Mshangai
JF-Expert Member
- Feb 16, 2008
- 468
- 1,086
Mimi ni mwanachama wa CCM. Sio mwanachama maslahi au mwanachama fuata upepo, la hasha bali mwanachama mwanzilishi hata kama nilijiunga 1978 mwaka mmoja tokea ianzishwe.
Ninafuatilia sana siasa za chama chetu, lakini niseme wazi kuwa tokea mwaka 2016 muda tuu baada ya awamu ya tano kushika hatamu CCM yetu imepotea na kuja kikundi cha aina fulani kuigeuza CCM yetu kutoka chama chenye heshima na utu na kuwa cha kihuni, uongo na tabia za kihalifu.
Shuhudia chaguzi za serikali yetu na sasa chaguzi zetu za ndani ya chama. Ni uhuni na rushwa ya hali ya juu haijapata kutokea tangu chama kianze.
Uongo ndio usiseme, ona tunabuni mpaka kupanga watu kutoa zawadi eti za jogoo njiani kwa Rais? Kweli Rais anaweza kupewa tuu barabarani jogoo na akampokea mikononi bila kujulikana usalama wa zawadi hiyo?
Sasa kwa ujinga unaoendelea kwa chama changu natangaza rasmi binafsi kujiunga na Chadema kama watamsimamisha Tundu Lissu kugombea Urais ili nimpe kura yangu.
Nategemea wengi ndani ya CCM wataniunga mkono kwa sababu za Lissu zifuatazo;
*Anaheshimu Katiba na Sheria.
*Sio muongo anapenda ukweli
*Ana uelewa mkubwa wa ndani na nje ya nchi.
*Anaheshimu Utu wa Mwanadamu
*Hana roho ya visasi.
OMBI;
Tanzania ni yetu, kuiacha tena miaka mitano mingine ipotee kama hii iliyopita ni kuitafuta laana ya vizazi vijavyo. Tuungane tufanye mabadiliko chanya, vyama ni vya kupita tuu lakini taifa lipo palepale. Chadema watuletee Lissu nasi tumpe kura.
Wasalaam aleikum!