LGE2024 CHADEMA na ACT Wazalendo nendeni mahakamani mkausimamishe Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Haa mnanikumbusha zidumu fikra za Muumba wetu
 
Mahakama zipi au mfumo uliopo wa kudhibiti wananchi kufurahia utawala wa kidemokrasia hauoni.Rejea kesi zilizoamriwa na mahakama ikiwepo ya covid 19
 
CCM walishasema kuwa hawawezi kuondolewa madarakani kwa njia ya kura na wataendelea kutumia dola(ikiwepo Mahakama) kuendelea kutawala. Ila ni vema tu kufungua kesi Mahakamani ili kuweka record vizuri kwani itafika tu wakati zitumikie njia nyingine mbadala na kesi hizi ambazo zitakuwa zimeamuliwa kwa maelekezo toka kwa Mwenyekiti wa CCM zitakuwa ushahidi kuwa njia zote za kistaarabu zilitumika kutafuta haki.
 
Moshi wa mwenge kazini!!
 
Moshi wa mwenge kazini!!
Heshimu mwenge kijana, ni alama ya taifa.

Ukiachana na hilo unadhani suluhu ni nini? Kususa?? Au kuwalilia mabeberu?

Huko US beberu Trump hataki shobo, sera yake ni America first. Wangine pambaneni na hali zenu.
 
Mahakama zipi au mfumo uliopo wa kudhibiti wananchi kufurahia utawala wa kidemokrasia hauoni.Rejea kesi zilizoamriwa na mahakama ikiwepo ya covid 19
Ni vema waende kwakuwa wameamua kushiriki. Ukiamua kupambana basi pambana mpaka mwisho. Watu waone kuwa haulutendewa haki kila mahali.

Kwamba hawana imani na mahakama ila wana imani na TAMISEMI ya mkwe?
 
Naam, kufungua kesi ni muhimu. Watu wajue kuwa hakuna matumanini yoyote. Si bunge wala mahakama, vyote viko na chama tawala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…