Mpasuko wazidi kuiandama Chadema kwa fununu za kuhamwa zapamba moto
Na Peter Edson
WAKATI uongozi wa Chadema ukisisitiza kuwa hali ni shwari na kwamba, Naibu Katibu wake Mkuu, Zitto Kabwe hakusudii kukihama chama hicho; hali ndani ya chama hicho inadaiwa kuwa bado ni tete.
Habari zilizopatikana zinaeleza inawezekana idadi ya watu wanaondoka ndani ya chama hicho ikaongezeka kutokana na kuzidi kuongezeka kwa ufa miongoni mwa wanachama.
Hata hivyo uongozi wa chama hicho umesema Katibu Mkuu Msaidizi, Zitto Kabwe haondoki Chadema.
Kaimu Katibu Mkuu ambaye ni Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Chadema, John Mnyika alisema jana kuwa chama hicho kiko imara na hakikusudii kumfukuza mwanachama yeyote na kwamba Zitto bado ni kiongozi wao.
“Chama hakiwezi kuyumba kwa namna yoyote ile na kipo tayari hesabu zake zikaguliwe na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali,†alisema na kuongeza kuwa hakuna kiongozi yeyote aliyefukuzwa uanachama ndani ya chama bali wapo waliojiondoa.
Mnyika alisema viongozi wake wa juu ambao ni Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa ni wasafi, hivyo hawapaswi kuchafuliwa wala kuchonganishwa na wananchi.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa kuna baadhi ya watu ndani ya chama hicho wanaowaunga mkono wanachama waliojiondoa hivi karibuni kwa madai kuwa waliwekewa mazingira magumu ya kuwafanya kujiondoa.
Kutokana na hali hiyo, viongozi wa juu wa chama hicho wanahaha kuweka mambo sawa ili kumaliza tofauti hizo za kimtizamo zilizojitokeza.
Mwasisi wa chama hicho, Edwin Mtei alipoulizwa jana kutoa maoni yake kuhusu hali ndani ya chama hicho alisema yuko safarini kuja jijini Dar es Salaam.
Hivi karibuni aliyekuwa ofisa wa habari wa chama hicho aliyeondolewa katika nafasi hiyo na uongozi, David Kafulila na mshirika mwingine mkubwa kisiasa wa Zitto Danda Juju, wamekikimbia chama hicho.
Wakati akitangaza kukihama chama hicho, Juju alikitupia kombora chama hicho na kumtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kukagua hesabu za chama hicho kwa tuhuma za ufisadi wa ruzuku.
Kujitoa Chadema kwa mshirika huyo wa Zitto ambaye alikuwa ni Ofisa Mwandamizi wa Bunge na Halmashauri, kumetokea wakati inadaiwa kuwa Kafulila na Juju walikuwa na watu wengine wanaowaunga mkono ndani ya chama hicho ambao wanaweza kuondoka wakati wowote.
Alisema amelazimika kutoa taarifa hiyo ya ufafanuzi baada ya kutokea kwa mfululizo wa habari zenye kujaribu kuhusisha maamuzi hayo na uchaguzi wa ndani wa chama uliofanyika mapema Septemba mwaka huu.
Hata hivyo, akizungumza na Mwananchi Jumapili kwa njia ya simu jana, Kafulila alimpongeza Danda kwa uamuzi wake wa busara wa kukihama chama hicho na kudai kuwa kitaendelea kumeguka kutokana na kuendeshwa kama kampuni.
“Wamiliki wa chama siku zote ni wanachama na si mtu binafsi, unapoona chama kinaanza kuongozwa kwa sera za mtu binafsi ujue kuwa hizo ni dalili za kuzikwa,†alisema Kafulila.
Alisema hawezi kuongelea jambo lolote kuhusu Naibu Katibu mkuu wa chama, Kabwe kwani anaamini kuwa uamuzi wa yeye kuendelea na chama upo mikononi mwake, hata hivyo alisema kuwa Zitto atafanya maamuzi ambayo yatakuwa sahihi.
“Sisi tumefanya kazi na Zitto kwa umakini mkubwa sana, lengo letu lilikuwa ni kukuza chama kwa namna yoyote ile, tuna imani kuwa jambo hili lililotufika linamuumiza sana, hawezi kulifumbia macho, tunaamini kuwa atafanya maamuzi sahihi,†alisema Kafulila.
Alisema ufike wakati viongozi waandamizi wa Chadema waelewe kuwa chama hicho kinapita katika wakati mgumu hivyo kama wasipokuwa makini na kuhakikisha kuwa wanakifanya chama kiwe mali ya wanachama basi kitapoteza muelekeo.
“Mimi si mtabiri, lakini vitendo vinavyoendelea vinaonyesha dhahiri kuwa Chadema kipo katika njia panda,†alisema Kafulila.
Mwanachama mmoja wa chama hicho ambaye hakupenda kutajwa jina lake alionya kuwa iwapo viongozi wa juu wa chama hawatamaliza tofauti hizo chama kitameguka.
Mnyika hata hivyo, aliziponda shutuma zilizotolewa na Kafulila katika mkutano wake na waandishi wa habari Novemba 18, mwaka huu kuwa Chadema kimejaa uovu na kwamba kutenguliwa kwa uteuzi wa Kafulila na Danda hakutokani na sababu zozote bali kulifanywa na katibu mkuu wa chama baada ya wao kukiuka kanuni, maadili na itifaki Mnyika anaongeza kuwa tuhuma hizo za uongo dhidi ya chama na viongozi wake wamezitoa baada ya kutenguliwa uteuzi wao, hivyo Izingatiwe kuwa kikatiba, maofisa wa chama si wajumbe wa sekretarieti ya chama wala kamati kuu ya chama.
Alisema Chadema haijawahi kujadili wala kufikiria kumfukuza Zitto uanachama na viongozi wa chama wamesisitiza kuwa hivi karibuni kuwa hakuna mvutano wala makundi ndani ya chama hivi sasa kwa kile kinachodaiwa kuwa mpasuko kutokana na uchaguzi wa ndani ya chama.
Kanda2,jitahidi kuwapunguzia wasomaji usumbufu.Mara mojamoja u-BAK sio mbaya.By the way,sijaona jipya wala cha mno humo.