CHADEMA mwendo mdundo

hivi wewe mbona unawashwa san na mambo ya CHADEMA??kama unapenda siasa si uanzishe chama chako.personally unini bore sana.Unakuwa kama voyeur ...kazikuchungulia mambo ya watu

Duh,mzee nimecheka kama mwehu hapa...........nimekumbuka yule jamaa mwenye majibu ya hovyohovyo
 

Mzoefu wa kuua vyama Mrema, na yeye pia ameona kasheshe la CHADEMA lakini bwana mdogo Mnyika anatuambia eti mambo yote shwari, who do you think you are lying to. For CHADEMA to survive, just like the original NCCR, Mbowe and Mtei had to go.

you people why dont you give CHADEMA a break..by the way kikifa au kisipokufa inawahusu nini ?hamkuwepo kilipokuwa kinaanzishwa then what is the issue here???
 
The party should be the star and not the individuals. Tuchukulie mfano CCM. CCM ina uwezo wa kumimamisha mgombea asie julikana na akashinda. Najua kuna watu watasema wizi nk but CCM haiibi mara zote na in some cases hai hitaji kuiba. Sasa mtu akisha kua maarufu kuliko chama ndiyo watu wanapo kosa pumzi waki sikia anaondoka. Naamini Chadema inaweza kuwepo bila Zitto.
 

Mpasuko wazidi kuiandama Chadema kwa fununu za kuhamwa zapamba moto

Na Peter Edson
WAKATI uongozi wa Chadema ukisisitiza kuwa hali ni shwari na kwamba, Naibu Katibu wake Mkuu, Zitto Kabwe hakusudii kukihama chama hicho; hali ndani ya chama hicho inadaiwa kuwa bado ni tete.

Habari zilizopatikana zinaeleza inawezekana idadi ya watu wanaondoka ndani ya chama hicho ikaongezeka kutokana na kuzidi kuongezeka kwa ufa miongoni mwa wanachama.

Hata hivyo uongozi wa chama hicho umesema Katibu Mkuu Msaidizi, Zitto Kabwe haondoki Chadema.

Kaimu Katibu Mkuu ambaye ni Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Chadema, John Mnyika alisema jana kuwa chama hicho kiko imara na hakikusudii kumfukuza mwanachama yeyote na kwamba Zitto bado ni kiongozi wao.

“Chama hakiwezi kuyumba kwa namna yoyote ile na kipo tayari hesabu zake zikaguliwe na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali,” alisema na kuongeza kuwa hakuna kiongozi yeyote aliyefukuzwa uanachama ndani ya chama bali wapo waliojiondoa.

Mnyika alisema viongozi wake wa juu ambao ni Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa ni wasafi, hivyo hawapaswi kuchafuliwa wala kuchonganishwa na wananchi.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa kuna baadhi ya watu ndani ya chama hicho wanaowaunga mkono wanachama waliojiondoa hivi karibuni kwa madai kuwa waliwekewa mazingira magumu ya kuwafanya kujiondoa.

Kutokana na hali hiyo, viongozi wa juu wa chama hicho wanahaha kuweka mambo sawa ili kumaliza tofauti hizo za kimtizamo zilizojitokeza.

Mwasisi wa chama hicho, Edwin Mtei alipoulizwa jana kutoa maoni yake kuhusu hali ndani ya chama hicho alisema yuko safarini kuja jijini Dar es Salaam.

Hivi karibuni aliyekuwa ofisa wa habari wa chama hicho aliyeondolewa katika nafasi hiyo na uongozi, David Kafulila na mshirika mwingine mkubwa kisiasa wa Zitto Danda Juju, wamekikimbia chama hicho.

Wakati akitangaza kukihama chama hicho, Juju alikitupia kombora chama hicho na kumtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kukagua hesabu za chama hicho kwa tuhuma za ufisadi wa ruzuku.

Kujitoa Chadema kwa mshirika huyo wa Zitto ambaye alikuwa ni Ofisa Mwandamizi wa Bunge na Halmashauri, kumetokea wakati inadaiwa kuwa Kafulila na Juju walikuwa na watu wengine wanaowaunga mkono ndani ya chama hicho ambao wanaweza kuondoka wakati wowote.

Alisema amelazimika kutoa taarifa hiyo ya ufafanuzi baada ya kutokea kwa mfululizo wa habari zenye kujaribu kuhusisha maamuzi hayo na uchaguzi wa ndani wa chama uliofanyika mapema Septemba mwaka huu.

