CHADEMA msipoyakabili/kuyakemea haya magazeti yatawayumbisha wafuasi wenu na kuleta mgawanyiko, yakemeeni

CHADEMA msipoyakabili/kuyakemea haya magazeti yatawayumbisha wafuasi wenu na kuleta mgawanyiko, yakemeeni

Habari kamili ya gazeti hilo ni hii hapa👇👇👇👇 chini nimeikopi na kuipesti kama ilivyo..

Kila mtu aisome kwanza kabla ya kutoa maoni yake


=====================================
MBOWE, LISSU: MSIMAMO TOFAUTI KUHUSU MARIDHIANO

Wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikiendelea na operesheni +255 Katiba Mpya katika Kanda ya Kaskazini, kauli kinzani zimeibuka kati ya viongozi wa juu wa chama hicho -- mwenyekiti Freeman Mbowe na makamu wake, Tundu Lissu.

Viongozi hao wanaoongoza timu mbili zinazoshiriki operesheni hiyo wamekuwa na kauli tofautikuhusu suala la maridhiano baina ya chama hicho, Serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Kutofautiana huko kumeibua mijadala ndani na nje ya chama na kuwaacha baadhi ya wanachama wasijue la kufanya.

“Unajua maridhiano yana faida, hata hii mikutano ya hadhara ambayo Lissu anaitumia kusema maridhiano hayajaonyesha matokeo, msingi wake ni maridhiano, wanachama wetu wenye kesi mbalimbali wameachiwa, kesi zenyewe za Lissu zimefutwa,” alisema kiongozi mmoja wa kamati kuu ya chama hicho.

“Hata ruzuku tumechukua msingi wake ni maridhiano. Ni kweli yawezekana kuna mambo hajaridhika, ila maridhiano yameonesha matokeo makubwa.”

Wakati kigogo huyo akieleza hayo, aliyewahi kuwa mbunge kupitia chama hicho aliyeomba jina lihifadhiwe alisema “maridhiano haya yanaturudisha nyuma sisi. Yanatufanya tuonekana kama tumesalimu amri, ni bora tuendelee na ujenzi wa chama, hawa tunaoridhiana nao si wa kuwaamini sana.”

Hata hivyo, Mbowe kwenye moja ya mikutano wa hadhara ya operesheni +255 mkoani Kigoma alisema wanaodai yeye (Mbowe) na Lissu hawaelewani wanakosea, hilo halipo na wanaendelea kuchapa kazi kama kawaida.

Mbowe akieleza hayo na kusisitiza kuwa maridhiano yataendelea, Lissu katika mikutano anayoongoza yeye Kigoma na Katavi amekuwa akikosoa mambo mbalimbali yanayoendelea, akisisitiza kuwa “maridhiano ya kweli ni kupatikana kwa Katiba mpya.”

Awali, akiwa Singida, katika mwendelezo wa mikutano yake ya hadhara, Lissu alisema, “kuna maneno mengi ya upatanisho, lakini maridhiano pekee ni upatikanaji wa Katiba mpya, tusipokuwa na Katiba mpya tumeliwa. Maridhiano ambayo hayana ukweli, watu waliumizwa sana lakini hawajaambiwa kwa nini waliumizwa, wala nani aliyeamuru waumizwe wala kufidiwa,” alisema.

Alipoulizwa jana, Lissu alisema mikutano ya hadhara imeruhusiwa kutokana na shinikizo la ndani na nje ya nchi kwa serikali ya Samia na wafungwa wa kisiasa na kesi za kubambikiza vivyo hivyo, pia hata

Mbowe hakuachiliwa kwa sababu ya maridhiano bali kwa presha kubwa ndani na nje ya nchi.

“Kesi ilishabuma. Rais Samia hakuwa na jinsi bali kukubaliana na shinikizo hilo,” alisema.

Alisema yale yote yanayohitaji mabadiliko ya sera, sheria na katiba (kwenye maridhiano) hayajatekelezwa hata moja na mchakato wa Katiba Mpya haujaanza lakini muda hautusubiri.

Alisema hata yake ambayo hayahitaji mabadiliko yoyote ya kisheria au kisera, kama vile kuwaondoa wabunge 1p wa viti maalumu ambao Chadema iliwafukuza uanachama Rais Samia ameshindwa au kukataa kuyafanya.

