CHADEMA mkoa wa Rukwa wachachamaa, wazuiwa kupanda miti, Aida na wenzake wauwasha moto

CHADEMA mkoa wa Rukwa wachachamaa, wazuiwa kupanda miti, Aida na wenzake wauwasha moto

Nimeshika neno gharama za mafuta kuwazuia watu kupanda miti, hapo kwenye ardhi wanapo panda miti kuna sanduku la kura? miti hiyo inatunza vizazi na vizazi sasa aliye ipanda na atakae nufaika na kivuli au matunda ni tofauti na mpandaji, kwanini hatuipendi nchi tunapenda chama? Hapa kuna mahala hatujui tuna hitaji nini kwenye nchi na hatuhitaji nini kwenye nchi.
 
ERTUGRUL BEY HAYA LAND HOV jitokezeji mliokuwa mnajifanya mnahubiri amani, tujue ni akina nani wanaharibu amani. Macjawa sugu uwanja huo wa jinsi cdm ilivyokufa na kinachowaua Tlaatlaah Lucas Mwashambwa THE BIG SHOW
Polisi wapo sahihi katika hili kwasababu CHADEMA imesimaishwa kufanya shughuli zake za kisiasa,je hili nalo ni la kulalamikiwa?

Sasa kama hiyo sheria iliwakandamiza Chadema ni swala lingine na polisi kusimamia sheria ni jambo lingine,tusipenda kulalamika hovyo wakati ukweli unajulikana
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Matendo kama haya ndio yanazidi kuijenga Chadema. Hasa baada ya yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa mwaka jana. Kwa nini zinatumiwa nguvu zote hizo kwa chama ambacho kiongozi wake mkuu yuko rumande, hakina mbunge wala diwani hata mmoja?

Kwa nini bado wanakihofia hivyo chama ambacho hakipati ruzuku yeyote?

Amandla...
Inasikitisha sana.

Chama kimoja tu ndio kina ruhusa ya kufanya siasa hapa nchini kwa uhuru.
 
Polisi wapo sahihi katika hili kwasababu CHADEMA imesimaishwa kufanya shughuli zake za kisiasa,je hili nalo ni la kulalamikiwa?

Sasa kama hiyo sheria iliwakandamiza Chadema ni swala lingine na polisi kusimamia sheria ni jambo lingine,tusipenda kulalamika hovyo wakati ukweli unajulikana
Kuotesha miti ni siasa? Hata hivyo ni kesi gani hiyo isiyokwisha kama kweli sio kutumia mahakama kukomoa wapinzani?
 
Back
Top Bottom