Hata hivyo, akizungumza na Mwananchi Jumapili kwa njia ya simu jana, Kafulila alimpongeza Danda kwa uamuzi wake wa busara wa kukihama chama hicho na kudai kuwa kitaendelea kumeguka kutokana na kuendeshwa kama kampuni.

“Wamiliki wa chama siku zote ni wanachama na si mtu binafsi, unapoona chama kinaanza kuongozwa kwa sera za mtu binafsi ujue kuwa hizo ni dalili za kuzikwa,” alisema Kafulila.

Alisema hawezi kuongelea jambo lolote kuhusu Naibu Katibu mkuu wa chama, Kabwe kwani anaamini kuwa uamuzi wa yeye kuendelea na chama upo mikononi mwake, hata hivyo alisema kuwa Zitto atafanya maamuzi ambayo yatakuwa sahihi.

“Sisi tumefanya kazi na Zitto kwa umakini mkubwa sana, lengo letu lilikuwa ni kukuza chama kwa namna yoyote ile, tuna imani kuwa jambo hili lililotufika linamuumiza sana, hawezi kulifumbia macho, tunaamini kuwa atafanya maamuzi sahihi,” alisema Kafulila.

Alisema ufike wakati viongozi waandamizi wa Chadema waelewe kuwa chama hicho kinapita katika wakati mgumu hivyo kama wasipokuwa makini na kuhakikisha kuwa wanakifanya chama kiwe mali ya wanachama basi kitapoteza muelekeo.

“Mimi si mtabiri, lakini vitendo vinavyoendelea vinaonyesha dhahiri kuwa Chadema kipo katika njia panda,” alisema Kafulila.

Mwanachama mmoja wa chama hicho ambaye hakupenda kutajwa jina lake alionya kuwa iwapo viongozi wa juu wa chama hawatamaliza tofauti hizo chama kitameguka.

Mnyika hata hivyo, aliziponda shutuma zilizotolewa na Kafulila katika mkutano wake na waandishi wa habari Novemba 18, mwaka huu kuwa Chadema kimejaa uovu na kwamba kutenguliwa kwa uteuzi wa Kafulila na Danda hakutokani na sababu zozote bali kulifanywa na katibu mkuu wa chama baada ya wao kukiuka kanuni, maadili na itifaki Mnyika anaongeza kuwa tuhuma hizo za uongo dhidi ya chama na viongozi wake wamezitoa baada ya kutenguliwa uteuzi wao, hivyo Izingatiwe kuwa kikatiba, maofisa wa chama si wajumbe wa sekretarieti ya chama wala kamati kuu ya chama.

Alisema Chadema haijawahi kujadili wala kufikiria kumfukuza Zitto uanachama na viongozi wa chama wamesisitiza kuwa hivi karibuni kuwa hakuna mvutano wala makundi ndani ya chama hivi sasa kwa kile kinachodaiwa kuwa mpasuko kutokana na uchaguzi wa ndani ya chama.


Kanda2,jitahidi kuwapunguzia wasomaji usumbufu.Mara mojamoja u-BAK sio mbaya.By the way,sijaona jipya wala cha mno humo.
 
mi sijaelewa the whole concept ya Zitto kuondoka CHADEMA na chama kufa!! CHADEMA was there before Zitto na amekuwa maarufu kwa ajili ya CHADEMA as such hata akiondoka CHADEMA itaendelea kuwepo tu..na aondoka bana
 
Chama chochote madhubuti kina uwezo wa kutambua wanachama makini wenye potential waka wanadi kwa wananchi na waka kubalika. kwa maana hiyo haijalishi wataondoka wanachama wangapi. Labda nitoe mfano mmoja nje ya siasa. Chukulia timu ya mpira. Kama timu ya mpira ina uwezo wa kutambua wachezaji wazuri na wakaweza kuwaanda vizuri haijalishi wachezaji wangapi wazuri wataondoka bado timu itaendelea kuwa tishio. Members wengine wanakuaga extra baggae tu na wala kuondoka kwao hakuathiri chama. CCM wamehama wangapi? Tena itakua vizuri kwa Chadema kama members wasiyo loyal au wasio ndani ya chama kwa moyo mkunjufu wakaondoka.
 
Personally I'm a big fan of Chadema. I think it is a party with a lot of potential and probably the party with the most "stars" on the side of the opposition. I think Chadema can be very competitive and if they can build the party from bottom up, phase by phase, we could be seeing a two party system in Tanzania( Meaning two parties which actually have a chance to win). I'm a big fan of Chadema and as a young man I'm happy that the party is giving chances to the youths to shine.
 
sio chini ya uongozi wa Mbowe.
 

