wewe ungefanaya nini baada ya jitihada zote kushindwa ?

MK,

Mkuu afadhali ukae kimya maana kadri unavyoandika, unaanza kuonekana kama yule waziri wa habari wa Saddam.

Hizo SPINS wengine tumezikia mno, yaani ni vichekesho tupu.

Wengine tunaamini garbage in garbage out. Kama mwenyekiti wenu kachafua process
nzima ya kushughulikia migogoro unafikiri hata hizo busara za hao wazee zingesaidia nini? Hapo walitakiwa wachague upande na wamechagua upande.
 
Mbowe,

Chama kimekushinda, itisha uchaguzi ili wana CHADEMA waamue wanataka kuongozwa na nani. Haya mambo ya kufukuzana uongozi wa siasa yamepitwa na wakati.

Sababu zote mlizotoa zinaonyesha ni ugomvi wa mafahari wawili, hapo hakuna cha maadili au katiba. Ni mafahari wawili ambao kwasababu zao wameamua kulimana na sasa wanataka kuonyeshana umwamba.

Kama unaungwa mkono na CHADEMA basi itisha uchaguzi, vinginevyo kaa kimya.

Pia usitupotoshe kwamba Wangwe alichaguliwa na kamati kuu, hata kama sijui katiba ya CHADEMA na wala sina hata muda wa kupoteza kusoma katiba inayoruhusu mambo mliyofanya jana, lakini nakumbuka kabisa ilijadiliwa hapa JF. Wangwe hakuchaguliwa na kamati kuu ya CHADEMA, alichaguliwa na chombo kikubwa kuliko kamati kuu. Kwenye kamati kuu naamini Wangwe asingeshinda. Kama nimekosea nisahihishe.

Kwanza niweke rekodi sahihi mimi sio Mbowe.

Pili huyu aliteuliwa/kuchaguliwa na Baraza Kuu, na huyu kama akiona ameonewa katiba inampa fursa ya kukata rufaa kwenye ngazi ya baraza kuu sasa mshauri akate rufaa kama unaona kuwa kaonewa ama hakutendewa haki na anaweza kukata rufaa mpaka mkutano mkuu wa chama ..au hata kwenda kutafuta haki yake mahakamani.
 
Uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti na jinsi ulivyoitikisa CHADEMA
Theopista Nsanzugwanko
HabariLeo; Tuesday,January 08, 2008 @00:04

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni moja ya vyama vikubwa vya siasa nchini. Kilianzishwa kwa juhudi za waasisi kadhaa wa chama hicho, ambao ni pamoja na Edwin Mtei na Bob Makani.

Mkutano mkuu wake wa kwanza wa chama hicho, ulifanyika katika kituo cha Msimbazi Dar es Salaam kuanzia Desemba 15-17, 1992. Mkutano huu ulihudhuriwa na wajumbe kutoka mikoa yote ya Tanzania na ulichagua viongozi wa kwanza wa chama hicho, majina na vyeo vyao kwenye mabano ni: Edwin Mtei (Mwenyekiti), Ali Suleiman Ahmed (Makamu Mwenyekiti upande wa Zanzibar), Brown Ngwilulupi (Makamu Mwenyekiti Bara), Bob Makani (Katibu Mkuu), Mustafa S. Simba (Naibu Katibu Mkuu Zanzibar) na Eric Mchatta (Naibu Katibu Mkuu Bara).

Tangu mwaka huo 1992, chama hicho kimeendelea kukua na kufanya uchaguzi wa viongozi wake kila inapobidi. Pia, tangu mwaka huo kimekuwa kikishiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na Rais. Matokeo ya kura katika chaguzi hizo yamekuwa ya kuridhisha na hali ya utulivu imekuwa pia inaridhisha.

