CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

Ajifunze kwa Bw. Mtungirehi (sijui kama nimepatia jina) jamaa anahaiba ya uongozi kwani ni mtulivu, hata akitoa hoja inakuwa na mantiki & muwasilisho unaostahili. Ndiyo maana anaweza kuwa Makamu Mwenyekiti wa Mrema. Naombea Mtungirehi arudi bungeni 2010.
 
Mhe. Chacha Wangwe alishaonyesha kwamba hana haiba ya uongozi hata kabla ya kuchaguliwa katika nafasi hiyo, ila anafaa kwenye ubunge kwani anaweza kutetea watu hasa kwa kulalamika na kulalama. Mimi nadhani CHADEMA wamwfanya sahihi ili kukinusuru chama chao.

Kumpatia Umakamu Mwenyekiti huyo Mheshimiwa na sawa na CCM kumpatia Mhe. Shibuda awe Makamu Mwenyekiti.

Nziku,

Wangwe alichaguliwa na wala hakuteuliwa, inatakiwa waliomchagua ndio wamwondoe na sio kamati ndogo ambayo hata wakati anachaguliwa walimpinga.

Siku tutakapowaamini wananchi wetu na wanachama wetu, vyama na jumuia zingine Tanzania zitaepukana na matatizo.

Watu wote sio sawa na hata siku moja hatuwezi kulazimisha watu wote wawe na misimamo au tabia zinazofanana. In fact kadri chama kinavyokuwa na watu wa aina tofauti ndivyo kinavyokuwa imara zaidi.

Nasikia CHADEMA wana uchaguzi December, kulikuwa na haja gani kukimbilia kumsimamisha badala ya kuwaachia wanachama kuamua hapo December?

Walichofanya ni sawa na kwenda kuogelea kwenye bwawa ambalo unajua limejaa mamba, CHADEMA wamewapa CCM nafasi ya wazi ya kuwalima.

Pamoja na tofauti zetu lazima tuweze kuzijadili na kuzimaliza ndani ya vyama au jumuia zetu lakini sio haya mambo ya kuanza kufukuzana, kusimamishana uongozi nk.

Yaani hapo CHADEMA hawana tofauti na uongozi wa UDSM, kusimamisha wanafunzi kila siku.

Mimi nimeishiwa nguvu juu ya hili. Nawaonea huruma wapenzi na wanachama wa CHADEMA kwa hili. Wote juzi tuliona picha ya Obama na Clinton, hao si ndio walikuwa wanarushiana mabomu kila siku? Leo wanashikana mabegani utafikiri wameopoana, jamani, jifunzeni siasa!
 
Safi sana endeleeni kusambaratika. Mimi naamini mtu anaweza kujirekebisha.

Hapo ni kuwa Chacha alikuwa anamtishia mwenyekiti wake kwenye kugombea urais...Lol

Bado sana. Mtanzania nakuunga mkono demokrasia Africa bado sana.
 
Mnyika, Zitto Mpo Wapi Mbona Hatuoni Comments Zenu On This Thread?? Hebu Kuweni Wazalendo Kidogo
 
Any way, Chadema ina vichwa vingi tu Mwanaidi, Anne n.k.
 
bob makani.jpg​
Muasisi wa CHADEMA, Mzee Bob Makani, akijipumzisha kwenye viwanja vya Bunge, Dodoma, wakati akiwasubiri wajumbe wa chama hicho waliotembelea bungeni jana. (Picha na Emmanuel Kwitema)
 
Nziku,

Wangwe alichaguliwa na wala hakuteuliwa, inatakiwa waliomchagua ndio wamwondoe na sio kamati ndogo ambayo hata wakati anachaguliwa walimpinga.

Siku tutakapowaamini wananchi wetu na wanachama wetu, vyama na jumuia zingine Tanzania zitaepukana na matatizo.

Watu wote sio sawa na hata siku moja hatuwezi kulazimisha watu wote wawe na misimamo au tabia zinazofanana. In fact kadri chama kinavyokuwa na watu wa aina tofauti ndivyo kinavyokuwa imara zaidi.

Nasikia CHADEMA wana uchaguzi December, kulikuwa na haja gani kukimbilia kumsimamisha badala ya kuwaachia wanachama kuamua hapo December?

Walichofanya ni sawa na kwenda kuogelea kwenye bwawa ambalo unajua limejaa mamba, CHADEMA wamewapa CCM nafasi ya wazi ya kuwalima.

Pamoja na tofauti zetu lazima tuweze kuzijadili na kuzimaliza ndani ya vyama au jumuia zetu lakini sio haya mambo ya kuanza kufukuzana, kusimamishana uongozi nk.

Yaani hapo CHADEMA hawana tofauti na uongozi wa UDSM, kusimamisha wanafunzi kila siku.

Mimi nimeishiwa nguvu juu ya hili. Nawaonea huruma wapenzi na wanachama wa CHADEMA kwa hili. Wote juzi tuliona picha ya Obama na Clinton, hao si ndio walikuwa wanarushiana mabomu kila siku? Leo wanashikana mabegani utafikiri wameopoana, jamani, jifunzeni siasa!
Mbona hata huko CCM kamati kuu ndiyo yenye mandate ya kufanya hivyo?kama mtu anaenda kinyume na maadili ya chama hiyo ndiyo solution labda atajirekebisha. Hapo kasimamishwa tu(suspension) hajafukuzwa.soma hapa "Mjumbe mwingine wa kikao cha Kamati Kuu ambaye jana alizungumza na Tanzania Daima Jumapili, alisema kimsingi uamuzi wa kusimamishwa kwa Wangwe unatokana na pendekezo la vikao hivyo vya wazee, ambako awali aliitwa na kuonywa na yeye akaomba radhi kwa makosa yaliyokuwa yakimkabili.

Hata hivyo, hatma ya uongozi kwa Wangwe itaamuliwa na kikao cha Baraza Kuu la chama hicho.

