CHADEMA na Minyukano : Fursa , Makosa na Anguko

CHADEMA na Minyukano : Fursa , Makosa na Anguko

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Posts
15,773
Reaction score
32,431
Mpambano wa FAM na TAL una afya
''Chawa Wanashona Sanda, Wapambe wanachimba kaburi


Kwa wiki, habari zinazotamalaki ni mpambano wa Uenyekitiki wa CHADEMA (CDM) kati ya Mh Mbowe (FAM) na Mh Lissu (TAL). Mvutano kati yao umepandisha joto la siasa nchini kuliko wakati mwingine.

Joto la siasa limezaa kinachojulikana kama (The good, the bad and the ugly) kwa tafsiri isiyo rasmi 'uzuri, ubaya na ubovu' kwa maana katika utatu lipo jema , baya na bovu. Huo ndio msingi wa kusema kuna fursa, makosa na kisha anguko!

CDM wanaita ''minyukano ndani ya chama''. Mwandishi Mark Twain aliwahi kusema '' History never repeats itself, but it does often rhyme'' akimaanisha tukio halitokei tena katika hali ile ile lakini mara nyingi laweza kuwa na ufanano sana unaoleta hisia kama zile za awali

Waziri mkuu wa Uingereza Bw. W.Churchill alisema '' study history, study history. In history lies all the secrets of statecraft'' akimaanisha jifunze historia, ndani yake yapo maarifa ya kiutawala

Sehemu ya I: Historia ya minyukano
Si rahisi kupitia matukio kwa kina au usahihi wake hata hivyo ni muhimu tukapata ufahamu wa nini kilitokea ili tujifunze na tuoanishe na mnyukano uliopo

NCCR , kamati ya kupigania mageuzi ya katiba na mifumo ya nchi, baadaye ikawa chama cha siasa NCCR-Mageuzi. Masumbuko Lamwai (R.I.P) akawa diwani, kisha Mbunge akiwa na Mabere Marando. CCM ikaingia mtafaruku na Mrema aliyehamia NCCR-Mageuzi. Uchaguzi wa 1995 NCCR ilikuwa tishio hadi CCM walipofanya ''maarifa' yao!

Bundi akatua NCCR, mgogoro wa uongozi kati ya ' Wasomi na Mrema'' ukazuka.
Mkutano wa Tanga ukaisha kwa ngumi na mateke. Mrema akatambua hatma si nzuri akatimkia TLP.

NCCR ikabaki na makovu makubwa kwasababu Mrema alikuwa na Wafuasi.
Mh J.Mbatia na S.Mvungi ( R.I.P) wakajitahidi kukirejeshea chama uhai.

Katika Uchaguzi wa Mwenyekiti uliofanyika Diamond na kuonyeshwa na TV, kila Mtanzania alikubali kwamba NCCR-Mageuzi ilifanya uchaguzi bora sana ukiwa na uhindani wa hoja na si matusi.

Mwenyekiti Mbatia akafanikiwa kuirudisha NCCR katika ''ramani'.

Kosa la mbatia ni kufanya ' Maridhiano' na JPM. Kwa ukubwa wa makovu ya siku nyuma , NCCR ikawa '' vulnerable'' ikishambuliwa na CCM kwa msaada wa Ofisi ya vyama! NCCR imebaki katika kabrasha.

Minyukano haikuiacha NCCR salama ingawa ilidhaniwa itatoka salama kwa ukubwa wake.

CUF: Minyukano kati ya Maalimu Seif (R.I.P) and J.Mapalala (R.I.P). Mgogoro ukamhusisha Hamad Rashid, Maalimu alikuwa na Prof Lipumba. Katika hali isiyotarajiwa Lipumba akakacha CUF.

Maalimu akafanya kosa la kifundi, akabaki na chama akiwa yeye ndiye taasisi.
Lipumba akarejea na kutumia hoja za kiufundi akisaidiwa na CCM, Mahakama na Ofisi ya vyama.

Maalimu Seifu hakuwa na pa kutokea, akatimkia ACT Wazalendo. CUF ikabaki na makovu ya minyukanano na haijawahi kutengemaa tena. Minyukano haijaiacha CUF Salama.

UDP: Chama kilichokuwa na nguvu kanda ya ziwa. Mgogoro ukazuka kati ya Mwenyekiti M.Cheyo na Amani Nzugile (Jidulamambambasi). Mh Cheyo akapigiwa pande na CCM.
DP ikabaki mfukoni kwa Cheyo. Minyukano haijaiacha UDP Salama.

ACT Wazalendo: Uchaguzi ukamhusisha Babu Duni na Othman Masoud (OMO).
Duni akionekana mwanafunzi aliyefuzu wa Maalimu. OMO akionekana msomi mwenye misimamo mikali. Busara ikatumika, Duni ''akatema Bungo'' si kwa hiari, ni kwa shari.
Tayari kulikuwa na minyukano iliyotishia kukigawa Chama. Busara zikanusuru madhara

CHADEMA:
Waheshimiwa Mtei na Makani katika uongozi kwa miaka 10. Mh Mbowe akachukua uongozi 2003.

C.Wangwe akaonyesha nia ya kutaka kiti, mtafaruku ukarindima. Bahati akafariki kwa ajali ya gari.

Zitto Kabwe akisaidiwa na K,Mkumbo na Mwigamba wakaanda mpango kimya kimya.
Hoja zao zilikuwa na mashiko, namna waliyotaka kutekeza mpango ilikuwa ni hovyo, hawakuungwa mkono.

Mh F.Sumaye akagombea nafasi ya kanda. Tetesi zikaenee anautaka uenyekiti.
Katika hali ya kushangaza aligaragazwa 'mchangani' katika kanda na ilikuwa 'inside job' ikiongozwa na ' Vijana' watiifu.

Mwaka huu, TAL akijua mbinu nyingi chafu alivuta muda na kushtukiza dakika za mwisho, anautaka uenyekiti. Hili ndilo chimbuko la mnyukano ambao ni mkubwa kuliko misuko suko ya nyuma!

Je, mnyukano huu utaibeba CDM au historia itajidhihiri kwa namna ile ile ingawa si kwa chama kile kile!

Sehemu ya II inafuata
 
Mpambano wa FAM na TAL una afya
''Chawa Wanashona Sanda, Wapambe wanachimba kaburi


Kwa wiki, habari zinazotamalaki ni mpambano wa Uenyekitiki wa CHADEMA (CDM) kati ya Mh Mbowe (FAM) na Mh Lissu (TAL). Mvutano kati yao umepandisha joto la siasa nchini kuliko wakati mwingine.

Joto la siasa limezaa kinachojulikana kama (The good, the bad and the ugly) kwa tafsiri isiyo rasmi 'uzuri, ubaya na ubovu' kwa maana katika utatu lipo jema , baya na bovu. Huo ndio msingi wa kusema kuna fursa, makosa na kisha anguko!

CDM wanaita ''minyukano ndani ya chama''. Mwandishi Mark Twain aliwahi kusema '' History never repeats itself, but it does oftern rhyme'' akimaanisha tukio halitokei tena katika hali ile ile lakini mara nyingi laweza kuwa na ufanano sana unaoleta hisia kama zile za awali

Waziri mkuu wa Uingereza Bw. W.Churchill alisema '' study history, study history. In history lies all the secrets of statecraft'' akimaanisha jifunze historia, ndani yake yapo maarifa ya kiutawala

Sehemu ya I: Historia ya minyukano
Si rahisi kupitia matukio kwa kina au usahihi wake hata hivyo ni muhimu tukapata ufahamu wa nini kilitokea ili tujifunze na tuoanishe na mnyukano uliopo

NCCR , kamati ya kupigania mageuzi ya katiba na mifumo ya nchi, baadaye ikawa chama cha siasa NCCR-Mageuzi. Masumbuko Lamwai (R.I.P) akawa diwani, kisha Mbunge akiwa na Mabere Marando. CCM ikaingia mtafaruku na Mrema aliyehamia NCCR-Mageuzi. Uchaguzi wa 1995 NCCR ilikuwa tishio hadi CCM walipofanya ''maarifa' yao!

Bundi akatua NCCR, mgogoro wa uongozi kati ya ' Wasomi na Mrema'' ukazuka.
Mkutano wa Tanga ukaisha kwa ngumi na mateke. Mrema akatambua hatma si nzuri akatimkia TLP.

NCCR ikabaki na makovu makubwa kwasababu Mrema alikuwa na Wafuasi.
Mh J.Mbatia na S.Mvungi ( R.I.P) wakajitahidi kukirejeshea chama uhai.

Katika Uchaguzi wa Mwenyekiti uliofanyika Diamond na kuonyeshwa na TV, kila Mtanzania alikubali kwamba NCCR-Mageuzi ilifanya uchaguzi bora sana ukiwa na uhindani wa hoja na si matusi.

Mwenyekiti Mbatia akafanikiwa kuirudisha NCCR katika ''ramani'. Kosa la mbatia ni kufanya ' Maridhiano' na JPM. Kwa ukubwa wa makovu ya siku nyuma , NCCR ikawa '' vulnerable'' ikishambuliwa na CCM kwa msaada wa Ofisi ya vyama! NCCR imebaki katika kabarasha.

Minyukana haikuiacha NCCR salama ingawa ilidhaniwa itatoka salama kwa ukubwa wake.

