CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

Mi sisemi hivyo lakini najua muda si mrefu kuna watu wakiingia humu watasema ni kwa kuwa tu si mchaga!

KKN, watu wakitaka kusema watasema, lakini kuna wengi ndani ya CHADEMA ambao si wachaga.
 
Chacha asingeondoka, CHADEMA ingeondoka. Huyu ni mtu ambaye yuko tayari kufanya kitu chochote anachoamini kuwa kinamjenga kisiasa bila kujali athari za kitu anachofanya. Huyu kwa wanaomfahamu hana tofauti na kina Guninita, Akwilombe, Mrema... Kama kiongozi wa CHADEMA leo hii anaweza kuendesha vikao vya siri na kina Kabouru, viongozi wenzake waendelee kumuamini ? Huko NCCR alikotokea wanamfahamu vizuri zaidi kuliko Mbowe na wenzake wanavyomfahamu.
 
16th March 2008, 09:48 PM

chinga chinga has no status. Banned Join Date: Fri Nov 2006

Mbowe Ampiga Vita Chacha Wangwe

Mwenyekiti Wa Chadema Bwana Mbowe Amekuwa Akipita Kila Tawi La Chadema Na Kumpa Shutuma Kali Makamu Mwenyikiti Wake Kuwa Hana Nia Njema Na Chadema. Ugomvi Wao Ulianza Wakati Wa Uchaguzi Wa Kutafuta Makamu Wa Mwenyekiti Wa Taifa Chadema Ambapo Bwana Mbowe Alikuwa Akimsupport Bwana Alfu.

Lakini Chacha Wangwe Alishinda Kiti Na Sasa Anahujumiwa Na Mbowe.

Mkuu Chinga alisema haya mwezi March, na leo yametokea now tumuamini Chinga kuwa alikuwa na ukweli au tumuamini Mbowe kuwa huu ulikuwa ni uamuzi wa chama yeye hahusiki kabisa na hapa kuna ushahidi wa Chinga uliuotolewa mapema?

Mkuu Kieleweke, ninaomba maoni yako hapa kabla sijatoa hukumu yangu on this ishu!
 
tuwe wakweli,balaa lote hili limesababishwa na jamaa kugombea pesa ya ruzuku(nasikia ni kama sh 60m kwa mwezi).Baada ya kuzidiana ujanja wameona bora timua timua,yetu macho maana hata Yesu aliponzwa na vipande 30 vya dhahabu!
 
Kwani nimesikia tetesi kwamba uchaguzi wa CHADEMA ni mwezi wa nane si wangesubiri mpaka muda huo ili wasimrudishe kwenye hicho kiti au? itakuaje tena kwa muda uliobaki nani atakahimu tena nafasi hii?

Je katika majukumu ya kila ikatokea kwamba umepata ajali na kuumia, utavipa huduma ya kwanza vidonda vyako ama utasubiri mpaka kufika pahala penye hospital?

ni muhimu maamuzi ya msingi na mazito kufanyika pale inapohitajika yafanyike.
 
Mkuu Chinga alisema haya mwezi March, na leo yametokea now tumuamini Chinga kuwa alikuwa na ukweli au tumuamini Mbowe kuwa huu ulikuwa ni uamuzi wa chama yeye hahusiki kabisa na hapa kuna ushahidi wa Chinga uliuotolewa mapema?

Mkuu Kieleweke, ninaomba maoni yako hapa kabla sijatoa hukumu yangu on this ishu!

Kuna mambo ya kuzingatia kabla ya kutoa hukumu , kwanza kabisa nafikiri kama mmesoma tamko la Kamati Kuu utaweza kuona kuwa ni jinsi gani viiongozi wenzake walijitahidi kuhakikisha kuwa wanasaidia na kusaidiana .

Uongozi maana yake ni kusaidiana na kufanya kazi kama timu na sio kufanya kazi kwa kugawanyika.

