CHADEMA na Minyukano : Fursa , Makosa na Anguko

Yatatokananayo CHADEMA

1. Mbowe (FAM) na Huruma
Kampeni zimeendelea kwa kasi kwa kutumia vyombo vya habari. Tumeeleza awali, hata vyombo ''mahasimu' hutoa nafasi (air time) kwa Wagombea wa CDM! kinyume kabisa na taratibu zao!!!

FAM akihojiwa alisema kwa hisia sana kuhusu fadhila zake kwa Wapinzania wake akiwemo Mh G Lema.

Kwa nadra sana, akihojiwa ,FAM alisema akichaguliwa ataweka kipindi cha uchaguzi cha miaka 3 ili kuwiana na chaguzi za Serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu.

Hoja: Tulieleza Team FAM wanatafuta huruma kwa kueleza nini waliwafanyia wapinzania wao na si nini watafanyia Chama. Tulionya Team TAL wakiingia katika malumbano hayo watapoteza.

Katika hali ya kushangaza Team TAL wameingia katika malumbano ya fadhila wakitekeleza hoja zao za nini wanataraji kufanya wakipewa uongozi. Katika hili, Team FAM imewavuta wakaingia 18.

Hoja ya vipindi 3 iliyotolewa na FAM haina mashiko. Miaka 5 ingeweza kupangwa kwa kuangalia kalenda za chaguzi za Kitaifa. Swali, ni kwanini kwa miaka 21 FAM hakuweza kuliona hili au kulifanyia kazi?

Uongozi wa miaka 3 haumpi nafasi kiongozi kutekeleza azma na ahadi au mipango yake Kichama

2. Tundu Lissu (TAL) na Urpokaji
Kuna tuhuma kutoka Team FAM kwamba TAL ni mropokaji, wakiitumia kumdhalilisha au kumdunisha.

Hoja: Kuropoka kwa maana ya kiswahili kunaweza kuwa na maana mbili

Kwanza, kuongea jambo bila ithbati au uhakika. Ni aina ya uzushi unaojengwa bila mantiki
Pili, kuropoka ni kutoa maneno yaliyokuwa siri kwa kudhamiria au kwa bahati kutoka

TAL anapotoa hoja mara zote zinajengwa kwa mantiki na hutoa hadi chanzo.
Mfano, alibanwa aeleze ushahidi wa kuhongwa pesa. TAL alijibu, aliyetoa habari hizo ni Marehemu.
TAL akaendelea kusema ikiwa ni uzushi itolewe video inayoonyesha aliomba radhi.

Kwa tafsri, TAL anakuwa mropokaji kwa hoja ya pili hapo juu, kwamba anatoa habari ambazo zilitakiwa ziwe siri. Inaweza kuwa kweli lakini je wanaomtuhumu huzingatia ukweli kwamba TAL anahitaji kujitetea?

TAL anapojitetea huambiwa ni Mropokaji, anazungumza yasiyotakiwa kuzungumzwa.
Wanaomtuhumu hawafikirii gharama za tuhuma, na wangependa TAL akaekimya.
Kanuni za asili (natural justice) hazipo hivyo.
Ni dhahiri, uropokaji waousema watuhumu wake ni ili kumtaka akae kimya anapotuhumiwa

Wasira na Mkutano Mkuu wa CCM
Mzee Wasira (80) amechaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara.

Katika hotuba ya kushukuru, Mzee alizungumzia suala la maridhiano akisema CCM itaendelea nayo, na kwamba maridhiano si mtu mmoja, kuna yanayohusu jamii kama viongozi wa dini n.k.

Hoja: Mzee Wasira ameongelea maridhiano makusudi kabisa.

Kwanza, kujibu hoja za wanaosema maridhiano yalikuwa Utapeli na hasa kambi ya TAL.

Pili, Mzee anachomeka maridhiano katika kumtetea muasisi wa Maridhiano Mh FAM.
Mzee Wasira anaposema 'si mtu mmoja' ana maanisha maridhiano si baina ya CCM na TAL ambaye amekuwa mwiba mkali bali CCM na Taasisi

Hoja ya maridhiano imechomekwa makusudi kuonyesha CCM ina dhamira na mtu anayeweza kuwa mshirika ni FAM. Kwa kujua au kutojua Mzee Wasira atakuwa ameshadidia hoja ya TEAM TAL kwamba CCM wanamtaka FAM kwasababu wana mmudu.
Huu ulikuwa mkakati mbaya sana wa Mzee Wasira, hakusoma mazingira.
 
Kauli za Rose Mayemba
Hoja 4 za FAM


Tumezungumzia uchaguzi wa mkoa wa Njombe na madudu ya kigaila, kijana wa FAM mabandiko yaliyopita. Leo akiwa makao makuu, Rose Mayemba, mhusika wa sakata la Njombe anazungumza na kuelezea kilichojiri katika video ya bandiko 22.

Hakuna shaka Mwenyekiti FAM alifahamishwa na alijua tatizo kwa maneno ya Rose.
Kwamba kuenguliwa kwa mkoa wa Njombe ni mbinu ya kufifisha uchaguzi wa kanda.

