CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

Wale wote wenye akili nyingi na kufikiri kuwa baada ya kumuondoa madarakani Chacha, then malalamiko yake yaliyoungwa mkono na wajumbe wa mkutano mkuu CHADEMA yataisha naomba wanyooshe mikono...........



 
Baada ya kufuatilia historia ya mgogoro huu, matatizo (kama ni matatizo) yaliyosababisha Chacha atolewe kwenye uongozi ni yaleyale aliyokuwa nayo kabla ya kuchaguliwa kuwa kaimu makamu mwenyekiti, na ukifuatilia vizuri ndio sababu hizohizo ndizo zilimfanya achaguliwe, kwa hiyo kama aliyemtoa Chacha kwenye nafasi aliyokuwa akishikilia siyo aliye muweka ni dhahiri kuwa uamuzi huo unapingana na walio wengi (waliomchagua Chacha). Ni sababu zipi zilimfanya Dr. Slaa na Zitto watake kujiuzulu???? Hoja za Chacha zichambuliwe na zifanyiwe analysis objectively na independent analyst anayekifahamu CHADEMA bila biasness yoyote. Kwangu mie (mzalendo nisiye na chama cha siasa) nayaona madai ya Chacha yana uzito zaidi (relatively) na sababu zilizotolewa za kumfukuza. Ushauri kwa CHADEMA ijipange upya na isizichukulie juu juu hoja za Chacha, otherwise i am sorry to say bila kufanya hivyo mtajifanya yameisha leo ila kesho yataibuka tena na yatawamaliza.
 
Mtanzania,
Wangwe ni mbunge wa Tarime. Sijasikia popote kuwa amevuliwa ubunge wake. Wangwe alichaguliwa makamu mwenyekiti wa CHADEMA na kikao hicho hicho ambacho kimeamua kumsimamisha wadhifa huo. Wangwe hajavuliwa uanachama wa CHADEMA. Sasa ujinga unaouzungumzia ni upi?

Mkuu Jasusi,

Hakuna niliposema Wangwe amevuliwa ubunge. Nilichoandika ambacho Pundit ameamua kukitafsiri tofauti ni kwamba ni kwamba "alichaguliwa na wananchi kwenye mkutano mkuu wa CHADEMA". Kitu pekee ninachoweza kubadilisha hapo ni kwamba Alichaguliwa na wananchi kwenye baraza kuu la CHADEMA.

Baraza kuu la CHADEMA sio kamati kuu. Ukisoma maandiko yangu ya leo, nimemwuliza MK, anifafanulie vinginevyo aache kutudanganya hapa kwamba kikao kilichomwondoa ndio hicho hicho kilichomchagua. Akaamua kujibu kiujanja. Wengine tuko kwenye siasa kwa muda mrefu japo ni kupitia keyboards. Mtu akisema hivyo tunajua ni maana ya kwamba alichoandika mwanzoni sio sahihi.

Naona na wewe unarudia kitu hicho hicho. Wangwe hakuchaguliwa na kamati kuu ya CHADEMA, alichaguliwa na baraza kuu tena baada ya kamati kuu kujaribu kuzuia jina lake na hata kutishia kuahirisha uchaguzi.

Kwenye baraza kuu Wangwe alikuwa ni chaguo la wanachama wa kawaida wa hicho chama toka mikoani, wakati yule chaguo la vigogo alibwagwa chini.
 
Baada ya kufuatilia historia ya mgogoro huu, matatizo (kama ni matatizo) yaliyosababisha Chacha atolewe kwenye uongozi ni yaleyale aliyokuwa nayo kabla ya kuchaguliwa kuwa kaimu makamu mwenyekiti, na ukifuatilia vizuri ndio sababu hizohizo ndizo zilimfanya achaguliwe, kwa hiyo kama aliyemtoa Chacha kwenye nafasi aliyokuwa akishikilia siyo aliye muweka ni dhahiri kuwa uamuzi huo unapingana na walio wengi (waliomchagua Chacha). Ni sababu zipi zilimfanya Dr. Slaa na Zitto watake kujiuzulu???? Hoja za Chacha zichambuliwe na zifanyiwe analysis objectively na independent analyst anayekifahamu CHADEMA bila biasness yoyote. Kwangu mie (mzalendo nisiye na chama cha siasa) nayaona madai ya Chacha yana uzito zaidi (relatively) na sababu zilizotolewa za kumfukuza. Ushauri kwa CHADEMA ijipange upya na isizichukulie juu juu hoja za Chacha, otherwise i am sorry to say bila kufanya hivyo mtajifanya yameisha leo ila kesho yataibuka tena na yatawamaliza.