Hata hivyo, hivi karibuni chama hicho kimetikiswa sana na suala la uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti wa Chadema upande wa Tanzania Bara. Hali hiyo ilijitokeza dhahiri katika vikao vya Kamati Kuu na Baraza Kuu vilivyofanyika Dar es Salaam, ambapo baada ya mvutano wa muda mrefu hatimaye alipatikana mshindi, ambaye ni Mbunge wa Tarime kwa tiketi ya chama hicho, Chacha Wangwe.

Wakati wa kampeni ya kugombea nafasi hiyo, madai mengi yalitolewa na baadhi ya wanachama wao, kuhusiana na chama hicho hadi ikafika mahali Katibu Mkuu wao, Dk.Wilbrod Slaa na Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe, kudaiwa kutaka kujiuzulu nyadhifa zao.

Wanadaiwa walitaka kujiuzulu baada ya kuchukizwa na kitendo cha Chacha Wangwe, ambaye alikuwa mgombea wa nafasi hiyo ya Makamu Mwenyekiti, kukishutumu chama kupitia vipeperushi vilivyosambazwa nchi nzima. Katika vipeperushi hivyo, Wangwe anadaiwa kusema kwamba chama kimegeuzwa kuwa mali ya ukoo na baadhi ya viongozi wa makao makuu.

Vipeperushi hivyo vilisambazwa na wafuasi wa chama hicho, waliokuwa wakimuunga mkono Wangwe katika kinyang'anyiro hicho. Habari kutoka ndani ya kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho, zinadai Dk Slaa ambaye ni Mbunge wa Karatu na Zitto ambaye ni mbunge wa Kigoma Kaskazini, walifikia uamuzi huo, baada ya hoja kuhusu vipeperushi hivyo kujadiliwa katika kikao hicho.

Hata hivyo, waasisi wa chama hicho, Edwin Mtei na Bob Makani walifanya kazi ya ziada kuwashawishi Dk Slaa na Zitto kubadili uamuzi wao wa kujiuzulu na kuendelea na nyadhifa zao ili kulinda chama kisigawanyike. Chanzo chetu kilichokuwa ndani ya kikao hicho cha Kamati Kuu, kilisema kuwa "Ni kweli Zitto na Slaa walitangaza kujiuzulu nyadhifa zao kutokana na vipeperushi vya Wangwe, lakini baada ya mambo kuwekwa sawa na waasisi hao wa chama, walikubali kurejea kwenye nyadhifa zao."

Kutokana na kitendo hicho, Kamati Kuu ilimuonya Wangwe na pia Kamati Kuu ilitishia kufuta uchaguzi huo. Hata hivyo, baadaye Kamati Kuu iliridhia kuwa uchaguzi huo ufanyike. Ilitoa uamuzi huo baada ya wajumbe wa kamati hiyo kupiga kura, ambapo 14 walisema ufanyike na 11 wakasema usifanyike. Ndipo kikao hicho kilifanyika chini ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ili kuandaa ajenda ambazo zingejadiliwa katika kikao cha Baraza Kuu.

Nalo Baraza Kuu baada ya kujadili ajenda hizo, liliendelea na ajenda ya kumchagua mwanachama atakayejaza nafasi ya Makamu Mwenyekiti, iliyoachwa wazi na Amani Walid Kabourou, aliyejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka jana. Lakini, pamoja na kuonywa, Wangwe aliendelea kushikilia msimamo wake ulioko kwenye vipeperushi vyake katika kikao hicho pia. V

ipeperushi hivyo vinawatuhumu baadhi ya viongozi wa Chadema kuendesha chama kwa upendeleo, hasa katika mgawo wa ruzuku. Pia, kinawatuhumu viongozi wa Chadema kwa ubaguzi wa misingi ya kidini na Kikanda. Katika vipeperushi hivyo, Wangwe anadai kuwa kutokana na kasoro hizo, atahakikisha analeta mabadiliko ya kweli ndani ya chama ili kukiepusha kuendeshwa kama shirika lisilo la kiserikali (NGO).

