- Thread starter
- #21
Hamna asiyejua umuhimu wa katiba, ila unataka kusema katiba ndio itaondoa umaskini au mnataka katiba Ili nyie wanasiasa mpate vyeo tu mjineemeshe, mbona kipindi kile cha katiba mlifika mkawa mnagombania serikali mbili mara tatu na mkasusA bunge huku mkiacha vitu vingine vya msingi kwenye katiba kuliko hvo vyeo vyenu vya madaraka
Inatia moyo kuwa hakuna asiyejua umuhimu wa katiba mpya. Bila shaka basi suala ulilomaliza nalo la madaraka ni kujichanganya tu.
Ila bado umekwenda kunilisha maneno lukuki nisiyo husika nayo kabisa. Laiti ungekuwa umenisoma vyema na kutambua kuwa:
"Hayuko adui wala rafiki wa kudumu bali agenda," bila shaka usingefanya hivyo.
Hata hivyo kwa bahati mbaya zaidi hukujibu swali langu la msingi:
"Kwenye harakati hizi, kuna wadai, wadaiwa, maadui, washirika na wasiohusika."
Nakazia: Wewe ni yupi katika hao?