Kwa kuzingatia ukweli kwamba FAM alikuwa na taarifa na kwamba hadi leo mzozo hauna ufumbuzi, kuna mengi sana ya kujiuliza. Mosi, FAM ana uzoefu wa miaka 21. Hili ni tatizo la kushindwa kulimaliza kwa dakika?
Pili, kuelekea uchaguzi wa 21 nini hatma ya Wajumbe wa Mkoa wa Njombe ikiwa M/Kiti wao hajulikani?

Kuna taswira kwamba suala la Rose ni mbinu chafu za Team FAM ku disfranchise wapiga kura wasiokubaliana na kambi yake.

FAM na ajenda Kuu

Mh ameorodhesha mambo makuu 5 atnakayotekeleza atakapochaguliwa
1. kuunda Tume ya ukweli na upatanishi
2. Program ya kustawisha Chama
3. Kuamsha vugu vugu la Kati,ba mpya
4. Program za kuandaa wagombea wa Chadema
5. Program ya kutoa elimu ya Uraia

Tutazipitia ajenda hizo moja baada ya nyingine. Tuanza na ajenda ya Tume ya Upatanishi.
FAM anaaminisha Wanachama kwamba baada ya uchaguzi ataunda Tume ya upatanishi.
Hili ni wazo la ajabu sana kwa kiongozi aliyekaa madarakani miaka 21.

FAM anajua wazi Wanachama hawana tatizo ikiwa haki itatendeka. Mfano, Tume gani ya upatanishi itakayowaweka Kigaila na Rose Mayemba pamoja? Tume gani itakayoweza kurudisha imani kwa Vijana kama Twaha Mwaipaya waliokatwa kwasababu ya kuamini tofauti na kambi yako?

Upatanishi haiwezi kuwa ajenda ya Chama si kitu kinachopaswa kuwepo.
Hakuna program ya upatanishi wakati dhulma na hujuma zikitamalaki tena kwa kuratibiwa.
 
Hoja za Mh FAM
Tunaendelea kuzipitia hoja za FAM ikiwa atachaguliwa

2. Program ya kustawisha Chama!
CDM haipaswi kustawishwa, inapaswa kushindana. FAM alisema baada ya miaka 7 ya kunyimwa fursa za kufanya siasa alitumia mwaka mzima kustwaisha Chama. Kwanini hakuwa na program wakati huo!

3. Kuamsha vuguvugu la Katiba mpya
Hoja inaonyesha kutapa tapa kwa Mh FAM. Ni yeye aliyeua vugu vugu la kudai Katiba baada ya kuitwa Ikulu siku aliyotoka magereza. Ile kauli ya kwamba ''amelamba asali'' ilikuja baada ya Maridhiano ambayo ndiyo yalitoa nafasi ya kuua vuguvugu la Katiba. Leo FAM aliyeua vugu vugu anataka kuamsha vugu vugu!
4. Program za kuandaa Wagombea wa Chadema
Kwa miaka 21 angefanya program hizo. Kwa wakati huu si suala la kuandaa Wagombea bali kuchuja Wagombea. Chama kimekuwa kikubwa kikiwa na Wagombea luluki, haihitaji program ya kuwaandaa.

Ni FAM huyu anayetumia Kamati kuu na Sekretariati yake kukata majina ya '' Wagombea potential '' kama Twaha Mwaipya na kutengeneza mazingira ya kushindwa kwa akina Catherine Ruge ndiye anaanda program ya kuwaanda Wagombea.
Kinachotokea kwa akina Rose Mayemba na wengine kinatosha kueleza hii si hoja ni kioja.

5. Program ya kutoa elimu ya uraia
Elimu ya Uraia ni jukumu la Serikali na taasisi zake zikiwemo civil society.
Vyama vya siasa vina mchango wake lakini si jambo la kulifanya kama kipaumbele

Ukizisoma hoja za FAM, hakuna inayoeleza amefanya nini miaka 21, anataka kufanya nini miaka 5 na kwasababu gani. Anachoeleza ni shughuli za kawaida za vyama vya siasa nchini.
 
Uchaguzi Umekwisha
TAL na Chama, majeraha yatapona?


Timu ya Mh Tundu A Lissu (TAL) imeshinda uchaguzi wa CHADEMA.
Ni uchaguzi uliovuta hisia za nchi kwa hali ya juu . Ni uchaguzi utakayoipaisha au kuikwamisha CDM

Mh Mbowe (FAM) ameshindwa uchaguzi. Yapo maoni tofuati katika jamii.
Kundi linaloamini FAM alipaswa kusoma alama za nyakati na kujiondoa mapema.
Kundi la pili linasema FAM amethibitisha ukubwa wa Demokrasia.

Kwa uchaguzi uliofuatiliwa usiku mzima, uliohudhuriwa na Wanadiplomasia, uliokuwa huru na wazi, aliyeshindwa alimpongeza aliyeshinda hakuna shaka ni ushindi mkubwa kwa CDM.

Wanaosema FAM angejitoa au ameshindwa hawa angalii upande wa pili wa shilingi. Ameiahcha CDM na nguvu zaidi, amedhihirisha ukubwa Demokrasia ya CDM kama funzo kwa Vyama ikiwemo CCM

Kwa wiki nzima NI cdm, tulizoea kuuona CCM sasa tunauona CDM katikati ya mkutano mkuu wa CCM. Mkutano mkuu uliokuwa na 'vituko' hasa kwa kukiuka katiba ya CCM. Mada ya siku nyingine!!

