Kwa siku mbili leo na jana CCM kinaendesha mchakato wa kupata wagombea wa nafasi za ubunge kwenye majimbo ya uchaguzi.
Na taifa zima limeelekeza macho kwenye huu mchakato ili kujua nani ataibuka kidedea ili aingie kwenye tatu bora kisha kamati za siasa za CCM za wilaya, mikoa na kisha halmashauri kuu kuchagua jina moja ambalo linafaa kwa ajili ya kugombea kiti cha ubunge.
Kwa jana watu wengi masikio na macho yao yalikuwa kwenye matokeo ya jimbo la Kigamboni na huko mshindi wa kwanza ni Dk Ndugulile na wa Pili ni Paul Makonda...