"Tunataka kiwe chama cha siasa chenye lengo la kuking'oa madarakani Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010," anasema Wangwe. Anasisitiza kuwa jambo kubwa linalokitia dosari CHADEMA ni ofisi za wilaya na kata kutokuwa na mawasiliano na makao makuu, hasa katika mgawo wa ruzuku na uteuzi wa wabunge wa viti maalumu.

Wangwe anadai mgawo wa ruzuku na uteuzi wa wabunge wa viti maalumu, vimekuwa vikitolewa na uongozi wa Chadema kwa kuangalia upande mmoja wa wanachama wanaotoka Kanda ya Kaskazini hapa nchini. "Chama kimekuwa mali ya koo na familia fulani. Tunataka kiwe cha wanachama," anadai Wangwe, ambaye baadaye alifanikiwa kupata nafasi hiyo ya Makamu Mwenyekiti.

Alimshinda Mbunge wa Mpanda Kati kwa tiketi ya Chadema, Said Arfi. Wafuasi wa chama hicho wanaomuunga mkono Wangwe katika kinyang'anyiro hicho, waliendelea kusambaza vipeperushi hivyo vinavyotuhumu kuwapo na upendeleo katika mgawo wa ruzuku za chama na ubaguzi wa kidini na kikanda katika chama hicho.

Vipeperushi hivyo vilitawanywa makao makuu ya Chadema, mikoani, wilayani na katika eneo ambalo Kamati Kuu ilikutana na vinadai kwamba chama hicho kimekuwa kikipata ruzuku ya Sh milioni 60 kila mwezi, lakini fedha hizo zimekuwa zikiishia makao makuu huku matumizi yake hayawekwi bayana.

"Tunasema inawezekana kila mkoa ukapata Sh milioni 1.5 kila mwezi na makao makuu itabaki na zaidi ya Sh milioni 10 ambazo zinawatosha kwa shughuli za chama," inaeleza sehemu ya kipeperushi hicho.

Kipeperushi kinadai kuwapo kwa "ubinafsi" katika chama, ambao umesababisha karibu wabunge wote wa viti maalumu kuteuliwa kutoka katika mkoa mmoja uliopo eneo la Kaskazini mwa nchi. "Tumchague Chacha ili aweze kubeba majukumu hayo na kuyavalia njuga ili ruzuku igawanywe katika mikoa yote. Chacha pambana kama unavyopambana na CCM katika Jimbo lako la Tarime," kinaeleza kipeperushi hicho.

Kipeperushi hicho kinawataka wajumbe wa Kamati Kuu na Baraza Kuu kutoingia kwenye mtego wa kidini, kwa madai kwamba chama hicho siyo msikiti wala kanisa. "Ni chama cha siasa kinachotaka kuendelezwa na kiongozi jasiri kama Chacha (Wangwe). Hatusemi kwa ushabiki, angalia ukweli hapo makao makuu. Chadema ni chama chetu siyo kampuni ya watu binafsi, tubadilishe hali hii," kilieleza kipeperushi hicho.

Baada ya kutolewa kwa malalamiko hayo yaliyopo katika vipeperushi, Dk.Slaa alikanusha madai yaliyotolewa na kusema kuwa pesa zote za ruzuku, hutumika kutokana na maamuzi ya vikao vya chama.

Pia, alizungumza kuhusu wabunge wa viti maalumu karibu wote kutoka upande mmoja wa Kaskazini, ambapo alisema kutokana na chama hicho kuwa na wabunge wachache, inawabidi kutafuta wenye uwezo katika kutoa hoja za msingi bungeni. "Wabunge huteuliwa kwa kuangalia utendaji wa kazi zao ambazo zinaonekana wakiwa bungeni.

Kule bungeni hatupeleki sura, bali watendakazi ambao ndio jeuri ya chama chetu," anasema. Dk Slaa anasema shutuma zilizotolewa na Wangwe, ambaye alikuwa anagombea umakamu mwenyekiti, ni maneno tu ya kumtaka apate nafasi hiyo.