Tatizo kwa CDM si viongozi tena bali malumbano ya Wapambe. Mwenyekiti TAL akemea malumbano na kiunganisha Chama. Kazi ya kukiunganisha Chama si rahisi, ni ngumu na inahitaji uvumilivu na muda

Kati ya changamoto anazokabiliana nazo TAL ni kufanya kazi na mahasimu wake wengi walioparurana kwa kama Mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti Bw Wenje, mjumbe wa Kamati kuu.

Mfano, ikiwa TAL alimshutumu Wenje kama ''project ya CCM'' vipi watapanga mikakati ndani ya Kamati kuu bila kuvuja au kufika isikotakiwa? TAL ana uwezo gani wa kumuondoa Wenje katika uongozi?

Uchaguzi wa Mh Mnyika kama Katibu Mkuu umepokelewa kwa uvugu vugu.
Wapo wanaosema ni wakati wa nguvu mpya wakimtaja G.Lema kama mtu sahihi.
Hakuna tuhuma dhidi ya J.Mnyika! Hata hivyo kushindwa kwa sekretariati yake ya akina Kigaila ni doa

Kwanini TAL amemchagua Mnyika? Huu ni mkakati mahususi kwasababu kuu mbili
1. Mnyika anajua mambo mengi ya Chama hasa mikakati ya utafuataji fedha. Ni mtu sahihi ana uzoefu
2. J.J.Mnyika anaheshimika na makundi yote yanayohasimiana, ni kiunganishi kizuri cha Wanachama

Kigaila na Salum Mwalimu nje!
Hawa walifanya madudu uongozi uliopita, wake zao ni COVID-19 wakidanganya Umm
Pili , walichukua upande wakati wa uchaguzi kwa kumhujumu TAL kupitia chaguzi za kanda.

Uteuzi Rose Mayemba ni chaguo sahihi. Rose ni CDM ''lilia lia'' wengi walimfahamu kwa harakati katika ngazi za chini. Ni ''mshehereshaji ' mzuri, uteuzi umelenga kupooza machungu ya watu wa nyanda za juu

Catherine Ruge
Msubhati ana misimamo thabiti, haongozwi na masilahi. Catherine aliwakatalia COVID kwenda Bungeni. Aliteuliwa Katibu mkuu BAWACHA katika mazingira magumu sana. Ni mmoja wapiganaji wazuri na anafahamu mbinu nyingi hasa kwa kundi la akina mama.

S. Kiwanga
Ni mkongwe ndani ya CDM na anafaa kuwaongoza mabinti. Ni 'potential' kinyang;anyiro cha Ubunge

G.Lema kuteuliwa kamati kuu ni sahihi na pengine nafasi ya usemaji wa Chama ingemfaa zaidi.

Twaha Mwaipya na J.Pambalu. Ni Vijana wanaopaswa kuwa na sehemu yao katika uongozi wa TAL
Ni wapambanaji wazuri, CDM kwao ni sehemu ya maisha yao.

Kazi ya ujenzi wa CDM ianze kuponya makovu. Mtu wa kutibu majeraha ni Makamu Mwenyekiti Heche.
Mwl Heche ana misimamo mikali na lugha yenya ''command'' lakini ni mjenga hoja mahiri

Baada ya Uchaguzi wa CDM hakuna muda wa kupoteza, ni wakati wakutambua wagombea wa majimboni.
Hapa panahitajika uangalifu sana yasijetokea ya uchaguzi wa kanda za nyanda uliozaa balaa lote na kuondoka na FAM. Tutafanua bandiko lijalo
 
Kazi nzuri Mkuu Nguruvi3 umeweka kumbukumbu sawa toka mchakato wa uchaguzi chadema uanze, hata ambaye hakufuatilia atakuja hapa kujua kila hatua.
 
Yatokanayo na Uchaguzi wa CHADEMA na CCM
Kauli ya Catherine Ruge, COVID-19 na Kituko Dodoma


Baada ya uchaguzi wa CDM kuna mambo yanajitokeza kama kawaida ya chaguzi.

Mwenyekiti Lissu (TAL)
Amezungumzia Wabunge wa COVID-19. TAL anasema iwapo wanataka kurudi wanapaswa kueleza nani alisaini fomu zao, na wale waliokuwa magereza nani aliwatoa.

TAL ni mwanasheria na lugha yake hunyooka kwasababu ndio lugha aliyozoea.
TAL kwa sasa ni Mwenyekiti wa Taasisi ya kisiasa, hawezi kujitenga na lugha ya kidiplomasia.

TAL anasaidiwe kuelewa lugha ya Kidiplomasia kwa wadhifa wake kwa maswali ya mitego kama la COVID.

Jibu la TAL ni sahihi, Wanachama wengi watakaubaliana naye kwamba, COVID ni Wasaliti.

Taratibu za Chama zinaeleza wakitaka kurudi baada ya kufukuzwa uanachama watatakiwa wafanye nini. Hii ni pamoja na kuomba Uanachama katika ngazi za mashina na kuendelea kama kuna tatizo.