CUF: Minyukano kati ya Maalimu Seif (R.I.P) and J.Mapalala (R.I.P). Mgogoro ukamhusisha Hamad Rashid, Maalimu alikuwa na Prof Lipumba. Katika hali isiyotarajiwa Lipumba akakacha CUF.

Maalimu akafanya kosa la kifundi, akabaki na chama akiwa yeye ndiye taasisi.
Lipumba akarejea na kutumia hoja za kiufundi akisaidiwa na CCM, Mahakama na Ofisi ya vyama.

Maalimu Seifu hakuwa na pa kutokea, akatimkia ACT Wazalendo. CUF ikabaki na makovu ya minyukanano na haijawahi kutengemaa tena. Minyukano haijaiacha CUF Salama.

DP: Chama kilichokuwa na nguvu kanda ya ziwa. Mgogoro ukazuka kati ya Mwenyekiti M.Cheyo na Amani Nzugile (Jidulamambambasi). Mh Cheyo akapigiwa pande na CCM.
DP ikabaki mfukoni kwa Cheyo. Minyukano haijaiacha DP Salama.

ACT Wazalendo: Uchaguzi ukamhusisha Babu Duni na Othman Masoud (OMO).
Duni akionekana mwanafunzi aliyefuzu wa Maalimu. OMO akionekana msomi mwenye misimamo mikali. Busara ikatumika Duni ''akatema Bungo'' si kwa hiari, ni kwa shari.
Tayari kulikuwa na minyukano iliyotishia kukigawa Chama. Busara zikanusuru madhara ya minyukano.

CHADEMA:
Waheshimiwa Mtei na Makani katika uongozi kwa miaka 10. Mh Mbowe akachukua uongozi 2003.

C.Wangwe akaonyesha nia ya kutaka kiti, mtafaruku ukarindima. Bahati akafariki kwa ajali ya gari.
Zitto Kabwe akisaidiwa na K,.Mkumbo na Mwigamba wakaanda mpango kimya kimya.
Hoja zao zilikuwa na mashiko, namna waliyotaka kutekeza mpango ilikuwa ni hovyo, hawakuungwa mkono.

Mh F.Sumaye akagombea nafasi ya kanda. Tetesi zikaenee anautaka uenyekiti.
Katika hali ya kushangaza aligaragazwa 'mchangani' katika kanda na ilikuwa 'inside job' ikiongozwa na ' Vijana' watiifu.

Mwaka huu, TAL akijua mbinu nyingi chafu alivuta muda na kushtukiza dakika za mwisho, anautaka uenyekiti. Hili ndilo chimbuko la mnyukano ambao ni mkubwa kuliko misuko suko ya nyuma!

Je, mnyukano huu utaibeba CDM au historia itajidhihiri kwa namna ile ile ingawa si kwa chama kile kile!

Sehemu ya II inafuata
Edit DP to UDP.
 
Sehemu ya II
Fursa: CDM, Chama kinachojinasibu na demokrasia kimepata fursa inayotokea kwa nadra sana.

Kwanza, uwepo wa Wagombea wa nafasi kubwa kama ni kielelezo cha ukuaji wa Chama.
Pili, kutoa nafasi za Wagombea na si '' form 1' ni fursa ya kufundisha demokrasia nchini zaidi ya CCM
Tatu, kwa wiki mbili habari ni za CDM , CCM haisikiki tena. Hii ni 'publicity' ya hali ya juu sana.
Nne, ni nafasi pekee ya kuondoa hofu kwa Umma kuhusu utayari wa CDM kama taasisi.

Ushindani ndani ya Chama ni jambo lenye afya, na hili lingeweza hata kuiambukiza CCM.
Kwa mtazamo wowote, ushindani kati ya FAM na TAL ni afya kama utaangaliwa kwa umakini.

Vyama vya siasa lazima vije na miundo tofauti na ile ya CCM ikiwemo '' Form 1' na vikao vya kitapeli tu huku watu wakiwa na majina yao mifukoni ( rejea sakata la Ed Lowassa).

Makosa: Katika mnyukano unaoendelea kuna makosa yanajitokeza yasiyo ya lazima kwa pande zote.
Makosa yanatokana na minyukano katika mitandao ya kijamii inayotengenezwa na makundi mawili

1. ''Kundi la Chawa'' ( KLC): Wanatumia mbinu zile zile ''character assassination''. KLC linamuunga mkono Mwenyekiti FAM likiamini lina nguvu na mbinu nyingi. KLC wanaamini katika nguvu ya Mwenyekiti. Kuingia kwa TAL dakika za mwisho limewaweka KLC ''off guard''

KLC kumuunga mkono FAM si tatizo. Kwa bahati mbaya KLC wameshindwa kutoa hoja au kutetea uamuzi wa FAM kuendelea. Ikitokea wanajaribu , hoja zao ni dhaifu.

Kwa mfano, kwamba FAM aendelee kwasababu ana pesa!!!

Na kwavile KLC hawana hoja, ombwe linazibwa na matusi na kashfa.
Viongozi wa juu akiwemo FAM wameshindwa kukemea KLC au kuwajenga kwa hoja

2. Kundi Wapambe (KW). Wamauunga mkono TAL na wengi ni '' Wanaharakati'' na Wahafidhina.
KW wana uwezo wa kumjengea hoja nzito TAL kwanini awe mwenyekiti.

Kwa makosa, KW wanaingia mtego wa kujibu hoja za KLC kwa ghadhabu na matusi.

KW lina watu wenye misimamo mikali hata kama jahazi linazama! KW wanaamini katika Taasisi

Makundi yote mawili yana tatizo moja, upofu.
CDM itaendelea hata baada ya uchaguzi.Viongozi na Wanachama wa makundi mawili watafanya kazi kwa pamoja. Kubomoana hakutoi nafasi yoyote ya ustawi wa Chama siku za baadaye.

Minyukano ya makundi hayo imetoa nafasi kwa CCM kuingilia kati na kuchomeka yao kama ilivyokuwa siku za nyuma. CCM sasa wana 'upande' wanaoutaka! na wanachochea moto hasa

Ikiwa FAM na TAL hawatakemea makundi yao, CDM itaingia hatua ya mwisho , Anguko.

Kwa hali ilivyo sasa ikiwa FAM na TAL hawatakubaliana kushindana kwa hoja, wakaruhusu Chawa na Wapambe waendeleze ubabe, kilichotokea NCCR, CUF, DP, ACT hakiepukiki! Anguko

Je, CHADEMA wana nafasi ya kufanya uchaguzi bora na kubaki salama!

Itaendelea
 
Sehemu ya III
Mtazamo wa FAM na TAL kwa CDM ijayo.

Tutazame hoja za wagombea na si 'Chawa au Wapambe'

Mbowe (FAM)
Majuzi alitembelewa na wafuasi wake wakimtaka agombee, FAM akaomba saa 48 za kutafakari
Wafuasi walimtembelea FAM kukiwa na maandalizi, baadhi wakisema waliitikia wito wa Mwenyekiti!!

Jumamosi, FAM akaita mkutano wa Wahariri wa vyombo vya habari kuutaarifa Umma kuhusu tafakuri.
Ni kawaida viongozi kuita Wanahabari wakiwa na jambo popote, hivyo hakuna tatizo na mwito.

Mshangao ni jinsi mkutano ulivyoandaliwa kiufundi ( well choreographed) chini ya mwenyekiti wa Wahariri Bw. Balile akiwa ''MC'. Kwa mazingira ya kawaida, FAM na timu yake(wenyeji) walipaswa kuongoza shughuli si Wahariri!

Balile ana historia tata akinyooshewa vidole katika mambo kadhaa. Wiki chache zilizopita Balile akiwa na Mzee Warioba alihoji kuhusu Wapinzani kushindwa kusimamisha wagombea bila kugusia chochote kuhusu kuenguliwa.
Balile alionekana kujitetea zaidi kana kwamba alihisi '' back lash'' kwa kazi ya ushereheshaji shughuli ya FAM

Mkutano wa FAM ulihudhuriwa na vyombo vya habari vya Umma, kawaida, rafiki na hata mahasimu wa CHADEMA.
Wenyeviti wa kanda za CDM (isiookuwa Pemba) walihudhuria bila kuelezwa ni kwa nafasi ipi ! ya kichama au kirafiki.

Washiriki waliokosekana ni KM JJ Mnyika, na Naibu KM B.Kigaila. Kwa nafasi zao, pengine wanataka 'neutrality'. Mahojiano ya Kigaila na k TV yana maswali mengi kuhusu 'neutrality' na mgongano wa masilahi (conflict of interest)

Mitandaoni kulikuwa na shauku kubwa !Mahasimu wa CDM walifuatilia kwa makini mkutano wa FAM na kuonyesha kuridhishwa na shughuli nzima ikiwemo tamko la uchukuaji wa Form.

FAM alieleza historia ya mapambano na harakati kuikuza CDM kwa miaka takribani 30, msisitizo ukiwa Indhara, madhila na hasara alizopitia. FAM alijibu tuhuma dhidi yake na TAL bila kueleza nini atafanya tofauti na miaka 21 iliyopita.

FAM alieleza msimamo wake wa kati (moderate) akiegemea maridhiano (reconciliation), falsafa na mrengo wa CDM (Centre right) mambo yaliyoibua kundi linalompinga likiongozwa na TAL, linaloamini katika ''Radicalism''

FAM alijibu hoja ya ukomo wa uongozi kwa mantiki. Mapungufu yake ni kutoeleza kwanini anataka Uenyekiti baada ya miaka 21, kutoeleza mfumo wa kifeddha unaolalamikiwa ikiwa ni pamoja na fedha za ''join the chain''. FAM hakueleza kwanini mikakati ya maridhiano imefeli na kwanini bado anaamini katika maridhiano licha ya kupigwa changa la macho kila mara.