Hata hivyo, alisema “sio sahihi kusema hatuoni kilichofanyika. Tunaona kilichofanyika, lakini sio kwa sababu zinazopigiwa chapuo.”

Mbowe hakupatikana jana kuzungumzia utofauti huo, lakini akizungumza wakati wa uzinduzi wa Operesheni +255 Katiba Mpya Mei 17, 2023, bila kuweka wazi alisema katika taasisi yoyote kutokuelewana hakukosekani.

Alisema pamoja na kuwepo changamoto hiyo, viongozi wa chama hicho wanaendeleza mapigano ya kuhakikisha Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi vinapatikana.

“Natambua kuna watu wanasema viongozi wa Chadema tuna kutoelewana, hiyo ni kawaida kwani hata vikombe vikiwa kabatini lazima vigongane ndivyo ilivyo, hata sehemu yenye watu wengi hapakosi migogoro, lakini niwahakikishie tunaendelea na maridhiano ili kuhakikisha Watanzania wanapatiwa Katiba Mpya,” alisema Mbowe

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa waliozungumza na gazeti hili, wamekuwa na mitazamo tofauti juu ya kauli hizo za Mbowe na Lissu kuhusu maridhiano, wakisema mapito waliyopita viongozi hao yanatofautiana, ndiyo maana hicho kinatokea.

Maridhiano vs harakati

Mchambuzi wa siasa, Rainery Songea alisema kupishana kauli viongozi kupo, lakini mwishowe kitakachoangaliwa ni msimamo wa chama chao.

Alisema Mbowe anaweza kuwa na maoni yake, vivyo hivyo Lissu, lakini ukiangalia msimamo wa Chadema inaunga mkono maridhiano.

“Kimsingi, pamoja na kupishana lakini kuna vitu wanakubaliana,” alisema.

“Ukimuangalia Mbowe na Lissu ni watu wanaopishana kidogo kimtizamo; Mbowe anaamini katika maridhiano, ila Lissu anaamini zaidi katika harakati, hii ndiyo tofauti yao,” alisema.

“Sasa wakipishana hivi, jambo kubwa linalopaswa kuangaliwa ni msimamo wa chama ukoje, yaani kamati kuu,” aliongeza.

Hata hivyo, Songea alisema ukiangalia kwa jicho la mbali zaidi, Mbowe na Lissu wanakubaliana na maridhiano, shida iliyopo ni mitizamo tu.

Ukiacha hali hiyo, Songea alisema maridhiano yameanza kuzaa matunda, kama vile watu kuandamana kwa ulinzi wa polisi.

Suala la matunda ya maridhiano pia linatazamwa na Dk Faraja Kristomus, msomi wa Sayansi ya Siasa, anayesema “maridhiano kati ya Rais Samia na Chadema yameleta matunda, ikiwemo kuondoa mikwamo mbalimbali ya kisiasa iliyowekwa kwa miaka mitano.”

Kwa upande wake Gabriel Mwang’onda, mchambuzi wa siasa na uchumi, alisema Chadema ni chama kikubwa kwa sasa na hivyo kutofautiana kimtazamo baina ya viongozi ni jambo la kawaida.

Hata hivyo, alisema inaogopesha pale mitazamo inavyotofautiana mbele ya umma.

“Hawa ni binadamu, wanaweza wakawa na mitizamo tofauti, lakini hii mitizamo si kwamba wanatofautiana sana, wote wana lengo moja, isipokuwa namna ya kufikisha ujumbe wao ndiyo tofauti.

“Mara kadhaa Mbowe amekuwa akisisitiza hajalambishwa asali na kwamba harakati zao za mapambano hazififishwi na maridhiano. Lakini Lissu pamoja na kutoelezea, fursa ya kufanya mikutano ya hadhara au kurejea nchini ni matunda ya mazungumzo,” alisema Mwang’onda.

Alisema alichokifanya Rais Samia na Mbowe ni kitu cha kupigiwa mfano na anaamini anachokifanya Lissu ni jambo la kawaida na ajenda za kisiasa ili kuonekana uwepo wake na kuhoji masuala yaliyojitokeza miaka mitano iliyopita.

“Inasaidia kutisha ili hayo yasitokee tena, kujenga uelewa kwa Watanzania kwamba haya yaliyotokea miaka mitano iliyopita yalikuwa na madhila mabaya na hayatakiwi kujirudia. Kukiri kwa Serikali kumeshafanyika, nadhani umesikia ile kamwe…tusirudi tulikotoka,” alisema.

