Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,734
- 5,750
Kwa siku mbili leo na jana CCM kinaendesha mchakato wa kupata wagombea wa nafasi za ubunge kwenye majimbo ya uchaguzi.
Na taifa zima limeelekeza macho kwenye huu mchakato ili kujua nani ataibuka kidedea ili aingie kwenye tatu bora kisha kamati za siasa za CCM za wilaya, mikoa na kisha halmashauri kuu kuchagua jina moja ambalo linafaa kwa ajili ya kugombea kiti cha ubunge.
Kwa jana watu wengi masikio na macho yao yalikuwa kwenye matokeo ya jimbo la Kigamboni na huko mshindi wa kwanza ni Dk Ndugulile na wa Pili ni Paul Makonda.
Pia watu walifuatilia kwa ukaribu matokeo ya jimbo la Kinondoni na Temeke ambapo waliokuwa wabunge wa majimbo hayo hawakupata hata nafasi ya kutinga tatu bora.
Kinachoshangaza ni kuwa baada ya matokeo ya Kigamboni kutoka na Paul Makonda kushika nafasi ya pili wafuasi na wanachama wa CHADEMA wamefurahi na kucheka mpaka jino la mwisho linaonekana. Na hapo ndipo wameonekana kuwa ni wapuuzi na hawana fikra chanya.
Sababu hizi ni kura za maoni tu na kwa CCM zinatoa mwelekeo namna gani wagombea wanakubalika, lakini mchakato ni mrefu. Sababu majina matatu lazima yajadiliwe na kamati za siasa za wilaya, mkoa na kisha NEC kupitisha jina linalofaa. Na kwa mantiki hiyo mchakato bado na mpaka sasa haijulikani nani atapita.
Wao hao wafuasi wa CHADEMA kama wangekuwa na akili timamu wangeshughulika na ya kwao hasa kujinasua sababu CHADEMA sasa haina mvuto tena kwenye jamii ndio maana hata kura za maoni za CHADEMA hakuna anaefuatilia maana ni hawakubaliki na wananchi.
Kama Chama makini walipaswa kuangalia watajisafisha vipi kwa wananchi na kashfa za ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi zinazokikabili chama chao? Sio kukaa na kufurahia Makonda kushika nafasi ya pili.
Ni upuuzi na kukosa fikra chanya za kisiasa. Mambo ya CCM yanawahusu nini? Wakati wo ni mgonjwa aliyekata kauli.