Kwa mwendo huu wa maandamano wala cdm hamtafika popote.
Swali: mkimaliza kufanya maandamano mikoa yote mtafanya nini ukizingatia ccm haitabadilisha msimamo wake wa kutowajibisha mafisadi. "Kwa kuwa kuwawajibisha mafisadi sie wananchi wenye kusoma situation tumeishaona haitawezekana'
Kwa hiyo kwa kuwa wewe umeshaona kuwa haitawezekana wao kuwajibishwa ndo watu wakae kimya na kuendelea kuteseka? Naona kama unataka kuleta propaganda kuwa tujikalie tu kwa sababu haiwezekani, ina maana nchi hii haina sheria? kama zipo kwa nini haziwafikii hawa mafisadi. Ningekushauri kuwa hata weye hapo ulipo kama kweli unaitakia mema Tanzania, andamana hapo ulipo ukiwaambia watu ubaya wa ufisadi ili hao watu waweze kuchukuliwa hatua.
"Fisadi anawajibishwa kwa kufilisiwa na siyo kufanya maandanao kama chadema. Na natumai ni Rais wa nchi tu ndio anaouwezo wa kuwafilisi hao mafisadi"
Naona kama unajichanganya, kama ushasema tumeshakubaliana kuwa hawawezi kufanywa lolote, je utawafilisi vipi? Ni nani anatakiwa kuwafilisi? Je kama hao ambao wanatakiwa kuwafilisi hawafanyi kazi yao, huoni kuna umuhimu wa kuwaondolea hayo mamlaka waliopewa ili watu wenye uwezo waweze kuwafilisi?, Hebu saidia kutoa njia mbadala hao chadema wafanyeje au watanzania wanaotaka hawa mafisadi wafilisiwe wafanyeje? Nina imani na weye ni katika watanzania ambao unataka kuona hawa watu wakifilisiwa na kuchukualiwa hatua, ila tufanyeje?
Hivyo chadema hizi ni mbio za sakafuni. Ni bora kama kweli mnaipenda tz mngeanza juhudi kuwasemea na kuwaanika kwa vidhibiti mafisadi na kufuatilia vijisenti wanavyoweka mabenki ya huko ulaya na america ili msaidie intel ya kushinikiza kuwafilisi vizuri.
Hili ni wazo zuri, lakini je chadema wana uwezo wa kufanya hivyo kama sio chama TAWALA? kwa nini usiwashauri CCM hili ambao wapo kwenye position nzuri ya kupata ushirikianao na hayo mabenki ili mradi wajenge argument kuwa hawa watu ni viongozi katika serikali hii na wamehujumu uchumi na wanataka kuwashtaki? Kama vipi labda kama katiba yetu ingekuwa inaturuhusu sie waDanganyika ili kuhoji hayo ma-acount!
Just to advice u.
And don't think you are the most clever pple to talk for this nation, no, you are just pple who have ambition to shout against CCM and doubtly not for the nation's benefit.