Kuongoza ni sawa na timu ya mpira ,inapotokea kuwa mchezaji mmojawapo hapendi kuwapasia wengine na anakimbia na mpira peke yake uwanja mzima na hata kutaka kujifunga kwa makusudi kwa faida ya adui yake ,kocha mzuri ni yule anayeweza kumwona na kumpunguza na kuingiza mchezaji mwingine wa akiba.

Slaa,zITTO ET ALL bungen wamejitahidi sana kupasiana mpira ila huyu mwenzetu yeye sioni kwa nini hawapasii na hata akiwapasia basi harudishi pas kwo tena ila anampatia hata adui......

Kuna haja ya kutafakari kwa kina maamuzi ya Kamati Kuu na kuangalia kama waliweza kufuata njia zote ama walifanya kwa pupa .ila hukumu ni mpaka uwe na taarifa sahihi.
 
Je katika majukumu ya kila ikatokea kwamba umepata ajali na kuumia, utavipa huduma ya kwanza vidonda vyako ama utasubiri mpaka kufika pahala penye hospital?

ni muhimu maamuzi ya msingi na mazito kufanyika pale inapohitajika yafanyike.

Huu ni ujumbe mahususi sana .
 
Mkuu Kieleweke,

Sina uhakika kama jibu lako linajibu swali la alert iliyotolewa na Chinga, toka mwezi wa March on ishu hii ambayo imekuja kutokea kama alivyotabiri mapema,

Lakini anyway, mimi ninawa-support wale wanaotaka kutuletea mabadilko kwa taifa letu, bila ya kujali sauti hizo zinatokea wapi, kama ni CCM au Chadema au upinzani in general, tunachotaka ni mabadiliko ya the way we do aour things as a nation, sina clear record ya Wangwe na hili, mambo ya ndani ya Chadema siyapi umuhimu sana kwa wakati huu.

Ingawa ushauri wangu kwako ni kwamba, waachie wengine wafanya hii kazi ya spin unayoifanya, kwa sababu kitendo cha wewe kuivalia njuga inaweza kuamsha hisia kuwa una something more kuhusu hii ishu, katika siasa huwa tunamuachia katibu mkuu ndiye hasa kazi yake hii, ninaweza ku-dig more lakini kwa faida ya nani huwa siamini siasa za kuwapiga vita upinzani ambao kwa kweli wanatusadia sana taifa na viongozi wahuni.

Ahsante Mkuu!
 
Mtanzania,
Wangwe ni mbunge wa Tarime. Sijasikia popote kuwa amevuliwa ubunge wake. Wangwe alichaguliwa makamu mwenyekiti wa CHADEMA na kikao hicho hicho ambacho kimeamua kumsimamisha wadhifa huo. Wangwe hajavuliwa uanachama wa CHADEMA. Sasa ujinga unaouzungumzia ni upi?
 
hakuna kitu kibaya kuliko kuchagua aliekuwa mvuta bangi na mwanachama wa wapuki kuwa ndio kiongozi wa chama,

muhuni muhuni tu


na la kuvunda halina ubani

msitafute kajamba nani nyinyi wenyewe hamna ngoma mmepwerewa pwere
 
Kuna mambo ya kuzingatia kabla ya kutoa hukumu , kwanza kabisa nafikiri kama mmesoma tamko la Kamati Kuu utaweza kuona kuwa ni jinsi gani viiongozi wenzake walijitahidi kuhakikisha kuwa wanasaidia na kusaidiana .

Uongozi maana yake ni kusaidiana na kufanya kazi kama timu na sio kufanya kazi kwa kugawanyika.

Kuongoza ni sawa na timu ya mpira ,inapotokea kuwa mchezaji mmojawapo hapendi kuwapasia wengine na anakimbia na mpira peke yake uwanja mzima na hata kutaka kujifunga kwa makusudi kwa faida ya adui yake ,kocha mzuri ni yule anayeweza kumwona na kumpunguza na kuingiza mchezaji mwingine wa akiba.

Slaa,zITTO ET ALL bungen wamejitahidi sana kupasiana mpira ila huyu mwenzetu yeye sioni kwa nini hawapasii na hata akiwapasia basi harudishi pas kwo tena ila anampatia hata adui......