Kitendo cha TAL kuwawekea ''ngumu'' ni sahihi kwa mtizamo wa hasira, kwa jicho la sheria inamaanisha anawawekea vikwazo vya lazima na kukiuka haki zao za Kikatiba. Wapewe haki ya kuomba na maswali ya
TAL yataulizwa kwenye vikao wanakochukua Uanachama. TAL angesema kirahisi '' wafuate taratibu'

Catherine Ruge na ''Patriarchy''
Patriarchy ni mfumo wa Wanaume kuwa na nguvu za kiutawala dhidi ya Wanawake.
Catherine alikuwa Katibu wa BAWACHA Taifa kabla ya kushindwa. Kauli yake ina 'ukweli' kwa mtazamo wa haraka. Kwa mtazamo wa kina kauli ya Catherine haina mantiki.

Uchaguzi wa CDM ngazi zaKanda Wanawake hawakujitokeza.
Uchaguzi wa Taifa , Bi Ruge hakuchukua Fomu ya Uenyekiti au Umakamu alichukua ya BAWACHA KM.

Miaka takribani 5 akiwa Katibu Mkuu, Catherine alipaswa kuandaa Wanawake kwa nafasi za Uongozi.
Ni kwa hoja ipi anaweza kunyooshea vidole 'Patriarchy' ndani ya CDM ikiwa hakufanya chochote kuzuia?

Hoja ya Ruge inashadidia hoja ya TAL kwamba Wanawake wawe na Ubunge wa viti maalumu kwa miaka 5.
Hii itasaidia kuondoa mawazo ya ''upendeleo'' kama ya Catherine na kuleta ushindani wa kisiasa.

Mkutano wa CDM na Kituko cha CCM Dodoma
''Gold standard'' ni msemo unaomaanisha ubora wa kitu wa kuigwa kama kipimo cha wengine.

TAL alisema uchaguzi wa CDM ni 'gold standard' kwa maana hiyo. Viongozi mbali mbali Nchini wanapongeza CDM. Ni uchaguzi uliokuwa huru na Uwazi lakini kubwa aliyeshindwa alikubali matokeo.

CCM, chama kikongwe kilipaswa kuwa ''gold standard ya kila jambo la kisiasa nchini'.
Katika wiki ya uchaguzi wa CDM , CCM walikuwa na jambo lao Dodoma, mkutano mkuu ambao agenda ilikuwa ilani na kumchagua Makamu wa M/kiti.

Katika hali ya kuduwaza Mkutano Mkuu wa CCM ukaja na ''azimio' la kupata wagombea wa Uchaguzi Mkuu

Rais Mstaafu JK alikuwa na wakati mgumu sana kukubaliana na hali hiyo. Kikwete alisema hata yeye alipitishwa na Mkutano mkuu mwezi May. Alionyesha kutoridhisha na ''surprise'' na haraka hiyo.

Tangu Uhuru MgOmbea Urais wa Nchi katika mifumo yote miwili ya Chama kimoja na Vyama vingi kumekuwepo na utaratibu wa kupata jina kwa Vikao.

Katika vyama vingi Wagombea wamekuwa zaidi ya mmoja ndani ya Chama
Mwaka 1995 akina Maelecela , Kikwete n.k.
Mwaka 2005, Kikwete n.k.
Mwaka 2010 , Lowassa , January, Magufuli, Asha Rose n.k.

Nini kilitokea Dodoma ? na kwanini ni tofuati na siku za nyuma? Kwanini Katiba ya CCM ilivunjwa mchana?
Wako wapi Wazanzibar ?

Inaendelea...
 
Kilichotokea Dodoma ni ''kituko'' cha CCM

Tunaendelea na mjadala wa kilichotokea Dodoma ambako M/Mkuu wa CCM ulipitisha majina mawili ya kinyang'anyiro cha Urais wa Muungano na wa SMZ.

Kabla ya kujadili ya Dodoma tupitie ya kada wa Iringa Katika maandamano ya kuunga mkono azimio la Dodoma. kada wa CCM katetea hoja ya Mkutano Mkuu akiwaita wanaohoji ni Wapotoshaji.

Hoja yake imejikita katika Uhalali wa Mkutano Mkuu kuthibitisha majina mawili ya Wagombea.
Amenukuu Ibara 101 ya Katiba ya CCM 1977 toleo la 2022.

Ni kweli, Ibara hiyo imetoa mamlaka kwa Mkutano Mkuu kama sehemu ya kazi zake kuthibitisha majina ya Wagombea Urais wa Muungano na Zanzibar yaliopendekezwa na Halmashauri Kuu

Kada huyo kwa kutojua katiba ya CCM, kupotosha au Uchawa anaaminisha Umma mchakato wa kugombea nafasi za CCM katika uchaguzi wa nafasi za Urais unaanzia Mkutano Mkuu!

Kwa faida ya kada wa Iringa na Wasomi wa CCM huu ndio utaratibu kwa mujibu wa Katiba ya CCM ya toleo la 2022

Mjadala wote utakuwa katika Fungu VII la Katiba ya CCM 1977 toleo 2022, Vikao vya Taifa.

