CHADEMA na Heche wakivuka na hili CCM watakuja na lipi?

Lee Van free

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2024
Posts
2,833
Reaction score
8,777
Nimesema CHADEMA na Heche wakivuka na hili,maana yake wameshapitia matukio mengi ya kutengenezwa na walivuka.

Sasa limekuja hili la Heche kuzushiwa kula Hela.
Najiukiza hivi,ikiwa CHADEMA itavuka hili,na Nina uhakika itavuka kwa maana ni ushuzi TU,wala sio uzushi.

Na ikiwa Heche atavuka hili,na inshala atavuka,
Je Wazushi na watesi wao yaani CCM watakuja na lipi?
Kwa tathmini yangu ndogo naona kabisa CCM kwa kupitwa kwao na wakati bila kujua wamtangaza sana Bwana Heche,wamepelelea kumfanya Heche awe maarufu kuliko alivyokua mwanzo, Sasa hivi hata wale waliokua hawafatilii siasa kwa sana mfano wanawake, wasichana na watoto ambao bado kidogo TU kufikisha miaka 18 wameshamjua Heche ni nani na CHADEMA ni Nini.

CCM wameishiwa mbinu za mchezo.
Hapa maana yangu ni ndogo TU mwaka 2030 si mbali,na uchaguzi utakua huru na wa haki,CCM mtake mistake.

Kwa kifupi CCM kwa ujinga wamemtangaza Heche na CHADEMA mara dufu kuliko ilivyokua kabla ya kadhia hii.
Heche anaweza asiwe mgombea Urais,lkn Umaarufu wake aliopewa na CCM utamsaidia sana mgombea atakae pitishwa na CHADEMA na kuleta madhara makubwa sana Kwa CCM.

Kumbuka nimesema Uchaguzi ujao utakua huru na wa haki.
 
Riz moko hatakubali uchaguzi uwe huru na wa HAKI😀
 
CCM wanapoteza nguvu sana maana kila wanapojaribu kuficha au kuchafua sifa ya Heche, ndivyo wanavyozidi kumfanya awe viral na kupata umaarufu mkubwa zaidi kwa vijana wa Gen Z.
Na Kwa bahati mbaya hawana hata wataalam wa kutafasi alama za nyakati.
Mfano hebu ona CHADEMA ilifungiwa osifanye siasa na ikanyimwa ruzuku,walipofanya hivyo Kwa akili zao zisizoweza kutambua alama za nyakati walizani CHADEMA itadhoofika,waliporuhusu walichokuja kukuona hawakuamini macho Yao.
Maana watu walijutokeza kwa maelfu kwenye mikutano ya CHADEMA bila hata vivutio vyovyote,chakushangaza zaidi sio watu kujitokeza TU,Bali kuchangia tonetone kwenye mikutano Yao.
Hii ni tofauti ya mbigu na ardhi kati ya CCM na CDM.
Wakati CCM inawapa watu Hela ili waende kwenye mikutano Yao, CDM inapewa Hela na watu kwenye mikutano Yao kwa njia ya michango ya tonetone.
Hali hii inatisha kwa kweli.
 
Bado wanaamini monetary influence itashinda digital advocacy and grassroots movement.

Wanawekeza kwenye visibility, acha CHADEMA tuendelee kuwekeza kwenye credibility.
 
Uongozi bora huanzia ndani, heche angepisha kiti ili uchunguzi huru ndani ya chama ufanyike, kama atakuwa hajapita na bakuli la tonetone ukweli utadhihiri na ataendelea na nafasi yake!! Heche ishi unachohubiri!!
 
Riz moko hatakubali uchaguzi uwe huru na wa HAKI😀
Riz Moko ni mtu mdogo sana kwenye uso wa Dunia.
Sasa hivi mapambano ya kuikomboa nchi hii yamechukua sura mpya.
Sasa hivi mapambano imekua ni CCM against the world (jumuiya ya kimataifa).
Ni kama vile kipindi kile South Afrika against the world.
Sisi Tanzania tukiwa mstari wa mbele katika harakati za kuikomboa Afrika Kusini ya akina Mandela dhidi ya utawala wa Makaburu..
 
Bado wanaamini monetary influence itashinda digital advocacy and grassroots movement.

Wanawekeza kwenye visibility, acha CHADEMA tuendelee kuwekeza kwenye credibility.
Hizo njia za monetary influence zilishatumika sana huko nyuma sehemu kadhaa duniani,lkn hua hazidumu muda ukifika.
Kwa Tanzania Sasa hivi muda umeshafika.
Hata ndani ya chama choa tu Cha CCM zilifikia muda zikafeli pakukwa.
Unaikumbuka story ya WAJUMBE?
Kuna WAJUMBE walipokeaga Hela lakini kura wakapeleka kwa wengine.
Mgombea aliepigwa Hela yake alisikika akilalamika kua "WAJUMBE sio watu"
 
CCM wameshindwa kusoma alama za nyakati , nature itawafundisha somo hilo vyema.
Hebu fikiria CCM inamtuhumu mtu kua kala Hela,halafu wanatokea watu wakamuomba huyo mtuhumiwa awape namba yake ya Benki ili wamuwekee Hela yeye binafsi ili kama kuzila azile zaidi
Hii spirit inawatisha sana watesi wa Heche.
 
