Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
wamefanya vizuri sana kujisalimisha kwa Mungu na kwa kanisa,Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mara kimewasilisha ripoti maalum kwa Kanisa Katoliki, ikielezea matukio ya watu waliouawa au kupotea katika mkoa huo. Sambamba na hilo, chama hicho kimetumia nafasi hiyo kueleza msimamo wake wa No Reform No Election, ukimaanisha kwamba kitazuia uchaguzi wowote iwapo mabadiliko ya sheria na mfumo wa uchaguzi hayatatekelezwa.
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mara, Chacha Heche, amesema wamechukua hatua hiyo kwa sababu wamedanganywa mara nyingi kuhusu maridhiano ya kisiasa, huku wakihisi kuwa mfumo wa uchaguzi bado hauna usawa. Heche amewataka viongozi wa dini kuunga mkono juhudi za kupigania haki za wananchi, hususan katika kuimarisha demokrasia.
Diwani wa Kata ya Mbogi, Jimbo la Tarime Vijijini, Steven Nyahiri, ameainisha changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Novemba 2024, akisema uchaguzi huo ulikumbwa na mapungufu makubwa. Ameeleza kuwa viongozi wa dini wana nafasi muhimu katika kupaza sauti na kusaidia kuleta mabadiliko ya kweli ya kisiasa na kijamii.
Kwa upande wake, Veronica Sando, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) Mkoa wa Mara, amesema kuwa licha ya mkoa huo kuwa na rasilimali nyingi kama mbuga za wanyama, badala ya kuwa baraka kwa wananchi, rasilimali hizo zimekuwa chanzo cha madhila, huku baadhi ya watu wakijeruhiwa au hata kuuawa.
Katibu wa Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma, Cleophas Sabure, amethibitisha kupokea ripoti hiyo na kuahidi kuiwasilisha kwa Askofu wa Jimbo. Amesema baada ya Askofu kupitia ripoti hiyo, CHADEMA itaitwa kwa majadiliano zaidi ili kufanyia kazi malalamiko yao.
Ww ni padri unakuja na conclusion za kusadikika?wamefanya vizuri sana kujisalimisha kwa Mungu na kwa kanisa,
bilashaka yoyote wataambiwa kutokutii mamlaka za dunia zilizotoka kwa Mungu ni dhambi,
na kwahiyo no reform no elections ni sin, null and void mbele ya kanisa na mbele za Mungu. 🐒
maandiko yako wazi gentleman,Ww ni padri unakuja na conclusion za kusadikika?
Wataambiwa na nani? As nimekuuliza ww ni padri?maandiko yako wazi gentleman,
wataambiwa waache kiburi kwa mamlaka za wanadamu zilizotoka kwa Mungu,
fuatilia vizuri sio muujiza ni Ukweli na uhalisia mtupu gentleman 🐒
Ccm nao wapeleke ripoti yao ila najaribu kuwaza hapa kwanini ni katoliki na sio, K.K.T, AGT, AICT, EFATHA, BAKWATA, TGA, FPCT N.K kulikoni huko catholic?
kwani wao wameenda kujisalimisha wapi, kwanani?Wataambiwa na nani? As nimekuuliza ww ni padri?
maandiko yako wazi gentleman,
wataambiwa waache kiburi kwa mamlaka za wanadamu zilizotoka kwa Mungu,
fuatilia vizuri sio muujiza ni Ukweli na uhalisia mtupu gentleman 🐒
Kanisa Moja,Takatifu na la Mitume.Ccm nao wapeleke ripoti yao ila najaribu kuwaza hapa kwanini ni katoliki na sio, K.K.T, AGT, AICT, EFATHA, BAKWATA, TGA, FPCT N.K kulikoni huko catholic?
Safi sana
Huu ndo mwendo
Chama kiwasilishe majina yote ya waliotekwa kwa TEC na Viongozi wengine wa dini
Siku viongozi wa dini wakisema tu watashiriki na kuunga mkono NO Reforms No Election na watashiriki maandamo hakika huo ndo urakuwa mwisho wa CCM na udhalimu wao.
we kijana,Unatakiwa kumtii Mungu kuliko kitu chochote. Mamlaka inayoteka na kuua watu, ni mamlaka ya kutoka kwa shetani. Mwanadamu hastahili kuwa na ushirika na shetani.
CCM hii ya sasa ya kuteka na kuua wanaomkosoa Rais, ni ya shetani. Watu wa Mungu wanatakiwa kujitenga nayo.
Kama wayahudi wangemtii Pharao, wasingeondoka Misri
Chadema ni wabaguzi na wadini!Ccm nao wapeleke ripoti yao ila najaribu kuwaza hapa kwanini ni katoliki na sio, K.K.T, AGT, AICT, EFATHA, BAKWATA, TGA, FPCT N.K kulikoni huko catholic?
Kanisa itawasaidia nn hao nyumbu, bila kuwa mwehu huwezi kuwa mwanachama wa chadema. Nani wa kuzuia uchaguzi, wataharisha hizo bangiChama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mara kimewasilisha ripoti maalum kwa Kanisa Katoliki, ikielezea matukio ya watu waliouawa au kupotea katika mkoa huo. Sambamba na hilo, chama hicho kimetumia nafasi hiyo kueleza msimamo wake wa No Reform No Election, ukimaanisha kwamba kitazuia uchaguzi wowote iwapo mabadiliko ya sheria na mfumo wa uchaguzi hayatatekelezwa.
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mara, Chacha Heche, amesema wamechukua hatua hiyo kwa sababu wamedanganywa mara nyingi kuhusu maridhiano ya kisiasa, huku wakihisi kuwa mfumo wa uchaguzi bado hauna usawa. Heche amewataka viongozi wa dini kuunga mkono juhudi za kupigania haki za wananchi, hususan katika kuimarisha demokrasia.
Diwani wa Kata ya Mbogi, Jimbo la Tarime Vijijini, Steven Nyahiri, ameainisha changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Novemba 2024, akisema uchaguzi huo ulikumbwa na mapungufu makubwa. Ameeleza kuwa viongozi wa dini wana nafasi muhimu katika kupaza sauti na kusaidia kuleta mabadiliko ya kweli ya kisiasa na kijamii.
Kwa upande wake, Veronica Sando, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) Mkoa wa Mara, amesema kuwa licha ya mkoa huo kuwa na rasilimali nyingi kama mbuga za wanyama, badala ya kuwa baraka kwa wananchi, rasilimali hizo zimekuwa chanzo cha madhila, huku baadhi ya watu wakijeruhiwa au hata kuuawa.
Katibu wa Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma, Cleophas Sabure, amethibitisha kupokea ripoti hiyo na kuahidi kuiwasilisha kwa Askofu wa Jimbo. Amesema baada ya Askofu kupitia ripoti hiyo, CHADEMA itaitwa kwa majadiliano zaidi ili kufanyia kazi malalamiko yao.
Kunayo mengi na siri lukuki kuhusu RC na BakwataCcm nao wapeleke ripoti yao ila najaribu kuwaza hapa kwanini ni katoliki na sio, K.K.T, AGT, AICT, EFATHA, BAKWATA, TGA, FPCT N.K kulikoni huko catholic?