Ibara 99 (4) Kamati maalumu ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa (Zanzibar). kwa makusudi tuanzie hapa.
Ibara 110 (7)(b) Kamati Maalumu itapendekeza majina kwa Kamati kuu CCM Taifa kwa Wanachama wanaoomba kuteuliwa nafasi ya Urais, Uwakilishi na Ubunge Zanzibar

Hoja: Mchakato wa kumpata Mgombea Urais wa Zanzibar unaanza kwa kuchukua Fomu kisha kujadiliwa na Kamati maalum ya H/Kuu CCM Zanzibar.
Hoja hii ni muhimu kwasababu ya mifumo miwili ya chaguzi za CCM

Kamati Kuu ya CCM.
Ibara 104 (1)(7)(b) Kamati Kuu itapendekeza kwa Halmashauri kuu majina yasiyozidi matano ya Wanaoomba kugombea kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano.
104 (1)(7)(d) kufikiria na kupendekeza majina yasiyozidi majina matatu ya Wanachama wanaotaka kugombea kiti cha Rais wa Zanzibar

Hoja : Kamati Kuu itapokea majina kutoka kwa Wanachama (wengi) waliochukua Fomu za kugombea na kuyajadili na kuyapeleka matano H/Kuu ya Taifa.
Maana yake Mchakato unaanza na kuchukua Fomu ili majina yachujwe na kubaki matano

Halmashauri Kuu ya Taifa
Ibara 103(12) (b na c) itapendekeza kwa Mkutano Mkuu wa Taifa majina yasiyozidi matatu kwa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano , na jina moja kwa nafasi ya Rais wa Zanzibar

H/Kuu
itapendekeza majina hayo kwa Mkutano Mkuu wa CCM

Mkutano Mkuu

Ibara 101 (5)(c) Kuchagua jina moja kwa atakayesimama uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Hoja: Hadi hapo tunaona Mchakato unaanzia kuchukua Fomu na kujadiliwa na Vikao mbali mbali kuanzia Kamati Kuu, H/Kuu na Kamati Kuu Zanzibar.

Swali; ni lini kulitangazwa kuchukua Fomu?
Lini mchujo ulifanywa na Kamati Kuu na Kamati maalum Zanzibar na H/Kuu Taifa?

Kada yule wa Iringa angeelewa kwamba Katiba inasema hivi;

Ibara 101 (7) linatoa Uhuru wa Mkutano Mkuu Kukasimu shughuli zake kwa Halmshauri kuu ya CCM isipokuwa kifungu (c) kinachokataza Mkutano Mkuu kukasimu madaraka ya uteuzi wa mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano, na (d)Kuthibitisha mgombea Urais wa Zanzibar.

Kada wa CCM Iringa aelewe ibara 101 inakataza kurudi nyuma na kuanza vikao kwasababu kazi hiyo haikasimiwi. Hapa ndipo pia Rais Mstaafu JK alipoelekeza isivyo, kwamba akina ''Emanuel' waaangalie taratibu za kisheria. Huwezi kuweka mkokoteni mbele ya Farasi !!! hata Farasi atashangaa

Hakuna taratibu itakayoweza kuhalalisha mchakato huo kwasababu Katiba ya CCM ipo wazi.
M/Mkuu hauwezi kukasimu madaraka ya shughuli za uteuzi wa Wagombe Urais kwa chombo kingine.

Na kwamba, Wanachama waliotaka kuchukua Fomu wamenyimwa haki Kikatiba ya kuchagua au kuchaguliwa. Hoja ni kwamba utaratibu uliotumika ni kinyume na taratibu za Katiba ya CCM!
Kama sivyo, mwenye hoja tofauti atuelimishe

Kamati Maalum Zanzibar haikufanya kazi yake kwa mujibu wa Katiba.
Hili linajenga hali ya kuaminisha Umma kwamba viongozi wa Zanzibar wanachaguliwa Dodoma.
Wapinzani wa CCM wakiitumia hoja vizuri wataidhoofisha CCM Zanzibar, lakini ni tatizo la kujitafutia!

Kwa upande mwingine, tambo za CCM kama ''Baba wa Demkrasia'' zimefutika.
Michuano iliyokuwepo zama za Nyerere imefutika , CCM imebaki kuwa kikundi na si Chama cha wote.
Wapi CCM inaweza kusimama na kuhubiri Demokrasia?

Kwa kutazama Mkutano Mkuu wa CCM na CHADEMA, kwa kilichotokea Dodoma, CCM imewaheshimisha sana CHADEMA mbele ya Umma.

Hata kama CCM watakubaliana kwamba limefanyika kwa ni njema, hili litajenga hali ''precedent'' siku za mbeleni kwa viongozi kutafuta njia za mkato (short cut).

Ipo siku kiongozi wa CCM atalazimisha Kamati Kuu au H/Kuu impitishe.
Yaani itajenga hali ya kukwepa viunzi na mfano huu wa Dodoma ukiwa ndio kigezo
 
Hotuba ya TL
Wanawake ni sehemu ya ''CDM Brand''

Hotuba ya Mwenyekiti TAL ikisisitiza hakuna mabadiliko hakuna uchaguzi imepokelewa kwa hisia tofauti.
CCM wanasisitiza na '' kuwanasihi'' CDM wasisusie Uchaguzi wa Novrmber 2025

2025 ni uchaguzi utakaosimamiwa na Taasisi na sheria zile zile za 2020.
Kwa namna nzuri, uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 umeonyesha pasi na shaka , CCM haipo tayari kuwa na uchaguzi huru na wa Haki. Yaliyotokea 2024 yanawaeleza Wananchi kilicho mbele yao na hapo ndipo TAL anapoungwa mkono

