Wakubwa na wadogo... Amani iwe kwenu!!!!!!!!!
Haya tena CHADEMA ni chama cha udikteta na mafisadi walioko pale makao makuu kama alivyosema mzee Yusuf Halimoja.
Ninaweza kabisa kuzungumzia sababu za hoja hii kuvuma na kusambazwa kwa bidii kubwa. Lakini nitafanya hivyo nitakapojiridhisha kuwa wasomaji wangu hapa hawalijui jukumu la CHADEMA bungeni wala katika majukwaa ya siasa Tanzania. Kwa ajili ya ukweli huo mimi nitazungumzia tu ulazima wa akina RA, EL, JK na wengine wengi ambao wana uhakika wa kuendelea kutawala kwa kupitia CCM, kuajiri watu na kulipa fedha nyingi kwa mission ya kupandikiza migogoro ndani ya CHADEMA.
Historia ya Tanzania inaonyesha kuwa toka miaka ya 1980 tumekuwa tukiibiwa. Na kila miaka ilivyosonga licha ya nchi kuwa na wasomi wengi, vyombo vingi ya habari, wanasiasa wengi wajuzi; ndivyo pia na kasi na ukubwa wa kuibiwa kwa rasilimali za Tanzania ilivyoongezeka.
Hadi ilipofikia CHADEMA kwa msaada wa watanzania waliochoka kuvumilia wizi unaofanyiwa nchi yao na kutishika kuwa muda si mrefu nchi itabakia sega tupu, walitokeza hadharani na kuanza kuwavaa wazi wazi wezi wa rasilimali zetu. Iliwakilishwa Buzwagi, Ikafuata orodha ya Mafisadi, hatimaye ikawezekanishwa kashfa ya Richmonduli. Wakubwa wakajiuzulishwa, na mengine mengi yameendelea kujiri na yatakuja zaidi.
Ulitaka CHADEMA ifanye uchokozi gani zaidi ya huu. Mijitu ilizoea kula kwa kwenda mbele. Chini yao kuna watu wanasubiri wapukutishiwe makombo. Hawa ndo wanapiga kelele Oooh!!! CHADEMA ina ukabila, Eti CHADEMA inatumia vibaya fedha za ruzuku!!!!!! Na makelele mengine mengi tu!!
Hasira yao si ukabila ndani ya CHADEMA, wala si matumizi mabaya ya ruzuku.
Wanachokasirika ni jjinsi ambavyo wanavuliwa nguo na CHADEMA. wameamua kuajiri watu wa kukisambaratisha chama.
CHADEMA inapata shilingi ngapi jamani hadi tunaijadili namna hii??? Wao CHADEMA wanapewa 60,000,000/= tu kwa mwezi. Wenzao CCM wanapewa 2,000,000,000/= (shilingi bilioni mbili kwa mwezi) maana yake ni kuwa kila siku CCM inachukua 80,000,000/= kutoka katika hazina ya taifa. Kwa nini wanaochukizwa na matumizi mabaya ya ruzuku wasifuatilie hili??
Nilikuwa ninawasubiri watanzania wenye nia njema watokeze hadharani kuipongeza CHADEMA kwa kuweza kupambana na lichama kama CCM ambacho kinapata fedha nyingi kwa siku moja kuliko ambazo CHADEMA inapata kwa mwezi mzima. CHADEMA inaweza kuishikisha adabu CCM ambayo ina mabilionea wengi ambao wamevipata vijisenti vyao hivyo kwa kutumia mwavuli wa chama. CHADEMA inaibana na kuitisha CCM ambayo viongozi wake wengi wanatumia fedha za umma kukiimarisha chama. Sungura anapambana na tembo jukwaani na tembo ameridhika wazi kuwa kazidiwa. Sasa analazimika kutumia mbinu za ziada. Hiloo!!! kubwa zima hovyo*
Napeleka salamu kwa Mafisadi wanaojibidiisha sana kupandikiza migogoro CHADEMA, kwamba saa yenu ya kujitetea ni sasa. Lakini punde chaja kizazi ambacho hakitawapa ngau muda finyu wa kujitetea. Kizazi hiki hakitawapa nafasi mkidanganye na bakshishi. Hatakuwepo wa kununuliwa aanzishe migogoro CHADEMA. Na pengine aina ya siasa wakati huo haitakuwa ya vyama kama tuliyo nayo sasa.
Kama ninyi ni wevi mtaimbwa kila pahala kwa ushujaa wenu wa kuiba. Kama ninyi ni mafisadi na wala rushwa mtaimbwa hivyo hivyo kwa heshima ya uchafu wenu mlioifanyia nchi. Kutengeneza migogoro CHADEMA haitawajenga kwa muda mrefu.
Ninyi mliowekwa kuichachafya CHADEMA: tambueni mahitaji ya nchi yetu ya Tanzania. Tunahitaji wanamapinduzi wa kweli wanaoweza kupambana na ufisadi wa CCM. Tukiunyamazia tunawaacha watu wetu wengi hapa Tanzania wakiangamizwa na uharamia wa CCM. Pamoja na wajibu mliopewa na lamba lamba ambayo mmeahidiwa; hebu waacheni waliojitoa sadaka kutetea mustakabali wa masikini wazawa wa Tanzania waendelee kufanya hivyo. Oneni aibu kwa ajira mliyopewa.
Wanachama makini wa CHADEMA...... vita mbele, endeleeni kwa moto zaidi. Mamluki wanapopandikizwa kwenye chama washughulikiwe mapema kabla hawajajikita zaidi.
Karuzuku kadogo tunakopata tukatumie kwa makini kuwamaliza kabisa mafisadi.
Aluta kontinua