CHADEMA mnaendelea kupotosha kuhusu suala la Ngorongoro, ila mtafeli kama mlivyofeli la bandari

CHADEMA mnaendelea kupotosha kuhusu suala la Ngorongoro, ila mtafeli kama mlivyofeli la bandari

Samia amemsikiliza Lema.Mlaumu Sasa mama yako kuungana na Lema tukusikie kama huna msimamo wa jogoo kusimamia mguu mmoja,mtupie punje moja uone atakavyo kugombea hiyo punje na vidaranga!
Jogoo ana hulka za kifala sana kama CHADEMA, mfano wako nimeupenda sana,ha ha 😂 😂 ,,, besides Samia na serikali yake lazima waendelee na mpango wa kuwatoa wale mbugani.
 
Bila shaka sasa wewe umeelewa kinachoendelea.....Kila kitu kinarudishwa kama zamani.....sisi ni ndugu, ubaguzi hauna nafasi
Nani kakuambia hivyo,we UNADHANI plan ya kuwahamisha kwenda msomera ni plani ya kujaribu??
 
Friends and Our Enemies,

Jana nimemsikiliza Godbless Lema,Kada na Mbunge za zamani wa jimbo la Arusha akiendelea na siasa zake za upotoshaji na kuganga njaa kuhusu suala la wamasai na kinachoendelea ngorongoro.

Lema anasema kwamba,Serikali inakosa mantiki katika kuwaondoa wamasai huku ikiendelea na kutoa vibali vya ujenzi wa hoteli mbali mbali za kitalii ambazo hizo ndizo zitakuwa kinara wa kuharibu ecologia na kuleta pollution kwenye hifadhi na kuathiri wanyama pori.

Well,Ifikie wakati hawa wanasiasa uchwara waache kujitoa ufahamu na kudhihirisha ujinga na upumbavu wao wazi wazi namna hii.

Suala la Ujenzi wa hoteli za kitalii ndani ya mbuga halifanyiki kiholela tuh bila mpangilio maalum,ni suala la kitaalam na siyo mbuga za Tanzania tuh eti ndiyo pekee zinajihusisha na suala la kujenga hoteli na kudesign utalii wa aina hiyo,yeye Lema na CHADEMA wanajua fika kuwa suala hilo linafanyika kote duniani na kila aina ya tahadhari inachukuliwa,na siyo kila mtu tuh atapewa ruhusa ya kujenga kwa kuwa tuh ana mtaji wa kufanya hivyo,kuna study kadhaa zimeshafanyika na kuangalia sustainability ya jambo hilo kwa kuzingatia uhifadhi na maendeleo yake kwa ujumla.

Wamasai ni Jamii ambayo imeendelea kuongezeka na kuzaliana miaka na miaka,na itaendelea kuzaliana hifadhini wao pamoja na mifugo yao.

Ni Jambo ambalo liko wazi tuh kuwa kutokana na kuendelea kwao kuzaliana wao na wanyama obviously population yao itazidi kuongezeka na kupelekea kuathiri maisha na uhai wa hifadhi na wanyama wale kwa maslahi ya kizazi cha sasa na cha baadae.

Sasa,kuna kosa gani kwa serikali inapochukua hatua za makusudi katika kunusuru hali hiyo??wao CHADEMA na wanaharakati uchwara wanataka Serikali ikae kusubiri hadi lini kunusuru hali hiyo kwa mbuga zetu??

Wanakuja na siasa za kishamba eti ooh wamasai wanaondolewa ili mbuga wauziwe waarabu,ujinga ule ule waliokaja nao kwa kusema Bandari imeuzwa kwa waarabu ili mradi tuh kujenga taharuki na kukwamisha mambo ya msingi kuendelea.

Even kipindi cha Magufuli walikuwa mstari wa mbele kupinga ujenzi wa bwawa la Mwalimu Nyerere kule Rufiji eti kwa kigezo cha kuharibu mazingira ila hivi sasa wao wenyewe wamekaa kimya na kuishiwa maneno.

CHADEMA na wanaharakati uchwara yanapokuja mambo ya msingi ya kitaifa kama mnapinga basi mje na hoja za maana na zinazoeleweka na siyo mnakuwa kama watu ambao hamna akili timamu.

Hoja zenu kuhusu suala hili za ngorongoro zitafeli kama zilivyofeli kwenye sakata la Bandari.

Bado una msimamo huo au kuna kitu umeelewa sasa
 
ni nzuri tu :pulpTRAVOLTA:
Nani kakuambia hivyo,we UNADHANI plan ya kuwahamisha kwenda msomera ni plani ya kujaribu??
Mjinga katika ubora wako. Rejea Tena kuisoma ile mada yako!!

Naona huko Zanzibar mna tatizo vichwani!!

Mjinga mkubwa, hata bi Mkubwa kakupuuza!! Kama ulipata posho ya kuandika ule utumbo basi rudisha hizo pesa
 
Mjinga katika ubora wako. Rejea Tena kuisoma ile mada yako!!

Naona huko Zanzibar mna tatizo vichwani!!

Mjinga mkubwa, hata bi Mkubwa kakupuuza!! Kama ulipata posho ya kuandika ule utumbo basi rudisha hizo pesa
muerevu na mihemko tu 🤣

sasa unapanic nini kwa mfano, dah 🐒
 
Back
Top Bottom