Kutokana na kikao cha jana, uongozi wa juu wa CHADEMA, leo unatarajiwa kufanya mkutano wa hadhara mjini Dodoma katika uwanja ambao gazeti hili halikufanikiwa kuufahamu hadi linakwenda mitamboni.

Katika mkutano huo ambao utahutubiwa na viongozi wote wa juu wa CHADEMA, ndipo panapotarajiwa kutolewa maelezo na viongozi hao ya nini kilichotokea ndani ya Kamati Kuu jana".
 
Last edited:
WanaJF,
Hili ni jambo la kusikitisha sana kwa maendeleo ya demokrasia nchini, kwani inaweza ikawa ndio mwanzo wa kumomonyoka kwa kimoja ya vyama kilichoonyesha kuwa na nafsi nzuri sana ya kuiongoza nchi.

Lakini haya ni matokeo ya CHADEMA kukubali kuendeshwa kama kampuni binafsi kutokana na watu wachache kuwa na ushawishi mkubwa sana kupindukia kiasi.

Nilishaonya hapo awali na kujaribu kuwashawishi wana-CHADEMA kuanza kuuliza maswali magumu ili kuwe na mabadiliko ndani ya chama, maana mambo mengi yalikuwa yako wazi wazi, badala ya kufanya hivyo wakayatetea hayo maovu. Migawanyiko kama ilivyokuwa NCCR, TLP n.k., ilianza hivi hivi kwa kusimamishana uongozi.

Nina uhakika kabisa sababu zozote zitakazotolewa zitakuwa ni zile za kupikwa tu, ila ukweli ni kuwa wenye chama walikuwa tayari hawamtaki Bw. Wangwe na ninahisi ni kwa vile alionyesha wazi kuwa na msimamo wa kujitegemea kimawazo.

Hapa tusubiri siku Zitto na Dr. Slaa nao watakapoamua kuyatolea uvivu yale niliyosema siku nyingi. Hivi sasa bado wanaoneana aibu, lakini sidhani kama ni wajinga kiasi cha kutoyaona unless kama nao wanafaidika kivyao.

CHADEMA wanahitaji maombi yetu maana ni muhimu kwa wao kuwepo TZ kama chama chenye nguvu na sio chama ruzuku.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
NA
WANANCHI WA TANZANIA

KUSIMAMISHWA KWA MHESHIMIWA CHACHA ZAKAYO WANGWE (MB.) KUWA KAIMU MAKAMU MWENYEKITI WA TAIFA (BARA) WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO

Ndugu wanahabari na wananchi wenzangu,

Tarehe 28 Juni 2008 Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo katika kikao chake cha kawaida kilimsimamisha Mheshimiwa Chacha Zakayo Wangwe kama Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Taifa (Bara) wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kumpigia kura ya siri ya kutokuwa na imani naye. Huu ni uamuzi mzito na ambao haujawahi kufanywa katika historia ya miaka 16 ya CHADEMA. Tunapenda kuwafahamisha wananchi wetu kwamba uamuzi huu mzito ulichukuliwa baada ya mjadala na tafakuri ya muda mrefu. Kamati Kuu ya chama chetu ilifikia hatua hiyo dhidi ya baada ya kuridhika na ushahidi kwamba Mh. Chacha Wangwe amekiuka maadili ya uongozi na hivyo kupoteza sifa mahsusi za kuendelea kuwa kiongozi wa kitaifa wa CHADEMA kwa sababu zifuatazo:

1. Amekuwa akijihusisha na/au kushiriki katika vikundi na/au vitendo vya uchonganishi na/au kuzua migogoro ndani ya uongozi wa chama na/au wanachama wake.

Mheshimiwa Chacha Wangwe amejihusisha na/au kushirikiana na kikundi cha waliokuwa viongozi wa chama wa Mkoa wa Dar es Salaam ambao walifutwa uongozi na vikao halali vya chama na kwa kufuata Katiba na Kanuni za chama. Kujihusisha na/au kushiriki huko ni pamoja na kuandaa, kufadhili na kushiriki katika mikutano ya siri kwa lengo la kuendeleza migogoro na hujuma kwa chama. Mikutano hii ilifanyika Ndugumbi, Dar es Salaam na pia Mwanza na ilimshirikisha pia Dr. Amani Walid Kabourou aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Taifa (Bara) kabla hajahamia Chama cha Mapinduzi mara tu baada ya kushindwa kutetea kiti chake cha ubunge katika Jimbo la Kigoma Mjini. Kitendo cha kuandaa, kushiriki na/au kufadhili mikutano ya siri ya watu ambao wamechukuliwa hatua za kinidhamu na vikao halali vya chama na/au ambao wamekihama chama baada ya kupoteza ridhaa ya kuwaongoza wananchi kina tafisiri moja tu ya msingi: Kuendeleza migogoro na/au hujuma dhidi ya chama kwa lengo la kukidhoofisha na kukifanya kishindwe kuendeleza vita kubwa dhidi ya ufisadi uliojikita ndani ya Serikali na CCM ambayo imekipatia chama chetu sifa kubwa na uhalali kwa watanzania. Vitendo hivi vinapingana moja kwa moja na maadili ya viongozi wa chama kama yalivyoelezwa katika Sura ya Kumi ya Katiba, Kanuni, Maadili na Itifaki za CHADEMA.
2. Amekuwa akitoa tuhuma nzito lakini zisizokuwa na msingi dhidi ya viongozi wenzake wa kitaifa na watendaji wa chama pasipo kupitia vikao halali na wala kuzingatia taratibu za chama