Wlizungumzia baadhi ya matumizi yaliyoamuliwa katika vikao vya chama, kuwa ni pamoja na kuzunguka nchi nzima kukitambulisha chama kwa Watanzania, ambazo ukiacha usafiri na gharama nyingine zimetumika zaidi ya Sh milioni 200 kutengeneza bendera, kadi na vipeperushi.

Dk. Slaa anasema matumizi kama hayo siyo kwa manufaa ya makao makuu pekee, bali kwa mikoa yote waliyotembelea, ukiacha Mtwara na Lindi, ambayo bado hawajaitembelea kwa lengo la kuwajulisha Watanzania walioko mikoani sera za chama hicho.

"Hakuna chama kingine cha siasa ukiacha chama tawala kilichoweza kuzunguka mikoani na kujitambulisha kwa wananchi kama tulivyofanya sisi kwa shilingi milioni 60 kila mwaka," anasisitiza. Akifungua Baraza Kuu la chama hicho, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alidai suala la kusitishwa kwa mjadala wa Katiba ni ukiritimba. Anasema katiba inapaswa kujadiliwa wakati wowote kwa kuwa ni mali ya wananchi.

Pia, alisema baada ya kutimiza miaka miwili, Rais Jakaya Kikwete inabidi afanyiwe tathmini ya uongozi wake na pia alidai kuwa wananchi wamechoka na kauli za kutia matumaini huku hali ya maisha ikizidi kuwa ngumu. Pia, Mbowe anawataka Waziri wa Fedha, Zakia Meghji, kutoa ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwani kampuni iliyopewa kazi ya kuichunguza ilipewa siku 28 tu kukamilisha uchunguzi na kutoa ripoti.

Anadai kuwa siku zimeisha, lakini wananchi bado hawajapewa ripoti hiyo. Baada ya kumalizika kwa kikao hicho cha Baraza Kuu, Mbowe alikanusha kuwa kuna migogoro katika chama chake hicho. Pia, alisema kuwa Chadema itaendelea kutumia helikopta katika awamu nyingine ya ziara zake, baada ya kutafakari gharama za ziara za helikopta.

"Baraza Kuu limetafakari gharama za ziara za helikopta na kuwianisha na ziara nyingine na kuazimia kwa kauli moja kuendelea kutumia usafiri huo katika awamu nyingine ya ziara," anasema.

Mbowe anasema maazimio mengine waliyoyafikia ni pamoja na kuweka hadharani hesabu ya mapato na matumizi, kwani kila mwanachama wa chama hicho ana uhuru wa kufahamu hilo. Alitaka wengine wanaotaka kujua hesabu hizo wafike makao makuu. Pia, Baraza Kuu liliamua kuendeleza ushirikiano wa vyama kwa lengo la kudumisha demokrasia nchini na kuunganisha nguvu katika kutetea maendeleo na hatimaye upinzani uweze kuchukua dola. Baraza hilo lilipitisha azimio la kutangaza ratiba ya uchaguzi wa chama hicho, utakaofanyika kuanzia mwezi Januari hadi Desemba.

Anasema uchaguzi huo utaanzia katika vitongoji, kata, jimbo, wilaya, mikoa na Kanda. Pia, kutakuwa na uchaguzi wa wajumbe wa Kamati Kuu, Baraza Kuu na Mkutano Mkuu wa Taifa. Katika uchaguzi wa Makamu wa Mwenyekiti upande wa Tanzania Bara, Baraza Kuu lilimchagua Chacha Wangwe kushika nafasi hiyo, baada ya kupata kura 56 kati ya 94 zilizopigwa. Mpinzani wake Mbunge wa Mpanda Kati, Said Amour Arfi, alipata kura 38. Akitoa shukrani zake baada ya kutambulishwa rasmi kuwa Makamu, Wangwe anasema atatumia nafasi hiyo kurudisha demokrasia iliyoanza kupotea katika chama hicho. Anasema atafanya hivyo kwa kutumia vikao vya viongozi wa ngazi za juu.