Well said Kinto.

Zaidi ya hayo, kulingana na Habari Leo, ni kuwa wanachama wa CHADEMA walimchagua Wangwe ili akakisafishe chama. Inaelekea kamati kuu haikuafikiana na hao waliomchagua.
 
Zitto, Kitila, Mnyika, Mbowe na allegedly Mwanakijiji, mnajulikana kuwa viongozi wa juu wa CHADEMA, kwa nini hamchangii mada na kuiweka sawa?

Zitto imesemekana ulitaka kuachia ngazi, je ni kweli? Kama ndivyo ni sababu zipi zilikufikisha bapo? Tunaomba michango yenu wakuu ASAP.
 
Huyu bwana kwa kweli alikuwa anakera sana wakati mwingine! Yaani si mtu makini kama tulivyowazoea viongozi wengine wa CHADEMA. Najua yafuata maneno mengi na labda watu wa tarime watareact sana, lakini lazima tukubali ili kuwa na upinzani makini lazima na watu wake wawe makini sana! Mimi naamini wabunge wa upinzani (individually) ni competent zaidi ya wale wa CCM kwa sababu wanafanya kazi na kushinda katika mazingira magumu sana. Pia hata ukinagalia wanavyojenga hoja, za wapinzani nyingi utakuta zimejaa akili. CCM imejaza watu weak sana! Upinzani pia labda kuna problem kidogo kwa baadhi ya wabunge wanaotokea upande wa Zanzibar ukiachia akina Hamad Rashid na wengine wachache

So on individual basis, they are competent, what about their parties? Do we need to push for independent Wagombea?


Maana kauli yako ni kweli kuwa sasa hivi Wabunge ni mvuto binafsi na si muelekeo au kupitia nguzo za vyama (this includes CCM)!
 
mi nakuwa nashindwa kuelewa kama hizi ni Spinning na ushabiki wa hapa JF, maana watu wanasubiri kitu kiandikwe kisha wanatafuta mabaya ndani yake...ilimradi tu la kuongea liwepo ama Chama Mbadala kinapoteza dira...

na tumesiKia upande mmoja wa Chama na kwa jinsi nnavyomfahamu Chacha sidhani kama atakuwa amekaa kimya, kwa nini asije nae kisha tukasikia upande wake kisha tukajadili.

husiana na kachaguliwa na nani na kusimamishwa na nani nadhani tunahitaji kupitia katiba ya chama.

Concern inakuja tu kwa vile nilianza kukiamini chadema kuwa kiko stable. Mambo kama haya ndio yaliyoiua nccr, isingependeza yatokee chadema.

Kama chacha kumsimamisha genuinely kwa manufaa ya kukiimarisha chama chenu mtapata hongera. Kama kusimamishwa kwa chacha kunakuwa chanzo cha kusambaratika kwa chadema basi pole kwa watanzania.

It will come o a conclusion kwamba tanzania hakuna upinzani na hata ukiwepo bado umegubikwa na gubu na sio wakati mufaka kwa wananchi kuwapa nchi. Upinzani wa kweli utakuja pale sisiemu itakapogawanyika.
 
"Mjumbe mwingine wa kikao cha Kamati Kuu ambaye jana alizungumza na Tanzania Daima Jumapili, alisema kimsingi uamuzi wa kusimamishwa kwa Wangwe unatokana na pendekezo la vikao hivyo vya wazee, ambako awali aliitwa na kuonywa na yeye akaomba radhi kwa makosa yaliyokuwa yakimkabili.

