Chadema na dharau kwa amri ya mahakama.

Hapa tunacho jadili ni kauli za viongozi wa chadema na wameyaongea na wewe umesikia kabisa na ni wazi wame ujadili uanachama wa zitto.

Hata kama unavyodai Chadema imekiuka amri ya Mahakama, hivi nikuulize kwa akili yako fupi Mahakama inaweza ikarejesha uanachama wa Zitto...?

Unajisumbua..
 
amri ya mahakama ilikuwa uanachama wa zitto usijadiliwe ...sio kila kitu kuhusu zito kisijadiliwe..

asante kwa hilo.

Sikia .
Lissu anasema zitto ataendelea kuwa mwanachama kwa sababu ya mahakama tuu. Hapo ana maanisha kuwa wao wamesha mjadili na wamesha mvua uanachama ina maana wao walisha maliza kazi.

Wakati tunajua kuwa hatma uanachama wa zitto ulitakiwa kujulikana baada ya hukumu na ulitakiwa kuto jadiliwa.

Lissu amesema tena wana chama wasihudhurie mikutano ya zitto akimaanisha kuwa hawamtambui kama mwana chama wao na hapo bila shaka waliujadili uanachama wake kwenye kamati kuu na ni kinyume na agizo la mahakama.
 
Hii thread ifungwe haina mashiko....Ni mipasho ya misukule ya Zitto..

Mods ndio watapima hili, huna sababu ya kuandika hapa tumia kitufe kureport mkuu tedo.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Rutashoshoborwa naona umeanza kukongoloka kichwani,hii ni matokeo ya kugonga valuu na viroba mapema.
 
hata kama unavyodai chadema imekiuka amri ya mahakama, hivi nikuulize kwa akili yako fupi mahakama inaweza ikarejesha uanachama wa zitto...?

Unajisumbua..

mahakama haiwezi fanya hivyo lakini hina mamlaka ya kuzuia jambo fulani lisifanyike hili kupima kwanza.

Na ikumbukwe kwamba chadema walikubali kuto ujadili uanachama wa zitto.

Lakini matamko yao yameonesha kuwa wame ujadili uanachama wake.
 
hebu rejea tamko la mnyika kwa mapana yake acha utoto!
 
Ujielewi wewe!Je mtu anapokua na nyumba au shamba,ambayo ameipangisha,alafu anaamua kuuza kesho kutwa,na mpangaji akaenda kuzuia mahakani sababu yeye kama mpangaji haki zake zimekiukwa!mahakama ikazuia,je wewe utauza nyumba tu sababu hatujui ulipataje?Jitambue,kuna taasis isiyo na katiba?
 
Soma maneno ya dr slaa ndio utaelewa nasema nini. kwa maneno ya dr slaa ni wazi wameujadili uanachama wa zitto.
mahakama iliizuia kamati kuu kujadili uanachama zitto na wamezingatia hilo ndo maana zitto bado ni mwanachadema. Tamko lile limetolewa kwenye mkutano na wanahabari. Subiri baada ya kesho km utamsikia tena huyo kibaraka wa ccm.
 