Mwang’onda alisema huwezi kumzuia mtu kuzungumza, hasa Lissu ambaye madhila yaliyomtokea ni tofauti na Mbowe. Alisema Lissu alijeruhiwa kwa risasi, wakati Mbowe alifungwa jela sambamba na kuharibiwa biashara zake.

“Hatuwezi kupima uchungu wa Lissu, maana ilikuwa kufa au kupona, acha atoe ya moyoni ili kupata ahueni zaidi. Si kwamba Mbowe hakuathiriwa, tena alipata changamoto ndani ya utawala huu pia,” alisema Mwang’onda.

Hatua za maridhiano, faida zake

Majadiliano ya kwanza ya maridhiano yalifanyika Ikulu ya Chamwino, Dodoma Mei 20, mwaka jana ambapo Rais Samia akiambatana na viongozi waandamizi wa CCM na Serikali walikutana na ujumbe wa viongozi wa Chadema ulioongozwa na Mbowe.

Kikao kingine cha faragha kilifanyika Novemba 5, 2022 jijini Dar es Salaam na vigogo wa CCM wakiongozwa na makamu mwenyekiti (Bara), Abdulrahman Kinana na upande wa Chadema uliongozwa na Mbowe.

Moja ya mafanikio ya mazungumzo hayo, Rais Samia alihudhuria na kuhutubia kongamano la Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) lililofanyika Machi 8, mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Akihutubia kongamano hilo, alisema maridhiano waliyoanza hayatawaacha salama kwa sababu kuna wahafidhina kwenye vyama ambao hawataridhika.

Rais Samia alisema utamaduni wa kukaa chini na kuzungumza si jambo rahisi kwa watu wengi na unakuwa na vikwazo kwa pande zote za mazungumzo.

“Kwa hiyo mwenyekiti (Mbowe), wahafidhina wapo kwangu na kwako pia,” alisema Rais Samia.

Jambo jingine kubwa la maridhiano linalotajwa ni kuwa Godbless Lema, mbunge wa zamani wa Arusha Mjini aliyekuwa akiishi uhamishoni Canada tangu mwaka 2020 kutokana na hofu ya kutishiwa maisha yake naye amerejea Tanzania.

Vivyo hivyo, mikutano ya hadhara imerejea huku mchakato wa Katiba mpya ukifanyiwa kazi na Serikali ilitangaza kuongeza takribani Sh9 bilioni katika bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria ya mwaka 2023/24.

Maridhiano hayo kwa namna moja au nyingine, yamesababisha Chadema kuchukua fedha za ruzuku walizokuwa wamesusia tangu mwaka 2020, kwa kile walichodai hawakukubaliana na matokeo ya uchaguzi mkuu.

Mei 11 wanawake wa Bawacha walifanya maandamano ya kushinikiza Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson kuwaondoa wabunge 19 waliofukuzwa uanachama na kupoteza sifa ya kuwa wabunge ambayo yalilindwa na jeshi la polisi, jambo ambalo huko nyuma lisingewezekana.

===================================

In my opinion:

1. Hakuna tofauti yoyote kati yao yenye kuleta mgswanyiko au damage yoyote

2. Isipokuwa ni kweli Kuna kutokukubaliana kwenye baadhi ya maeneo. Hili ni la kawaida sana popote pale palipo na watu wawili au zaidi..

3. Hata ndani ya familia ya mume na mke wanaopendana sana huwa na maoni tofauti katika baadhi ya mambo ya siku kwa siku yahusuyo familia yao lakini hilo huwa halifanyi familia iparanganyike bali hukubaliana katika kutokukubaliana na maisha kusonga mbele na jambo lililopangwa likafanyika..

4. Familia zinazoparanganyika na kusambaratika ni zile ambazo tofauti zao zimejengwa katika msingi wa usaliti, uongo, udanganuifu, ufisadi wa kingono, choyo na roho ya uuaji.

5. Vivyo hivyo katika vyama vya siasa, tofauti zinazoweza kuparanganyisha na kukisambaratisha chama ni zile zilizojengwa katika misingi ya usaliti, uongo, ubinafsi, udanganyifu na yafananayo na hayo lakini Kamwe si tofauti za kimitizamo na kimaoni juu ya jambo fulani..!
 
