Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umeeleza vizuri sana, lakini sidhani kama Ruttashobolwa atakubaliana na wewe !
Mwanzoni nilifikiri haelewi nami nikabishana naye kwa posts kadhaa....baadaye nikaconclude kwamba hataki kuelewa kwa makusudi !
Chadema ni chama chenye ndoto za kushika dola na kilitegemewa kiwe chama cha kwanza kuheshimu amri za vyombo vya dola ikiwemo mahakama.
Sote tuna fahamu zitto kabwe aliweka zuio mahakamani dhidi ya kamati kuu ya chadema kujadili uanachama wake na kutokana na mwenendo wa shauri hilo mahakami, mahaka iliagiza chadema kutojadili uanachama wa mh zitto kabwe hadi mwisho wa shauri yani hukumu.
Siku ya ijumaa John Mnyika alionekana kwenye vyombo vya habari akisema hawatojadili uanachama wa zitto kutokana na agizo la mahakama na shauri linalo endelea.
Lakini cha ajabu leo kwenye kikao cha chadema na waandishi wa habari kilicho kuwa na lengo la kutoa na kueleza maazimio ya kamati kuu, wameonesha wazi kuwa wame kahidi agizo la mahakama na kuya dharau na ni wazi walijadili uanachama wa zitto.
Kurugenzi ya Habari imenukuu maneno yaliyo somwa na dr slaa ya kionesha kamati kuu imejadili uanachama wa zitto.
Na nukuu
" chama kina wataka wanachama wote na wapenzi wote kuto shiriki mikutano ,ama shughuli zozote za kisiasa zitakazo andaliwa na zitto kabwe na washirika wake kwa jina la chadema"
kwa hayo maneno hapo juu haihitaji kuwa profesa kuelewa kuwa chadema wamemjadili zitto pamoja na uanachama wake hivyo wame kahidi maagizo ya mahakama na kuyasigina kabisa kama hawatambui uwepo wake.
Hayo maneno yaliyo somwa na dr slaa leo yanaonesha kabisa chadema kuto heshimu mamlaka za nchi.
Wananchi wanatakiwa kujua hawa chadema mambo yanapo kwenda kombo kwa upande wao ndio huwa wa kwanza kusema wanaonewa.
Nimejiuliza kilicho wafanya chadema kuto subiri jumatatu baada ya hukumu ndio wajadili uanachama wa zitto?
Hivi kwanini mh Tundu Lissu unashindwa kuwa mshauri mzuri kwa chama chako?
Chadema kwa hili la leo ni dharau kubwa kwa mahakama.
Karibuni wana jamvi.
msome dr slaa umuelewe.
Kama ulivyo sema anasema kama isingekuwa mahakama angeunganishwa na wenzie, lakini tukubaliane kuwa kauli hiyo ina maanisha walisha ujadili uanachama wake, kama sio mahakama na yeye wange mtangaza amefukuzwa kama wenzie.
Ka ame kwenda mbali zaidi kwa kusema wana chama wasi hudhurie mikutano yake aki maanisha hawamtambui kama mwana chama maana walisha ujadili uanachama wake na kumvua uanachama kinyume na agizo la mahakama.
inawezekanaje mtu awekewe kikwazo hichi na aendelee kuwa mwana chama?
inawezekanaje mtu awekewe kikwazo hichi na aendelee kuwa mwana chama?
Jaribu kufikiri vizuri, Zitto alitakiwa ajitetee mbele ya kamati kuu kwa nini asifukuzwe kutokana na ule wa waraka, lakini yeye akakimbilia mahakamani uanachama wake usijadiliwe, lakini zuio la mahakama halifuti intention ya CC ya kumfukuza Zitto chamani kama angepatikana na hatia. Najua mapenzi yako kwa Zitto yanaweza kukufanya usione ukweli kwani kila mwanadamu ni victim wa mapenzi.