Mkisikia kuua Demokrasia ndio huko. Hiki kikao cha "Wazee" kina nafasi gani kikatiba kufanya maamuzi au kutoa shinikizo ambalo linafanya Kamati Kuu au Halmashauri kuu ya Chadema imsimamishe Wangwe uongozi? Doesn't this sound DICTATORIAL like CCM?

Sasa Upinzani ujue wazi kuwa wameshapoteza jimbo! Damn, damn, damn, always pulling reckless stunts at wrong time!

Sasa hivi Wananchi badala ya ku-focus kwenye Bajeti na Uozo wa CCM, attention iko Chadema, kesi za Ufisadi zitapeta, kikao cha Bunge kuahirishwa huku Chadema wakigombana na CCM kuwadhalilisha!
 
Zitto, Kitila, Mnyika, Mbowe na allegedly Mwanakijiji, mnajulikana kuwa viongozi wa juu wa CHADEMA, kwa nini hamchangii mada na kuiweka sawa?

Zitto imesemekana ulitaka kuachia ngazi, je ni kweli? Kama ndivyo ni sababu zipi zilikufikisha bapo? Tunaomba michango yenu wakuu ASAP.

wanadiscuss in private, labda na wao wameshtushwa na hili!
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
NA
WANANCHI WA TANZANIA

KUSIMAMISHWA KWA MHESHIMIWA CHACHA ZAKAYO WANGWE (MB.) KUWA KAIMU MAKAMU MWENYEKITI WA TAIFA (BARA) WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO

Ndugu wanahabari na wananchi wenzangu,

Tarehe 28 Juni 2008 Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo katika kikao chake cha kawaida kilimsimamisha Mheshimiwa Chacha Zakayo Wangwe kama Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Taifa (Bara) wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kumpigia kura ya siri ya kutokuwa na imani naye. Huu ni uamuzi mzito na ambao haujawahi kufanywa katika historia ya miaka 16 ya CHADEMA. Tunapenda kuwafahamisha wananchi wetu kwamba uamuzi huu mzito ulichukuliwa baada ya mjadala na tafakuri ya muda mrefu. Kamati Kuu ya chama chetu ilifikia hatua hiyo dhidi ya baada ya kuridhika na ushahidi kwamba Mh. Chacha Wangwe amekiuka maadili ya uongozi na hivyo kupoteza sifa mahsusi za kuendelea kuwa kiongozi wa kitaifa wa CHADEMA kwa sababu zifuatazo:

-----------------------------------------------
Freeman A. Mbowe
MWENYEKITI

By reading this, ina maana Chacha Zakayo Wangwe alikuwa Kaimu, actinge vice chairman and not Vice Chairman. Sasa alikaimu kwa misingi ipi na kutokana na mapungufu gani? kwa nini hakuwekwa kuwa makamu kamili?
 
Ndugu wananchi na wanahabari,

Kamati Kuu ya CHADEMA haikufikia uamuzi huu mzito kwa haraka na/au bila kufikiria kwa kina madhara yake kwa chama na kwa taifa letu. Kamati Kuu imefikia uamuzi huu baada ya jitihada mbali mbali za kumsaidia Mh. Chacha Zakayo Wangwe kujisahihisha na kujirudi kushindikana kabisa. Jitihada hizi mbali mbali ni kama vile:

a. Vikao mbali mbali na vya muda kati yake mwenyewe, Mwenyekiti Taifa na Katibu Mkuu kujadili tofauti na/au migongano kati yao na/au ndani ya chama;

b. Kusuluhishwa na Kamati ya Wazee wa Chama ambapo Mh. Wangwe alitakiwa kuandika maandishi kwamba ataacha vitendo vyake dhidi ya chama, viongozi wa kitaifa na watendaji wa chama;

c. Kamati Kuu ya chama kumuonya kuacha vitendo vyake hivyo dhidi ya chama;

d. Baada ya jitihada zote hizi kushindikana, Kamati Kuu ilimsihi kujiuzulu kwa hiari yake yeye mwenyewe na hivyo kujiepusha na adha ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye na kusimamishwa na Kamati Kuu.