Inaendelea... TAL
 
Tundu Lissu (TAL)

TAL alifanya mkutano baada ya kuchukua ''Form'' akieleza ni kwanini anataka kugombea.
Kama alivyofanya FAM, TAL aliungwa mkono na Wafuasi wake. Mkutano ulikuwa wa kawaida bila ''coverage''

TAL akama FAM alieleza historia yake akisisitiza uadilifu kwa kunukuu katiba ya Chama chake. Hotuba yakeilikuwa ya kifundi sana akitembea juu ya katiba na kuchagua maneno yake kutoka kwenye katiba.

Tofauti na FAM, TAL alieleza maono 5 anayodhani ni muhimu kwa Chama katika nyakati hizi;

1. Kuamsha ari ya Wanachama kwa kuwa na uongozi wenye mbinu mpya, uadilifu na misimamo thabiti

2. Maboresho ya katiba na ukomo wa viongozi ili kuwa na mawazo mapya, kuondoa uchawa na upambe na kuweka ukomo wa Viti maalumu kwa Wabunge na Madiwani kwa kuandaa viongozi wapya na kuwafanya wazamani watafute fursa nyingine ndani ya Chama.

3. Kukifanya Chama kifuate Katiba. Chama kitengeneze mfumo huru na wa haki kuendesha chaguzi zake

4. Kuunda kitengo kitachokuwa na jukumu la kutafuta rasilimali na kuratibu shughuli za matumizi ya fedha

5. Kuunda upya sekretariati za chama ngazi ya Taifa na Kanda ili kuongeza ufanisi na uwajbika nje ya makao makuu.

Mambo aliyoeleza TAL yanahusiana na falsa ya ''radicalism'' kwamba ili CDM kitoke kilipo lazima kuwepo na mageuzi ya kimifumo. Mfano,TAL anaeleza kwamba utawala wa nyakati za sasa ni wa kiimla, maridhiano hayana nafasi yoyote ya kuleta mabadiliko.

Kuhusu Chaguzi, TAL amerudia akisema Chama kimeacha kufuata Katiba na chaguzi zina kasoro.
Katika hilo ameshauri kuunda chombo kitakachosimamia uchaguzi akisema aliyeshindwa akubali na akikata rufaa isikilizwe na chombo huru na kwa wakati.

Kwa mtazamo wetu hapa duru, TAL anazungumzia uchaguzi wa kanda ya nyanda za juu kusini uliomhusisha Msigwa katika kanda na Rose Mayemba katika mkoa. TAL anatoa hisia kwamba rufaa ya Msigwa haikusikilizwa na chombo huru na kwa wakati.

Tunakumbuka B.Kigaila akilalamikiwa kuingilia uchaguzi huo akiegemea kambi ya FAM na ndiye anaratibu shughuli za rufaa. Hali ipo hivyo kwa mkoa wa Njombe ambako Rose Mayemba aliyetangaza kumuunga mkono Msigwa katika kanda, rufaa yake haijasikilizwa hadi leo kwasababu tu yupo kambi tofuati na ile ya FAM

Kwanini TAL amesisitiza sana uchaguzi?
Jibu ni kwamba anapoelekea uchaguzi wa Mwenyekiti anaingia kama ''underdog''.

Licha ya ukubwa wa jina lake, mifumo tayari ilishaandaliwa kuteka Wajumbe wa Mkutano mkuu kupitia chaguzi. Waratibu wa shughuli hizo ni Watendaji wa makao makuu , KM na Manaibu KM na Sekretariati nzima.

Naibu KM Kigaila katika mahojiano na TV moja ameonyesha wazi udhaifu katika uongozi pamoja na 'conflict of interest'' hasa ya mkewe ambaye ni miongoni mwa COVID-19. Alishindwa kutetea hoja kwa mantiki !

FAM kama M/kiti aliyepo ''incumbent' ana fursa (advantage) zinazotokana na nafasi yake. Hata hivyo, kuwaita Wenyeviti wa kanda kwa shughuli binafsi za kuchukua Fomu si sahihi. Kwanini Watendaji hawakumweleza!

Kwa mantiki, KM na Manaibu wake ndio Waratibu wa uchaguzi wa January.
Hata kama watakuwa waadilifu kiasi gani,kuna wasi wasi juu yao, si tu kwa uchaguzi hata pale rufaa itakapoletwa na yeyote. Kwa maneno machache, KM na Sekretariati yake hawana credibility au integrate ya kusimamia uchaguzi wa January. Huu ndio msingi wa hoja kubwa ya TAL na ina mantiki.

Ili kuwa na uchaguzi huru hapo January, tunashauri yafuatayo

Inaendelea sehemu ya IV
 
Sehemu IV

Uchaguzi Huru na wa Haki

Mnyukano CDM umetengeneza mazingira ya kutoaminiana.
Uchaguzi wa January unapaswa ufanyike bila madoa.

TAL amesisitiza sana suala la chombo huru cha uchaguzi na kufuatwa kwa katiba.
Tumesema awali, kuelekea January 20 TAL ni ''underdog''.
Zipo kauli na matendo ''yanayoashiria'' haki haitatendeka hata kama ni dhana tu ya kufikirika

1. Kwamba M/kiti anapaswa awe na pesa.
Kauli hii inajenga dhana kwamba pesa zitatumika katika hongo za uchaguzi

TAL alituhumu rushwa ndani ya chama. Inapodhaniwa ' kwamba ' Kiongozi wa chama lazima awe na pesa', ni ngumu kuondoa dhana ya rushwa katika mawazo! hata kama si kweli

2. Wenyeviti wa kanda kuhudhuria shughuli binafsi ya Mwenyekiti
Kwamba FAM na timu yake wametumia chaguzi kujenga mtandao utakaokwenda mkutano mkuu.

TAL anasema chaguzi zisizo huru zinatoa viongozi ''Chawa'' .
Kuna dhana kwamba Wajumbe wa mkutano mkuu wameapatikana katika mazingira ya rushwa

3. Kukosa imani na ''sekretariati' iliyopo kwasababu ya 'experience' ya mauza uza ya chaguzi zilizopita.
Hapa kuna tatizo.

TAL anasema , rufaa hazishughulikiwi kwa wakati. Mfano hai ni rufaa ya Rose Mayemba.
Vikao vinakaa lakini rufaa haijadiliwi kwasababu Rose si timu ya FAM. Sekretariati nzima ni timu ya FAM
Kuna dhana kwamba sekretariati inatumika kuhujumu walio nje ya timu FAM kama Rose Mayemba.

January 20
Hoja 1 na 2 zinaweza kuwa kweli au dhana, si hoja zenye nguvu.

Hoja ya 3 ina nguvu sana. Timu ya Watendaji makao makuu haiwezi kuwa '' fair'' katika uchaguzi ikijulikana pasi na shaka ni timu FAM yenye masilahi mengi yanayohitaji kulindwa.
sekretariati ina shtuma za fedha, ina mwingiliano wa masilahi na imekosa viongozi wenye weledi

Hakuna namna sekretariati iliyopo ikasimamia uchaguzi kwa uhuru na haki.
Kuna 'bias' tayari na hii inatoa ''credence'' kwamba sekretariati ni timu FAM.
Hata kama uchaguzi utakuwa huru, dhana hiyo haiwezi kuepukika na itakuwa doa

Ili kuepusha matatizo na uchaguzi uwe huru na haki sekretatiati ya makao makuu isihusishwe na uchaguzi.

Iundwe kamati maalumu ya kusimamia uchaguzi kwa muundo utakao ondoa shaka

1. FAM ateue viongozi wawili wa dini kutoka Waislam na Wakristo wakiwakilisha madhehebu yao mengine
2.TAL ateue viongozi wawili wa dini kutoka Waislam na Wakristo wakiwakilisha madhehebu yao mengine
3. Wawakilishi 2 kutoka chama cha wanasheria( TLS), FAM ateue mmoja na TAL ateue mmoja
4. Wawakilishi 2 binafsi, kutoka kwa FAM na TAL kila mmoja
5. Mzee Mmoja mwenye heshima kutoka katika jamii atakayekubaliwa na wote wawili, FAM na TAL

Hapo kutakuwa na Wajumbe 9 wanaowakilisha pande mbili bila kuacha chembe ya shaka.
Bila kufanya hivyo, Uchaguzi utafanyika lakini Chama hakitaepuka yale ya CUF, NCCR. UDP n.k.

Kuelekea 2025 Uchaguzi mkuu, itachukua muda mrefu kukijenga chama kilichopata makovu na hilo ndilo litakuwa anguko.

Hakuna namna uchaguzi utafanyika katika mazingira ya sasa, ukakiacha chama salama! hakuna!

Nini kinaweza kutokea baada ya uchaguzi wa January 20?

Itaendelea...
 
Sehemu V
Yaliyojiri mkutano wa Tundu Lissu (TAL-Club House & Maria Space)

Baada ya bandiko IV mjadala umefanyika club house na Maria space, TAL akiwa mzungumzaji mkuu.
Hoja na maswali yamefafanuliwana TAL lakini tutarejea yale tuliyojaili bandiko IV hapo juu

1. TAL amesema wazi hana imani na Usimamizi wa Uchaguzi. TAL amefafanua Katiba ya Chadema inasema '' Uchaguzi mkuu utasimamiwa na Wazee wastaafu wa Chama kwa kushirikiana na sekretariati''

TAL anauliza, Wazee wa Chama kwa sasa ni akina nani!

