CHADEMA na kutochukua tahadhari ya Corona katika mikutano yake

CHADEMA na kutochukua tahadhari ya Corona katika mikutano yake

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2020
Posts
12,077
Reaction score
12,786
Wameendelea kutovaa barakoa.

Ni CHADEMA hawahawa walioishinikiza serikali ya awamu ya 5 itoe takwimu za kila siku za wagonjwa wa UVIKO-19.

Ni CHADEMA hawahawa walioupinga msimamo wa jemedari Hayati Dkt. Magufuli juu ya kutowekwa lockdown nchi nzima/maeneo yenye msongamano.

Kipi kilitarajiwa kwao?

Kubwa tulilolitarajia kwao ni kuiunga mkono Serikali ya awamu ya 6 na kusimamia misimamo yao ile ya zamani dhidi ya UVIKO-19 kwa angalau kuvaa barakoa ndani ya mikutano yao ya ndani inayoendelea huko kanda ya ziwa.

Kinyume chake ni haya:

1) Mh. Mwenyekiti Mbowe havai barakoa.

2) Uongozi wa BAWACHA taifa hawavai barakoa.

3) John Heche na wenzake hawavai barakoa.

***************************

Je, huu si "Ukinyonga" na undumilakuwili wa CHADEMA?
 
Wenzako wakishaongea wanadelete hata kumbukumbu hawaachi. Hao CDM bana.
 
Tahadhari gani tena jamani? Si tumekubaliana kwa mujibu wa Mkuu mwendazake kuwa Tanzania hakuna corona? !!!!
 
Wameendelea kutovaa barakoa.

Ni CHADEMA hawahawa walioishinikiza serikali ya awamu ya 5 itoe takwimu za kila siku za wagonjwa wa UVIKO-19.

Ni CHADEMA hawahawa walioupinga msimamo wa jemedari Hayati Dkt. Magufuli juu ya kutowekwa lockdown nchi nzima/maeneo yenye
Wavaaji wa barakoa hapa Tanzania ni wengi mno hata kwenye shughuli za kiserikali,Bungeni,kwenye hospitali zetu,vyombo vya usafiri wa umma nk.Huko nako unashaurije?

Suala jingine muhimu ni upatikanaji wa barakoa zenye ubora na gharama za kuzipata.
 
Back
Top Bottom