Kila mtu aisome kwanza kabla ya kutoa maoni yake
Ahsante kwa makala hiyo uliyoweka hapo, nami naondoa haya niliyoandika hapo juu
Inashangaza kidogo kuona hawa nao wamegeuka na kuwa sehemu ya CCM?

Inashangaza na kusikitisha.
Hata hivyo, mwandishi wa makala hiyo hakuwa mwangalifu katika kutengeneza a'kichwa cha habari" kinachoendana na taarifa iliyomo ndani ya makala.
Wakati akitafuta kuvuta wasomaji kwenye makala yake, wakati huo huo anawafukuza wasomaji wengine wasipoteze muda na taarifa inayoelezwa kwenye kichwa cha habari.

Mwisho, inanilazimu pia nirudie yale yale niliyokwishayasema siku nyingi baada ya Mbowe kutangaza msimamo wake juu ya maridhiano yake na Samia; msimamo aliouzungumzia kwa mara ya kwanza kwenye mkutano wake na waTanzania waishio ughaibuni.
Maridhiano hayafanyiki kubadili yanayosimamiwa na chama cha CHADEMA, wala yale yanayosimamiwa na CCM.
Maridhiano kwa uelewa wangu hayalengi kuviunganisha hivi vyama viwili vya siasa kiwe chama kimoja.

Kama hivyo ndivyo, sioni tatizo linapotokea wakati Tundu Lissu akizungumzia anayoona kuwa yanaifunga mnyororo CHADEMA isiendelee na juhudi zake za kuiondoa madarakani CCM

Kama Mbowe alikwishaamua kuiunganisha CHADEMA na CCM, kwa vile tu sasa hivi ni Samia ndiye anayeendesha mambo ya CCM, hapo ni wazi patakuwepo na tatizo.
Na kama kweli hili lipo, sioni ni namna gani mgogoro unavyoweza kuzuilika ndani ya CHADEMA.
 
Kama Mbowe alikwishaamua kuiunganisha CHADEMA na CCM, kwa vile tu sasa hivi ni Samia ndiye anayeendesha mambo ya CCM, hapo ni wazi patakuwepo na tatizo.
Na kama kweli hili lipo, sioni ni namna gani mgogoro unavyoweza kuzuilika ndani ya CHADEMA.
Tatizo langu liko hapo ☝️☝️☝️tu..

Hivi hili linawezekanaje kwa mfano?

Na mimi nadhani, mashaka na wasiwasi walionao baadhi ya wapenzi, mashabiki na wanachama wa CHADEMA ni usiri wa kinachozungumzwa kwenye hicho kinachoitwa "maridhiano" kiasi cha watu kuanza ku - speculate kuwa Freeman Mbowe anaweza kukipasua chama kama alivyofanyaga Prof Ibrahim Lipumba..

Ni kweli binadamu ni kiumbe fragile & kiko vulnerable na kinaweza kubadilishwa na mazingira wakati wowote. Na wahenga waliwahi kusema, "moyo wa mwanadamu ni kichaka chenye giza". Aujuaye moyo huo ni Mungu muumba peke yake..

Hata hivyo, Freeman Mbowe Kwa hiki kinachodhaniwa kumhusu, anaweza kuhukumiwa kwa kuiangilia historia yake na CHADEMA na kumpima ktk hiyo ili kujua anaweza kweli kufanya hiki tuanachokidhania au la..

Mimi siamini hata kidogo. !!

Freeman Mbowe pamoja na kuwa tunamjua kama mwanasiasa na mfanyabiashara tu, lakini mimi namuona kwa sura nyingine pia kuwa, huyu jamaa ni jasusi na mwanamikakati mzuri sana wa siasa za kiafrika..

Huyu jamaa angekuwa ni mtu wa kukiuza chama hiki na kuwasaliti wanahaharakati na wapigania uhuru wenzake, hakika angeweza kufanya hivyo ktk kipindi cha utawala wa mateso wa Hayati John P. Magufuli (2015 - 2021)..

Hayati Rais John P. Magufuli si tu kwamba alikuwa na dhamira ya dhati na ovu ya kuifuta CHADEMA (msisitizo: si vyama vingine ila CHADEMA tu) katika siasa za Tanzania, bali alitaka kuhakikisha "viongozi vichwa" wote wa CHADEMA wanaondolewa kwa aidha kuuwawa (kuuliwa) au kununuliwa wahamie CCM..

