LGE2024 CHADEMA na ACT Wazalendo nendeni mahakamani mkausimamishe Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mzalendo Uchwara

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2020
Posts
4,437
Reaction score
13,836
Kwakua mmekubali kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa na kujiingiza kwenye mtego wa kuhalalisha haramu ya CCM, basi nawashauri tumieni mbinu zote halali kudai haki yenu.

Nendeni mahakani mkaiombe mahakama mambo yafuatayo.

1. Uchaguzi usimamishwe mpaka kasoro kubwa zilizojitokeza zitatuliwe.

2. Pelekeni orodha ya kasoro zilizojitokeza na kuiomba mahakama iiamuru TAMISEMI ( Mkwe mwenye kifua kipana ) izitatue kasoro zote na kuipelekea mahakama ushahidi ndipo uchaguzi uendelee.
 
Tangu mwanzo mahakama ilikwisha jionesha upande iliyoko.
 
Unatwanga maji kwenye kinu unaowashauri wala hawana habari wanajuw atayari wameshashindwa uchaguzi
 
Hicho wangekifanya tangu mwanzo
 

Kangaroo Courts.

Wala haitasaidia kitu.
 

Attachments

  • Screenshot_2024-07-16-21-00-20-1 (1).png
    420.8 KB · Views: 4
  • 20240907_095744 (1).jpg
    116.1 KB · Views: 1
  • IMG-20200726-WA0000.jpg
    43.7 KB · Views: 3
  • 5810871-156c33252d331784831e630b50148deb.mp4
    2 MB
  • 5811523-6041f5af6e2b5c7600d07027005d6658.mp4
    3.7 MB
Waende Mahakama ya Kenya au Tanzania? Tuanzie hapo kwanza, maana huenda umesahau kuwa hii nchi inaitwa Tanzania sio Kenya au South Africa
 
Chadema na ACT wanaweza kuungana msibani pekeyake, na sio kwenye mambo mengine gentleman πŸ’
 
You can't be serious, huko mahakamani si ndio wengine walienda kuizuia Tamisemi isisimamie huu uchaguzi na ikawa hola? Unatoa wapi imani na mahakama, wakati inategemea maagizo toka serekalini?
 
You can't be serious, huko mahakamani si ndio wengine walienda kuizuia Tamisemi isisimamie huu uchaguzi na ikawa hola? Unatoa wapi imani na mahakama, wakati inategemea maagizo toka serekalini?
Sasa kwanini wamekubali kushiriki huo uchaguzi? Ukiamua kupambana basi pambana mpaka mwisho.
 
Hakuna tatizo
Uchaguzi upo kama kawaida, hayo matatizo ya kutengeneza mnayajua wenyewe
 
Kwa watoa hukumu wa dunia ya teuzi,kamwe haitatokea tanzania.
 
Waende Mahakama ya Kenya au Tanzania? Tuanzie hapo kwanza, maana huenda umesahau kuwa hii nchi inaitwa Tanzania sio Kenya au South Africa
Wameamua kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa Tanzania unaosimamiwa na wizara iliyo chini ya mkwe wa mwenyekiti wa CCM, basi hawana ku exhaust option zote zilizopo mezani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…