Kuna haja ya kutafakari kwa kina maamuzi ya Kamati Kuu na kuangalia kama waliweza kufuata njia zote ama walifanya kwa pupa .ila hukumu ni mpaka uwe na taarifa sahihi.
hiyo taarifa ya kamati kuu iko wapi?au mwenzetu ni mjumbe?
 
MK,

Website yenu kule haifanyi kazi, rekebisheni maana uki click kwenye kamati kuu, hakuna kitu. Tunataka kuwajua hao walioamua kumsimamisha Wangwe.

Wanaanchi walikuwa wanaanza kuwa na imani na hawa CHADEMA sasa nao wanaanza kuchemsha, kweli Waafrika ndivyo tulivyo.
Bado nina imani na CHADEMA.
Sijaona chama makini kama hiki. Hata CCM hamna kitu.
Si unajua shida zenu ni nyingi? Kiongozi akivurunda mnampokea kwa ushujaa eti kwa sababu alichaguliwa na wengi. Upuuzi huo.
Kiongozi akivurunda nje. Na hii ni kwa sababu katiba ambayo wamejiwekea na wananchi hao hao waliomchagua wakaipitisha inasema hivyo.
Maana yake ni kwamba hao waliomchagua ni hao hao walioweka utaratibu kwamba kama uteuzi wake utaonekana haufai basi kamati kuu imuondoe. Sasa wewe MTANZANIA shida yako iko wapi? acha kuingilia mambo yasiyokuhusu. Hiyo nikuchonganisha tu. Na hilo halisaidii maana bado tunaukubali uongozi wa Chadema kuwa ni makini.
 
Waungwana,

Mimi kwa kweli nadhani CHADEMA wamefanya uamuzi wa busara, provided wametumia katiba yao..

Siku zote maneno ya Huyu Chacha Wangwe ni Controversial ... mimi simtofautishi Chacha Wangwe na Makamba ni viongozi wa namna moja!

Ningeshauri waandishi wa Habari waishie hapo!!! kwa moyo wa kujenga Taifa...

Lau waandishi wa habari wakapaza sauti na ku-kibomoa chama... CHADEMA watakuwa hawajawatendea haki Watanzania...

Naomba kuwaachia wengine jamvi!!!
 
Mkuu Kieleweke,

Sina uhakika kama jibu lako linajibu swali la alert iliyotolewa na Chinga, toka mwezi wa March on ishu hii ambayo imekuja kutokea kama alivyotabiri mapema,

Lakini anyway, mimi ninawa-support wale wanaotaka kutuletea mabadilko kwa taifa letu, bila ya kujali sauti hizo zinatokea wapi, kama ni CCM au Chadema au upinzani in general, tunachotaka ni mabadiliko ya the way we do aour things as a nation, sina clear record ya Wangwe na hili, mambo ya ndani ya Chadema siyapi umuhimu sana kwa wakati huu.

Ingawa ushauri wangu kwako ni kwamba, waachie wengine wafanya hii kazi ya spin unayoifanya, kwa sababu kitendo cha wewe kuivalia njuga inaweza kuamsha hisia kuwa una something more kuhusu hii ishu, katika siasa huwa tunamuachia katibu mkuu ndiye hasa kazi yake hii, ninaweza ku-dig more lakini kwa faida ya nani huwa siamini siasa za kuwapiga vita upinzani ambao kwa kweli wanatusadia sana taifa na viongozi wahuni.

Ahsante Mkuu!
I beg to differ,kama ni ku dig ndugu yangu viongozi wa sasa na potential leaders wa kesho wote lazima ku wa dig.what is a point kuacha ku wadig sasa kisha baadae wakiukwaa uongozi ndo tuanze kulalama? viongozi wa CHADEMA au chama kingine kama wanafanya madudu waanikwe tu,hii ni kwa faida ya wote leo na kesho.
 
Kwanza niweke rekodi sahihi mimi sio Mbowe.

