Jana Jumapili ya tarehe 23/07/2023, CHADEMA na SAUTI YA WATANZANIA, walikuwa na mkutano mkubwa sana juu ya kupinga uuzwaji/ubinafsishaji wa Bandari za Tanzania.
Mimi kama mmoja ya wahudhuriaji wa mkutano huo, nilifurahia sana jinsi mkutano ulivyoratibiwa kwa umakini wa hali ya juu.
Kilichonisikitisha ni baadhi ya waalikwa ambao walipata nafasi ya kuhutubia mkutano huo, kwanza walionekana ni waoga, wasiojiamini na nasikitika kusema walitumia muda wa mkutano vibaya kwa kuongea maneno ya kuwatisha wazungumzaji wengine.
Yule Mzee Luhigo pamoja na Bw. Thomas, binafsi waliniboa sana pamoja na wahudhuriaji wengine, maana walijitanabaisha kujipendekeza kwa Rais na kuwatisha wazungumzaji wengine jasiri kama Wakili Msomi Mwabukusi na wale Maaskofu wote waliokuwepo, ambao tunamshukuru Mungu kwa kuwa hawakuogopa kusema kile walikusudia kusema licha ya maneno ya "vibaraka" hao waliokuwa na nia ovu.
Nimalizie kwa kusema, Maandiko Matakatifu katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati 20:8 yanasema; Mwenye HOFU (mwoga) na MNYONGE hakutakiwa kwenda vitani asije akaiyeyusha mioyo ya wenzake! (akawaambukiza woga wengine). Uoga unaambukiza kama ukoma!
Tafadhalini sana Chadema na Sauti ya Watanzania, tunaomba kabla ya kuwaalika watu watakaokuja kutuhamasisha kwenye mikutano yenu ya huko mbeleni, ikiwezekana muwasikilize kwanza au kupitia hotuba zao kabla ya kuwapandisha majukwaani. Na endapo wakileta ujinga na ushenzi jukwaani, msiwaonee aibu kama mlivyofanya kwa sehemu jana. Mabadiliko hayawezi kuja kwa kuoneana aibu kwa wapumbavu wachache wanaoturudisha nyuma.
Vinginevyo, siku ya jana mmefanya jambo kubwa sana litakalokumbukwa na historia pamoja na vizazi vyetu vyote.
Hatutakubali Bandari na Raslimali zingine za Taifa letu, kuhodhiwa kwa manufaa ya watu wa wachache, bali zitumike kwa ajili ya faida ya Watanzania wote.
Aluta continua.