Hizo njia za monetary influence zilishatumika sana huko nyuma sehemu kadhaa duniani,lkn hua hazidumu muda ukifika.
Kwa Tanzania Sasa hivi muda umeshafika.
Hata ndani ya chama choa tu Cha CCM zilifikia muda zikafeli pakukwa.
Unaikumbuka story ya WAJUMBE?
Kuna WAJUMBE walipokeaga Hela lakini kura wakapeleka kwa wengine.
Mgombea aliepigwa Hela yake alisikika akilalamika kua "WAJUMBE sio watu"
Hili suala la kuamini wana control kwa sababu wana rasilimali ndiyo linawapoteza haswa.

Kuhusu stori ya wajumbe, nimekumbuka imebidi nicheke.
 
Uongozi bora huanzia ndani, heche angepisha kiti ili uchunguzi huru ndani ya chama ufanyike, kama atakuwa hajapita na bakuli la tonetone ukweli utadhihiri na ataendelea na nafasi yake!! Heche ishi unachohubiri!!
Kupisha kiti ndio mtego wa watesi wa Heche ulipo,akipisha nao ndio watapata nafasi ya kufanikisha malengo Yao.
Mimi nasema Heche hakuna kupisha chochote.
Ustaarabu huo ungekua na mashiko kama wale walioshika madaraka ya nchi hii wao ndio wangekua wa kwanza kupisha vitu vyao ili uchunguzi ufanyike.
Mfano.
Wale wote waliotajwa ktk ripotibza CAG tokea mwaka 2005 wangepisha nafasi zao
Wale waliotajwa ktk malalamiko ya kukodishwa kihuni kwa bandari zetu,
Waliotajwa kwenye kashfa za EPA,Kagoda ,meremeta,Tegeta Escrow,
Uingizaji wa kontena la silaha n.k
 
Hebu fikiria CCM inamtuhumu mtu kua kala Hela,halafu wanatokea watu wakamuomba huyo mtuhumiwa awape namba yake ya Benki ili wamuwekee Hela yeye binafsi ili kama kuzila azile zaidi
Hii spirit inawatisha sana watesi wa Heche.
Na watu saa hizi wanarecord video wakiwa wanachangia michango yao .

Ni kengele ya mwisho kama CCM hawaoona jukwaa limeelea upande usio wao waamke au liwaangukie .

Hizo 1000 watu wanazotoa wakiwa milioni 1 ji zaidi ya bilioni anayotoa fisadi mmoja asifuatiliwe kwenye kukwepa kodi na biashara zake haramu na hata siku upepo ukibadilika anaweza kukimbia nchi ila hao watu milioni 1 watabaki kupambana na utawala haramu.

Ghadafi alikua tajiri na aliwalipa walinzi wake vizuri , akawaita waandamanaji wanaompimga kuwa ni mende na hatokimbia Tripoli, upepo ulivyobadilika alijikuta mafichoni jangwani na walinzi wawili tu na ndio ikawa mwisho wake.
 
Hili suala la kuamini wana control kwa sababu wana rasilimali ndiyo linawapoteza haswa.

Kuhusu stori ya wajumbe, nimekumbuka imebidi nicheke.
Kwa kifupi Mkuu muda wao wa kudanganya kwa kutumia vitu kama kofia ,tisheti,Hela,vitisho umekwisha,
Kuna mabadiliko makubwa sana,kutoka kwenye kutisha watu Hadi wao Sasa kutishwa na watu.
Kitu pekee walichobakiza ni Matumizi ya mtutu.
NATO njia hii Sasa imeshawaharibikia kwa sababu nilizozitaja huko juu kwamba,harakati za kisasi haki hapa Tanzania zimesambaa kutoka Kwa watanzania Hadi kua za Jumuiya ya kimataifa.
Leo hii Kwa ujinga na upofu wao wamejikuta wanapambana na CNN,BBC,DW, Commonwealth,EU,US,ICC,Human rights organization of the world, etc,
Huko nyuma haikua hivi kwa Tanzania
Hata zamani hapa nchini pekee walikua wanapambana na CHADEMA TU,lkn Sasa hivi wanapambana na CDM + Gen Z + others.
Haya sio mambo madogo Mkuu.
 
Hakuna jipya hapa,umesahau yale ya ugaidi ya Mwigulu
Kweli kabisa ,CHADEMA ilipitia mengi mno na iikavuka.
Ukiondoa hiyo ya ugaidi wa Lwakatare,Kuna Ile ya mambomu ya Arusha,na Kuna Ile Mwigulu alimzushia Mnyika kua amemtumia meseji za kua atamuua.
Mwigulu akapelela malalamiko yake bungeni mbele ya Spika Anna Makinda.
Wakaanza kusuka mpango wa kukifuta CHADEMA.
Aliibuka Mabere Nayucho Marando akawaumbua CCM kwa kuonesha kua CCM walileta mtambo kutoka Israel unaweza kujitumia meseji.
Hapo ndipo kesi ikakoma na ndipo ukawa salama ya Mnyika.
 
Back
Top Bottom