CCM inatambua nguvu ya CDM katika siasa za leo. Uchaguzi wa uliofuatiliwa sana wa CDM ni ishara Watu wapo tayari kwa mabadiliko. Ni kupitia nguvu hiyo CDM wanaweza kufanikiwa kuishinikiza Serikali ya CCM

CCM inaandaa mbinu za zamani kwamba vyama vya siasa vipo vingi vitaingia katika uchaguzi na kupewa majimbo ili kukamilisha dhana ya uchaguzi wa vyama vingi.
CCM wanapaswa kujiuliza kwanini Mabalozi walialikwa na kuhudhuria mkutano Mkuu wa CDM kwa hamasa

CCM wana karata moja, kutumia ACT Wazaalendo kama chama kikuu cha Upinzani.
ACT wamepewa nusu mkate kwa miaka dahari bila kupata wanachostahili.
Chaguzi zote ndogo ACT walishiriki na walifanyiwa rafu kikamilifu.

Hata hivyo, ACT Zanzibar ni watiifu kwa Serikali ya CCM kwasababu inaongozwa na Mzanzibar.
Kelele na madai yao dhidi ya CCM, Katiba, Muungano kimya! , ACT wanapewa nusu mkate na Kaimati kama kawaida ya, wametulia. Hawa ndio tatizo siyo Wananchi

Tukirejea katika hotuba ya TAL kuna makosa mengi ya kifundi.
Haionekani kama mtayarisha hotuba alizingatia hali ya kisiasa na kijamii nchini.

Mfano, TAL aanapoongea na viongozi wa Dini alipaswa kuwa ''inclusive''. Hata kama kuna wenye misimamo yao kazi ya TAL ni kuwaleta pamoja . Inatosha kusema hotuba ilikuwa na mawaa na matatizo ya kiufundi.

TAL anapaswa kutambua Wanawake ni Injini ya CDM. Ni BAWACHA wanaoipamba brand ya Chama chake. Wanawake wa CDM ni mahairi kuliko Mabaraza mengine ya CHADEMA.
Ugomvi wa TAL na BAWACHA hauna tija. Uchaguzi umekwisha TAL ni Mwenyekiti waliomchagua na wasio.

TAL atambue Wanawake ni nguzo muhimu sana ya Chama chake! Ugomvi nao hautamsaidia
 
Tundu Lissu ( TAL) arejea Itungi
TAL ahutubia Taifa na ukweli mchungu kuhusu Muungano

Mwenyekiti wa CHADEMA Mh TAL amerejea Itungi na kupokelewa na ''Wanafamilia ndugu wa kisiasa''

Tunarejea rai ya bandiko lililotangulia, TAL awe na muafaka na Baraza la Wanawake (BAWACHA).
CDM haikusimama kwa nguvu za BAVICHA au BAZECHA

Katika mazingira na nyakati za raha na shida BAWACHA imekuwa Injini ya CDM katika kusema, kutetea, kusimamia na kutekeleza majukumu ya Chama.

Mifano ipo mingi inatosha kusema Mh TAL lazima amalize tofauti na kuifanya BAWACHA ing'are kama ilivyokuwa. Kinyume chake TAL ana wakati mgumu kukijenga Chama baada ya uchaguzi.

Katika tukio jingine TAL amehutibia Taifa. Moja ya hoja ni kuhusu mgawanyo wa majimbo.
Watu wengi wameshindwa kumsikiliza TAL walifikia hitimisho bila fikra kwamba TAL alizungumzia Wabunge kutoka Zanzibar.

Ukweli, TAL alizungumzia mgawanyo wa majimbo kwa sehemu zote mbili, Tanganyika na Zanzibar.

TAL ana kitu ambacho Wanasiasa wengi na Maprofesa wa Nchi yetu hawana, UTAFITI.

Kwa mafano, katika moja ya mijadala ya ''Chief Odemba'' Profesa mmoja maarufu na kada wa CCM alitoa madai kwamba Wanachama wa CDM walienguliwa uchaguzi kwa kukosea majina yao

Profesa alipoulizwa sheria gani imesema hayo, hakuwa na jibu akibaki kujiuma uma.
Ilikuwa ni aibu kwasababu kumtofautisha Profesa na mtu wa kijiweni ilikuwa ngumu sana

Kwa upande mwingine TAL hufanya utafiti na kisha kuja na majibu yenye ukweli unaoudhi.
Hii ndio sababu ya TAL kuitwa ''Mkorofi''

TAL aliweka Takwimu kutoka Tume ya uchaguzi ikiungwa mkono na maoni ya Wasimamizi wa Chaguzi wa Kimataifa tangu vyama vingi virejeshwe.

