Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Wanachama wa Chama cha CHADEMA mkoa wa Rukwa Wilaya ya Nkasi hii leo Januari 21, 2026 walijitokeza kupanda miche 1,600 ya miti mbali mbali katika wilaya hiyo katika kumbukizi ya miaka 33 ya kuanzishwa chama hicho.
Akizungumza na Wanahabari Mbunge mstaafu wa Nkasi Kaskazini na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake mkoa wa Rukwa, Aida Kenani ameshangazwa na kitendo cha Polisi mkoa wa Rukwa kuwazuia kupanda miche hiyo huku akisisitiza kuwa miti hiyo si kwa ajili ya CHADEMA pekee bali itawasaidia hata wana CCM na wananchi wote kwa ujumla.