CHADEMA na Makamanda tujifunze Mbinu za Medani #1

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Mabibi na mabwana elimu haina mwisho na katika zama hizi za "Delta Variant" kujikita "ki-dijitali" ni muafaka zaidi.

Tunapoikodolea macho katiba mpya ni muhimu tukajiridhisha kuwa tunafahamu yote yanayohitajika ili kutufikisha safari yetu salama.

Katika somo hili #1 ni muhimu tukaangazia umuhimu wa kuielewa hali halisi ya uwanja.

Ni muhimu maadui, washirika na wasio husika wakafahamika.

Ni muhimu ikajulikana kwanini huyu ni adui, yule ni mshirika na huyu hahusiki.

Jitihada za kupata washirika zaidi na kupunguza maadui ni sehemu ya mikakati sahihi ya ushindi.

Ni muhimu ikafahamika hayupo adui wala mshirika wa kudumu bali pana malengo (au maslahi) ya kudumu katika mapambano.

Ni muhimu kupambanua wazi kwanini ni lazima kupambana. Pia ni kwa namna gani ushindi utapatikana.

Karibu kwenye sanaa ya vita ambavyo inshallah vitatupa katiba mpya.

Katiba mpya kwa maslahi yetu na hata watoto wa wajukuu zetu.
 
Badilisheni strategy ya mambo yenu bila hivo mtadakwa kilaini ka kumbikumbi
 
Kudakwa si taabu. Hiyo ni sehemu ya yatokanayo kwenye mapambano. Na hasa kwenye hili lenye manufaa hata kwa watoto wa wajukuu zako, wala halitakiwi kumpa pressure mpambanaji yeyote aliyedhamiria na hata kidogo.
 
Umeelewa mada kweli?

Umeshadumazwa akili na manyanyaso ya polisi kwa Chadema umeyageuza ndio haki yao, huoni sheria zinavyovunjwa?

Sisi tunadai katiba kama walalamikaji. Mdaiwa wetu au mlalamikiwa ni mamlaka ambayo inafahamika kutokuwa na incentives zozote za kuwafanya kuridhia kirahisi.

Wote wanaovunja sheria ili kutuzuia kuifikia azma yetu halali hii, hao ni adui zetu wa moja kwa moja.

Wapo wanaodhani kuwa hawahusiki kama bidada hapo, japo waziwazi watoto wa wajukuu zao ni wanufaika. Hao ni kuwaelimisha. Wakikomaa basi pilipili wasizozila zitawahusu vipi tena?
 
Unataka wafanyaje ?
Nfano katiba wangeendesha online kampaign mikoa yote Ili kuepusha kukamatwa kwa misongamamo na kuwa jela huku kila kitu kinagoma na wanateswa jela wakija kuachwa wanachama wanakuwa disorganized.
 
Kudakwa si taabu. Hiyo ni sehemu ya yatokanayo kwenye mapambano. Na hasa kwenye hili lenye manufaa hata kwa watoto wa wajukuu zako, wala halitakiwi kumpa pressure mpambanaji yeyote aliyedhamiria na hata kidogo.
Sasa hiyo kamatwa kamatwa imesaidia nini zaidi ya kufanya wananchi wapuuze harakati na mda mwingi kutumia mkiwa jela baada ya kujenga chama na mda unaenda chama kudumaa na kukosa tumaini kwa wapenda mabadilikko Matokeo ni kupuuzwa na watu
 
Umeelewa mada kweli?

Umeshadumazwa akili na manyanyaso ya polisi kwa Chadema umeyageuza ndio haki yao, huoni sheria zinavyovunjwa?
Wewe ndio umedumaa hutaki kuelewa mambo kwa mkutadha mwingine, zaidi ya ulivo cremisha. Vipi ubabe umewafikisha wapi kwa kudai katiba zaidi ya kuishia jela na kulia lia munaomewa
 
Nfano katiba wangeendesha online kampaign mikoa yote Ili kuepusha kukamatwa kwa misongamamo na kuwa jela huku kila kitu kinagoma na wanateswa jela wakija kuachwa wanachama wanakuwa disorganized.
Watanzania wangapi watakuwa online kwenye wimbi la vifurushi bei juu na internet goigoi ?

By the way kwani kufanya makongamano ya hadhara kuna sheria wamevunja ?
 
Media ipi, TV, radio, au hata gazeti lipi litaachwa na mdaiwa kurusha habari zetu katika mazingira tuliyomo?

Platform ipi haitasukwa sukwa na mdaiwa wetu kama itaonekana kutoa uwezeshaji wa agenda ya wadai kusambaa?

Wananchi wangapi yenye uwezo wa kuwa na access ya online facilities kirasili mali (Fedha, vifaa, ujuzi nk)?

Kwa hali ya uwanja ilivyo, wingi wetu na kuyajaza kwetu magereza ni karata kubwa sana ya ushindi. Karata hii mdaiwa na adui zetu wanaijua na inawatisha vilivyo.

Niweke wazi zaidi: "bila kuyajaza magereza yao, haipo katiba mpya hapa!"
 
Watanzania wangapi watakuwa online kwenye wimbi la vifurushi bei juu na internet goigoi ?