Pili huyu aliteuliwa/kuchaguliwa na Baraza Kuu, na huyu kama akiona ameonewa katiba inampa fursa ya kukata rufaa kwenye ngazi ya baraza kuu sasa mshauri akate rufaa kama unaona kuwa kaonewa ama hakutendewa haki na anaweza kukata rufaa mpaka mkutano mkuu wa chama ..au hata kwenda kutafuta haki yake mahakamani.
MK unajua shida ya hawa wengine wamezoea uongozi usiofuata katiba sasa hata ukijaribu kumwambia hataelewa kitu. Mwache huyu!😱
 
Mkuu Chinga alisema haya mwezi March, na leo yametokea now tumuamini Chinga kuwa alikuwa na ukweli ...? !

Sidhani.

Chinga alikuwa na character issues zilizo vuka mipaka, kiasi cha kufanya afungiwe hapa. Kwangu hana credibility, sio Mkuu. Shutuma zake kwa wengine sidhani kama inabidi ziheshimiwe.
 
...ukisoma hoja za huku,

lawama kwa kamati kuu CHADEMA kwa kumuajibisha Chacha Wangwe!

...ukisoma za kule,

lawama kwa kamati kuu CCM kutowawajibisha Lowassa na Chenge!

Siasa za Tanzania, inasikitisha, lakini bora hivi mtizamaji tu!
 
Hivi vyama vyengine vitachezewa sana na CCM na kusambaratishwa ,niliwahi kusema na kuandika kuwa kiboko ya CCM ni CUF wenyewe hata wakiandika katika magazeti yao wanakiita Chama hasimu ,maana CCM wamegonga ukuta na imekuwa bahati kwamba hata WaTanzania walio wengi wanalifahamu suala la wanangangari , watu wa jino kwa jino active volcano na nyie subirini tu muone CUF itakavyoanza kuiwasha moto CCM na serikali yake ni Chama ambacho kimeishika na kuidhibiti amani ya Tanzania sio mchezo ni chama ambacho kikiamua na kutangaza sasa kazi basi mjue CCM na jopo la mafisadi wake watatafuta pa kujificha ,yaani CUF wamekamata funguo za amani ya Nchi hii na CCM na serikali yao wanalifahamu jambo hilo ,ila hawa wengine bado wapo katika matatizo ni vyama ambavyo huenda kuna mamluki wa CCM ndani yake wanahitaji kujichunguza kwanza ,halafu nani aliekuwa hajui kama CUF ni chama kikuu cha Upinzani Tanzania ,hapo kuna siri kubwa kuitwa hivyo japo mkuno huo CCM wanajaribu kwa hali na mali kuupindisha na kutaka kionekane ni chama ambacho kipo kule Zanzibar tu lakini wamechelewa as Active volcano inatokota ndani kwa ndani.
 
Kukmbuka maamuzi yaliyowahi kuchukuliwa na hao CCM katika kuhakikisha kuwa panakuwepo na uongozi wa pamoja ,kumbuka yaliyomkuta Seif ZNZ,JUMBE,ABDULWAKILI ET ALL.

Hapa ni suala la kuangalia principals na sio kufanya mambo kinyume na utaratibu halafu aachwe mtu .

Hakuna sababu ya kumuacha yeyote kwani kufanya hivyo ni kuharibu chama ,kama huyu kashindwa kujitetea mbele ya kamati ya wazee ambayo inaundwa na wazee hawa;

1.Mzee Mtei.
2,Mzee Bob Makani.
3.Prof.Baregu
4.Balozi Ngaiza
5.mzee Ndesamburo.

na hata kwenye kamati kuu alishindwa kutetewa na wajumbe kwani hao hao ndio walimuweka muda mchache uliopita sasa ni lazima mjue kuwa ni lazima wachache waumie ili kuelekea kwenye ukombozi........

na kama hao uliowataja ndio waliompigia kura ya kuwa na imani naye?

i chose to dis agree with you. thimk critically, it really pains.
 
Back
Top Bottom