Wangwe anasema kutokana na chama hicho kuwa cha kidemokrasia, mambo yote yaliyotokea ni harakati za kuimarisha demokrasia, hivyo yalikuwa ni sehemu ya midahalo tu; na wala sio migogoro, kama wengi walivyodhania.
 
Madai yote ya Kamati kuu na Wangwe - Yanaweza kukubaliwa na wananchi tu kwa sababu ndio wanayaona yote haya yakitokea kwao..Ni wananchi wenye kila haki ya kusema Wangwe hatakiwi ama kuna ukweli ktk madai yake hata kama viongozi wa Chadema hawaoni ubovu huo..Sisi sote binadamu, ni muhimu kujiangalia wenyewe ktk vioo kabla hujamsema mtu mwingine ubaya wake na vizuri ukiuliza wale unaokusudia kuwavutia!

Mabaya ya wangwe yalijulikana hata kabla hajachaguliwa na ajabu alichaguliwa yeye!...WHY?... hiki ndicho nataka kujua zaidi kwa nini Wangwe alichaguliwa na wana Chadema hata baada ya kuonyesha kuwa ni matatizo ama mzigo ktk chama..Pengine yale aliyowakilisha kwao ndio mapenzi ya wananchi na ukweli unaouma sana lakini UKWELI.
 
Kwanza niweke rekodi sahihi mimi sio Mbowe.

Pili huyu aliteuliwa/kuchaguliwa na Baraza Kuu, na huyu kama akiona ameonewa katiba inampa fursa ya kukata rufaa kwenye ngazi ya baraza kuu sasa mshauri akate rufaa kama unaona kuwa kaonewa ama hakutendewa haki na anaweza kukata rufaa mpaka mkutano mkuu wa chama ..au hata kwenda kutafuta haki yake mahakamani.

MK,

Hakuna sehemu nilipoandika wewe ni Mbowe. Mimi makala zangu zote nimeelekeza kwa Mbowe kwasababu yeye ndiye Mwenyekiti.

Sasa hapo Wangwe achaguliwe na baraza kuu lakini afukuzwe kazi na kamati kuu, hiyo wapi na wapi?

Tena mmeshaanza kusambaza propaganda zote hizi kwenye vyombo vya habari na kwa wanachama wenu. Ni haki gani ambayo Wangwe atakuwa nayo baada ya kuchafuliwa?

Hii habari ni ya kusikitisha sana. Mimi nilikuwa mfuasi mkubwa wa Mrema lakini yale mambo ya kufukuzana kila siku, binafsi nilijitihadi hata kuwashauri lakini bwana wee, watu hawataki hata kusikia.

Sasa leo wote tunaona nguvu yote ya Mrema imeishia wapi? Inasikitisha sana.

Ushauri wangu mimi kwa Mbowe bado ni ule ule, jiuzulu, itisha uchaguzi mpya na gombea ili wananchi waamue kama bado wanakutaka. Vinginevyo wengine watapata.
 
Tanzania kweli hakuna upinzani, kama hawa nao wanaonyesha kuwa incompetent katika uongozi wa ndani, nchi wataiweza kweli? Chadema kilikuwa kikiibukia kuwa chama chenye kuleta upinzani wa hali ya juu kwa CCM.
 
Mmmmhhhhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!! mambo yale yale ya CCM, ZANU, KANU na vyama vingine vya wajinga Afrika.

Aliyechaguliwa na wananchi kwenye mkutano mkuu wa chama, anasimamishwa na kamati ya wapambe.

Adhabu ya mwanasiasa inapatikana kwenye uchaguzi, haya mambo ya kusimamishana yananikumbusha vyama vya Wakomunisti na hivyo vyama vyetu vya Afrika vinavyojaza wapambe kwenye kamati kuu.