UPEO WANGU MDOGO WA KUFIKIRIA UNANIAMBIA CHADEMA KUNA FUKUTO, KUNA MGOGORO AMBAO WEWE MWENYE UPEO MKUBWA BADO HUJAUONA, Hivi wewe unatumia vigezo gani kumshusha ZITTO kuwa hana uwezo wa kuongoza chama kama Chadema kisichofata Demokrasia. Nadhani huna sababu hata moja zaidi ya ushabiki tu na labda kuwa na personal interest zako/zenu
nipe sababu nyingize za kumuwekea Zengwe Zitto na sio sifa za kuongoza Chama, hapo ntakuelewa,
Kama Mbowe anaongoza chama itakuwa Zitto bwana!
 
hivi wewe mbona unawashwa san na mambo ya CHADEMA??kama unapenda siasa si uanzishe chama chako.personally unini bore sana.Unakuwa kama voyeur ...kazikuchungulia mambo ya watu

Huyo Kanda2 pia nadhani ni wale wanaoondoka chadema!!! nduguye kafulia na jujuman!!
 

Jujuman ana matatizo makubwa... namuona ana tabia za nyumba ndogo!!! akiwa na mzee makeke, akiachwa oh mzee, oh hana pesa oh mke wake hivi

Jujuman kafulia
 

Watz wote hasa wapenda demokrasia hawana haja ya Uongozi wa Kitaifa wa CHADEMA kuja hapa JF kujaribu kupindisha ukweli wa mambo ulivyo:Ukweli ulio wazi ni kuwa kwenye chama cha CHADEMA kama haupo kwenye kambi ya Mbowe basi wewe utachukuliwa kama ni mhaini na UTATAFUTIWA MGOGORO ili uvuliwe madaraka yako yote!

Wanashindwa kumvua madaraka Zitto Kabwe maana wanaogopa nguvu za UMMA hasa ripoti ya RIDET iliwatisha;anyway wewe Mnyika kwa sasa upo salama kwa nafasi uliyonayo,lkn ukija kukosana na Mbowe na wewe utalia kama akina Kafulila!

Yaani CHADEMA
 
Hivi huyo Kafulia na Juju wakijitoa halafu Chama kinaingiza wanachama wapya 2000 Busanda, Moro, Kigoma, nk. faida iko wapi? Wenye kuendekeza njaa wasitufanya tuumize vichwa kujadili matendo yao
 

Ibara yako kuhusu Rostam kuivuruga CCM: Ni yeye huyu huyu Rosatam anaivuruga Chadema kwa kuwahonga akina Zitto, Kafulila nk mapesa ili wawakoroge akina Mbowe na Slaa. Haihitaji mtu kuwa na PhD kujua sababu yake -- ni kwamba akina mbowe na Slaa wamewaumbua sana mafisadi na hasa kinara wao Rostam katika kufichua maovu yao dhidi ya Watanzania.Rostam anataka kuonyesha kuwa viongozi wa juu wa Chadema si lolote kwa matumaini kuwa hoja zao dhidi ya ufisadi wake (Rostam) hauna mashiko na hivyo yeye yuko safi tu. Rostam anatumia pesa nyingi sana alizowaibia Watanzania kutimiza azma hiyo, hivyo tunajikuta Watanzania tunakaangwa kwa mafuta yetu wenyewe. Akina Kafulila ni sisimizi tu Chadema lakini Rostam anatunia pesa kuwakuza.Kweli: Miafrika ndivyo ilivyo!!!!!
 
Kamanda mara nyingi nakukubali (sio mara zote) kwa kuutwanga ukweli kama ulivyo. Hapa umepiga kichwani kabisa.
 
mi sijaelewa the whole concept ya Zitto kuondoka CHADEMA na chama kufa!! CHADEMA was there before Zitto na amekuwa maarufu kwa ajili ya CHADEMA as such hata akiondoka CHADEMA itaendelea kuwepo tu..na aondoka bana
Kigogo,jambo la ajabu ni kuwa Zitto mwenyewe ametamka hadharani kuwa haondoki Chadema kwani Chadema kwake ni zaidi ya Chama.
Sasa hao wanaopiga kelele kuwa Zitto yuko njiani kuondoka Chadema ni nani kwake? ni wake zake? mbona hajaoa yeye? maana mwanaume anaweza kuweka msimamo wake hadharani lakini chumbani akatamka vingine, mambo ya chumbani tunayajua. Naona upuuzi huu umezidi sasa, Mwenyewe kesha tamka basi, akiamua kubadili msimamo na kukana kauli zake atafanya hivyo mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…