Mheshimiwa Chacha Zakayo Wangwe aidha moja kwa moja ama kwa kuwatumia viongozi na/au wanachama walioadhibiwa na vikao halali vya chama amekuwa akiwatuhumu viongozi na watendaji wa chama kwa mambo ya uzushi na yasiyokuwa na ukweli na/au msingi wowote. Yeye mwenyewe amekuwa akisambaza uzushi kwamba kuna ufujaji na/au matumizi mabaya ya fedha za chama ambao amekuwa akidai unafanywa na viongozi wa kitaifa hususan Mwenyekiti wa chama Taifa na Katibu Mkuu na/au watendaji wa Makao Makuu ya chama. Aidha Mh. Chacha Wangwe amekuwa akisambaza uzushi kwamba viongozi wenzake wa kitaifa na watendaji Makao Makuu wamekuwa wakikataa ruzuku ya chama kupelekwa mikoani na wilayani nabadala yake wamekuwa wakiitumia ruzuku hiyo kwa shughuli za Makao Makuu na/au kwa manufaa yao binafsi. Uzushi huu umetolewa licha ya Kamati Kuu ya chama ambayo Mh. Chacha Wangwe alikuwa ni mjumbe kupokea na kupitisha taarifa zote zinazohusiana na mapato na matumizi ya fedha za chama na licha ya chama kutoa ruzuku ya vifaa na/au fedha taslimu tangu mwaka 2006 kabla hata ya yeye kuchaguliwa kuwa Kaimu Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA tarehe 17 Desemba mwaka 2007. Aidha Mh. Chacha Wangwe amesambaza uzushi huu licha ya kufahamu fika kwamba si yeye mwenyewe, wala si Makamu Mwenyekiti Taifa (Visiwani), wala si Mwenyekiti Taifa wala si Katibu Mkuu wala manaibu Makatibu Wakuu wote wa chama ambao wamepokea hata senti moja ya fedha za chama kama posho au mishahara. Tuhuma hizi za uzushi na uwongo juu ya kuwepo ufujaji na/au matumizi mabaya ya fedha za chama zina lengo moja tu: Kuwapaka matope viongozo wa chama wa kitaifa na watendaji wa ngazi za juu wa chama kwa lengo la kudhoofisha jitihada za chama kujijenga kwa wananchi na kuendeleza vita dhidi ya ufisadi ambayo imekipatia chama na viongozi wake umaarufu miongoni mwa wananchi wa Tanzania.

3. Amekuwa akikashifu chama, viongozi na watendaji wake bila kutofautisha kashfa na ukosoaji wa kisiasa na/au wa kiutendaji

Mheshimiwa Chacha Wangwe yeye mwenyewe na/au kwa kutumia wanachama na/au viongozi waliochukuliwa hatua za kinidhamu na vikao halali vya chama amekuwa akitoa kashfa dhidi ya chama, viongozi wake na/au watendaji wake. Bila ya kujali ushahidi uliopo hadharani wala maamuzi ya vikao vya chama ambavyo yeye mwenyewe alishiriki kuyafikia, Mh. Wangwe amekuwa akikituhumu chama, viongozi wenzake wa kitaifa na watendaji wake wa ngazi za juu kwa ukabila na/au udini. Licha ya ushahidi wa wazi kwamba viongozi wa ngazi za juu akiwemo yeye mwenyewe wametoka sehemu mbali mbali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Chacha Wangwe ameendelea kutuhumu kwamba kuna upendeleo kwa Wachagga na/au watu wa kaskazini ya Tanzania. Kivuli pekee cha tuhuma hizi potofu ni madai ya uwongo kwamba Wabunge watano kati ya sita wa Viti Maalumu wa CHADEMA katika Bunge la Jamhuri ni Wachagga. Kama wananchi wanavyofahamu, Wabunge Wachagga ni watatu tu na wengine ni Mzanzibari mmoja, Mpare mmoja na Muha mmoja. Aidha Mh. Chacha Wangwe anafahamu kwamba kati ya wajumbe thelathini na sita wa Kamati Kuu ya Chama kuna Wachagga watano tu sawa na wajumbe wa Mkoa wa Kigoma! Aidha Mh. Wangwe anafahamu fika kwamba kati ya wakurugenzi na watendaji wa ngazi za juu wa Makao Makuu wapatao zaidi ya ishirini, Wachagga wako watatu tu. Kwa msingi huo, lengo la kashfa za ukabila ndani ya chama zina lengo moja tu: kuwapaka matope viongozi na watendaji wa ngazi za juu wa chama kwa nia ya kuwadhoofisha na kuwapunguzia nguvu ya kuendeleza mapambano dhidi ya ufisadi ndani ya serikali na CCM.

4. Kuvujisha siri za vikao halali vya chama kwa watu wanaotaka kuhujumu chama

Mheshimiwa Chacha Zakayo Wangwe amehusishwa moja kwa moja na kosa la kutoa siri za vikao vya vya ndani vya chama. Kwa mfano, Mh. Wangwe ametoa siri na/au nyaraka za vikao vya Kamati ya Wazee wa Chama vilivyokutana kujadili tuhuma, uzushi na kashfa zake dhidi ya Mwenyekiti wa Taifa, Katibu Mkuu na Sekretariat ya Kamati Kuu ya Chama kwa watu ambao nao wamechapisha kwa kuzipotosha siri na/au nyaraka hizo katika vyombo vya habari vinavyomilikiwa na watu wanaokabiliwa na tuhuma za kuhusika na ufisadi mkubwa wa Richmond na EPA. Vile vile Mh. Wangwe ametoa siri na/au nyaraka hizo kwa kikundi cha wanachama na/au viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam waliofukuzwa uongozi na vikao halali vya chama. Lengo la kuvujisha na/au kupotosha nyaraka na/au taarifa za vikao vya ndani vya chama ni kuendeleza migogoro yenye lengo la kukidhoofisha chama na kukifanya kiache mapambano dhidi ya ufisadi ndani ya serikali na CCM.

