Mangisandy
JF-Expert Member
- Apr 23, 2012
- 2,652
- 2,273
Nimepokea kwa mikono miwili sera ya CHADEMA, hasa kuhusu mfumo elimu.
Sera yetu ya elimu na mfumo huu wa elimu siyo mzuri. Tuna mfumo wa elimu ambao umejikita kwenye kukariri ili kujiandaa na mitiani ya mwisho. Lengo ni kupata cheti cha ufaulu wa mitiani, na hatimaye kuajiriwa.
Kuna matatizo kadha yanayo tengenezwa na mfumo huu wa elimu:
Kwanza, mfumo huu haumpi mwanafunzi uwezo wa ubunifu, kujenga hoja binafsi, zaidi ya kukariri alicho elekezwa na mwalimu!
Pili, mwanafunzi hapati maarifa yalikusudiwa.
Tatu, mfumo huu unajenga mianya ya rushwa, siyo tu kufaulu mitiani yenyewe, lakini ndiko tabia za rushwa na ufisadi zinakozaliwa.
Mfumo huu wa elimu siyo shirikishi, kwa sababu mwanafunzi hapati nafasi za kushiriki darasa kwa kuchangia au kuuliza maswali. Ni mfumo wa “ndiyo mzee”, ambapo mwalimu ni ‘I know it all, na wanafunzi ni ‘you know nothing’! Hapa ukijumlisha na dhana ya ‘mkubwa hakoseagi’, unapata taifa la watu wasikosowa na kutopenda kukosolewa hata kama unakosea.
Matatizo hayo ya mfumo wetu wa elimu na pia uelewa mdogo wa lugha za kimataifa, ni kikwazo kikubwa cha soko la ajira ndani na nje ya nchi, hasa wakati huu wa utandawazi.
Asante sana Tundu Lissu na CHADEMA kwa utayari na uthubutu wenu wa ku-challenge mfumo wetu wa elimu. Nategemea kwamba sera yenu hii itakuja kutekelezwa kwa kuufumia kabisa mfumo wetu wa elimu, ili kujenga taifa lenye elimu bora, katika kutekeleleza kaulimbiu yenu ya Uhuru, Haki na Maendeleo ya watu.
Mungu ibariki Tanzania , Mungu ibariki CHADEMA, Mungu mmbariki Tundu Lissu!