TAL akaeleza kwamba Sekretariati ina majukumu muhimu katika uchaguzi lakini TAL muundo wake ni chaguo la Mwenyekiti FAM aliyeteua Katibu mkuu na manaibu wake kisha kuthibitishwa na Baraza kuu.

TAL hakuficha ukweli kwamba JJ Mnyika (KM), B.Kigaila (N-KM Bara), S.Mwalimu (N-KM Zanzibar) J.Mrema ni Timu ya FAM hivyo hawana integrity ya kuwa sekretariati ya Chama inayosimamia uchaguzi.

TAL ameshauri na kusisitiza Uchaguzi usimamiwe na ;
1. Viongozi wa dini
2. Wana Diplomasia
3. Msajili wa Vyama

Katika bandiko IV tuliorodhesha makundi 5 yanayoweza kusimamia uchaguzi.
Kwa mtazamo pengine makundi ya bandiko IV na ya bandiko V yangechanganywa ili muundo uwe;
1. Viongozi wa dini
2. Wawakilishi- Diplomasia
3. Wanachama wa TLS
4. Msajili wa Vyama

Ikiwa kuna wanaodhani hilo si jambo sahihi, je, Wazee wastaafu kikatiba ni akina nani?

Sekretariati ya JJ.Mnyika ipewe majukumu ya kawaida lakini pia inatakiwa iwe na wawakilishi wa TAL
Kikatiba inaweza kuwa si sahihi kwani sekretariati ni chombo cha kikatiba, lakini katika mazingira yaliyopo kujenga imani na uaminifu ndio jibu pekee la kuinusuru CDM

TAL ametaka pia uchaguzi ufanyike mchana na kwa uwazi.
Wajumbe wa Mkutano mkuu wasafirishwe na kuhudumiwa na Chama na si kujihudumia kukuzi rushwa.

Kwa ujumla TAL ameonyesha hofu ya ''hujuma'' katika uchaguzi kama tulivyoeleza na hilo linaweza kuwa tatizo kubwa sana. Uchaguzi unatakiwa utoe matokeo yanayokubaliwa,kinyume chake ni anguko la CDM

2. TAL amejibu swali la uchaguzi mkoa wa Njombe ukimhusisha Rose Mayemba.
Amesema Sekretariati ya CDM makao makuu ina figisu kwavile Rose siyo Team FAM.
TAL ametumia nafasi ya swali kuonyesha jinsi akina B.Kigaila wanavyomhujumu Rose Mayemba

Amesisitiza kwamba M/kiti alipaswa kuingilia kati na kimya ni kukubali uhuni wa Sekretariati -Kigaila.

Mahojiano na TAL yalikuwa na mambo mengi lakini kubwa lililojitokeza ni kuhusu '' Maridhiano na CCM''
TAL akiitumia hoja hiyo kikamilifu anaweza kubadilisha mawazo ya wajumbe! ni hoja inayoonekana kumwelemea FAM na timu yake haijaweza kuja na majibu!

Nini kinaweza kutokea baada ya Jan 20?

Itaendelea
 
Sehemu VI
Kuelekea January 20 nini kinachoweza kutokea

Kuelekea uchaguzi mkuu wa CDM ni wazi Mh Mbowe (FAM) ana nafasi kubwa akiwa ''incumbent'.
FAM ni kiongozi miaka 21 ana mtandao mpana, ame ''groo'' viongozi wengi
FAM ana 'mfumo' mpana wa 'chawa' waliodumu nae kwa muda mrefu
Sekretariati inayombeba kwasababu imeundwa naye

Viongozi wa mabaraza BAWACHA, BAVICHA, BAZECHA wamepatikana chini ya uongozi wa FAM
Wenyeviti wa kanda waliopo ni wanufaika wa mfumo unaomtetea FAM
FAM ni ''icon'' kwamba ukitaja CDM umentaja na kinyume chake

Kuelekea kampeni, FAM anaungwa mkono na CCM kwasababu ni 'moderate'

Tundu Lissu (TAL) ana umaarufu binafsi kwa ujenzi wa hoja za kisheria zenye tafiti
Hoja zimemuheshimisha ndani ya Jamii na nje ya mipaka. TAL ni 'extremist' katika misimamo yake

TAL anaungwa mkono na '' Wapambe' Wanaharakati , reformists and extremists
TAL si maarufu katika Uongozi wa CDM kutokana na ujenzi wa hoja na misimamo mikali
Anaonekana ni kizingiti hasa kwa ''establishment' wanaonufaika na mfumo uliopo

Kupigwa risasi kumenfanya awe ''symbol' ya uonevu na Upinzani katika jamii

TAL ana 'advantage' iliyotengenezwa serikali za CCM kwa kuiandama CDM jambo lilobadilisha ''moderate' kuwa 'extremists' wanaomuunga mkono sasa hivi. Wapambe wa TAL ni Wasomi na Wanaharakati wenye ushawishi sana katika mitandao

Kizazi cha ''90+'' wanahisi kuchelewa wakihitaji ' radicalism'' ndani ya chama

TAL anabebwa na hoja 4. ''
Kwanza ''Maridhiano' yaliyomdhoofisha sana FAM kiungozi.
Uchaguzi wa akina Kigaila ulioudhi sehemu kubwa ya Wanachama
Tatu, matumizi ya rasilimali yasiyo na maelezo ya kuridhisha
Chuki kutoka kwa CCM, jambo linalomtofautisha na FAM

Uchaguzi wa January si 'take away' , utakuwa na ushindani mkali pamoja na ukweli TAL ni underdog.

Ni uchaguzi halali na wa haki tu! ukisimamiwa na kamati au Tume maalumu utakaoiweka CDM Pamoja

Dhana ya 'Chawa' wa FAM kwamba atakaye aondoke kwasababu walikuwepo wakaondoka ni ya hatari sana. Nyakati ni tofauti na hali ilivyo kuna uwezekano wa kutoboa jahazi au kulivunja wagawane mbao.
 
Sehemu VII

Hoja ya ukomo wa madaraka

Hoja inayorindima uchaguzi wa CDM ni ukomo wa madaraka. Hii si mara ya kwanza kujitokeza.
Hoja iliwahi kujitokeza kwa namna tofauti na iligharimu watu japo si moja kwa moja

Katiba ya CDM ilikuwa na ukomo wa madarak kabla ya kufutwa. Mbowe (FAM) na Tundu Lissu (TAL) wanakubaliana kufutwa ukomo kulilenga kukiwezesha chama kukua. Ni hoja yenye mantiki kwa wakati huo

Ni hoja inayoonekana ya CDM lakini madhara yake ni makubwa kitaifa.
Wakati JPM anaongoza kipindi cha pili, Wabunge walizungumzia kubadili katiba ya nchi aongezewe muda.
Hoja yao ilikuwa '' Kama Wananchi wanaona anafaa, aendelee'' Vyama vya upinzani vilipiga kelele kuhusu hilo

Wafuasi wa FAM wanatumia hoja hiyo kuzuia ukomo wa madaraka, wanasahau CCM inaweza kubadili Katiba na kuongeza muda wa Rais.Ikitokea hivyo, Wapinzani watakuwa na hoja gani ya kupinga?

Hoja ya ukomo wa Viti Maalum
Ukomo wa uongozi unaoshauriwa umelenga pia Wabunge wa kuchaguliwa. Tume ya Mzee Warioba ilikua na hoja hiyo. TAL anasema, Wabunge wa Viti Maalumu kwa Udiwani na Ubunge wawe na ukomo.

Hoja ya TAL si ngeni, na iliwahi kuleta matatizo CDM kwa swali la vigezo gani vinatumiwa kupata Viti maalumu.
Mfano Mzuri ni COVID-19 ambao baadhi waligombea , waliposhindwa wakapewa viti maalumu.

Kuweka ukomo wa viongozi kuna faida nyingi.
Kwanza, kujenga mfumo endelevu wa taasis wa kizazi kipya kinachorithi. Hii inaitwa succession plan

Miaka 21 iliyopita Mbowe ali recruit akina Zitto, John Heche, G.Lema , Henje n.k. Kwa umri wanakaribia kumaliza prime time' kipindi chenye nguvu sana na mchemko wa fikra. Miaka 5 baadaye watakuwa Wazee! succession plan ipo wapi? Hata akipatikana kijana kama Pambalu kutakuwa na generational gap! ambalo ni tatizo.

Pili, viti maalum ni kuwaanda Wanawake kugombea majimboni. Ukomo wa miaka 5 utawasaidia kujifunza na kujiweka tayari wakiwa Bungeni. Hili litatoa nafasi kwa Wanawake wengi wadogo kushiriki siasa kabla ya umri na majukumu ambayo ni kikwazo kwao.

Tatu, Ukomo wa viongozi unaondoa Uchawa ambao huviza na kuduma Vijana kufikiri sawa sawa.
Mfano, suala la Rose Mayemba linapigwa dana dana kwasababu Sekretariati ina maslahi yake.