Ndugu wananchi na wanahabari,

Kamati Kuu ya CHADEMA haikufikia uamuzi huu mzito kwa haraka na/au bila kufikiria kwa kina madhara yake kwa chama na kwa taifa letu. Kamati Kuu imefikia uamuzi huu baada ya jitihada mbali mbali za kumsaidia Mh. Chacha Zakayo Wangwe kujisahihisha na kujirudi kushindikana kabisa. Jitihada hizi mbali mbali ni kama vile:

a. Vikao mbali mbali na vya muda kati yake mwenyewe, Mwenyekiti Taifa na Katibu Mkuu kujadili tofauti na/au migongano kati yao na/au ndani ya chama;

b. Kusuluhishwa na Kamati ya Wazee wa Chama ambapo Mh. Wangwe alitakiwa kuandika maandishi kwamba ataacha vitendo vyake dhidi ya chama, viongozi wa kitaifa na watendaji wa chama;

c. Kamati Kuu ya chama kumuonya kuacha vitendo vyake hivyo dhidi ya chama;

d. Baada ya jitihada zote hizi kushindikana, Kamati Kuu ilimsihi kujiuzulu kwa hiari yake yeye mwenyewe na hivyo kujiepusha na adha ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye na kusimamishwa na Kamati Kuu.

Kwa vitendo na matukio yote haya, Kamati Kuu ya CHADEMA imejikuta haina njia yoyote ile ya kuepuka mgogoro mkubwa zaidi na usio na maana au msingi zaidi ya kumchukulia hatua za kinidhamu Mh. Chacha Zakayo Wangwe. Kwa matendo haya ni wazi Mh. Chacha Zakayo Wangwe amepoteza sifa mahsusi za kuendelea kushikilia dhamana kubwa ya uongozi ambayo vikao halali vya chama vilimpatia. Kamati Kuu imelazimika kutumia mamlaka yake ya kikatiba ya kumsimamisha uongozi wa kitaifa Mh. Wangwe kwa kumpigia kura ya siri ya kutokuwa na imani naye. Azimio la kumsimamisha Mh. Wangwe kuwa Kaimu Makamu Mwenyekiti Taifa (Bara) liliungwa mkono na wajumbe ishirini na nne kati ya thelathini na moja waliohudhuria na kushiriki katika kikao cha Kamati Kuu. Idadi hii ni zaidi ya theluthi mbili ya kura za wajumbe wa Kamati Kuu inayohitajika kikatiba ili kumsimamisha uongozi kiongozi yeyote wa kitaifa kama alivyokuwa Mh. Chacha Zakayo Wangwe. Kamati Kuu imechukua hatua hii ngumu na nzito ili kukiokoa chama kutokana na migogoro ambayo imesambaratisha vyama vingine vya siasa hapa nchini.

Asanteni sana

-----------------------------------------------
Freeman A. Mbowe
MWENYEKITI
 
6b-chacha.jpg

sawa wazee kazi imeanza

tuliwaambia mapema nyinyi wapinzani hamjaiva, sasa mnaona mmegeuka samaki mnalana nyinyi kwa nyinyi

ukweli muamini kuwa ccm gari kubwa msije kusema ccm ndio iliokufanyeni muwe mapogo
 
View attachment 1750

Kukmbuka maamuzi yaliyowahi kuchukuliwa na hao CCM katika kuhakikisha kuwa panakuwepo na uongozi wa pamoja ,kumbuka yaliyomkuta Seif ZNZ,JUMBE,ABDULWAKILI ET ALL.

Hapa ni suala la kuangalia principals na sio kufanya mambo kinyume na utaratibu halafu aachwe mtu .

Hakuna sababu ya kumuacha yeyote kwani kufanya hivyo ni kuharibu chama ,kama huyu kashindwa kujitetea mbele ya kamati ya wazee ambayo inaundwa na wazee hawa;

1.Mzee Mtei.
2,Mzee Bob Makani.
3.Prof.Baregu
4.Balozi Ngaiza
5.mzee Ndesamburo.

na hata kwenye kamati kuu alishindwa kutetewa na wajumbe kwani hao hao ndio walimuweka muda mchache uliopita sasa ni lazima mjue kuwa ni lazima wachache waumie ili kuelekea kwenye ukombozi........
 
Mbona hata huko CCM kamati kuu ndiyo yenye mandate ya kufanya hivyo?kama mtu anaenda kinyume na maadili ya chama hiyo ndiyo solution labda atajirekebisha. Hapo kasimamishwa tu(suspension) hajafukuzwa.soma hapa "Mjumbe mwingine wa kikao cha Kamati Kuu ambaye jana alizungumza na Tanzania Daima Jumapili, alisema kimsingi uamuzi wa kusimamishwa kwa Wangwe unatokana na pendekezo la vikao hivyo vya wazee, ambako awali aliitwa na kuonywa na yeye akaomba radhi kwa makosa yaliyokuwa yakimkabili.

Hata hivyo, hatma ya uongozi kwa Wangwe itaamuliwa na kikao cha Baraza Kuu la chama hicho.

Kutokana na kikao cha jana, uongozi wa juu wa CHADEMA, leo unatarajiwa kufanya mkutano wa hadhara mjini Dodoma katika uwanja ambao gazeti hili halikufanikiwa kuufahamu hadi linakwenda mitamboni.

Katika mkutano huo ambao utahutubiwa na viongozi wote wa juu wa CHADEMA, ndipo panapotarajiwa kutolewa maelezo na viongozi hao ya nini kilichotokea ndani ya Kamati Kuu jana".

Sasa unatuletea mambo ya CCM ambayo ndiyo tunailaumu kila siku? Kama CHADEMA wataanza kujilinganisha na CCM kweli watapotea.
 
CHADEMA wanaongozwa na katiba ,kanuni na taratibu za chama chao sasa kuna tatizo gani kama wakitumia taratibu zao kuwajibishana ?

Ama unataka wawe kama CCM kuwa hata kama mtu akikosea huwa wanalindana bila kuwajibishana?
 
