Pre GE2025 CHADEMA mnashindwa kuwa na Tv, radio kweli?

Pre GE2025 CHADEMA mnashindwa kuwa na Tv, radio kweli?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Chama cha siasa nguvu yake na kiburi kinatoka kwa wananchi. Ukiona chama cha siasa kinakuwa kinyonge ujue hakina nguvu ya uma ya kutosha. Kusema ukweli chadema ilikuwa na nguvu sana 2010 to 2015 ila JPM alitufanya tuone chadema hawapo kwa ajili ya wananchi yaani aliwaumbua kweli kweli hiyo kitu ni ngumu mno kusahulika kwa wananchi wenye akili itachukua muda sana kuanza kuwaamini uponzani.

Ni kweli wananchi wanaweza pigia kura kiongozi wa upinzani kwa kumuamini yeye kama yeye na sio kubebwa na chama kiama ilivyokuwa siku za nyuma chadema hakikua chama cha mchezo mchezo yaani alikua akipanda jukwaani Dr. Slaa akimwaga sera unaona kabisa jamaa anafaa kupewa nchi. Embu nambie ukweli leo hii upinzani ni nani anaweza kupewa nchi akafikia hata robo ya kiwango cha JPM. Wengi wao ni waongeaji ila utendaji zero nahao ndio wengi wapo kwenye vyama vya siasa sio chadema wala ccm.
 
Tunakumbushana tu! Jamani publicity ni muhimu sana katika propaganda za Siasa.

Piga ua chadema mnahitaji TV na Radio.
Erythrocyte , rafiki tunakwama wapi?

Pia Soma
- CHADEMA anzisheni kituo cha television kabla ya uchaguzi wa 2025
Mimi ni Mwanachama wa Chadema nakiri kusema Kitengo cha Management Habari Maelezo Hakina Kazi hata Zero.

Ni kitengo cha hovyo chenye watu wasio na uwezo hata kidogo.
.habari za Chadema zinasambaa tu kwa sababu ya Mapenzi ya watanzania kupenda kuhabarishana kuhusu Chama Chao ila hiyo management ya Habari Maelezo ni ya Hovyo ni Ya hovyo Kweli kweli
 
Ni kweli wananchi wanaweza pigia kura kiongozi wa upinzani kwa kumuamini yeye kama yeye na sio kubebwa na chama kiama ilivyokuwa siku za nyuma chadema hakikua chama cha mchezo mchezo yaani alikua akipanda jukwaani Dr. Slaa akimwaga sera unaona kabisa jamaa anafaa kupewa nchi. Embu nambie ukweli leo hii upinzani ni nani anaweza kupewa nchi akafikia hata robo ya kiwango cha JPM.
Binaadam tumeumbwa wote kwa Usawa lakini tunazidiana viwango vya ubora na upungufu wa Usawa huo.

Marehemu JPM kapitishwa lini Kama SI Unit ya ubora wa Urais?
Wengi wao ni waongeaji ila utendaji zero nahao ndio wengi wapo kwenye vyama vya siasa sio chadema wala ccm.
 
Binaadam tumeumbwa wote kwa Usawa lakini tunazidiana viwango vya ubora na upungufu wa Usawa huo.

Marehemu JPM kapitishwa lini Kama SI Unit ya ubora wa Urais?
Ukitumia akili ta kuzaliwa utagundua alikuwa raisi wa viwango. Ili ujue mtu ni mfupi lazima umuone aliyemzidi kwa urefu.
 
Mkuu sio rahisi kiivyo, unakumbuka gazeti la Tanzania Daima?
Wakianzisha kila siku watashinda mahakamani kwa kesi za uchochezi,
Pia kumbuka boss wa wanahabari ni Nape Mnauye
Chadema kazi yao kulia lia tu ndiyo wanaiweza,lakini hawaendi na wakati hawaamini katika njia mbalimbali za uenezi na mawasiliano na wananchi. chama kikubwa hakina TV wala Redio. kipindi hiki cha huyu mama ndiyo kingefaa kuomba TCRA. Wao ni mikutano tu. Hawawezi kuwafikia wote. Badilikeni
 
Nani awape CHADEMA leseni?
Hivi mleta mada unadhani Chadema hawajawahi kuomba kuanzisha vyombo vyao vya habari kama Redio na Tv?
All in all, ni muhimu sana kwa CHADEMA kuwa na TV yao.
Mwenye Saccos hapangiwi
 
Wanaweza anzisha ila watakosa pesa za kuendesha
 
Mimi naamini kabisa kile kibatali kinaitwa mwenge wa uhuru kimewataahirisha watanzania wengi sana kiasi kwamba ni kazi ngumu sana kuwakomboa kifkra. Kwa hali ya kiuchumi ya Tanzania ilivyo duni chini ya utawala wa CCM kwa zaidi ya miaka 60 sasa ilitakiwa hata bila ya kushawishiwa na chama chochote cha siasa Watanzania wote waikatae CCM kwa nguvu zote.
 
Wakianzisha itafungiwa watapata hasara hata wasijisumbue, Wabaki youtube pekee inatosha mpaka utawala utakapobadilika.
 
Tunakumbushana tu! Jamani publicity ni muhimu sana katika propaganda za Siasa.

Piga ua chadema mnahitaji TV na Radio.
Erythrocyte , rafiki tunakwama wapi?

Pia Soma
- CHADEMA anzisheni kituo cha television kabla ya uchaguzi wa 2025
Chadema wana Tv na redio zao kule X(Twitter)

𝗞𝖚𝖓𝖆 ....𝗧𝗩_ 🅼🅼🅼-🄼🅃🄸🄺🄸🄻🄰
𝗡𝗮 𝑩𝒐𝒏𝒊 𝒀𝑨𝑰 🅣🅥 𝑬𝒙_𝑴𝒂𝒚𝒐𝒓

𝗛𝗮𝘁𝗮 𝗺𝗮𝘁𝗮𝗻𝗴𝗮𝘇𝗼 𝘆𝗮 𝘃𝗶𝗳𝗼 𝘂𝗻𝗮𝘆𝗮𝗽𝗮𝘁𝗮 𝗵𝗮𝗽𝗮.
 
Yaani mijitu mingine...kweli kwa akili zenu mnaamini Chadema au chama chochote cha upinzani kitaruhusiwa kuendesha kituo cha television! Redio tu hawawezi kuruhusiwa na hili genge la wahalifu sembuse television! Hivi ukiwa chawa hata akili ya kawaida kabisa lazima uikabidhi kwa hilo genge la wahalifu.
 
Ikianzishwa inakua ya familia ya mbowe chama tu hadi sasa hakina gari hata moja magari yote ni ya Mtei na Mbowe
 
Back
Top Bottom