Uchaguzi 2020 CHADEMA na ACT-Wazalendo kutangaza kujitoa kwenye nafasi za Ubunge na Udiwani walizoshinda

Uchaguzi 2020 CHADEMA na ACT-Wazalendo kutangaza kujitoa kwenye nafasi za Ubunge na Udiwani walizoshinda

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Posts
33,895
Reaction score
20,392
Wadau, amani iwe kwenu.

CHADEMA na ACT-Wazalendo sasa wamevurugwa. Wamechanganyikiwa na wamevurugikiwa na akili. Kuna msemo unaosema kuwa ukiwa na hasira au furaha iliyopitiliza usifanye maamuzi yoyote makubwa. Hilo CHADEMA hawajalizingatia.

Ni hivi, nimedokezwa na Wasiri wangu wa Kuaminika ndani ya CHADEMA na ACT-Wazalendo kuwa pamoja na mambo mengine kwenye kikao chao cha leo pale Mtaa wa Ufipa kwenye kijibanda cha Makao Makuu ya CHADEMA wanatangaza kujiondoa kwenye nafasi zote za Udiwani na nafasi moja ya Ubunge waliyoshinda kwenye uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020. Tayari Mbunge wa Nkasi, KHENANI ameshawishiwa kujiondoa na amekubali na anachosubiri ni tamko la leo.

Hayo yatakuwa maamuzi mabaya sana kuweza kuchukuliwa na vyama vya upinzani. Kususa kwao uchaguzi wa Serikali za mitaa uliopita ndio umeleta Anguko Kuu kwenye uchaguzu Mkuu wa mwaka huu. Ni dhahiri kwamba maamuzi hayo yanaenda kuvifuta kabisa vyama hivyo kwenye ulingo wa siasa hapa nchini.

Sisi tunawachora tu kwa pembeni na tunawacheka Kwi kwi kwi kwiiiiii
 
Usichojua ni kwamba UONGOZI ni mchakato usio na mwisho, uhalali wa kiongozi unatokana na uwepo wa uchaguzi huru na haki, ushiriki wa watu katika mazingira ya usawa. Kwa aina ya uchaguzi huu, vyema wakajitoa kabisa nafasi hizo, CCM itimize azma yake ya kuleta maendeleo kwenye majimbo bila kikwazo.
 
Hasira hasara ndiyo mjue kuwa hivyo siyo vyama mtu umehangaika kupiga kampeni umetumia garama halafu mpumbavu mmoja anakuja kukuambia ujivue ubunge uliopata karibuni CCM wabunge wateule tutawarudisha tena bungeni
 

Kwa matokeo haya, uongozi mzima wa CHADEMA unapaswa kujitathmini na kuachia madaraka
 

Kwa matokeo haya, uongozi mzima wa CHADEMA unapaswa kujitathmini na kuachia madaraka
Usijaribu kuficha upuuzi wenu kwa kupeleka lawama kwingine, shame on you all.
 
hasira hasara ndiyo mjue kuwa hivyo siyo vyama mtu umehangaika kupiga kampeni umetumia garama halafu mpumbavu mmoja anakuja kukuambia ujivue ubunge uliopata karibuniccm wabunge wateule tutawarudisha tena bungeni
Ungekuwa na akili ungemwona mpumba mmoja anaezuia wenzake walioshinda na waliofanya kampeni kwa gharama zao wasitangazwe. Jifunze kugeuza shingo 360°
 
Ninachokijua mimi kuna madiwani hawatajitoa, kuna jamaa namfahamu kapambania udiwani kwa awamu tatu bila mafanikio, awamu hii kapata unafikiri huyo mtu atakubali umpokonye tonge mdomoni?

Thubutuu
 
Wadau, amani iwe kwenu.

CHADEMA na ACT Wazalendo sasa wamevurugwa. Wamechanganyikiwa na wamevurugikiwa na akili. Kuna msemo unaosema kuwa ukiwa na hasira au furaha iliyopitiliza usifanye maamuzi yoyote makubwa. Hilo CHADEMA hawajalizingatia.

Ni hivi, nimedokezwa na Wasiri wangu wa Kuaminika ndani ya CHADEMA na ACT Wazalendo kuwa pamoja na mambo mengine kwenye kikao chao cha leo pale Mtaa wa Ufipa kwenye kijibanda cha Makao Makuu ya CHADEMA wanatangaza kujiondoa kwenye nafasi zote za Udiwani na nafasi moja ya Ubunge waliyoshinda kwenye uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020. Tayari Mbunge wa Nkasi, KHENANI ameshawishiwa kujiondoa na amekubali na anachosubiri ni tamko la leo.

Hayo yatakuwa maamuzi mabaya sana kuweza kuchukuliwa na vyama vya upinzani. Kususa kwao uchaguzi wa Serikali za mitaa uliopita ndio umeleta Anguko Kuu kwenye uchaguzu Mkuu wa mwaka huu. Ni dhahiri kwamba maamuzi hayo yanaenda kuvifuta kabisa vyama hivyo kwenye ulingo wa siasa hapa nchini.

Sisi tunawachora tu kwa pembeni na notunawacheka Kwi kwi kwi kwiiiiii

Wakijitoa then katika wale kumi magu atachagua wapinzani
 
Back
Top Bottom