Haya ndio aliyosema Zitto kuhusu fisadi Mbowe."Lissu anasema nimepewa magari
2 na Mzee Mkono. Anasema
kaambiwa na Mkono. Naamini
Mkono alimwambia pia mwaka
2005 alimpa Freeman Aikaeli
Mbowe tshs 40m ili Mbowe
asifanye kampeni Musoma vijijini.
Nadhani alimwambia pia mwaka
2008 (baada ya orodha ya
mafisadi kutangazwa 2007) Mkono
alimpa Freeman tshs 20m za
uchaguzi wa Tarime na Freeman
akasema kwenye chama ametoa
mkopo na akalipwa. Nadhani
alimwambia pia kuwa Mwaka 2010
Mkono alimpa Mbowe tshs 200m
za kampeni ya Slaa. Pia
hakusahau kumwambia kuwa
Rostam Aziz alimpa Mbowe tshs
100m za kampeni. Lissu anajua
kuwa gazeti la Tanzania Daima
limeanzishwa na fedha za chama
kutoka Conservative party?
Nimefanya internship yangu kwa
Mkono and Company Advocates
kuhusu masuala ya mikataba.
Mzee Mkono ni Mzee wangu na
alisaini petition ya kumtoa Waziri
Mkuu Pinda.
Lissu awaambie waliyemtuma
wamwambie ukweli wote. Lissu
ajue yeye ni kifaranga tu, Mimi
namtaka mama wa kifaranga
ajitokeze. Aeleze aliingia deal gani
na Kinana na Sumaye mwaka 2005
kufuatia deni lake NSSF. Aweke
wazi mkataba kati yake na NHC
kuhusu nyumba ya Umma ilipo
Club Bilicanas.
They must know I am not a push
over. Chacha died, I won't.
Mtu ambaye hawezi kuheshimu
mke wake aliyemzalia watoto
hawezi kunyooshea mtu kidole
kuhusu maadili
 
shauri uanachama wa zitto ndani ya chadema kutojadiliwa na kamati kuu.

Agizo la mahakama lina wataka chadema kutojadili uanachama wa zitto hadi mahakama itakapo toa hukumu.

"chama kina wataka wanachama wote na wapenzi wote kuto shiriki mikutano ,ama shughuli zozote za kisiasa zitakazo andaliwa na zitto kabwe na washirika wake kwa jina la chadema"

Mkuu hiyo ni nukuu uliyoiweka kwa nia ya kutuaminisha kuwa Chadema wamekiuka tamko la mahakama.

Hivi huoni kama hilo ni agizo la Chadema kwa wanachama wake?

Hivi katika agizo hilo kuna mahali popote unapoona Mh. Zitto Kabwe anapokea shurti yoyote?

Je kwa namna gani tamko hilo linautaja na linauweka rehani uanachama wa Mh. Zitto Kabwe?
 
Kuna tofauti kati ya kumjadili zitto na kujadili uanachama wa zitto. Shughulisheni bongo zenu, msilete mihemko isiyo na msingi.

We Genius ni noma sana,yaani umebobea katika sheria,na utakuwa umesomea Harvad
 
Zitto kasema hayo maneno lini na wapi ?

Aliyeleta huu upuzi kwa mara ya kwanza alidai ameuota kwenye facebook page ya Zitto.....

Kwenye face book ya Zitto hakuna kitu kama hiki........

Sasa nyie maCCM mlivyoishiwa maneno ya propaganda (manake propaganda zote zimeshindwa kulipa), mmeamua kumwekea kipenzi chenu maneno mdomoni....poleni sana !

Na hivi karibuni tunampiga chini !

 

Upo wewe kifaranga!mlamba viatu
 
Kuna tofauti kati ya kumjadili zitto na kujadili uanachama wa zitto. Shughulisheni bongo zenu, msilete mihemko isiyo na msingi.

Ruttashobolwa did not use his head but his fingers but i think now he may start using his head.
 

Hataki kuingiza serikali katika gharama za uchaguzi mdogo
 

Ngoja mchinjane wajemeni sisi yetu macho na maskia wagalatia nyie.
 
USilete mambo ya hisia hapa, lete vielelezo, bush lawyer.
 

Mkuu,

Kwa matendo yote ambayo Zitto ameitendea Chadema, unayoyajua na usiyoyajua, ulitaka Kamati Kuu imchukulie hatua gani ili uone imefanya vema?

Zitto analijua kosa lake na anajua adhabu yake na ndio maana alikimbilia Mahakamani ili azuie asijadiliwe kwa lengo la kulinda maslahi yake binafsi

Ila..... Usiku mwema
 
Last edited by a moderator:
kama hiyo thread ipo kwenye ukurasa wa zzk wa facebook mletaji atufafanulie huyo zzk ana kurasa ngapi maana nimemfollow cjaona kitu kama hicho. na kama ni kwelizzk amepost basi hakuna haja ya kuendelea kuwaamini wanasiasa kumbe wote wizi mtupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…