Haina shaka hata kidogo, kuwa, viongozi vichwa vya CHADEMA kwa wakati ule, sasa na hata kesho ni wawili tu; Freeman Mbowe (M/kiti - Taifa) na Tundu Lissu (msaidizi wake)

Magufuli na wenzake walikuwa wanalijua hili. Samia Suluhu Hassan na wenzake huko CCM wanalijua hili. Hata makakati wa Rais Samia na CCM kuanzisha propaganda hizi kupitia magazeti na vyombo vingine vya habari zinalenga kuwafarakanisha hawa jamaa. Yeye mwendazake alitumia mbinu zote. Moja kubwa ni kutumia kanuni ya "piga mchungaji, kondoo watatawanyika tu"

Magufuli alianza nao hawa na Rais Samia anakwenda nao ila kwa mtindo mwingine ambao ulitumiwa na Jakaya Kikwete na ulishindwa vibaya..

Hebu rudi nyuma na angalia mateso waliyopitia hawa jamaa wawili wakati wa mwendazake. Ni taabu na kifo/mauti ya mwili waziwazi wao binafsi na familia zao na yeyote aliyehisiwa kuwa mshirika wao.

✓ Huo ndio ulikuwa wakati wa hawa jamaa kufarakanishwa na pengine ulikuwa wakati wa kusema ya nini haya...!

✓ Huo ndio ulikuwa wakati wa ku - surrender kila kitu ili wamwabudu mungu mtu Magufuli!!

✓Huo ndio ulikuwa wakati wa kulipwa fedha yoyote ambazo wangetaka. Na kwa Magufuli wote tunajua kuwa kama fedha ingeshindikana kuwanunua angeweza kuwanunua kwa damu ya makamu wake yaani mama Samia au kiongozi yeyote huko CCM..!!

To cut it short ni kuwa, huo ndio ulikuwa wakati wa kukiuza chama huku wakiacha vumbi kubwa la fedheha na aibu kwa wapenzi na wanachama wa CHADEMA kwa namna mbaya sana.!!

,##Lakini hawa wanaume hawakufanya hivyo. Walikubali kuyaweka maisha yao rehani yao Kwa ajili ya chama Chao na walio nyuma kiasi ambacho wengine ni walemavu (TL) na wengine fedha na mali zao ziliporwa..

##Hivi leo katika mazingira yenye dalili zote kuwa usiku wa giza nene unatoweka, kunakwenda kupambazuka na jua la ushindi linakwenda kuchomoza Freeman Mbowe auze chama..??

No, no ......... I don't believe!

Mimi ninachoamini ni opposite kabisa. Hawa jamaa wako kwenye mkakati MAALUMU..

Tunachokijadili hapa ni WA ni propaganda za kuwadhoofisha ili wagombane wakidhani wanachama na wapenzi watavurugika na kukidharau chama hiki..
 
Hata hivyo, Freeman Mbowe Kwa hiki kinachodhaniwa kumhusu, anaweza kuhukumiwa kwa kuiangilia historia yake na CHADEMA na kumpima ktk hiyo ili kujua anaweza kweli kufanya hiki tuanachokidhania au la..
Ngoja nianze na hili, kwa sababu ndilo jepesi sana kujibu katika andiko lako zuri.

CCM ya Samia, siyo ile CCM ya Magufuli, wala ya Mkapa, na hata ya Mzee Ruksa.

CCM hii ipo karibu sana kama siyo sawa na ile ya Kikwete; ingawaje hata hiyo ya Kikwete ilikuwa bado ina vimelea vingi sana ya vile vya CCM asili iliyoundwa mwaka.....

Ukiondoa haya yanayosemwa kuwa "Masukuma Gang"; kiukweli napata shida sana kuiona CCM hii ya Samia ikiwa mbali na CHADEMA ya Mbowe, toka mwanzo wa siasa zake.
Nitaachia hapa hili.
Na mimi nadhani, mashaka na wasiwasi walionao baadhi ya wapenzi, mashabiki na wanachama wa CHADEMA ni usiri wa kinachozungumzwa kwenye hicho kinachoitwa "maridhiano" kiasi cha watu kuanza ku - speculate kuwa Freeman Mbowe anaweza kukipasua chama kama alivyofanyaga Prof Ibrahim Lipumba
Hili hapa umeliweka vizuri sana.
Na ubaya wa "usiri" huo ni kuona baadhi ya mambo yakifanywa na Rais, kuwa kama kinyume cha maridhiano yenyewe yanayosemwa yapo yanaendelea.