Sekretariati inaona tishio la ajira zao zilizodumu miaka mingi ikiwa FAM hatakuwa Mwneyekiti.
Hata wanaoitwa Chawa, hofu yao si TAL ni hatma yao. Huu uchawa unaharibu taasisi kwa kukosa rotation

Kigezo cha ' kama Wananchi wanataka kiongozi aendelee, kusiwe na ukomo'' hakina mantiki wala mashiko

Waasisi wa CDM waliweka ukomo! Wanaopinga waje na hoja, kuna ubaya gani viti maalumu au Ubunge kuwekewa ukomo? Kuna ubaya gani kiongozi kupewa term limit ya miaka 10? Ni kipi kiongozi atafanya ambacho hakuweza kufanya kwa miaka 10 au 20?
 
Sehemu ya VIII

Mbowe [FAM] ana Haki
Rose Mayemba atendewe Haki


Wiki ya pili tangu Tundu Lissu (TAL) na Mh Mbowe watangaze nia kumekuwa na upotoshaji mkubwa

Kwanza, ni vema na afya kwa Demokrasia kuwa na Wagombea wanaochuana kwa nafasi mbali mbali
Muundo wa kuwa na 'Fomu moja' uliasisiwa wakati wa JPM kipindi cha utawala usiozingatia Demokrasia

Mchuano kati ya FAM na TAL ni jambo zuri , uheshimiwe na uthaminiwe

Pili, kumekuwapo na hoja kwamba Mh Mbowe ajitoe eti kwasababu amekuwa kiongozi miaka 21
Kauli hii ina maana ya kuwarudisha CDM katika utaratibu wa mgombea mmoja au Fomu 1 kama CCM

Upotoshaji mkubwa ni kuhusu ukomo wa nafasi mbali mbali.
Wapo wanaodhani ukomo ni kikwazo kwa Mh Mbowe kugombea.
Haya ni mambo ya kuwachanganya watu bila sababu.
Ukomo uliondolewa kikatiba na hadi leo Katiba ya CDM haina ukomo. Ni haki kwa Mh FAM kugombea

Kinachosemwa ni maono, kwamba, Katiba iweke ukomo na hiyo ndiyo hoja ya TAL.
Lini litafanyika ni suala jingine lakini kwa maono yake atahakikisha kuna ukomo. Hii ni kwa nyakati zijazo baada ya uchaguzi

Rose Mayemba
Chaguzi za kanda zilijaa vituko vingi nje ya Katiba ya CDM. Maafisa kutoka makao makuu walitumwa kusimamia chaguzi na aliyjitokeza sana ni B Kigaila.

Huyu aliingilia uchaguzi wa kanda ya Nyasa kwa cheo kisichotajwa kikatiba.
Kigaila ni chanzo cha malalamiko akitajwa kumwakilisha M/Kiti

Uchaguzi wa Njombe umefanyika mara Mbili mbele ya Kigaila na umeshindikana.
Kigaila amefumbia macho vurugu zilizotokea ikisemwa '' anatimiza maelekezo''. Iwe ni kweli au la, Kigaila ni Mhusika

Inaelezwa , Rose Mayemba amekata rufaa lakini sekretariati imekaa kimya.
Rekodi zinaonyesha Rose alimuunga mkono Msigwa katika uchaguzi wa kanda ya nyasa.

Haijulikani kwanini suala la Njombe limbaki kuwa kitendawili na ni ugumu gani usioweza kutatuliwa na sekretariati au Mwenyekiti wa CDM au Kamati kuu

Wanaotilia shaka uchaguzi ujao wanatoa mfano wa kesi ya Rose kama kielelezo cha Sekretariati ya CDM ya akina JJ Mnyika na Afisa Chaguzi Naibu KM B.Kigaila kuwa corrupt and compromised na kwamba imepoteza sifa za kuratibu au kuwa sehemu ya uchaguzi mkuu

Ni wakati Katibu Mkuu Mnyika na Mwenyekiti FAM walitolee ufafanuzi suala hili.

Kinyume chake wanaoeneza habari za kuvurugwa uchaguzi kwa kutumia sekretariati watakuwa na hoja tena yenye mashiko na nguvu
 
Mkuu Nguruvi3

Uongozi wa CDM ukijumuisha mwenyekiti na makamu wake ambao wanaenda kuchuana unastahili lawama kwa kuruhusu hali hii ya minyukano kuelekea uchaguzi. Timing ya uchaguzi sio nzuri ikiwa imebaki miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu na sioni yeyote kati yao atakaeshinda ambae ataweza kukiunganisha chama na kuponya majeraha ya hii minyukano kabla ya uchaguzi mkuu na itawagharimu sana!

Mbowe ameshindwa kusoma alama za nyakati alipaswa kujiandaa mapema na vema zaidi namna atakavyosimamia suala la uchaguzi na uamuzi wa yeye kugombea au la... Ile drama ya wafuasi kumtembelea nyumbani eti kumuomba agombee na yeye kusema apewe masaa 48 inaonesha uzito wa maamuzi upande wake.

Kwa upande wa TL, pamoja na hoja zenye mashiko alizotoa ikiwemo tuhuma dhidi ya uongozi hususan mwenyekiti najiuliza anazitoa kama mwanachama wa kawaida au makamu mwenyekiti? Anataka kutuaminisha kwamba kwa kipindi chote akiwa makamu amekuwa hahusishwi kwenye maamuzi ya chama? Kama jibu ni ndio basi alipaswa kujivua wadhifa wake muda mrefu akawasilishe hoja zake kwa wanachama THEN aje kum-challenge mwenyekiti kwenye uchaguzi... Kinyume na hapo ni yeye kukwepa collective responsibility na kutaka kumtwisha mwenyekiti wake madhambi yote ya chama ambapo yamkini na yeye ni mshiriki! Na hii naiona kama udhaifu wa kiuongozi kwa upande wake.

All in all bundi ameshatua CDM, sumu imeshamezwa na inasambaa kwa kasi, yeyote atakaeshinda kiti ana kibarua kizito kuunganisha chama kabla ya uchaguzi na wamewarahisishia kazi CCM!

Mbowe's political career is heading towards the end whether he wins or not... TL has various options akishindwa anaweza kwenda ACT, CCM au akaanzisha chama kipya na hapo ndio itakuwa kipimo cha impact yake kama mwanasiasa.
 
Mkuu Nguruvi3

Uongozi wa CDM ukijumuisha mwenyekiti na makamu wake ambao wanaenda kuchuana unastahili lawama kwa kuruhusu hali hii ya minyukano kuelekea uchaguzi. Timing ya uchaguzi sio nzuri ikiwa imebaki miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu na sioni yeyote kati yao atakaeshinda ambae ataweza kukiunganisha chama na kuponya majeraha ya hii minyukano kabla ya uchaguzi mkuu na itawagharimu sana!
Mwalimu
Mazoea ni kitu kibaya s! Haya ni matokeo ya mazoea , kwamba, Mwenyekiti atapita bila kupingwa.

Hakuna aliyeangalia mbali kwamba kuelekea uchaguzi mkuu kunahitajika muda na rasilimali.
Kilichotokea ni hii surprise ya TAL kugombea ! Wenyewe walijua ni mkutano mkuu wa kumthibitisha Mwamba
Mbowe ameshindwa kusoma alama za nyakati alipaswa kujiandaa mapema na vema zaidi namna atakavyosimamia suala la uchaguzi na uamuzi wa yeye kugombea au la... Ile drama ya wafuasi kumtembelea nyumbani eti kumuomba agombee na yeye kusema apewe masaa 48 inaonesha uzito wa maamuzi upande wake.
Kalenda ya uchaguzi ndani ya Chama ilipaswa kuakisi mambo mawili . Kwanza, uzoefu wa siku za nyuma kuhusu muda . Pili, mahitaji ya rasilimali . Leo wanafanya uchaguzi wa Kanda miezi 11 kabla ya Uchaguzi Mkuu.

Ideallly uchaguzi wa ndani ulipaswa kukamilika mwaka 2023 ili 2024 viongozi wanapanga mikakati ya Uchaguzi mkuu

Yote yanatokana na kiongozi kuongoza kwa mazoea na si fikra wala mawazo. Huwezi kumishawishi kwamba hii ni '' experience ya miaka 21'' !
Kwa upande wa TL, pamoja na hoja zenye mashiko alizotoa ikiwemo tuhuma dhidi ya uongozi hususan mwenyekiti najiuliza anazitoa kama mwanachama wa kawaida au makamu mwenyekiti? Anataka kutuaminisha kwamba kwa kipindi chote akiwa makamu amekuwa hahusishwi kwenye maamuzi ya chama? Kama jibu ni ndio basi alipaswa kujivua wadhifa wake muda mrefu akawasilishe hoja zake kwa wanachama THEN aje kum-challenge mwenyekiti kwenye uchaguzi... Kinyume na hapo ni yeye kukwepa collective responsibility na kutaka kumtwisha mwenyekiti wake madhambi yote ya chama ambapo yamkini na yeye ni mshiriki! Na hii naiona kama udhaifu wa kiuongozi kwa upande wake.
Naomba nimnukuu TAL '' Maamuzi yaliyofanyika nilikuwepo na siwezi kukwepa lawama pale tulipokosea''
Amekiri wazi kwamba alihusika.

Ninachokiona kwa TAL ni kushindwa kusikilizwa kwa hoja kwasababu Mwenyekiti ana nguvu sana na hutumia vikao kama rubber stamp. Hili linaonekana hata leo. Katika chaguzi za ndani amepanga watu wake kama Wenje.