Kwa vitendo na matukio yote haya, Kamati Kuu ya CHADEMA imejikuta haina njia yoyote ile ya kuepuka mgogoro mkubwa zaidi na usio na maana au msingi zaidi ya kumchukulia hatua za kinidhamu Mh. Chacha Zakayo Wangwe. Kwa matendo haya ni wazi Mh. Chacha Zakayo Wangwe amepoteza sifa mahsusi za kuendelea kushikilia dhamana kubwa ya uongozi ambayo vikao halali vya chama vilimpatia. Kamati Kuu imelazimika kutumia mamlaka yake ya kikatiba ya kumsimamisha uongozi wa kitaifa Mh. Wangwe kwa kumpigia kura ya siri ya kutokuwa na imani naye. Azimio la kumsimamisha Mh. Wangwe kuwa Kaimu Makamu Mwenyekiti Taifa (Bara) liliungwa mkono na wajumbe ishirini na nne kati ya thelathini na moja waliohudhuria na kushiriki katika kikao cha Kamati Kuu. Idadi hii ni zaidi ya theluthi mbili ya kura za wajumbe wa Kamati Kuu inayohitajika kikatiba ili kumsimamisha uongozi kiongozi yeyote wa kitaifa kama alivyokuwa Mh. Chacha Zakayo Wangwe. Kamati Kuu imechukua hatua hii ngumu na nzito ili kukiokoa chama kutokana na migogoro ambayo imesambaratisha vyama vingine vya siasa hapa nchini.

Asanteni sana

Kama kapoteza sifa ya Uongozi, je ana sifa gani kuendelea kuwa Mwanachama?
 
Mtanzania,
Wangwe ni mbunge wa Tarime. Sijasikia popote kuwa amevuliwa ubunge wake. Wangwe alichaguliwa makamu mwenyekiti wa CHADEMA na kikao hicho hicho ambacho kimeamua kumsimamisha wadhifa huo. Wangwe hajavuliwa uanachama wa CHADEMA. Sasa ujinga unaouzungumzia ni upi?

Jasusi.

sio kweli kuwa watu watano walimsimamisha jana ndio waliompa nafasi ya umakamu wa mwenyekiti Wangwe.wangwe alipigiwa kura na watu zaidi ya 94.sio kikundi cha watu watano tena wenye sauti ni watatu,Ndesamburo,Mtei na Bob Makani hao wawili ni waigizaji tu.
 
Waheshimiwa!!!

Chacha Wangwe ni Mzigo... sikiliza tu hata hoja zake Bungeni... si mpenda fuata taratibu hata kidogo...

Mimi kwa hili niko na CHADEMA...

Jamani muikivuruga CHADEMA tutakuwa tumekwisha!!! nakubaliana nao kwamba hawajafikia kukabidhiwa nchi lakini tunatamani kwamba wapate wabunge angalau 20 to 30% kwenye Uchaguzi ujao...

Sasa kuanza kuwavuruga kwa kweli hamuitendei nchi yetu!
 
Kamati Kuu ya chama chetu ilifikia hatua hiyo dhidi ya baada ya kuridhika na ushahidi kwamba Mh. Chacha Wangwe amekiuka maadili ya uongozi na hivyo kupoteza sifa mahsusi za kuendelea kuwa kiongozi wa kitaifa wa CHADEMA kwa sababu zifuatazo:

1. Amekuwa akijihusisha na/au kushiriki katika vikundi na/au vitendo vya uchonganishi na/au kuzua migogoro ndani ya uongozi wa chama na/au wanachama wake.

