Pre GE2025 CHADEMA mwombeni Rais Donald Trump ku-push hoja yenu ya uchaguzi huru na haki

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
🌤️🙋‍♂️✍️🎯👏👌👍👊🤝🙏🆒
 
Mabadiliko ya nchi yanaletwa na wananchi wenyewe!
Kama wananchi wanaogopa virungu harafu wanatarajia mtu mwingine aje awapiganie hiyo sahau!
US yuko bize na mambo yake.
 
Chadema imeshuka kiushawishi, mwaka 2020 ilikua 20% mwaka 2025 ina 10%.
Muhimu ni kuongeza ushawishi kwa wananchi, hizo zingine ni kelele za chura tu
 
Hawezi kuwasikiliza

Tuko against ushoga
 
Sisi tuna nchi yetu na wao wana nchi yao wasitupangie CCM DAIMA SAMIA MITANO
 
Ni bahati mbaya sana kwa Chadema kwamba Marekani ya leo ya Trump haiamini katika sera za nje. Yenyewe ina deal na mambo ya ndani tu. Na mbaya nyingine sijui kama Trump anawajua Chadema.
 
Hoja yangu ni kutafuta influncial people, na nchi na sio kutegemea tu nguvu ya Tanzania BAdo sana ,uchawa umeota mizizi kila kona ya nchb
Badala ya kutafuta influential people kwanini tusiondoe tatizo la uchawa? Yaani matatizo yetu tuyakwepe tukatafute msaada nje? Kama sio utumwa ni nini sasa?
 
Unaona eee. Nguvu ya kuzuia uchaguzi kwanini usiitumie kushinda?
 
Upo sahihi mkuu, shida ni uchawa ndani Tanzania, inahitajika elimu ya kizalendo sanaaaaaaaaa
Mkuu kwa jinsi Trump anavyoidharau Africa sioni anaingiliaje noma ya hapa kwetu. Na kwa taarifa yako unaweza kukuta hata Trump hajui kuwa kuna nchi inaitwa Tanzania. Na hata kama anajua ipo anajuwa wote ni manyani kuanzia viongozi, hadi wanaotawaliwa. Inshort anachukia watu weusi kuliko kawaida.
 
Ni kweli mkuu anachukia kwa sbb ya akili za viongozi wa afrika, wanaiba fedha ndani ya nchi zao wanaenda kuficha marekani, ,hoja yangu ni kuwa nguvu ya uma kwa Tanzania kuweza kuzuia uchaguzi ni ngumu sana, ksbb ya uchawa, na kukosa elimu ya uzalendo.ni muhimu kutafuta nchi rafiki kuinga mkono chadema na sio kutegemea nguvu ya uma, kwa Tanzania hii, never ever, ladba miaka 50,ijayo
 
Unaona eee. Nguvu ya kuzuia uchaguzi kwanini usiitumie kushinda?
Kabisa mkuu, kama anaweza kuzuia uchaguzi basi anaweza kushinda pia simple logic, chadema kwa sasa wangejikita kujimalisha CHAMA katk mioa yote,
 
Upo sahihi mkuu, kuondoa uchawa, maana yake ni kupata katiba mpya ndo suluhisho , lakin chadema wamekulupuka sana, juu ya hii hoja no reform no election, mpaka sasa vyama vyote vimetangaza wagombea urais BAdo chadema tu
 
Hakuna NCHI RAFIKI duniani. Nakukumbusha. HAKUNA NCHI RAFIKI DUNIANI.
Pili nguvu ya umma pekee ndio inaweza kufanya mabadiliko. Mwaka 2014 wananchi wa Burkina Faso waliandamana na kufanikiwa kumtoa madarakani Blaise Compaoré muuaji wa Thomas Sankara. Kama wa Burkinabé wangetegemea nchi rafiki, Compaoré angeendelea kuwanyonya hadi leo. Jifunze kwa raia wa Burkina Faso waafrika wenzio.
 
Kwanini tusijikite kuelimisha raia ili wawe tayari kupambania haki zao? Hiyo ndo njia pekee ya mafanikio ya uhakika. Kutafuta wageni watusaidie ni short cut na siku zote short cut is a wrong cut. Ukraine walisaidiwa na Marekani mwaka 2014 kumtoa madarakani Rais wao, nadhani umeona matokeo ya msaada wa Marekani kwa Ukraine.
 
Hahahahahah, na sio watanzania, ambao wakihojiwa tu na polisi wanatetemeka, je kuandamna? Never ever, labda baada ya miaka 20 ijayo,. Watanzania wamefungwa sana kaitka swala la kupigania haki, hilo halipo mkuu,ndo maana unakuta tunamwachia chadema pekee, jambo la kitaifa, Tanzania kuna shida mkuu, elimu ya kupigania haki ni ndogo sana
 
Triump alivyokuwa mbabe usishangae anawafurumusha akina lissu Kwa spidi ya mwendokasi
 
Dawa ni kuondoa huo uoga na sio kwenda kujipa utumwa wa hiari kwa kutafuta msaada. Kama hatuwezi kuondoa uoga basi tusilalamike , tufurahie matunda ya uoga wetu.
 
Dawa ni kuondoa huo uoga na sio kwenda kujipa utumwa wa hiari kwa kutafuta msaada. Kama hatuwezi kuondoa uoga basi tusilalamike , tufurahie matunda ya uoga wetu.elimu

Dawa ni kuondoa huo uoga na sio kwenda kujipa utumwa wa hiari kwa kutafuta msaada. Kama hatuwezi kuondoa uoga basi tusilalamike , tufurahie matunda ya uoga wetu.
Hapo ndo shida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…