Hii kampeni ya kuchanga ili kumnunulia gari jipya la kifahari Makamu Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani ni dhihaka iliyopitiliza kwa mwananchi wa kawaida. Tofauti kati ya wabunge wanaopitisha bajeti za kujinunulia magari ya kifahari na viongozi wa CHADEMA hakuna. Kama viongozi wa CHADEMA nao wanawawaza V8 VXR, LC300 na magari mengine ya kifahari kunakuwa na tofauti gani na CCM wanaowalaumu kila siku? Inakera sana.
Kama pamoja na ruzuku na stahiki alizolipwa Lissu hazijaweza kumnunulia gari itoshe kusema CHADEMA haitoshi kabisa kuongoza hii nchi. Potelea mbali acha CCM iendelee kuwepo kuliko kuchagua hili genge la Mbowe linalowaza bata muda wote. Halafu Lissu hajashindwa kujinunulia gari. Kinachofanyika kwa sasa ni uhuni tu wa kupiga hela kupitia michango.
Ninamshauri Lissu akatae hili suala la kuchangiwa ili kulinda hadhi yake na ya chama chake.