Kitendo cha kuandaa, kushiriki na/au kufadhili mikutano ya siri ya watu ambao wamechukuliwa hatua za kinidhamu na vikao halali vya chama na/au ambao wamekihama chama baada ya kupoteza ridhaa ya kuwaongoza wananchi kina tafisiri moja tu ya msingi: Kuendeleza migogoro na/au hujuma dhidi ya chama kwa lengo la kukidhoofisha na kukifanya kishindwe kuendeleza vita kubwa dhidi ya ufisadi uliojikita ndani ya Serikali na CCMambayo imekipatia chama chetu sifa kubwa na uhalali kwa watanzania.
-----------------------------------------------
Freeman A. Mbowe
MWENYEKITI


Hapa nafikiri Mwenyekiti Mbowe amezusha au kudanganya;
  1. Mikutano ya siri - Sijui ilijulikanaje na hasa kuwa ilifadhiliwa na Wangwe
  2. Aliyofanya yanaifanya CHADEMA ishindwe kwenye vita ya EPA - Hii ni spin na uzushi mkubwa unless tufahamishwe wanashindwaje. Otherwise kwa mwelekeo huu anaweza kuzushiwa hata mauaji. Kwa hizi charges tu si uanachama alitakiwa awe amevuliwa? Ingekuwa hiki ni chama tawala labda angezushiwa hata na uhaini.
 
Waheshimiwa!!!

Chacha Wangwe ni Mzigo... sikiliza tu hata hoja zake Bungeni... si mpenda fuata taratibu hata kidogo...

Mimi kwa hili niko na CHADEMA...

Jamani muikivuruga CHADEMA tutakuwa tumekwisha!!! nakubaliana nao kwamba hawajafikia kukabidhiwa nchi lakini tunatamani kwamba wapate wabunge angalau 20 to 30% kwenye Uchaguzi ujao...

Sasa kuanza kuwavuruga kwa kweli hamuitendei nchi yetu!

Mheshimiwa,

Sijaona hapa mtu anajadili uwezo na utendaji kazi wa Wangwe. Nadhani watu wanajadili utaratibu uliotumika kumuondoa, demokrasia na stability ndani ya upinzani, na busara ya kumuondoa katika kipindi hiki. (Kama nakosea nisahihishwe.)

Nadhani mada ni jinsi CHADEMA walivyo utua huo "mzigo" kama ulivyo uita.
 
Bado nina imani na CHADEMA.
Sijaona chama makini kama hiki. Hata CCM hamna kitu.
Si unajua shida zenu ni nyingi? Kiongozi akivurunda mnampokea kwa ushujaa eti kwa sababu alichaguliwa na wengi. Upuuzi huo.
Kiongozi akivurunda nje. Na hii ni kwa sababu katiba ambayo wamejiwekea na wananchi hao hao waliomchagua wakaipitisha inasema hivyo.
Maana yake ni kwamba hao waliomchagua ni hao hao walioweka utaratibu kwamba kama uteuzi wake utaonekana haufai basi kamati kuu imuondoe. Sasa wewe MTANZANIA shida yako iko wapi? acha kuingilia mambo yasiyokuhusu. Hiyo nikuchonganisha tu. Na hilo halisaidii maana bado tunaukubali uongozi wa Chadema kuwa ni makini.

Hivi wewe unavyochukia ufisadi unachonganisha? Mtanzania anachambua mambo kwa uelewa mkubwa sana na kuna faida kwa wanachadema hadi bwana Mbowe.

sasa kila anayekwenda kinyume na Mbowe ni mchonganishi? Wangwe kaweka wazi matatizo ya chadema, nadhani mngemshukuru kwa kuyaweka wazi ili yafanyiwe kazi kuliko kupita pembeni pembeni. sasa hata JF nako mnatukaza kuyajadili kwa uoni wetu,

hapa kuna ushahidi wa pande mbili kuwa Wangwe wamekuwa akishiriki kwenye vikao vya wasio wapenzi wa kweli wa Chdema hilo ni kosa la kufukuzwa kwa mujibu wa Mpaka kielewe.

lakini pia kuna ujumbe kauweka Field Marshal ES kuwa Mbowe nae alikuwa akipita nchi nzima kumpakazia WANGWE toka mwezi wa tatu, sasa ilitakiwa Wangwe nae mumpe nafasi ya kumsikiliza.