By the way kwani kufanya makongamano ya hadhara kuna sheria wamevunja ?
Watanzania wengi tu wanatumia internet kwa sasa why ignore that platform. Kukusanyika ni jambo liko kikatiba ila halifatwi sasa na mtu ukitumia njia iliyo blokiwa na kujiletea matatizo unakuwa na wewe ni shida hujaweza ku solve changamoto yako
 
Media ipi TV, radio, au hata gazeti itaachwa na mdaiwa wetu kurusha habari zetu katika mazingira ya kwetu?

Platform ipi haitasukwa sukwa na mdaiwa wetu kama itaonekana kutoa uwezeshaji wa agenda ya wadai kusambaa?

Wananchi wangapi yenye uwezo wa kuwa na access ya online facilities kirasili mali (Fedha, vifaa, ujuzi nk)?

Kwa hali ya uwanja ilivyo, wingi wetu na kuyajaza kwetu magereza ni karata kubwa sana ya ushindi. Karata hii mdaiwa na adui zetu wanaijua na inawatisha vilivyo.

Niweke wazi zaidi: "bila kuyajaza magereza yao, haipo katiba mpya hapa!"
Dah kwahyo solution kwenu ni kwenda jela social media sikuhizi haina umuhimu na watanzania hawaitumii so na nyie kukamatwa ndio ukombozi wa harakati zenu za kukua kisiasa?
Dunia ya sasa mitandao imerahisisha mengi tu kuliko hata TV
 
Sasa hyo kamatwa kamatwa imesaidia nini zaidi ya kufanya wananchi wapuuze harakati na mda mwingi kutumia mkiwa jela baada ya kujenga chama na mda unaenda chama kudumaa na kukosa tumaini kwa wapenda mabadilikko Matokeo ni kupuuzwa na watu

Ni wazi kuwa katiba mpya tunayoidai ni ya manufaa kwetu na hata kwa watoto wa wajukuu zetu. Hata SSH na CCM wanajua hivyo. Bila shaka hata wewe unajua hivyo.

Katiba hii haitakuja kwa kusubiria chini ya mwembe kama embe dodo. Bila shaka na wewe unajua hivyo.

Ni wazi kuwa ni lazima tupambane kuidai. Tena tupambane kweli kweli.

Tunajua baina yetu tutasumbuliwa sana, tutafungwa na hata wengine tutapoteza maisha. Yote haya ni baadhi malipo ambayo tunayajua na hatuna budi kuyakabili. Kwani maji tumekwisha kuyavulia nguo.

Kwenye harakati hizi, kuna wadai, wadaiwa, maadui, washirika na wasiohusika.

Labda nikuulize wewe ni yupi katika hao?
 
Nani kakwambi

Nani kakwambia kukaa jela viongozi ndio chama kinadhoofika, uliza Mandela alikaa jela muda gani, kama huna taarifa au haujui, as days goes on, we become stronger & STRONGER, hofu inakatibia kutoweka, kitakachoguata, hata Mimi naogopa kuandika
 
Hamna asiyejua umuhimu wa katiba, ila unataka kusema katiba ndio itaondoa umaskini au mnataka katiba Ili nyie wanasiasa mpate vyeo tu mjineemeshe, mbona kipindi kile cha katiba mlifika mkawa mnagombania serikali mbili mara tatu na mkasusA bunge huku mkiacha vitu vingine vya msingi kwenye katiba kuliko hvo vyeo vyenu vya madaraka
 
Nani kakwambi

Nani kakwambia kukaa jela viongozi ndio chama kinadhoofika, uliza Mandela alikaa jela muda gani, kama huna taarifa au haujui, as days goes on, we become stronger & STRONGER, hofu inakatibia kutoweka, kitakachoguata, hata Mimi naogopa kuandika
Usifananishe mandela na siasa zetu zilivo ni vitu viwili tofauti mandela alikuwa na support na WAnanchi na dunia pia tofauti na huku wananchi hata hawajali
 
Watanzania wengi tu wanatumia internet kwa sasa why ignore that platform. Kukusanyika ni jambo liko kikatiba ila halifatwi sasa na mtu ukitumia njia iliyo blokiwa na kujiletea matatizo unakuwa na wewe ni shida hujaweza ku solve changamoto yako
Unafikiri hizo platforms hawazitumii ?

Politics ni mapambano huwezi kufanya politics utegemee easy run against your opponents ambao wanadola.

Ukifanya politics bila kupewa attention yoyote na opponents jua you are irrelevant.

Hizo kashkash wanazofanyiwa ndiyo zinaidistance serikali na wananchi.

Lakin lazima uende kwa wananchi physically siasa siyo maneno matupu ni psychology pia.
 
Watanzania wengi tu wanatumia internet kwa sasa why ignore that platform. Kukusanyika ni jambo liko kikatiba ila halifatwi sasa na mtu ukitumia njia iliyo blokiwa na kujiletea matatizo unakuwa na wewe ni shida hujaweza ku solve changamoto yako
Unatumia fallacy of generalisation kujenga hoja.

Hebu tuambie sasa hivi wanatumia twitter space ni watanzania wangapi wanao access twitter space au wewe umewahi walau kuhudhuria hiyo twitter space hata moja ?
 
Back
Top Bottom