Wasiomuunga mkono kama Rose Mayemba uchaguzi wao umewekwa kapuni kwa kutumia Wapambe wake akina Kigaila! Kwamba ili uwe na nafasi lazima umuunge mkono Mwenyekiti

Sidhani kama ni uamuzi wa TAL kugombea, nadhani kuna watu wengi wenye mapenzi mema waliochoshwa na uongozi wa FAM ambao analysis haina nafasi bali zidumu fikra za Mwenyekiti.

Ndio maana tunasikia sababu za yeye kuchaguliwa ni pesa. Leo Wenje kajidhihiri ni Team M/Kiti na alishauriwa agombee umakamu ili kumuondoa TAL ambaye ni stubborn katika Vikao.
All in all bundi ameshatua CDM, sumu imeshamezwa na inasambaa kwa kasi, yeyote atakaeshinda kiti ana kibarua kizito kuunganisha chama kabla ya uchaguzi na wamewarahisishia kazi CCM!
Nina uhakika wa asilimia 90, historia ya NCCR na CUF itajirudia tena si kwa namna ile lakini kwa mfanano ule ule.
Mbowe's political career is heading towards the end whether he wins or not... TL has various options akishindwa anaweza kwenda ACT, CCM au akaanzisha chama kipya na hapo ndio itakuwa kipimo cha impact yake kama mwanasiasa.
Uchaguzi ume mweka mahali pagumu sana! Chama kitabaki lakini atapoteza zaidi ya 2/3 ya Wafuasi.
 

YA TAL NA WENJE


Kuna mambo mawili yamejitokeza yakihusisha vita ya Tundu Lissu na E. Wenje

Kwanza, tuhuma za TAL kwamba Wenje alimfuata ili ''aunge mkono jitithada'' kupitia Abdul.

TAL alilisema hadharani kwasababu kuu mbili, kwamba, siku ikibainika alifuatwa kuhongwa, hata kama alikataa swali litakuwa ''kwanini hakusema hujuma hizo''. Pili, kwamba, kiongozi wa juu anapofikia hapo, Chama kimeingiliwa.

Wenje alijibu tuhuma kwa interview. Majibu yake yaliondoa shaka kwa waliokuwa nayo!
Majibu yake yalithibitisha (corroborate) alichosema TAL badala ya kumsafisha.

Wenje alipaswa kutambua Mtoto wa Rais ana ulinzi '' security details'' kwasababu nzuri kabisa.
Ipo hivyo duniani kote kwa kujua Wana Familia wanaweza kuwa katika hatari kwasababu ya nyidhifa za Wazazi wao.

Kitendo cha kukutana naye katika hafla na kujuana siku hiyo na kisha kumpeleka kwa TAL si rahisi kiasi hicho.
Hata kama walijuana siku nyingi, kwenda kwa TAL kulihitaji maandalizi si rahisi kama Wenje anayoaminisha Umma

Wenje alijianika kwa kusema Uongo. Ukifuatilia interview, Wenje alilenga kujitetea namna alivyomfadhili TAL wakati wa matatizo ya shambulio la risasi. Wenje alitafuta (sympathy) na si kujibu tuhuma za kuhongwa.

Kosa jingine la Wenje ni kumutuhumu TAL kwamba aliomba radhi ndani ya Kamati kuu(CC) na alishindwa kuthibitisha madai ya hongo. TAL akajibu kwa ushahidi kwamba alizungumza ndani ya CC na madai yake yalithibitishwa na mtu ambaye ni Marehemu. Wenje anapaswa kutambua kina cha jambo analopigia ''debe''

Pili, Yapo madai kwamba Mbowe (FAM) aliandaa mazingira ya chaguzi za ndani kwa kuweka '' watu wake' na mmoja ni Wenje anayegombea Umakamu ili kumuondoa TAL.
Iwe hivyo au la Wenje ana haki ya kugombea na kum challenge TAL, ndiyo demokrasia.

Katika interview aliyofanya na radio ya Wasafi, Wenje amefanya makosa mengine.
Kwanza, amethibitisha ni Team FAM na limethibitisha kwamba madai ya Mwenyekiti kutumia sekretariati kuvuruga uchaguzi wa ndani ni ya kweli. Kwamba Wenje alifanyiwa kampeni na Sekretariati ya FAM! ni kweli.

Wanaompinga FAM kama Rose Mayemba haki zao zimefunikwa na Sekretariati ya FAM kupitia akina Kigaila.
Hii maana yake, FAM anabeba mizigo ya Wenje na Sekretariati.

Wenje akatoa ushahidi, Mwenyekiti FAM ametoa pesa zake milioni 250 kufanikisha uchaguzi.

Hii maana yake ni kwamba FAM ananunua uchaguzi ! Hata kama alifanya hivyo kwa nia njema, suala linapomhusisha Wenje linakuwa na mnyororo mrefu hasa pesa ambao unamtumbukiza FAM katika mnyororo huo.

Mwisho, Wenje kamtuhumu TAL kwa kutochangia pesa akiwa Mbunge. Wakati huo TAL alikuwa majeruhi akipigani kuchangiwa DAMU ili aokoe maisha yake. Hakuwa na pesa za matibabu na alifukuzwa Ubunge.

Hii inaonyesha jinsi Wenje alivyokosa Ubinadamu! Inajenga dhana kwamba hata anayotuhumiwa nayo ni kweli.
Kikubwa zaidi, Wenje ni Team FAM. Mwenyekiti hawa Wapambe wanakuacha mahali pagumu.
 
KAULI YA Mwl. JOHN.HECHE WA CHADEMA

Miongoni mwa Nguli wa siasa za CDM ni Mh J.Heche Mbunge wa Zamani kwa tiketi ya Chadema
Kwa Muda mrefu Mh Heche amesita kuchukua upande,hata michango yake katika mitandao imepungua

Majuzi Mh Heche ameandika mtandao wa X (Tweeter) akisema '' ... Tundu Lissu ni Mkweli, Muwazi na Muadilifu''

Kauli ya Heche imchukuliwa kirahisi kwamba anamuunga mkono Mh TAL. Katika hali ya kisiasa ndani ya CDM inaonekana hivyo! Hata hivyo kauli ya Heche ina maana kubwa zaidi ya kumuunga mkono TAL

Kitendo cha kusema ni ''mkweli' kinamaanisha anathibitisha maneno ya TAL kuwa ya kweli.

Anaposema ni ''Muwazi'' anamaanisha anachosema TAL ni kwa uwazi kwasababu yapo mengi watu hawajui na mengine yamefichwa.

Ni ''Mwadilifu'' MwalimU Heche anamaanisha tuhuma zinazotolewa kuhusu TAL na uadilifu wake si za kweli.

Kwa kauli moja, Mh Heche anatoa ''endorsement' ya kauli za TAL ''ni kweli, yamewekwa wazi na mtu Mwadilifu''

Hech anatajwa sana katika nafasi za uongozi wa CDM. Ni kiongozi mahiri ana kauli thabiti na ana msimamo kwa yale anayoamini. CDM itafanya kosa kubwa kutokuwa na watu kama Mwalimu Heche katika safu ya Uongozi.

Heche pamoja na kuonekana ''conservative'' ukweli ni kwamba John Heche ni '' progressive conservative''
 
Interview ya Mbowe

Mwenyekiti wa Chadema Mh Mbowe (FAM)amefanya mahojiano na Radio ya Crown FM.
Moja ya mambo aliyoongelea na yanayoongelewa katika jamii ni kuhusu ukomo wa Uongozi.

Mh FAM anasema, mwandishi na mwanasheria aliyeshiriki kuondoa ukomo katika Katiba ya CDM ni Tundu Lissu (TAL)

FAM akasema katika Demokrasia kuweka ukomo wa muda ni kuwanyima fursa wengi wanaomhitaji kiongozi.
FAM akasema ''ukomo upo ndio maana kila baada ya mika 5 kuna chaguzi''

FAM ana hoja ya kweli kuhusu TAL kuwa Mwanasheria , kuondoa ukomo na kutozungumzia katika vikao.

FAM aliwahi kueleza sababu za kuondoa ukomo katika mkutano wake wa kuchukua Fomu akisema ilikuwa ngumu kupata viongozi, hivyo kuweka ukomo kungepunguza uwezekano wa kupata viongozi katika ngazi mbali mbali.

Katika mkutano wake mmoja TAL alikubaliana 100% na kauli za FAM na alikiri kwa maneno yake kwamba alishirikia kama Mwanasheria kuondoa ukomo wa viongozi akitoa sababu zile zile alizoeleza FAM
Wote wawili, FAM na TAL wapo katika ukurusa mmoja '' same page''

Tofauti yao ni kwamba TAL anataka marekebisho ya Katiba kuweka ukomo kuanzia sasa kuendelea si kwa viongozi tu hata wale wa kuchaguliwa kwa viti maalumu kama Madiwani na Wabunge

FAM anasema hapana, kana kwamba sababu alizotoa siku za nyuma bado zipo licha ya kukomaa kwa CDM
Hoja ya FAM ni kwamba kiongozi anatakiwa na wengi hivyo kuweka ukomo ni wa kuwanyima wengi fursa.

Kauli ya Mbowe ni ya hatari sana.
Kwanza, neno wengi haliwezi kuwa na mantiki hadi takwimu zitakapotolewa.
Pili, Je, hoja yake imewahi kujadiliwa na ''Familia ya CDM'' katika ngazi yoyote? Ikiwa la! wengi ni wapi hao!
Tatu, vipi kuhusu ukomo wa Viti maalumu kama Madiwani na Wabunge!