Kwa mfano teuzi za Rais za watu ambao wanajulikana wazi kuwa mambo mengi yanayoridhiwa sasa, wao walikuwa ni sehemu kubwa ya matatizo hayo.
Hata mwenendo mzima wa hii Katiba Mpya, ni kama janja janja tu na hadaa inayofanyika kulaza akili za waTanzania!

Tundu Lissu akiyagusa haya, kokosi kizima cha mashambulizi toka huko huko CCM kinakuwa kama kimeingiwa na wazimu!

Huwa sipendi sana kuandika au kusoma mabandiko marefu sana kwa mara moja humu JF, kwa hiyo ngoja nimalize kwa kusema kwamba Mbowe kajiweka mwenyewe kwenye kona ya kutoaminiwa. Ninamtambua Mbowe, kuwa kiongozi mwenye msimamo usiotetereka (hadi hivi karibuni), ambaye kwa hakika uwepo wa CHADEMA hadi wakati huu, ni sababu ya uongozi makini sana aliouonyesha toka huko nyuma, na hasa hasa wakati walipokuwa wanapitishwa kwenye tanuru la moto.
Kama katetereka kwa sababu yoyote ile, iwe binafsi, au ya chama chake kushirikishwa katika serikali zifuatazo, atakuwa amepoteza fursa kubwa kabisa ya heshima anayoistahiri ya kuwa kiongozi imara aliyeiokoa CHADEMA isiwe CUF, au NSSR(), au TLP.
 
Magufuli alianza nao hawa na Rais Samia anakwenda nao ila kwa mtindo mwingine ambao ulitumiwa na Jakaya Kikwete na ulishindwa vibaya..
Nilikuwa sijakusoma hadi huku chini.

Magufuli alikuwa amedhamiria moja kwa moja kuimaliza kwa njia yoyote ile CHADEMA, hili lipo wazi kabisa.

Hiyo kesi ya "ugaidi" ndio ungekuwa mwisho wa Mbowe; na Lissu tayari alikuwa ukimbizini, sasa hivi angekuwa yuko huko huko. Hawa viongozi wengine waliopo huko CHADEMA wanaofahamika kuwa na misimamo isiyoyumba, kama akina Henche, Mnyika, wao wangetolewa tu njiani kwa namna ambayo angeona inafaa.
CHADEMA wakati huu ingekuwa na hali tofauti sana; kama ingekuwa bado inaendelea kuwepo chini ya Magufuli.

Tatizo lililompata Mbowe, ni kama hivyo ulivyoligusia kidogo katika andiko lako.
Mbinu za maguvu alizotumia Magufuli kuimaliza CHADEMA kwa kuwashughulikia viongozi wake wakuu wenye msimamo, ulitikisa sana hawa viongozi hawa wawili.
Samia yeye kaja na mtindo tofauti kabisa na ule wa Magufuli, kujaribu kuwashughulikia viongozi hao hao kwa njia iliyo kinyume kabisa na ile ya mwanzo ya kutumia maguvu.

"Fanya kama unawasikiliza vizuri hawa viongozi,... sikiliza shida zao ni nini na fanya kama upo tayari kuwatimizia shida zao hizo. Onyesha ubinaadam; mbali kabisa na yale waliyopambana nayo wakati ule..."

Kiongozi anayeyaona yote haya, akayafaidi (kama haki yake) na akaendelea kudai anayoyasimamia yeye kama kiongozi, yasiyokuwa kwa manufaa yake binafsi, bali kwa manufaa ya nchi...; viongozi wa aina hiyo ni nadra sana kuwapata mahali popote duniani

Na kumbuka; mbaya zaidi, hasa kwa Mbowe, akikumbuka mateso yote waliyopitia, na wakati huo huo, watu/raia/waTanzania wakionekana kuwa kama hawayaoni/hawayajali.... Inataka moyo wa ajabu sana kwa kiongozi kuendelea kusimama imara na kuendelea na harakati za kutafuta anachokiamini moyoni mwake kwamba ndicho anachowatakia hao anaowapigania, na wasioonyesha shukrani kwake.

Ni matumaini yangu kwamba nimejieleza vya kutosha kueleweka.
 
Back
Top Bottom