Ndugu wananchi na wanahabari,

Kamati Kuu ya CHADEMA haikufikia uamuzi huu mzito kwa haraka na/au bila kufikiria kwa kina madhara yake kwa chama na kwa taifa letu. Kamati Kuu imefikia uamuzi huu baada ya jitihada mbali mbali za kumsaidia Mh. Chacha Zakayo Wangwe kujisahihisha na kujirudi kushindikana kabisa. Jitihada hizi mbali mbali ni kama vile:

a. Vikao mbali mbali na vya muda kati yake mwenyewe, Mwenyekiti Taifa na Katibu Mkuu kujadili tofauti na/au migongano kati yao na/au ndani ya chama;

b. Kusuluhishwa na Kamati ya Wazee wa Chama ambapo Mh. Wangwe alitakiwa kuandika maandishi kwamba ataacha vitendo vyake dhidi ya chama, viongozi wa kitaifa na watendaji wa chama;

c. Kamati Kuu ya chama kumuonya kuacha vitendo vyake hivyo dhidi ya chama;

d. Baada ya jitihada zote hizi kushindikana, Kamati Kuu ilimsihi kujiuzulu kwa hiari yake yeye mwenyewe na hivyo kujiepusha na adha ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye na kusimamishwa na Kamati Kuu.

Kwa vitendo na matukio yote haya, Kamati Kuu ya CHADEMA imejikuta haina njia yoyote ile ya kuepuka mgogoro mkubwa zaidi na usio na maana au msingi zaidi ya kumchukulia hatua za kinidhamu Mh. Chacha Zakayo Wangwe. Kwa matendo haya ni wazi Mh. Chacha Zakayo Wangwe amepoteza sifa mahsusi za kuendelea kushikilia dhamana kubwa ya uongozi ambayo vikao halali vya chama vilimpatia. Kamati Kuu imelazimika kutumia mamlaka yake ya kikatiba ya kumsimamisha uongozi wa kitaifa Mh. Wangwe kwa kumpigia kura ya siri ya kutokuwa na imani naye. Azimio la kumsimamisha Mh. Wangwe kuwa Kaimu Makamu Mwenyekiti Taifa (Bara) liliungwa mkono na wajumbe ishirini na nne kati ya thelathini na moja waliohudhuria na kushiriki katika kikao cha Kamati Kuu. Idadi hii ni zaidi ya theluthi mbili ya kura za wajumbe wa Kamati Kuu inayohitajika kikatiba ili kumsimamisha uongozi kiongozi yeyote wa kitaifa kama alivyokuwa Mh. Chacha Zakayo Wangwe. Kamati Kuu imechukua hatua hii ngumu na nzito ili kukiokoa chama kutokana na migogoro ambayo imesambaratisha vyama vingine vya siasa hapa nchini.

Asanteni sana
 
Last edited:
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
NA
WANANCHI WA TANZANIA

KUSIMAMISHWA KWA MHESHIMIWA CHACHA ZAKAYO WANGWE (MB.) KUWA KAIMU MAKAMU MWENYEKITI WA TAIFA (BARA) WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO

Ndugu wanahabari na wananchi wenzangu,

Tarehe 28 Juni 2008 Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo katika kikao chake cha kawaida kilimsimamisha Mheshimiwa Chacha Zakayo Wangwe kama Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Taifa (Bara) wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kumpigia kura ya siri ya kutokuwa na imani naye. Huu ni uamuzi mzito na ambao haujawahi kufanywa katika historia ya miaka 16 ya CHADEMA. Tunapenda kuwafahamisha wananchi wetu kwamba uamuzi huu mzito ulichukuliwa baada ya mjadala na tafakuri ya muda mrefu. Kamati Kuu ya chama chetu ilifikia hatua hiyo dhidi ya baada ya kuridhika na ushahidi kwamba Mh. Chacha Wangwe amekiuka maadili ya uongozi na hivyo kupoteza sifa mahsusi za kuendelea kuwa kiongozi wa kitaifa wa CHADEMA kwa sababu zifuatazo:

1. Amekuwa akijihusisha na/au kushiriki katika vikundi na/au vitendo vya uchonganishi na/au kuzua migogoro ndani ya uongozi wa chama na/au wanachama wake.

Mheshimiwa Chacha Wangwe amejihusisha na/au kushirikiana na kikundi cha waliokuwa viongozi wa chama wa Mkoa wa Dar es Salaam ambao walifutwa uongozi na vikao halali vya chama na kwa kufuata Katiba na Kanuni za chama. Kujihusisha na/au kushiriki huko ni pamoja na kuandaa, kufadhili na kushiriki katika mikutano ya siri kwa lengo la kuendeleza migogoro na hujuma kwa chama. Mikutano hii ilifanyika Ndugumbi, Dar es Salaam na pia Mwanza na ilimshirikisha pia Dr. Amani Walid Kabourou aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Taifa (Bara) kabla hajahamia Chama cha Mapinduzi mara tu baada ya kushindwa kutetea kiti chake cha ubunge katika Jimbo la Kigoma Mjini. Kitendo cha kuandaa, kushiriki na/au kufadhili mikutano ya siri ya watu ambao wamechukuliwa hatua za kinidhamu na vikao halali vya chama na/au ambao wamekihama chama baada ya kupoteza ridhaa ya kuwaongoza wananchi kina tafisiri moja tu ya msingi: Kuendeleza migogoro na/au hujuma dhidi ya chama kwa lengo la kukidhoofisha na kukifanya kishindwe kuendeleza vita kubwa dhidi ya ufisadi uliojikita ndani ya Serikali na CCM ambayo imekipatia chama chetu sifa kubwa na uhalali kwa watanzania. Vitendo hivi vinapingana moja kwa moja na maadili ya viongozi wa chama kama yalivyoelezwa katika Sura ya Kumi ya Katiba, Kanuni, Maadili na Itifaki za CHADEMA.
2. Amekuwa akitoa tuhuma nzito lakini zisizokuwa na msingi dhidi ya viongozi wenzake wa kitaifa na watendaji wa chama pasipo kupitia vikao halali na wala kuzingatia taratibu za chama