Nyerere angeweza kutawala hadi anafariki , wengi walitaka.
Mwalimu alielewe hilo lita 'set precedent' kwamba hata Dikteta ataita watu na kusema ni 'wengi' wanamhitaji agombee na atatumia nguvu za kidola achaguliwe na 'wengi' aliotengeneza.
Mwalimu akasema hapana, akaondoka kwanza kwa hiari, pili akaweka ukomo.

Viongozi waliofuata , Mwinyi, Mkapa na Kikwete waliheshimu hoja ya Mwalimu nao walitaka uwe utamaduni.

Magufuli (JPM) akataka kutumia ''Chawa'' kuongeza muda kwa hoja ile ile hatari ya Mbowe '' Wengi wanamtaka'' .

Baada ya kifo, hoja ikatulia lakini haijafa. Kuna uwezekano ikajirudia na mara hii itakuwa ngumu sana kwasababu hata ''KIONGOZI' wa Upinzani anasema '' ikiwa wengi wanamtaka kiongozi '' basi kusiwe na ukomo

Hoja za FAM zinaeleza kwa kina udhaifu wake kihoja na udumavu wa fikra.

Badala ya kujiingiza katika mijadala inayopoteza heshima yake, FAM aeleza Watu kwanini anataka miaka 5 licha ya miaka 21 madarakani. Ni kipi anachotegemea kukifanya miaka 5 ambacho hakukimalisha miaka 21
 
Mpambano wa Manguli Chadema
Busara isipotumika CDM kule kwa NCCR na CUF

Maridhiano na Chaguzi znavyoitafuna kambi ya Mbowe


Vita ya Mafahari imepamba moto. Awali, ilikuwa vita kati ya Chawa na Wapambe sasa vita ya ''Wakubwa''

Lau vita hii ingalikwa ya maono isingekuwa tatizo, tena lingeitangaza Chadema vizuri sana.

Vita imekuwa ya 'character assassination' kwa maana kushambuliwa wasifu wa mtu kwa kumbomoa.
Hili limetishia uhai wa Chadema na itakuwa ngumu kuwaunganisha Wanachama hata baada

Hatutajadili character assassination bali maudhui angalau yenye mantiki, kama yapo

Kambi ya Tundu Lissu (TAL) inasimama katika hoja kuu hizi;
1. Kwamba TAL amewasilisha maono yake 5 ikiwa atachaguliwa
2. Kambi inahoji maridhiano na mahusiano kati ya FAM na CCM
3. Kwamba kuna rushwa ndani ya Chama inayohitaji tiba

Kambi ya TAL imepata nguvu ya uwepo wa J.Heche anayewania Umakamu. Heche amerudia tuliyoandika mabandiko yaliyotangulia akisema '' Tundu Lissu ni Mkweli, Muwazi na Mwadilifu'' (bandiko #14)

Hoja za kambi ya Mbowe (FAM)
1. Kwamba FAM ameongoza kwa Busara na inahitajika kukiweka Chama pamoja
2.Kwamba FAM ana pesa na ni rahisi kuzitumia pesa zake kwa manufaa ya Chama
2. Chama kinaporwa na Wanaharakati

FAM ameelemewa na hoja za kwanini agombee baada ya miaka 21, na kipi atakamilisha miaka 5.
Ni hoja zinazomlazimu kuzijibu kwa ustadi. Hadi sasa kambi yake haijaweza kujibu.

Suala jingine kwa kambi ya FAM ni hoja ya maridhiano, wengi wakisema hayakuwa na uelekeo wala maana na kwamba kulikuwa na ''viasili'' vya rushwa ndani yake.
Kambi ya FAM haijafanikiwa kueleza kwa kina nini mantiki ya maridhiano na kipi cha maana kilipatikana.

Hoja ya FAM kwamba maridhiano yamepelea kuachiwa kwa Wanachama wengi inakabiliwa na matatizo.

Team TAL inasema, haukuwa msingi wa maridhiano, Wahanga walisingiziwa, kuachiwa si fadhila ni haki .

Kumeibuka nadharia ya hatari ''conspiracy theory' kwamba hata kuachiwa kwa Mwana Chadema Sanga na wenzake 2 ni matokeo ya CCM kutaka kumjenga FAM kwamba, yote ni matokeo ya maridhiano.

Hukumu ilikuwepo kabla ya TAL hajachukua Fomu, lakini, katika 'tension' ya uchaguzi ikiwa na character assassination hili linaonekana kweli

Suala jingine ni Uchaguzi wa Njombe ambako timu ya FAM haina ushwishi.
Imeelezwa figisu zinazofanywa na Sekretariati kuwanyima haki disfranchise Wajumbe wa Njombe kwasababu tu Rose Mayemba hakuwa Team FAM

Hoja ya Njombe inaeleza kwa kina mambo matatu makuu
1. Kwamba kila upande unaokwenda tofauti na FAM hutengenezewa zengwe
2. Uchaguzi wa Njombe unaeleza jinsi Sekretariati ilivyowekwa mfukoni na FAM
3. Uchaguzi unaeleza kwanini kuwepo na Tume au Kamati maalumu ya Uchaguzi wa Taifa

Kwa mwenendo wa majadiliano ndani ya jamii, Team FAM ina kazi ya ziada ya kujisafisha, kurudisha imani na kutumia incumbency kushinda.

Kwa sasa Team imeelemewa na inakabiliwa na mambo mengi ya ku address kama tulivyoonyesha juu
 
Mnyukano wapamba moto
FAM apata nafuu baada ya wiki kadhaa za kubanwa
TAL amtupia 'Taulo' kwa unforced error ! ampa FAM time out ya bure

T
angu awali tumeeleza uchaguzi wa CDM una afya ikiwa utafanyika katika misingi ya kuheshimiana, kukubaliana kutokubaliana na kupingana bila kupigana. Wagombea waiangalie kesho ya CDM pia

Katika hatua za awali Vijana wa Mbowe (FAM) walitumia mbinu ya character assassination kumdhoofisha Tundu Lissu (TAL). Walimiwta msaliti, muongo na kuendelea kuzitaja fadhila alizopokea au kupewa.

TAL alikuja na hoja 5 za kwanini anagombea Uenyekiti.

Hoja 5 ni kali kwa mantiki kwa aliyezipitia, Wanachama wengi wakitamani mambo mawili kutoka kwa FAM
1. Kwamba aeleze anataka kukamilisha nini kwa miaka 5 ambacho hakukifanya miaka 21
2. Ikiwa hana, ajibu hoja 5 za TAL kuonyesha makosa yake au mbdala wake

Kutokana na hoja 5, Timu ya FAM ikapukutisha wafuasi wakijitokeza hadharani kumuunga mkono TAL.

FAM alipoteza kile kinachoitwa incumbency advantage kwa Challenger TAL.
Hata advantage alizokuwa nazo kama Mwenyekiti zikatoa dalili za Timu yake ikadhoofika.

Timu ya TAL ikafanya kosa kubwa kisiasa, kwamba, ikaacha zile hoja 5 zilizoipa advantage na kukumbatia character assassianation. Hilo limeisaidia Timu ya FAM wenye mengi ya kusema kuhusu character assassination.

TAL ameingia katika mjadala wanaoutaka wao kwa msemo kwamba '' Never to wrestle with a pig. You get dirty and besides the pig likes it''

Kwa siku kadhaa , Timu ya FAM imeeleza Fadhila alizotendewa TAL.
Iwe ni kweli au si kweli, kuna yaliyoelezwa kama la shambulio na matibabu Nairobi kuwa ya Kweli.
Ni FAM aliyemwepusha TAL kwa kumpeleka Nairobi, vinginevyo tungezungumza mengine.

Ni FAM na CDM wali organize matibabu na shughuli nyingine. Hili halina kificho.
Umma unalifahamu vizuri na Timu FAM inalitumia kupata sympathy .

Wale waliovutika na hoja 5 za TAL wanapoona TAL akishughulisha na character assassination, wanasita. Huo ndio msingi wa kusema TAL ana wazuia wasijiunge naye

Pande zote zinapaswa kujiepusha na character assassination ili kujenga mustakabali mwema wa CDM.

Katika mchezo wa character assassnation, TAL ni loser. TAL amevutika na kuacha ujenzi wa hoja 5 alizokuwa nazo na badala yake amemtupia 'Taulo'' FAM aliyekuwa kwenye kona akipokea masumbwi.

Kwa ufupi TAL ametenda kosa linaloitwa unforced error na kumpa FAM time out!
 
Mwanya wa Rushwa kupitia mabunda ya Pesa

Moja ya matukio katika uchaguzi wa mabaraza ni hili la BAVICHA 'kukamata' watu na pesa

Tukio limepokekelewa kwa hisia kwenye mitandao, wengi wakisema '' ilikuwa ni uthibitisho kwamba kuna pesa zimemwaga na wafadhili nje ya chama kuokoa kambi ya FAM'' .

Taarifa za karibuni zimebaini pesa zilikuwa ni halali kwa wajumbe wa Kanda moja kwa ajili ya posho zao.

Kilichotokea kinaitwa 'preconceived notion' kwa maana ya 'hukumu halafu ushahidi''.

Kambi ya TAL imesema kuhusu rushwa na reaction yao kuhusu hizo pesa zilijengwa katika preconceived notion, na walipoona zinagawiwa wakaona ni ushahidi wa dhana yao.

