CHADEMA Mara wamkana kiongozi aliyehamasisha maridhiano

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252
Your browser is not able to display this video.

Chama cha Demokrasia Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mara kimemkataa Katibu wa mkoa huo Donald Felix Mwembe aliyesema kuwa chama hicho kikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wake John Heche kinatakiwa kuzungumza na watawala ili kufikiwa kwa muafaka wa kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu.

Soma pia: Donald Felix Mwembe: Lissu amekaa sana gerezani inauma, Heche akubali maridhiano atoke

Akizungumza Septemba 1, 2026 kwenye kikao Cha Baraza la mashauriano la CHADEMA Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mara Chacha Heche amesema yeye kama msemaji wa chama mkoa anasimamia msimamo wa chama hicho kuwa hakuna maridhiano.

“Hatutambui, hatupokei, hatuna mpango wa kuridhiana na Chama cha Mapinduzi kwenye hatua yoyote," amesema Chacha.

Hata hivyo amesisitiza wanachama wa chama hicho kutoyumbishwa na baadhi ya wanachama ambao wamekuwa wakitumika huku akimtaka Katibu Mwembe kujitafakari juu ya kauli alizotoa kwenye vyombo vya habari.

Ikumbukwe siku mbili zilizopita Mwembe alieleza kuwa viongozi wa chama hicho wakae na kuzungumza na serikali ili kutoka kwenye mtanziko na kupatikana kwa suluhu itakayowezesha Lissu kuweza kuachiwa.

Chanzo: Jambo TV
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…