Lissu hakuna alichokosea alichozungumzia ni kuwa Zitto bado ni mwanachama wa CHADEMA kwa sababu za kimahakama lakini kama zisingekuwepo angeungana na wale wenzie wawili waliofukuzwa leo na shitaka lao lilikuwa moja.
endelea na kunukuu mpaka wataja kunukuu na wewe mwenyewe ila mkae mkijua mtu wenu huyo zito ndiyo kafyekwa miguu,mkitaka na kama mnampenda kweli mchukue ili tuje kushuhudia mnavyoweza kwenda naye na siasa zake za usaliti-kama hataishia kum-kolimba.
Ukiwa na chama kama CHADEMA huweki kiamini ukakipa dola....hawana msimamo
Kesho wameisha, hawawezi kuendelea kudharau Katiba ya Nchi na amri ya mahakama
Haya ndio aliyosema Zitto kuhusu fisadi Mbowe."Lissu anasema nimepewa magari
2 na Mzee Mkono. Anasema
kaambiwa na Mkono. Naamini
Mkono alimwambia pia mwaka
2005 alimpa Freeman Aikaeli
Mbowe tshs 40m ili Mbowe
asifanye kampeni Musoma vijijini.
Nadhani alimwambia pia mwaka
2008 (baada ya orodha ya
mafisadi kutangazwa 2007) Mkono
alimpa Freeman tshs 20m za
uchaguzi wa Tarime na Freeman
akasema kwenye chama ametoa
mkopo na akalipwa. Nadhani
alimwambia pia kuwa Mwaka 2010
Mkono alimpa Mbowe tshs 200m
za kampeni ya Slaa. Pia
hakusahau kumwambia kuwa
Rostam Aziz alimpa Mbowe tshs
100m za kampeni. Lissu anajua
kuwa gazeti la Tanzania Daima
limeanzishwa na fedha za chama
kutoka Conservative party?
Nimefanya internship yangu kwa
Mkono and Company Advocates
kuhusu masuala ya mikataba.
Mzee Mkono ni Mzee wangu na
alisaini petition ya kumtoa Waziri
Mkuu Pinda.
Lissu awaambie waliyemtuma
wamwambie ukweli wote. Lissu
ajue yeye ni kifaranga tu, Mimi
namtaka mama wa kifaranga
ajitokeze. Aeleze aliingia deal gani
na Kinana na Sumaye mwaka 2005
kufuatia deni lake NSSF. Aweke
wazi mkataba kati yake na NHC
kuhusu nyumba ya Umma ilipo
Club Bilicanas.
They must know I am not a push
over. Chacha died, I won't.
Mtu ambaye hawezi kuheshimu
mke wake aliyemzalia watoto
hawezi kunyooshea mtu kidole
kuhusu maadili
mkuu asante kwa kuonesha na wewe umeungana nami kukubali kuwa chadema wameidharau mahakama.
Jaribu kufikiri vizuri, Zitto alitakiwa ajitetee mbele ya kamati kuu kwa nini asifukuzwe kutokana na ule wa waraka, lakini yeye akakimbilia mahakamani uanachama wake usijadiliwe, lakini zuio la mahakama halifuti intention ya CC ya kumfukuza Zitto chamani kama angepatikana na hatia. Najua mapenzi yako kwa Zitto yanaweza kukufanya usione ukweli kwani kila mwanadamu ni victim wa mapenzi.
Lissu hakuna alichokosea alichozungumzia ni kuwa Zitto bado ni mwanachama wa CHADEMA kwa sababu za kimahakama lakini kama zisingekuwepo angeungana na wale wenzie wawili waliofukuzwa leo na shitaka lao lilikuwa moja.
mkuu acha vituko. Asante kwa kuonesha mmetubamba kwa kukahidi agizo la mahakama.
Kama hauna cha kuandika bora ukalala maana kila siku naona maneno ya namna hii yanajirudiarudia,sasa buku saba inahusiana nini na topic hii au ndo mawazo finyu