Katika mazingira ya ushindani uliopo kundi la TAL lina kila sababu ya kushuku hasa kwa kuzingatia kuna '' watu waliwashawishi' viongozi wao kuhusu rushwa. Reaction yao inakuwa justified kwa mazingira yaliyopo

Swali , CDM kama taasisi imefikaje katika hali kwamba posho zinagawiwa katika vyumba vya uhaguzi?

Kugawa pesa si tukio la ajabu lakini linajenga mazingira tata sana hasa kunapokuwepo na preconceived notion. Laiti leo ungalikuwa uchaguzi mkuu huenda CDM wangekuwa na 'msiba'' kwa mapigano.

Kugawa pesa bila utaratibu tena katiaka vyumba vya mikutano si jambo jema.

Ni jambo linalojenga mazingira hatarishi.Mathalani watoa rushwa wanaweza kutumia mwanya wa '' Kugawa posho' kumbe wanatoa rushwa. Ni nani anayeweza kutenganisha rushwa na posho l

CDM kama taasisi haipaswi kugawa pesa kwa mabunda.

Kuna taratibu za hati za pesa ''cheque' na zama hii malipo ya kielektroniki.
Utaratibu wa kugawa pesa kwa mabunda ni wa kizamani na kishamba.

Hili lisipotazamwa, uchaguzi mkuu unaweza kuvurugika! hizi ni dalili tu kwamba mianya ya rushwa ipo wazi, taratibu za utoaji wa fedha ni za hovyo na huenda mpangilio mzima ni wa mawenge wenge
 
Aliyosema Lema!
Mwenyekiti ana wakati mgumu


Mwenyekiti wa zamani Kanda ya kaskazini Mh Godbless Lema (GBL) amezungumza na wanahabari mambo mengi nyeti na muhimu kwa mustakabali wa Chadema

1. Kuenguliwa
Mh GBL anaeleza mbinu chafu za kumuondoa uongozi wa kanda kwa kuratibiwa na FAM akitoa ushahidi wa kumweleza bila kujibiwa, ukiwa ni ushahidi FAM alijua nini kinatokea kwa GBL

Msigwa:
GBL anasema '' Uchaguzi wa nyanda za juu ulikuwa mbaya kuliko uchaguzi wa TAMISEMI' Msigwa alionewa''

2. COVID-19
GBL amezungumzia Wabunge wa COVID kwamba viongozi akina B.Kigaila na S.Mwalimu wana WAKE zao.
GBL akasema inawezekana vipi hawa wakatenda haki kwa chama na Familia zao kwa wakati huo huo?

3. Kuchagiwa kanisa: GBL amefunua kitendawili cha michango ya Kanisa kati ya FAM na Dkt Shoo wa KKT

4. Lissu Kuropoka: GBL anauliza , TAL ameropoka kitu gani katika yale anayosema?

Miongoni mwa mengi aliyoeleza , tupitie hayo machache kwa wepesi na uzito wake

1. GBL anashuhudia mpango wa kuwangea akina GBL, Heche, Lissu na Wenje akimtuhumu M/Kiti kutumia ''Mbowe machinery'' kubaki madarakani. Ni hoja inayoshahdidia yale ya Sumaye kushindwa kanda ya Pwani, akiwa PM mstaafu. GBL anatupa ushahidi Nyanda za Juu ulikuwa uhuni mtupu kama ilivyoripotiwa.

Mabaki ya Uhuni huo ni kesi ya Rose Mayemba ambayo M/Kiti kupitia Vijana wake wameiweka pembeni.

2. COVID: Tumehoji mara nyingi jinsi COVID walivyotinga Bungeni.
Kulikuwa na taarifa za uhakika kwamba walikuwa na mawasiliano na CCM.

Kilichoshangaza ni M/Kiti kujivuta vuta hadi kesi zikaenda mahakamani.
GBL anatueleza kwamba kulikuwa na WAKE wawili wa viongozi plus washirika wengine

Majuzi alipoulizwa kuhusu COVID, FAM alijibu, katiba hairuhusu kumwadhibu Mwenza wa Mwanacham.
FAM alimaanisha, Mke wa Kigaila na Salum Mwalimu siyo sababiu ya wao kuadhibiwa.
Ni kweli katiba haisemi waadhibiwe Waume au Wake wa Wanachama kwa makosa ya mmoja wao.

Naibu KM Kigaila aliwahi kusema ' yeye na mkewe hawaongei mambo ya siasa'.
Kigaila akageuza Watanzania ndondocha.

Katika mazingira ya ndoa Kigaila anatuaminisha kupokea pesa bila kujua mkewe kazitoa wapi.
Kigaila hajui mkewe anaishi wapi huko Dodoma. Kigaila akaonekana kituko mbele ya TV


Mwenyekiti FAM ametumbukia katika mtego wa COVID kwa namna tofauti. Kwamba hajui kinachoitwa ''conflict of interest''.

FAM hakutakiwa kuwaadhibu COVID bali kusimamia kanuni ya asili ya ''fair play'' kwamba haipaswi kuwepo conflict of interest za namna yoyote. FAM alikuwa na chaguo la kuwaambia Viongozi wa sekretariati yake ima wajiuzulu nafasi zao au wawatoe WAKE zao Bungeni.

GBL akaeleza kuhusu viongozi wa COVID kushiriki hafla za M/Kiti.
Tunakumbuka FAM aliwahi kusema ni wakati wa kusameheana, jambo lilizua minong'ono ya kuwasamehe COVID baada ya kuonekana katika michango mingi ya kanisani.

Inatosha kusema suala la COVID 19 wa CDM, M/Kiti FAM alipoteza kabisa udhibiti licha ya ukweli kwamba naye alikuwa na conflict of interest, za Vijana wake wa sekretariati pamoja na COVID wenyewe.

4. GBL amefunua ukweli wa michango ya Kanisa la FAM kule Machame alikopokea pesa za Rais Samia.

Alichokisema GBL ni kwamba wakati maridhiano yamekwama FAM alikuwa anapokea michango !
Suala la Maridhiano pekee ni mwiba kwa FAM, na alipokubali kulifungamanisha na pesa aliondoa mashaka ya wale wachache waliokuwa nayo juu yake.

FAM hawezi kujitenga kama Muumini wa Kanisa na M/Kiti wa CDM na alipaswa kuona kuna conflict of interest . Mathalan, FAM akikamatwa kanisa hatuwezi kumtenga na dhamana yake katika Chama.
Maridhiano yaliyofeli ni ishara kuu kwamba FAM amekuwa compromised.

Hii ndiyo sababu ya reaction tunazoziona kutoka makundi zikilenga kumuunga mkono Tundu Lissu

Kwa alichokieleza GBL, sijui kama FAM ana majibu! Jaribio la kujibu litamletea matatizo zaidi
 
CHADEMA : Fursa iliyopotea (A missed opportunity)

Tangu awali tumeeleza kinachotokea CDM kinaweza kuwa fursa kubwa kikitumiwa vizuri
Kwa wiki zaidi ya tatu vyombo vya habari vimehaha kueleza nini kinajiri ndani ya CDM

Hakuna shaka kwamba vyombo vya habari vimependa zaidi minyukano kwasababu hatujawahi kuona Wapinzani wa CCM wakipewa nafasi kubwa kiasi hiki (coverage)

Video ya ya mtangazaji wa Clouds akimhoji Tundu Lissu (TAL) inaonyesha uhasama ''hostility' ya baadhi ya 'Wanahabari'' na kwamba wanachokitafuta ni ima ushabiki au kukuza minyukano.

Mtangazaji huo wa Clouds ni kada wa CCM ameonyesha ubutu na uvivu wa kazi kiasi cha kuathiri taswira ya CLouds Media. Lengo la Mtangazaji huo lilikuwa ''ukada' na kuchukua upande wa minyukano CDM.
Ni kama vile alitumwa na Clouds kufanya kazi kwa niaba ya upande mwingine unaoungwa mkono na CCM

Licha ya matatizoya baadhi ya Wanahabri, CDM imepata coverage kubwa kuliko CCM .
Chaguzi za mabaraza, BAVICHA, BAZECHA na BAWACHA ni gumzo , si mkutano mkuu wa CCM, ilivyozoeleka.

Kwa bahati mbaya CHADEMA wameshindwa kuitumia fursa hiyo kwa faidi.

Haiingii akilini kwamba Wajumbe wa mikutano ya Mabaraza walifika Dar es Salaam bila malipo na kwamba hadi Wagome ndipo posho zao zinatoka. Taasisi kubwa kama CDM hili linawezekanaje?

Pili, mikutano ya mabaraza na chaguzi zinafanyika hadi usiku wa manane, asubuhi ni tuhuma za rushwa n.k. Hivi CDM wameshindwaje kuandaa ratiba itakayowezesha mambo yao kufanyika kwa utaratibu?

Kama tulivyoeleza, vyombo vya habari visioitakia mema CDM vinachukua fursa kuandika mauza uza na fyongo za maandalizi na chaguzi badala ya kueleza ushindani na weledi wa CDM.

Kwavile ni wiki ambayo CDM wamepata fursa ya vyombo vya habari, macho na masikio ya Watanzania yapo kwao, lakini si kwa mazuri tu hata mabaya yanayotokea na hili linajenga taswira mbaya .

Tatizo ni Sekretariati au kuna jingine? Haya yanatokeaje kwa taasisi kubwa kam CDM?
Kwa miaka zaidi ya 20, CDM imeshindwaje kuandaa mikutano ya chaguzi kwa mafanikio?

Wanaosema mabadiliko yanahitajika, wanakosea wapi?
 
Back
Top Bottom