Mheshimiwa Chacha Zakayo Wangwe aidha moja kwa moja ama kwa kuwatumia viongozi na/au wanachama walioadhibiwa na vikao halali vya chama amekuwa akiwatuhumu viongozi na watendaji wa chama kwa mambo ya uzushi na yasiyokuwa na ukweli na/au msingi wowote. Yeye mwenyewe amekuwa akisambaza uzushi kwamba kuna ufujaji na/au matumizi mabaya ya fedha za chama ambao amekuwa akidai unafanywa na viongozi wa kitaifa hususan Mwenyekiti wa chama Taifa na Katibu Mkuu na/au watendaji wa Makao Makuu ya chama. Aidha Mh. Chacha Wangwe amekuwa akisambaza uzushi kwamba viongozi wenzake wa kitaifa na watendaji Makao Makuu wamekuwa wakikataa ruzuku ya chama kupelekwa mikoani na wilayani nabadala yake wamekuwa wakiitumia ruzuku hiyo kwa shughuli za Makao Makuu na/au kwa manufaa yao binafsi. Uzushi huu umetolewa licha ya Kamati Kuu ya chama ambayo Mh. Chacha Wangwe alikuwa ni mjumbe kupokea na kupitisha taarifa zote zinazohusiana na mapato na matumizi ya fedha za chama na licha ya chama kutoa ruzuku ya vifaa na/au fedha taslimu tangu mwaka 2006 kabla hata ya yeye kuchaguliwa kuwa Kaimu Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA tarehe 17 Desemba mwaka 2007. Aidha Mh. Chacha Wangwe amesambaza uzushi huu licha ya kufahamu fika kwamba si yeye mwenyewe, wala si Makamu Mwenyekiti Taifa (Visiwani), wala si Mwenyekiti Taifa wala si Katibu Mkuu wala manaibu Makatibu Wakuu wote wa chama ambao wamepokea hata senti moja ya fedha za chama kama posho au mishahara. Tuhuma hizi za uzushi na uwongo juu ya kuwepo ufujaji na/au matumizi mabaya ya fedha za chama zina lengo moja tu: Kuwapaka matope viongozo wa chama wa kitaifa na watendaji wa ngazi za juu wa chama kwa lengo la kudhoofisha jitihada za chama kujijenga kwa wananchi na kuendeleza vita dhidi ya ufisadi ambayo imekipatia chama na viongozi wake umaarufu miongoni mwa wananchi wa Tanzania.

3. Amekuwa akikashifu chama, viongozi na watendaji wake bila kutofautisha kashfa na ukosoaji wa kisiasa na/au wa kiutendaji

Mheshimiwa Chacha Wangwe yeye mwenyewe na/au kwa kutumia wanachama na/au viongozi waliochukuliwa hatua za kinidhamu na vikao halali vya chama amekuwa akitoa kashfa dhidi ya chama, viongozi wake na/au watendaji wake. Bila ya kujali ushahidi uliopo hadharani wala maamuzi ya vikao vya chama ambavyo yeye mwenyewe alishiriki kuyafikia, Mh. Wangwe amekuwa akikituhumu chama, viongozi wenzake wa kitaifa na watendaji wake wa ngazi za juu kwa ukabila na/au udini. Licha ya ushahidi wa wazi kwamba viongozi wa ngazi za juu akiwemo yeye mwenyewe wametoka sehemu mbali mbali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Chacha Wangwe ameendelea kutuhumu kwamba kuna upendeleo kwa Wachagga na/au watu wa kaskazini ya Tanzania. Kivuli pekee cha tuhuma hizi potofu ni madai ya uwongo kwamba Wabunge watano kati ya sita wa Viti Maalumu wa CHADEMA katika Bunge la Jamhuri ni Wachagga. Kama wananchi wanavyofahamu, Wabunge Wachagga ni watatu tu na wengine ni Mzanzibari mmoja, Mpare mmoja na Muha mmoja. Aidha Mh. Chacha Wangwe anafahamu kwamba kati ya wajumbe thelathini na sita wa Kamati Kuu ya Chama kuna Wachagga watano tu sawa na wajumbe wa Mkoa wa Kigoma! Aidha Mh. Wangwe anafahamu fika kwamba kati ya wakurugenzi na watendaji wa ngazi za juu wa Makao Makuu wapatao zaidi ya ishirini, Wachagga wako watatu tu. Kwa msingi huo, lengo la kashfa za ukabila ndani ya chama zina lengo moja tu: kuwapaka matope viongozi na watendaji wa ngazi za juu wa chama kwa nia ya kuwadhoofisha na kuwapunguzia nguvu ya kuendeleza mapambano dhidi ya ufisadi ndani ya serikali na CCM.

4. Kuvujisha siri za vikao halali vya chama kwa watu wanaotaka kuhujumu chama

Mheshimiwa Chacha Zakayo Wangwe amehusishwa moja kwa moja na kosa la kutoa siri za vikao vya vya ndani vya chama. Kwa mfano, Mh. Wangwe ametoa siri na/au nyaraka za vikao vya Kamati ya Wazee wa Chama vilivyokutana kujadili tuhuma, uzushi na kashfa zake dhidi ya Mwenyekiti wa Taifa, Katibu Mkuu na Sekretariat ya Kamati Kuu ya Chama kwa watu ambao nao wamechapisha kwa kuzipotosha siri na/au nyaraka hizo katika vyombo vya habari vinavyomilikiwa na watu wanaokabiliwa na tuhuma za kuhusika na ufisadi mkubwa wa Richmond na EPA. Vile vile Mh. Wangwe ametoa siri na/au nyaraka hizo kwa kikundi cha wanachama na/au viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam waliofukuzwa uongozi na vikao halali vya chama. Lengo la kuvujisha na/au kupotosha nyaraka na/au taarifa za vikao vya ndani vya chama ni kuendeleza migogoro yenye lengo la kukidhoofisha chama na kukifanya kiache mapambano dhidi ya ufisadi ndani ya serikali na CCM.

