Pre GE2025 CHADEMA mwombeni Rais Donald Trump ku-push hoja yenu ya uchaguzi huru na haki

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mleta mada una shida sana. Wasubirini Democratic muwapelekee huo ujinga lakini kwa Trump sahau hiyo biashara, yaani aache kuhangaika na mambo ya nchini kwake aje kukusaidia wewe?
Trump hana haja ya democracy kwa nchi yake,atakuwaje mfuatiliaji wa democracy Tanzania?Futa kauli zenu za kutafuta vijimisaada vya kutunza familia zenu kwa jina la ubakaji demokrasia nchini kwetu.

Labda mpe deal za kuuza madini yote ya nchi ili muwe watawala kama Moitse Tchombe wa Congo enzi za Lumumba. Lakini hamtaweza Tanzania inayolindwa na kutetewa na mataifa makubwa ikiwemo China.
 
Hawezi kuwasikiliza

Tuko against ushoga
Zelensky analazimishwa akubali Dili la Madini yaliopo huko Ukraine kama anataka aendelee kupewa misaada !
Maana yake ni kwamba Amerika wanachoangalia zaidi ni maslahi yao.

Kwahiyo kama umeshawapa wanachokitaka kutoka kwako basi hawawezi kuingilia mambo yenu ya ndani !!
Ukiwanyima wakitakacho wanakuondoa madarakani kwa namna yeyote ile !!

Na ndio maana halisi ya hii Demokrasia waliotuletea Nchi hizi zetu masikini !

Ukitaka mubaki fanyeni moja mbili tatu !
Mkikataa mnang’ooka kisha mahasimu wenu wanashika hatamu 😂😂🤣😅

Mbona huko Uarabuni hawalazimishi Demokrasia ??!
Kwa sababu makampuni yote yanayochimba mafuta ni yao 😳🙄 !
Na wanapata kila kitu wanachokitaka huko !
 
Awamu ya tatu na ya Nne baliingia mikataba nyonya damu na Bazungu Barrick na wenzao !
Anko Magu akasema TUMEPIGWA !!
Akasema amekubaliana nao waongeze asilimia Angalau ziwe asilimia 16 badala ya asilimia 3 % 😳🙄😱 !

Kwahiyo kwetu sisi huku hakuna matata nao mambo ni poa tu 😅🤣🤣🤣 !
 
Watu hawajifunzi mbona Saudi Arabia hawapelekewi demokrasia? Mbona Mobutu dikteta alikuwa rafiki wao kipenzi? Mbona CIA iliongoza mapinduzi yaliyomtoa Kwame Nkrumah madarakani ? Kuna watu wanadhani eti Marekani inajali demokrasia, wanaamini maneno ya BBC na VOA. Wangejua Marekani haijawahi kujali demokrasia wangefuta haya mawazo. Kule Marekani watu wanaomchagua Rais wako mía mbili, hiyo ndo demokrasia?
 
Tungekuwa na vijana wazalendo ndani ya JWTZ wa kaliba ya Ibrahim Traore ndiyo wangeweza kuondoa huu ufedhuli wa CCM kwani kwa misingi waliyejiwekea CCM hawawezi kuondolewa kwa kura kwani wameondoa thamani ya kura, chaguzi zinazofanyika ni hadaa kwa dunia tu kuwa kuna uchaguzi. Ni mtutu wa bunduki tu ndiyo utaiondoa ccm madarakani.
 
Ameshindwa kumwelewa Zelensky mwenye kumiliki rasilimali kubwa Lissu fukara ataweza ht kukaa na Trump?
 
Upo sahihi mkuu, ni kwa sbb viongozi wa afrika hawezi kuwaongoza watu,wafrika akili zao ni za mbuzi, wafrika hawezi kujitawala wenyewe, uchawa kila kona,sio viongozi wa dini, sio wasomi, Mungu atusaidie
We ni mwafrika?
 
USA hawana muda na mudomoozzzz

Wanataka progress
 
Kuu za bandali na ngorongoro ni Sawa eti?
 
Kama taifa kuruhusu chama cha upinzani kijione hakina msaada ndani ya taiFa lake wHadi kiombe msaada nje ni kufeli kwa idara!!
Idara ndio inatakiwa ilee upinzani ili itoe changamoto Kwa chama tawala!

Ifikie hatua idara isaidie upinzani uaminike Ili kukipumzisha chama tawala kipate muda wa tafakuri na kufanya remedy kabla hakijashikishwa Dola tena!

Hii ni kwa ustawi wa taifa na sio chama tawala!taifa na jamhuri ni kubwa kuliko chama Cha siasa!!jamuhuri na taifa vilianza kabla ya chama chochote Cha siasa!!

Tumakinike!!
 
Ccm watakujakuondoka kwa nguvu ya uma, baada ya miaka 30, kizazi kingine na sio hiki cha uchawa,
 
Idara ipi?
 
Ni sahihi mkuu, lakini idara hii imemezwa na mfumo wa uccm na uchawa, wapo kwa ajili ya ccm na sio Taifa something which is very bad
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…