kumziba mdomo wake sio kujenga demokrasia ya chama chenu.

kama aliweza kupata kura kwenye mkutano vipi watu watano wamtoe kienyeji?

kama kusimamishwa wasimamishwe wote Mbowe na WANGWE. sio mmoja kumpendelea kwa vile baba mkwe wake(Mtei) ni mwasisi na mwenye chama.

uvundo huu mtauficha kwa muda kama hamtarekebisha yatakuja hayo hayo na kina Zitto nao hawatakuwa na muda mrefu.swali Chadema ni wanademokrasia vipi mnawasimamisha wale wote wenye dukuduku ili chama chao kiende? au ndio udikteta uliopo makao makuu uliyojadiliwa hapa?

Mpaka kieleweke.

Kwa maandishi yako inaonekana ni Mbowe au unatumiwa na Mbowe.

wewe umeleta thread hii lakini huwapi nafasi watu kuchangia kwa kuishupalia kuonesha una maslahi yako. au unatumia mtandao huu kumuua Wangwe, sio busara kumsakama mwanachama wenzio tayari mmemvua umakamu Wenyekiti ambao hamkutaka aupate lakini kwa nguvu zake Mola akaupata na sasa mmeyarudisha maamuzi yenu watu sita (wale watano wa Dodoma na wewe)na kupinga utashi wa wajumbe waliokuja kwenye mkutano kumchagua Wangwe mwezi desemba 2007.

unasema Baregu ni bingwa wa kutatua migogoro kashindwa kumsaidia wangwe, lakini Baregu huyo huyo ndio aliyeivuruga NCCR na akashindwa kusuluhisha huko.

Makani sio bingwa wa Administrative Law ni mwanasheria wa mambo ya Benki ndio maana huwezi kumuona kwenda kumtetea Mahalu au Zombe sio eneo lake, huyu bwana hawezi kwenda kinyume na bosi wake wa BOT bwana Mtei ambaye alikuwa gavana wa benki kuu na yeye akawa msaidizi.

MK hujaweka uzoefu wa Mtei na Ndesamburo ambao walikuwepo kwenye kikao, au unataka tuamini kuwa kikao na maamuzi yalitoka kwa hao watu watatu tu?

Mtanzania.

Endelea kumwaga vitu umetulia sana na tunakuelewa wasio kuelewa wana agenda yao, hawezi mtu kukuziba mdomo wako wamemziba Chacha na sisi wanataka tusiseme?

au ndio maana Mwanakijiji aliwahi kuandika makala na kipindi maalum kumlaani Wagwe wakati wa jeshi letu lilipoenda Ngazija.inawezekana ulikuwa ndio mkakati wa kumsambalatisha Wangwe, nilishangaa kuona Mwanakijiji anamlaani makamu mwenyekiti wa chama chake.

Tunaomba Kitila Mkumbo,Mnyika,Zitto na Mwanakijiji wape kutupa maoni yao ingawa inaonekana wazi kuwa watamtosa Chacha(Msemakweli) ila somo kwenu ni kuwa mwenzenu akinyolewa nyinyi tieni maji vichwa vyenu. lazima mjue kuwa Wangwe ana watu nyuma yake huko Tarime wamemuamini na wameikubali Chadema kupitia kwake.
 
Uzalendo HAKIKA nawaambia ni mgumu!

Nyie watu hamjui story za KIJASUSI?

Hawa Viongozi wa CHADEMA nawapa ushauri huu kabla hawajaendelea na mjadala huu.

Sitaki kutoa mfano sasa hivi.

MBOWE KUSEMA ATAPAMBANA NA EPA...Ni HATUA NZURI YA MWANZO.

Ila kama FMES alivyosema awali...Wote sasa ama baadhi yetu tunajua issue yote.

TAIFA LIKO NJIA PANDA NA HAKIKA NAWAHAKIKISHIENI WAZALENDO KUWA WE WILL BE VICTORIOUS.