Ndugu wananchi na wanahabari,

Kamati Kuu ya CHADEMA haikufikia uamuzi huu mzito kwa haraka na/au bila kufikiria kwa kina madhara yake kwa chama na kwa taifa letu. Kamati Kuu imefikia uamuzi huu baada ya jitihada mbali mbali za kumsaidia Mh. Chacha Zakayo Wangwe kujisahihisha na kujirudi kushindikana kabisa. Jitihada hizi mbali mbali ni kama vile:

a. Vikao mbali mbali na vya muda kati yake mwenyewe, Mwenyekiti Taifa na Katibu Mkuu kujadili tofauti na/au migongano kati yao na/au ndani ya chama;

b. Kusuluhishwa na Kamati ya Wazee wa Chama ambapo Mh. Wangwe alitakiwa kuandika maandishi kwamba ataacha vitendo vyake dhidi ya chama, viongozi wa kitaifa na watendaji wa chama;

c. Kamati Kuu ya chama kumuonya kuacha vitendo vyake hivyo dhidi ya chama;

d. Baada ya jitihada zote hizi kushindikana, Kamati Kuu ilimsihi kujiuzulu kwa hiari yake yeye mwenyewe na hivyo kujiepusha na adha ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye na kusimamishwa na Kamati Kuu.

Kwa vitendo na matukio yote haya, Kamati Kuu ya CHADEMA imejikuta haina njia yoyote ile ya kuepuka mgogoro mkubwa zaidi na usio na maana au msingi zaidi ya kumchukulia hatua za kinidhamu Mh. Chacha Zakayo Wangwe. Kwa matendo haya ni wazi Mh. Chacha Zakayo Wangwe amepoteza sifa mahsusi za kuendelea kushikilia dhamana kubwa ya uongozi ambayo vikao halali vya chama vilimpatia. Kamati Kuu imelazimika kutumia mamlaka yake ya kikatiba ya kumsimamisha uongozi wa kitaifa Mh. Wangwe kwa kumpigia kura ya siri ya kutokuwa na imani naye. Azimio la kumsimamisha Mh. Wangwe kuwa Kaimu Makamu Mwenyekiti Taifa (Bara) liliungwa mkono na wajumbe ishirini na nne kati ya thelathini na moja waliohudhuria na kushiriki katika kikao cha Kamati Kuu. Idadi hii ni zaidi ya theluthi mbili ya kura za wajumbe wa Kamati Kuu inayohitajika kikatiba ili kumsimamisha uongozi kiongozi yeyote wa kitaifa kama alivyokuwa Mh. Chacha Zakayo Wangwe. Kamati Kuu imechukua hatua hii ngumu na nzito ili kukiokoa chama kutokana na migogoro ambayo imesambaratisha vyama vingine vya siasa hapa nchini.

Asanteni sana

-----------------------------------------------
Freeman A. Mbowe
MWENYEKITI

BIG CRAP! Utafikiri imeandaliwa na akina Ngombale Mwiru au Mwakawago enzi zake.

Mbowe unashangilia kuvuja kwa siri za serikali hapa JF, unafikiri mukifanya mambo hovyo
CHADEMA watu watawafichia siri?
 
Ni nini cha hovyo kimefanywa toa ushahidi Mbowe akisema EPA anaonyesha na madudud yote yaliyopo kwenye hiyo EPA...
 
Ndugu wananchi na wanahabari,

Kamati Kuu ya CHADEMA haikufikia uamuzi huu mzito kwa haraka na/au bila kufikiria kwa kina madhara yake kwa chama na kwa taifa letu. Kamati Kuu imefikia uamuzi huu baada ya jitihada mbali mbali za kumsaidia Mh. Chacha Zakayo Wangwe kujisahihisha na kujirudi kushindikana kabisa. Jitihada hizi mbali mbali ni kama vile:

a. Vikao mbali mbali na vya muda kati yake mwenyewe, Mwenyekiti Taifa na Katibu Mkuu kujadili tofauti na/au migongano kati yao na/au ndani ya chama;

b. Kusuluhishwa na Kamati ya Wazee wa Chama ambapo Mh. Wangwe alitakiwa kuandika maandishi kwamba ataacha vitendo vyake dhidi ya chama, viongozi wa kitaifa na watendaji wa chama;

c. Kamati Kuu ya chama kumuonya kuacha vitendo vyake hivyo dhidi ya chama;

d. Baada ya jitihada zote hizi kushindikana, Kamati Kuu ilimsihi kujiuzulu kwa hiari yake yeye mwenyewe na hivyo kujiepusha na adha ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye na kusimamishwa na Kamati Kuu.

Kwa vitendo na matukio yote haya, Kamati Kuu ya CHADEMA imejikuta haina njia yoyote ile ya kuepuka mgogoro mkubwa zaidi na usio na maana au msingi zaidi ya kumchukulia hatua za kinidhamu Mh. Chacha Zakayo Wangwe. Kwa matendo haya ni wazi Mh. Chacha Zakayo Wangwe amepoteza sifa mahsusi za kuendelea kushikilia dhamana kubwa ya uongozi ambayo vikao halali vya chama vilimpatia. Kamati Kuu imelazimika kutumia mamlaka yake ya kikatiba ya kumsimamisha uongozi wa kitaifa Mh. Wangwe kwa kumpigia kura ya siri ya kutokuwa na imani naye. Azimio la kumsimamisha Mh. Wangwe kuwa Kaimu Makamu Mwenyekiti Taifa (Bara) liliungwa mkono na wajumbe ishirini na nne kati ya thelathini na moja waliohudhuria na kushiriki katika kikao cha Kamati Kuu. Idadi hii ni zaidi ya theluthi mbili ya kura za wajumbe wa Kamati Kuu inayohitajika kikatiba ili kumsimamisha uongozi kiongozi yeyote wa kitaifa kama alivyokuwa Mh. Chacha Zakayo Wangwe. Kamati Kuu imechukua hatua hii ngumu na nzito ili kukiokoa chama kutokana na migogoro ambayo imesambaratisha vyama vingine vya siasa hapa nchini.

