Zion Daughter
JF-Expert Member
- Jul 9, 2009
- 8,921
- 4,240
Kuna tofauti kati ya kumjadili zitto na kujadili uanachama wa zitto. Shughulisheni bongo zenu, msilete mihemko isiyo na msingi.
Soma maneno ya dr slaa ndio utaelewa nasema nini. kwa maneno ya dr slaa ni wazi wameujadili uanachama wa zitto.
Dean, wana maanisha kuwa wao walisha ujadili uanachama wa zitto na walisha mvua uanachama kinyume na agizo la mahakama na hawajali litakalo tokea maana wao walisha fanya maamuzi.
kama hiyo thread ipo kwenye ukurasa wa zzk wa facebook mletaji atufafanulie huyo zzk ana kurasa ngapi maana nimemfollow cjaona kitu kama hicho. na kama ni kwelizzk amepost basi hakuna haja ya kuendelea kuwaamini wanasiasa kumbe wote wizi mtupu.
Huyu kaka hakuwa na haja ya kwenda mahakamani.Ameonyesha jinsi gani yupo weak bila CDM .Angeanzisha tu chama chake nadhani anepata wafuasi.Ila sasa ameonyesha udhaifu.Nadhani washauri wake wanampoteza.
mkuu MBWA WA MANZESE jaribu kumsoma lissu utagundua ninacho sema hapa.
LISSU ANASEMA KUWA ZITTO ANAENDELEA KUWA MWANA CHAMA KWA SABABU YA MAHAKAMA TUU. HAPA ANA JARIBU KUMAANISHA KUWA WAO KAMA CHADEMA WAME SHAUJADILI UANACHAMA WA ZITTO KINYUME NA AGIZO LA MAHAKAMA NA WAMESHA MVUA UANACHAMA.
HIVI KWANINI CHADEMA WAMEDHARAU AGIZO LA MAHAKAMA?
Tumewabamba hatujawabamba???TumewaChadema ni chama chenye ndoto za kushika dola na kilitegemewa kiwe chama cha kwanza kuheshimu amri za vyombo vya dola ikiwemo mahakama.
Sote tuna fahamu zitto kabwe aliweka zuio mahakamani dhidi ya kamati kuu ya chadema kujadili uanachama wake na kutokana na mwenendo wa shauri hilo mahakami, mahaka iliagiza chadema kutojadili uanachama wa mh zitto kabwe hadi mwisho wa shauri yani hukumu.
Siku ya ijumaa John Mnyika alionekana kwenye vyombo vya habari akisema hawatojadili uanachama wa zitto kutokana na agizo la mahakama na shauri linalo endelea.
Lakini cha ajabu leo kwenye kikao cha chadema na waandishi wa habari kilicho kuwa na lengo la kutoa na kueleza maazimio ya kamati kuu, wameonesha wazi kuwa wame kahidi agizo la mahakama na kuya dharau na ni wazi walijadili uanachama wa zitto.
Kurugenzi ya Habari imenukuu maneno yaliyo somwa na dr slaa ya kionesha kamati kuu imejadili uanachama wa zitto.
Na nukuu
" chama kina wataka wanachama wote na wapenzi wote kuto shiriki mikutano ,ama shughuli zozote za kisiasa zitakazo andaliwa na zitto kabwe na washirika wake kwa jina la chadema"
kwa hayo maneno hapo juu haihitaji kuwa profesa kuelewa kuwa chadema wamemjadili zitto pamoja na uanachama wake hivyo wame kahidi maagizo ya mahakama na kuyasigina kabisa kama hawatambui uwepo wake.
Hayo maneno yaliyo somwa na dr slaa leo yanaonesha kabisa chadema kuto heshimu mamlaka za nchi.
Wananchi wanatakiwa kujua hawa chadema mambo yanapo kwenda kombo kwa upande wao ndio huwa wa kwanza kusema wanaonewa.
Nimejiuliza kilicho wafanya chadema kuto subiri jumatatu baada ya hukumu ndio wajadili uanachama wa zitto?
Hivi kwanini mh Tundu Lissu unashindwa kuwa mshauri mzuri kwa chama chako?
Chadema kwa hili la leo ni dharau kubwa kwa mahakama.
Karibuni wana jamvi.
Jaribu kufikiri vizuri, Zitto alitakiwa ajitetee mbele ya kamati kuu kwa nini asifukuzwe kutokana na ule wa waraka, lakini yeye akakimbilia mahakamani uanachama wake usijadiliwe, lakini zuio la mahakama halifuti intention ya CC ya kumfukuza Zitto chamani kama angepatikana na hatia. Najua mapenzi yako kwa Zitto yanaweza kukufanya usione ukweli kwani kila mwanadamu ni victim wa mapenzi.
Lissu hakuna alichokosea alichozungumzia ni kuwa Zitto bado ni mwanachama wa CHADEMA kwa sababu za kimahakama lakini kama zisingekuwepo angeungana na wale wenzie wawili waliofukuzwa leo na shitaka lao lilikuwa moja.
Jaribu kufikiri vizuri, Zitto alitakiwa ajitetee mbele ya kamati kuu kwa nini asifukuzwe kutokana na ule wa waraka, lakini yeye akakimbilia mahakamani uanachama wake usijadiliwe, lakini zuio la mahakama halifuti intention ya CC ya kumfukuza Zitto chamani kama angepatikana na hatia. Najua mapenzi yako kwa Zitto yanaweza kukufanya usione ukweli kwani kila mwanadamu ni victim wa mapenzi.
Lissu hakuna alichokosea alichozungumzia ni kuwa Zitto bado ni mwanachama wa CHADEMA kwa sababu za kimahakama lakini kama zisingekuwepo angeungana na wale wenzie wawili waliofukuzwa leo na shitaka lao lilikuwa moja.
Sijui Lissu alisoma cho gani.kitendo cha kuelezea hatima ya Zitto CHADEMA katika taarifa yake ya leo kitabadilisha maamuzi ya jaji.
lisu ni mlevi wa sheria na ameharibu mlengo wa kesi.
take from me.
usiku mwema.
jaribu kufikiri vizuri, zitto alitakiwa ajitetee mbele ya kamati kuu kwa nini asifukuzwe kutokana na ule wa waraka, lakini yeye akakimbilia mahakamani uanachama wake usijadiliwe, lakini zuio la mahakama halifuti intention ya cc ya kumfukuza zitto chamani kama angepatikana na hatia. Najua mapenzi yako kwa zitto yanaweza kukufanya usione ukweli kwani kila mwanadamu ni victim wa mapenzi.
Lissu hakuna alichokosea alichozungumzia ni kuwa zitto bado ni mwanachama wa chadema kwa sababu za kimahakama lakini kama zisingekuwepo angeungana na wale wenzie wawili waliofukuzwa leo na shitaka lao lilikuwa moja.