Unayesema Chadema haina Waislamu hukijui chama hicho. Wako wengi.
Zitto Kabwe Zubeiri ambaye ni Naibu Katibu Mkuu ni Muislamu. Bob Nyanga Makani aliyekuwa Mwenyekiti (Taifa) kabla ya Freeman Mbowe ni Muislamu. Mhe. Arfi (Mbunge wa Mpanda Magharibi), Mhe. Halima Mdee, Mhe Mhonga Said (Wabunge Viti Maalum) ni Waislamu. Aliyekuwa Katibu Mkuu kabla ya Mhe. Slaa, WAlid Kaburou na former Naibu Katibu Mkuu Akwilombe ambao wametoka Chadema ni Waislamu.
Wajumbe wengi wa Kamati Kuu ya Chadema k.m. Mzee Kasisiko wa Kigoma, Chiku Abwao wa Iringa ni Waislamu. Wajumbe wote wa Kamati Kuu toka Zanzibar ni Waislamu. Huo Ukristo mtupu Chadema uko wapi????????
Kuhusu msimamo wa Chadema re. suala la Mahakama ya Kadhi, hili ni jambo linalohusu Ibada. Hata Mufti amefafanua hivyo. CCM ilikurupuka mwaka 2005 ikaliweka kwenye Ilani ya Uchaguzi kinyume na Sheria ya Vyama vya Siasa na Katiba ya Tanzania, Ibara Na. 19(2). Hii ilikuwa ni janja janja ya CCM ya kuvutia kura za waumini ambao hawafahamu Katiba kwa kina.
Chadema hawawezi kudai kuweka sheria za dini ktk Sheria za Nchi. Zikiwekwa za Kiislamu, Wakristo nao watadai Canon Law iingizwe, wenye kuamini dini ya Kiyahudi watataka Torat na sijui sisi Wapagani tutaingiza sheria gani.
Endapo viongozi wa Kiislamu Tz. watafuata ushauri wa wanazuoni wengi kwamba waunde Mahakama ya Kadhi kama chombo chao chini ya Sheria ya Taasisi Zisizo za Kiserikali (Non-Governmental Organizations), na wakakigharimia kwa fedha za zaka na michango ya wafadhili wengine wa ndani na nje, naamini uongozi wa Chadema hautapinga. Huo ndio utatuzi wa suala ambalo linaweza kuleta mgawanyiko wa kidini Tanzania ambao si lazima.