CHADEMA mmejaribu kuichokoza polisi, mkaona haichokezeki. Mumeona isiwe shida mkajichomea kabanda kenu Arusha

CHADEMA mmejaribu kuichokoza polisi, mkaona haichokezeki. Mumeona isiwe shida mkajichomea kabanda kenu Arusha

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
339
Reaction score
678
Taarifa zilizosambaa leo asubuhi ni Ofisi ya Chadema Arusha kuchomwa moto. Nimepitia mijadala mbalimbali kwenye kurasa tofauti za mitandaoni ya kijamii. Nimeona nije hapa baada ya kuona Twitter ya Mh Mdee aliyewahi kuwa Mbunge wa Kawe tena mwanasheria kuhusisha jambo Hilo na CCM.

Mimi ni mwanasiasa, ninatambua fika toka Mh Lissu anakuja walitegemea kuna hali polisi watawafanyia ili waweze kuwatumia mabeberu kuwa wananyanyaswa. Haikutokea. Wameendelea kutafuta wadhamini mikoani kwa kufanya mikutano mikubwa ya hadhara wakitegemea Polisi watawazui ili wafanye fujo na kuwapelekea ndugu zao nje, Polisi wamekaa kimya.

Baada ya michezo yote kukwama mumeona ISIWE taabu, MKAJICHOMEA kakibanda kenu ili msingizie CCM. Wanaojua wanafahamu ni mchezo wa kisiasa uliofanywa na Chadema kutengeza sympathy na kuitangazia dunia kuwa munanyanyaswa. Mumefanya hivi baada ya mipango ya awali kukwama. CCM hawawezi kuchoma ofisi ya CDM, kwani haina madhara Kwao. Huo ni mchezo umefanywa na Chadema kujitafutia uhalali wa hoja.

Chadema wamekuwa na kawaida ya kujitengenezea matukio hasa pale wanapohisi kubanwa kwa hoja hapa nchini. Na kwa namna siasa ya mwaka huu ilivyo hasa kwa kuwa hoja za 2015 zilishafanyiwa kazi tutegemee matukio mengi ya kuchongwa chongwa.
 
Shetani hakosi wa kumsingizia.

Ofisi za uwakili za fatma karume zilizopigwa BOMU si ninyinyi?

Ofisi za uwakili za wakili wa Yusuf Manji, aliyekuwa na kesi dhidi ya jamuhuri si ni nyinyi mliziharibu?

Kama mliweza kuteka Roma, Ben saanane, Mo Dewji, Azory Gwanda, Mdude chadema, Tito magoti et all

Tundu Lissu kupigwa risasi mchana kweupe na eneo lina ulinzi masaa 24, na CCTV- Camera mkatoa kupoteza ushahidi kama pale Colosseum alipotekwa Mo dewji?

Mtashindwa kuchoma hizo ofisi?

Hakuna uchunguzi wa polisi uliowahi kukamilika na mtuhumiwa kupelekwa mahakamani kwenye mausuala ambayo upinzani unaonewa.
 
Kama ungemsikiliza Sirro pale ITV kwenye Dakika 45 ungekuwa na ufikiri mpana zaidi!
 
Daa. Bora nikafute fute gari napoteza mda bure nikisoma utopolo
 
Eti chadema wameishiwa hoja? M/kiti wako ana Hali mbaya huko aliko wewe unakuja kuhara hapa?
 
Mtoa mada mbona unaingilia kazi ya polisi kwa muhemuko wako...

Unapaswa uwe shahidi kwa haya uliyoandika hapa.
 
Wewe unashabikia serikali hii ya kishetani. Maccm ni maharamia haya kwao ni mambo ya kawaida kabisa
 
Kwahiyo we ni mwanasiasa uandike upupu huu hapa? Wewe ni msemaji wa chama au? Tatizo lako nini kwani umeambiwa ulipe fidia ya jengo lililochomwa?
 
Hilo si la ajabu Chadema

Chadema waliwahi kurusha bomu Arusha ili ionekane wanahujumiwa
 
Namba ya simu umesahau mkuu tuache unafiki police hawajafanya uchunguzi mmesha kuja na uchunguzi wenu ndio maana inaonekana ccm yetu kuna vichwa maji wengi tuache mihemko vyama vinaweza kufa lakini Tanzania itakuwepo vizazi na vizazi.

Moyo wa upendo
Moyo usio na hila
 
Kawaida yao hao Chadema kufanya matukio na Sasa wapo na speed Kali ya kutafuta matukio maana wameyakosa kabisa sa hivi.

Nafikir hiki chama waache usanii Sasa maaana chama chenyewe kimekaa kihuni huni, kiupigaji zaid n.k.
 
Taarifa zilizosambaa leo asubuhi ni Ofisi ya Chadema Arusha kuchomwa moto. Nimepitia mijadala mbalimbali kwenye kurasa tofauti za mitandaoni ya kijamii. Nimeona nije hapa baada ya kuona Twitter ya Mh Mdee aliyewahi kuwa Mbunge wa Kawe tena mwanasheria kuhusisha jambo Hilo na CCM.

Mimi ni mwanasiasa, ninatambua fika toka Mh Lissu anakuja walitegemea kuna hali polisi watawafanyia ili waweze kuwatumia mabeberu kuwa wananyanyaswa. Haikutokea. Wameendelea kutafuta wadhamini mikoani kwa kufanya mikutano mikubwa ya hadhara wakitegemea Polisi watawazui ili wafanye fujo na kuwapelekea ndugu zao nje, Polisi wamekaa kimya.

Baada ya michezo yote kukwama mumeona ISIWE taabu, MKAJICHOMEA kakibanda kenu ili msingizie CCM. Wanaojua wanafahamu ni mchezo wa kisiasa uliofanywa na Chadema kutengeza sympathy na kuitangazia dunia kuwa munanyanyaswa. Mumefanya hivi baada ya mipango ya awali kukwama. CCM hawawezi kuchoma ofisi ya CDM, kwani haina madhara Kwao. Huo ni mchezo umefanywa na Chadema kujitafutia uhalali wa hoja.

Chadema wamekuwa na kawaida ya kujitengenezea matukio hasa pale wanapohisi kubanwa kwa hoja hapa nchini. Na kwa namna siasa ya mwaka huu ilivyo hasa kwa kuwa hoja za 2015 zilishafanyiwa kazi tutegemee matukio mengi ya kuchongwa chongwa.

Kama mnashindwa wakamata wahusika tuamini vipi cdm ndo uhusika
 
Back
Top Bottom