Hivyo basi...Kabla hatujasonga mbele...Nitauliza swali ambalo labda linaweza lisiwafurahishe baadhi ya watu!

Ila tunataka tusonge mbele kwani sasa tunajua mitego ilikuwa,ama iko mingi tu.

Je...ILIKUWA NI BAHATI MBAYA KWA WATU WENYE UHUSIANO WA KARIBU NA MKAPA KWENDA KUOA KWENYE FAMILIA YA MBOWE?
 
2. Amekuwa akitoa tuhuma nzito lakini zisizokuwa na msingi dhidi ya viongozi wenzake wa kitaifa na watendaji wa chama pasipo kupitia vikao halali na wala kuzingatia taratibu za chama

Mheshimiwa Chacha Zakayo Wangwe aidha moja kwa moja ama kwa kuwatumia viongozi na/au wanachama walioadhibiwa na vikao halali vya chama amekuwa akiwatuhumu viongozi na watendaji wa chama kwa mambo ya uzushi na yasiyokuwa na ukweli na/au msingi wowote. Yeye mwenyewe amekuwa akisambaza uzushi kwamba kuna ufujaji na/au matumizi mabaya ya fedha za chama ambao amekuwa akidai unafanywa na viongozi wa kitaifa hususan Mwenyekiti wa chama Taifa na Katibu Mkuu na/au watendaji wa Makao Makuu ya chama. Aidha Mh. Chacha Wangwe amekuwa akisambaza uzushi kwamba viongozi wenzake wa kitaifa na watendaji Makao Makuu wamekuwa wakikataa ruzuku ya chama kupelekwa mikoani na wilayani nabadala yake wamekuwa wakiitumia ruzuku hiyo kwa shughuli za Makao Makuu na/au kwa manufaa yao binafsi. Uzushi huu umetolewa licha ya Kamati Kuu ya chama ambayo Mh. Chacha Wangwe alikuwa ni mjumbe kupokea na kupitisha taarifa zote zinazohusiana na mapato na matumizi ya fedha za chama na licha ya chama kutoa ruzuku ya vifaa na/au fedha taslimu tangu mwaka 2006 kabla hata ya yeye kuchaguliwa kuwa Kaimu Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA tarehe 17 Desemba mwaka 2007. Aidha Mh. Chacha Wangwe amesambaza uzushi huu licha ya kufahamu fika kwamba si yeye mwenyewe, wala si Makamu Mwenyekiti Taifa (Visiwani), wala si Mwenyekiti Taifa wala si Katibu Mkuu wala manaibu Makatibu Wakuu wote wa chama ambao wamepokea hata senti moja ya fedha za chama kama posho au mishahara. Tuhuma hizi za uzushi na uwongo juu ya kuwepo ufujaji na/au matumizi mabaya ya fedha za chama zina lengo moja tu: Kuwapaka matope viongozo wa chama wa kitaifa na watendaji wa ngazi za juu wa chama kwa lengo la kudhoofisha jitihada za chama kujijenga kwa wananchi na kuendeleza vita dhidi ya ufisadi ambayo imekipatia chama na viongozi wake umaarufu miongoni mwa wananchi wa Tanzania.
-----------------------------------------------
Freeman A. Mbowe
MWENYEKITI


Kwenye uchaguzi mkuu 2005, Mbowe alitumia zaidi ya 60% ya pesa ya chama. Ina maana wagombea ubunge walishindwa kugombea ipaswavyo.

Ukweli ni kuwa mikoani hawapati pesa ya kutosha bila ya hivyo wasingempigia Wangwe kura.
 
Nitarudi kwenye mjadala huu kama nikipewa jibu.
Na nisipopewa jibu hilo.
Basi mjadala huu utaelekea kule ambako hata FMES hakutaka twende.
TUSIPOTEZE MUDA!
Zitto is due DODOMA tommorow!
Wamalize mambo MARA MOJA THEN MKAWATUMIKIE WANANCHI HUKO BUNGENI.
NAWASIKILIZIA.
 
Back
Top Bottom