Kwamba majimbo yagawanywe kwa idadi ya watu kama ilivyokuwa wakati wa Uhuru hadi vyama vingi mwaka 1992. Kwasasa Tume inatumia kigezo cha 1. Njia za Mawasiliano 2. Jiografia

1. Kwamba Zanzibar ina wapiga kura 569,617 na majimbo 50 kwa wastani wa wapiga kura 11,000 kwa jimbo.
Diwaniwa Kata ya Dar es Salaam ana Wapiga kura 80,000 wengi kuliko Wabunge 7 wa Zanzibar (77,000)

2. Mkoa wa Dar es Salaam una Wapiga kura 3, 427, 000, idadi mara 6 ya wapiga kura Zanzibar, yenye Wabunge 50 na Dar es Salaam Wabunge 10

Hoja ya kipuuzi ni kwamba Zanzibar ni nchi. TAL anauliza, ikiwa hiyo ni sababu wapi imeandikwa kwamba Zanzibar kwavile ni Nchi inapaswa kuwa na Wabunge 50 ?
Wabunge wengine kama wa Donge akiwakilisha watu 3,000 sawa na Kitivo kimoja University of Dar es Salaam

Lakini TAL anahoja nzito , kwamba, Wabunge 50 wa Zanzibar wanaamua hatma ya Watu 3,427,352 wa Dar es Salaam tu achilia mbali Tanganyika yenye watu Milioni 60 tena kwenye mambo yasiyohusu Zanzibar wala masilahi ya Zanzibar!

Ukorofi wa TAL upo wapi? Kama upo ukorofi tunaweza kuuita ''good trouble''
 
Uteuzi wa Wajumbe wa Kamati Kuu CHADEMA
Wanachama wanapokaribisha tatizo lililosambaratisha CUF na NCCR


Kwa muda mrefu Wana CHADEMA wamelalamikia nafasi 5 za Ujumbe wa Kamati Kuu zitokanzo na uteuzi wa Mwenyekiti kuwa Wazi.

Mkutano Mkuu uliomalizika Mwenyekiti Tundu Lissu (TAL) alijaza nafasi hizo kukidhi matakwa ya kikatiba.

Katika siku za karibuni baadhi ya Wanachama wamehoji akidi iliyoidhinisha majina hayo.

Wanachama hao wana haki ya msingi na kikatiba kuhoji pale wanapoona kunahitajika maelezo au pale Katiba inaposiginwa kwa makusudi au bahati mbaya.

Si mara ya kwanza, uongozi wa Mbowe ulihojiwa pia. Inatosha kusema Wanachama wakiongozwa na Lembrus Mchome wana Haki.

Haki ya kuhoji ni tofauti na Hoja.

Haki ya kuhoji wanayo, lakini je wana hoja ?
Wanachama wanasema akidi haikutimia na wametoa ''namba'', hawakatai uteuzi wa Wajumbe.

Ni wajibu wa viongozi wa CHADEMA kuwajibu kwa hoja na namba kwasababu hoja inajibiwa kwa hoja.

Je, kumwandikia Katibu Mkuu iikuwa kosa? Jibu ni hapana kwasababu Katibu Mkuu ni mtendaji mkuu.
Katika Mkutano mkuu ndiye alikuwa kiongozi mwendeshaji na Sekretariati yake.

Hadi hapa hakuna tatizo kwasababu ni mambo ya CHADEMA na yanamalizwa kwa taratibu za Chama.

Swali linalozuka kwanini Wanachama hao wanatuhumiwa kuhujumu Chama!

Kuandika barua kwa suala linalohitaji ufafanuzi wa kichama lisilo na mgogoro haiwezi kuwa sababu ya kunukuu barua hiyo kwa Msajili wa Vyama vya siasa .

Katika mazngira ya kawaida 'ingekuwa na mantiki'' kwa kuzingatia historia ya Ofisi , ni tatizo kubwa sana.

CUF- Maalimu na mgogoro na Profesa Lipumba. Suala likatua Ofisi ya Msajili wa vyama.
CUF ikaingia katika vuta ni kuvute hadi Maalim alipobaini njama zinazotumiwa na mahasimu wa CUF kwa kutumia Taasisi za Umma kuzuia hatma yake uchaguzi uliofuata! akatimkia ACT Wazalendo mapema

NCCR ya Mh Mbatia haikuwa na tatizo, wakatokea Wanachama waliofikisha suala Ofisi ya Msajili.
Yaliyotokea yanabaki kuwa historia !

Katika mazingira ambayo CHADEMA ina kampeni mbili, ya ujenzi wa Chama na ile ya Uchaguzi wa mwakani, kila mbinu inaweza kutumiwa na Mahasimu wao wa CCM kuidhoofisha CHADEMA.

Viongozi wa CHADEMA kwa usalama wa Chama chenu hakikisheni suala hili linamalizwa haraka
Usipoziba ufa utajenga ukuta! Mwaliko uliotolewa na Lembrus kwa wasiohusika utawaeleta matatizo, ninyi siyo CCM! ninyi ni Wapinzani
 
'' LAST CALL ''
NI BAWACHA , WAKIWAACHA MTAJUTA

TONE TONE INAHITAJI BAWACHA

Ni mara ya nne tunarejea wito kwa viongozi wa CHADEMA, kwamba uchaguzi umekwisha.
Kazi kubwa si michango , ni kuponya Chama kutokana na makovu ya Uchaguzi

BAWACHA ni ''Brand' ya CHADEMA,walisimama kidete kwa nyakati . Hata pale viongozi walipokabiliwa na mitihani, ni BAWACHA iliyokuwa sauti ya CHADEMA. hakuna asiyetambua mchango wa BAWACHA

Uchaguzi ulikuwa na pande, na ingalikuwa jambo la kushangaza kama wote wangekuwa na mtazamo mmoja. Hata hivyo, uchaguzi ukiisha kazi ya kuimarisha Chama huanza mara moja

Ni wazi, baadhi ya BAWACHA walimtaka Mwenyekiti Mbowe kwa sababu zao. Hawa wamekwazika kwa kushindwa. Ni wajibu wa viongozi wa leo kuwafikia na kuwafuta machozi safari iendelee.