Asanteni sana

Mheshimiwa Mbowe,

Kwenye siasa, kama kuna migongano ya viongozi wa juu, wenye mamlaka ya kujua nani yuko sahihi ni wanachama.

Mulichotakiwa ni kuitisha mkutano mkuu wa wanachama wenu na kuomba kura zao. Wale
ambao wamepoteza dira wasingelichaguliwa tena. Utaniambia nisome katiba yenu, nitakuwa napoteza muda wangu kusoma katiba inayokapatia kakundi kadogo ka wapambe uwezo wa kumsimamisha makamu mwenyekiti wao. Mimi sitaki hata kuiona katiba ya namna hiyo. Ni sawa na kuniambia nisome katiba ya Mugabe.

Lakini kuanza kufukuzana, mnaturudisha kwenye ukiritimba wa CCM na marafiki zake mbalimbali hapo Afrika na kwenye nchi za Kikomunisti zamani.

Kwa mwendo kama huu Watanzania hatuwezi kutegemea makubwa kwenye hicho chama chenu. Labda wakati umefika kwa wanachama wengine makini wa CHADEMA kuamua kugombea uenyekiti na kukinusuru chama. CHADEMA ina vijana wengi ambao binafsi nawajua na labda ndio ukombozi wa baadaye wa nchi na CHADEMA.

Sikutegemea CHADEMA na nyie mnaona mtasolve matatizo yenu kwa kufukuza viongozi wenzenu. Yaani kweli ndio tulivyo! nakubaliani na Nyani.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
NA
WANANCHI WA TANZANIA

KUSIMAMISHWA KWA MHESHIMIWA CHACHA ZAKAYO WANGWE (MB.) KUWA KAIMU MAKAMU MWENYEKITI WA TAIFA (BARA) WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO

Ndugu wanahabari na wananchi wenzangu,

Kamati Kuu ya chama chetu ilifikia hatua hiyo dhidi ya baada ya kuridhika na ushahidi kwamba Mh. Chacha Wangwe amekiuka maadili ya uongozi na hivyo kupoteza sifa mahsusi za kuendelea kuwa kiongozi wa kitaifa wa CHADEMA kwa sababu zifuatazo:

1. Amekuwa akijihusisha na/au kushiriki katika vikundi na/au vitendo vya uchonganishi na/au kuzua migogoro ndani ya uongozi wa chama na/au wanachama wake.

2. Amekuwa akitoa tuhuma nzito lakini zisizokuwa na msingi dhidi ya viongozi wenzake wa kitaifa na watendaji wa chama pasipo kupitia vikao halali na wala kuzingatia taratibu za chama

3. Amekuwa akikashifu chama, viongozi na watendaji wake bila kutofautisha kashfa na ukosoaji wa kisiasa na/au wa kiutendaji

4. Kuvujisha siri za vikao halali vya chama kwa watu wanaotaka kuhujumu chama

Kamati Kuu ya CHADEMA haikufikia uamuzi huu mzito kwa haraka na/au bila kufikiria kwa kina madhara yake kwa chama na kwa taifa letu. Kamati Kuu imefikia uamuzi huu baada ya jitihada mbali mbali za kumsaidia Mh. Chacha Zakayo Wangwe kujisahihisha na kujirudi kushindikana kabisa. Jitihada hizi mbali mbali ni kama vile:

a. Vikao mbali mbali na vya muda kati yake mwenyewe, Mwenyekiti Taifa na Katibu Mkuu kujadili tofauti na/au migongano kati yao na/au ndani ya chama;

b. Kusuluhishwa na Kamati ya Wazee wa Chama ambapo Mh. Wangwe alitakiwa kuandika maandishi kwamba ataacha vitendo vyake dhidi ya chama, viongozi wa kitaifa na watendaji wa chama;

c. Kamati Kuu ya chama kumuonya kuacha vitendo vyake hivyo dhidi ya chama;

d. Baada ya jitihada zote hizi kushindikana, Kamati Kuu ilimsihi kujiuzulu kwa hiari yake yeye mwenyewe na hivyo kujiepusha na adha ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye na kusimamishwa na Kamati Kuu.

Kwa vitendo na matukio yote haya, Kamati Kuu ya CHADEMA imejikuta haina njia yoyote ile ya kuepuka mgogoro mkubwa zaidi na usio na maana au msingi zaidi ya kumchukulia hatua za kinidhamu Mh. Chacha Zakayo Wangwe.

Asanteni sana

-----------------------------------------------
Freeman A. Mbowe
MWENYEKITI

Hapa nanusa-nusa kaugomvi/msuguano ukiwa kati ya Mbowe na Wangwe tu, hao wengine naona wakaingizwa kwa ubavu wa mwenyekiti.

Hizi sababu, naziona zote ni za kijinga kabisaa. Sio sababu zakushindikana kutatuliwa mpaka kumfukuza mtu aliye nguzo ya chama. Suala hapa inaelekea lilikuwa tumfukuze, halafu sababu zikatafutwa. Labda watatueleza vitendo vipi alivirudia-rudia mpaka wakamchoka.

Haya huu ni upande wa Mbowe, ngoja tumsikie Chacha naye anasemaje.
 
Back
Top Bottom