Pre GE2025 CHADEMA Mbeya Mjini, Tafuteni Mgombea Mwingine

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
View attachment 3066360
Niko Mbeya Mjini kwa siku tatu hivi na nimeona upepo wa siasa za hapa. Siko upande wa CCM wala CDM. Nawashauri tu CDM kuwa wana nafasi kubwa ya kushinda Jimbo la Mbeya Mjini iwapo wataweka mgombea mwingine nje ya Joseph Mbilinyi aka Sugu. Kuna sababu tatu :-
1. Mbunge aliyekaa kwenye jimbo zaidi ya kipindi kimoja mara nyingi wapiga kura humchoka, wanataka ingizo jipya

2. Watu wengi wanadai Sugu HAKUFANYA lolote kwenye miaka 10 aliyokuwa Mbunge zaidi ya kujenga hoteli yake

3. Wengine wanaona hana uwezo kwa vile kisomo chake kidogo na ana pata umaarufu kwa sababu za kisela tu

NB:
CHADEMA kwa ujumla ina nafasi kubwa ya kushinda Jimbo la Mbeya Mjini kwa kuwa Mbunge wa CCM aliyepo sasa hivi licha ya kuwa Spika lakini hakubaliki sana kwa sehemu kubwa ya Mbeya. Anakubalika kata zilizopo Uyole za Itezi, Iduda, Igawilo tu. Anaonekana ni Mbunge aliyeletwa na Mwendazake lakini siyo kwa kura za wana Mbeya.

Pili Tulia achafuka sana kwa namna alivyoshughulikia suala la Bandari kwa DP WORLD na suala la Luaga Mpina kuhusu sukari.

KIUJUMLA kama kungekuwa na DEMOKRASIA ya kweli kwenye vyama vyote CHADEMA na CCM, hawa Watajwa wote wawili HAWAFAI kuchaguliwa kugombea viti vya ubunge wa Mbeya Mjini
Chadema ndio watafute mgombea,Mbeya tuna vipaombele vyetu , Bandari waulize watu wa Pwanai kama imehamishwa au vinginevyo
 
Kwa uchaguzi gani ulioko hapa Tanzania, iwe sugu ama mgombea mwingine wa cdm, Tulia atatangazwa mshindi kwa nguvu ya vyombo vya dola. Sana sana wanaMbeya wakikaza wataishia kuuwawa, wengine wataachwa na vilema vya maisha, na wengine kubambikiwa kesi.
Ufedhuli wa 2020 hauwezi kurudiwa tena. Consciousness ya wapiga kura imeongezeka na wapiga kura wanauwezo wa kulinda kura zao
 
Kwani Tulia amesema hagombei?
Kama Tulia atagombea maana yake Sugu anagombea.
Mara ya mwisho Tulia akiwa bungeni alipendekeza jimbo la Mbeya mjini waligawe mara mbili ili amkwepe Sugu. Sugu akasema, hata jimbo likigawiwa mara mbili, kule atakapokwenda Tulia kugombea ndio huko huko naye atakwenda kugombea.
Hawa wote wawili ni chupa na mfuniko. Ila wapambe wa kila mmoja huwaambii kitu juu ya wagombea wao.

Siasa za ushabiki zitaigharimu Mbeya
 
Vijana ndio tunaliangusha taifa hili hatupigi kura mwisho wa siku mnawaachia wazee ndio wanaenda piga kura... Huwezi tegemea miujiza hapo
 
Mw
View attachment 3066360
Niko Mbeya Mjini kwa siku tatu hivi na nimeona upepo wa siasa za hapa. Siko upande wa CCM wala CDM. Nawashauri tu CDM kuwa wana nafasi kubwa ya kushinda Jimbo la Mbeya Mjini iwapo wataweka mgombea mwingine nje ya Joseph Mbilinyi aka Sugu. Kuna sababu tatu :-
1. Mbunge aliyekaa kwenye jimbo zaidi ya kipindi kimoja mara nyingi wapiga kura humchoka, wanataka ingizo jipya

2. Watu wengi wanadai Sugu HAKUFANYA lolote kwenye miaka 10 aliyokuwa Mbunge zaidi ya kujenga hoteli yake

3. Wengine wanaona hana uwezo kwa vile kisomo chake kidogo na ana pata umaarufu kwa sababu za kisela tu

NB:
CHADEMA kwa ujumla ina nafasi kubwa ya kushinda Jimbo la Mbeya Mjini kwa kuwa Mbunge wa CCM aliyepo sasa hivi licha ya kuwa Spika lakini hakubaliki sana kwa sehemu kubwa ya Mbeya. Anakubalika kata zilizopo Uyole za Itezi, Iduda, Igawilo tu. Anaonekana ni Mbunge aliyeletwa na Mwendazake lakini siyo kwa kura za wana Mbeya.

Pili Tulia achafuka sana kwa namna alivyoshughulikia suala la Bandari kwa DP WORLD na suala la Luaga Mpina kuhusu sukari.

KIUJUMLA kama kungekuwa na DEMOKRASIA ya kweli kwenye vyama vyote CHADEMA na CCM, hawa Watajwa wote wawili HAWAFAI kuchaguliwa kugombea viti vya ubunge wa Mbeya Mjini
Endazake alisema wazi bila kumung'unya kuwa majimbo yote yenye wabunge wa upinzani hayatapata pesa za maendekeo, ulitegemea Sugu apate wapi pesa hizo!
 
Ufedhuli wa 2020 hauwezi kurudiwa tena. Consciousness ya wapiga kura imeongezeka na wapiga kura wanauwezo wa kulinda kura zao
Hakuna uwezekano wa ccm kukubali kushindwa tena, iwapo wanajua mbinu ile ilifanikiwa, kwani mazingira ni yaleyale, na utekaji sasa umerudi upya kama enzi za dhalimu magu.
 
Kwa uchaguzi gani ulioko hapa Tanzania, iwe sugu ama mgombea mwingine wa cdm, Tulia atatangazwa mshindi kwa nguvu ya vyombo vya dola. Sana sana wanaMbeya wakikaza wataishia kuuwawa, wengine wataachwa na vilema vya maisha, na wengine kubambikiwa kesi.
Sugu Uchaguzi wa mwisho akiwa mbunge,alikuwa the most voted member of the parliament.

Alimpiga gap mpinzani wake kwa kura 60,000.

Kunapokuwa na gap kubwa baina ya wagombea ni ngumu sana kuchakachua ile ulijue.

Ila range ya kura 3500 zinachakaculiwa vizuri ndani ya vituo vya kata Mbili.

Kwa upepo ulivyo TULIA atapigwa gap la kura 35,0000 hivi.

Na utaratibu kura zikipigwa na kuhesabiwa matokeo yanabandikwa vituoni, kwahiyo kila mtu ana uwezo wa kujua matokeo ya ubunge kabla ya tume kutangaza.
 
Back
Top Bottom