Wapo BAWACHA wengi muhimu , kwa muktadha wa mjadala tutawataja wachache.
Catherine Ruge Msubhati, alikuwa Katibu wa BAWACHA akikacha kuambatana na COVID-19.
Alifanya kazi nzuri sana kuijnga BAWACHA. Yupo Mwana mama Suzan Kiwanga, mjenga hoja mahiri na akina Devota Minja. Viongozi hao kwa uchache wanasikilizwa wenzao (Respected)

Wanawake wana ''hulka' moja ya kuwaamini wenzao kutokana na mfumo wetu uliowakandamiza kwa muda mrefu. Inatosha kusema ushiriki wao katika ujenzi wa Chama ni muhimu sana.

Tukio la Jana la kuchangisha fedha za Chama lilitawaliwa na Wanaume badala ya wao kuwa ''organizer' na akina Mama kuwa wapiga debe. nI tukio liliLo onyesha, BAWACHA wameachwa au Kususwa.

Hili ni jambo la hatari. Mwl Heche (Vice) ,Mh Godbless ninyi ni watu makini liangalieni hili.
Shughuli yenu ya jana ingefana mara dufu kama akina Mama wa BAVICHA ''Brand' wangeshirikishwa.

Fikirieni kidogo, kurejea kwa Boni Yai kulikuwa na hamasa kubwa na ni habari ya mjini.
Vipi wangekuwepo akina Catherine, Kiwanga na wengine waliotengeneza BAWACHA brand!

Pamoja na hayo, CHADEMA isiwe na malumbano ya hovyo. Kuna video ya Mwenyekiti TAL akieleza mfumo wa uchaguzi wa 2020 na jinsi alivyopatikana mbunge mmoja.

Alichokieleza TAL ni kweli , CCM hawakumtaka Mbunge wao lakini pia walitaka kuonyesha sura ya vyama vingi, wakampa Aida Kenan. CCM wangetaka wangemtanganza wanayemtaka, walikuwa na uwezo huo

Hoja ya TAL inaingia ukakasi anaposema Aida Kenan hajui kama aliwahi kuzungumza nini Bungeni.

Mwenyekiti TAL anaweza kuwa na ''bifu' au duku duku na jinsi Aida alivyokubali kwenda Bungeni. Anachopaswa kuelewa Aida ni kiongozi wa Chama.

Uchaguzi wa BAWACHA Aida alisimamia vizuri sana. Hata kama akiwa Bungeni hakufanya aliyotarajia TAL, huo ni upungufu wa kibinadamu, aikufaa kabisa kumdhalilisha. TAL anapaswa kumuomba Msamaha

Katika kampeni ya Tone Tone, Aida Kenan (MB) anaweza kuwasaidia sana na kama kiongozi wa Chama. Mchango wake usidogoshwe. Inapotokea TAL kama Mwenyekiti anatoa kauli kali dhidi ya Mwanamke, huku BAWACHA wakiwa pembeni, kuna tatizo! ni kama anathibitisha kinachosemwa.

Hii ni last call, siyo BAVICHA siyo BAZECHA! ni BAWACHA ndio wajenzi wa Brand ya CHADEMA
 
BAWACHA NA SIKU YA WANAWAKE
TAL ''AONJA'' NGUVU YA BAWACHA


Siku ya Wanawake imeadhimishwa duniani. Moja ya matukio hapa nchini ni la Wanawake wa CHADEMA kufanya kongomano. Miongoni mwa walioshiriki wametoka mikoani wakiwemo viongozi wa zamani

BAWACHA wanajiita ''jeshi kubwa'' na shughuli yao siku zote ni pevu.
Mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa CHADEMA , Mh TAL ambaye alifanya matukio mawili muhimu

1. Kwanza, kutambua mchango wa Mbunge Aida Kenan aliyepewa tuzo na Wanawake wenzake.
Kitendo hicho ni cha kiungwana na kimesaidia kuondoa ukakasi wa kauli za TAL alizotoa kumdogosha.

Hata hivyo TAL atambue kwamba , Wanawake wanampomtambua mwenzao ni ishara ya kumthamini

2. TAL kama kawaida yake alinyooka kuhusu mfumo wa Utawala unaowatenga Wanawake.
Katika hili hakuacha ukweli kwamba CHADEMA kama ulivyo mfumo wa nchi inamapangufu katika safu ya uongozi kwa upande wa Wanawake.

Haikuwa kauli rahisi lakini TAL aliitoa akisema '' wanapowanyooshea vidole wengine nao wanapaswa kujitathmini''. Ni kauli ya kiungozi haswa ! kukiri mapungufu ni sehemu ya kujitathmini

Kuna swali la kujiuliza! kwanini TAL alipoteua viongozi wa Sekretariati ikiwemo Katibu Mkuu na Manaibu wake hakuliona jambo hili?

Pengine kwa kuona nguvu waliyo nayo BAWACHA , TAL anabaini kitu alichokuwa hakioni.
Hapa ndipo anapaswa kuanzia!

Kwamba, '' Wanawake ni Jeshi kubwa'' basi majemedari wa kumsaidia watoke katika jeshi hilo pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…