Nilikuwa nafikiri CHADEMA ni chama makini, kumbe na wao ni yale yale tu. Je vipi Wangwe hajaanguka kwa BP?

Mkuu MK, wengine tunajua ulikuwepo kwenye hiyo kamati yenu, tuambie kilichotokea na sio hizi craps za taarifa ya chama. Naona hapa naangalia picha ambayo nilishaiona mwanzoni, tofauti tu ni mchezaji kabadilika. Badala ya main actor kuwa CCM sasa nao CHADEMA mnacheza kamchezo kale kale. Aibu kweli kweli.

Mkuu Mtanzania,

Ninavyoelewa ni kwamba watu wa CHADEMA wamemtoa Wangwe katika uongozi wa chama, kazi ambayo hakupewa na wananchi ila CHADEMA.

Unachosema kingekuwa sahihi kama CHADEMA wangemvua ubunge, kitu ambacho kisingekuwa kizuri sana kwa sababu inakuwa ni kumvua mtu kazi aliyopewa na wananchi bila ya kupewa mandate hiyo na wananchi.Lakini hata hilo linaweza kuwa justified kwa sababu Wangwe (na kila mtu for that matter in Tanzania) anaposhindania ubunge, hashindanii kama Wangwe, bali kama mwanachama wa CHADEMA, akitumia platform, manifesto na resources nyingine za CHADEMA.As such watu wengi tu wamempigia kura kwa sababu yeye ni mtu wa CHADEMA na siyo kwa sababu ni Wangwe (we will not know for sure how many, thats why we need private candidacy)

Viongozi wetu wanahitaji kuheshimu principles za collective responsibility, na kuheshimu misingi ya vyama vilivyowajenga na wanavyoviwakilisha.Ama sivyo wanahitaji kujiuzulu. Moja ya injustice kubwa ya kutokuwa na private candidacy ni kwamba mtu kama Wangwe anaweza kujichomeka CHADEMA just because bila ya kuwa na chama hawezi kuwa muwakilishi.
 
hizi shutuma za chinga zilikuwa na ukweli ndani yake nini
 
mi nakuwa nashindwa kuelewa kama hizi ni Spinning na ushabiki wa hapa JF, maana watu wanasubiri kitu kiandikwe kisha wanatafuta mabaya ndani yake...ilimradi tu la kuongea liwepo ama Chama Mbadala kinapoteza dira...

na tumesiKia upande mmoja wa Chama na kwa jinsi nnavyomfahamu Chacha sidhani kama atakuwa amekaa kimya, kwa nini asije nae kisha tukasikia upande wake kisha tukajadili.

husiana na kachaguliwa na nani na kusimamishwa na nani nadhani tunahitaji kupitia katiba ya chama.
 
Nimeshindwa hata cha kuzungumza ,habari hii imenishtua kweli kweli . Mimi nadhani Mbowe hapa ameonyesha ya kuwa sio mtu makini kulikuwa kuna njia kabisa ya kumtoa huyu bwana kwenye hiko cheo bila ya kusababisha damage kwa chama . Kinachoniuma hapa ni kuwa timing ya hili jambo , kuna ishu muhimu sana zimekuwa zikiongelewa huko Bungeni ambazo tulitakiwa tuconcentrate . Sasa hili jambo limebadilisha topic !

Je Mbowe ana mpango wa kukibomoa chadema ? au ni part and parcel ya CCM ? au anaona ya kuwa Wangwe ni threat kwake ?
 
Kwani nimesikia tetesi kwamba uchaguzi wa CHADEMA ni mwezi wa nane si wangesubiri mpaka muda huo ili wasimrudishe kwenye hicho kiti au? itakuaje tena kwa muda uliobaki nani atakahimu tena nafasi hii?
 
Back
Top Bottom