CHADEMA na Udikteta Makao Makuu

Mzee Kifimbo, uwe na ujasiri basi, kwanini unataka mimi nijibu swali lako?

Nimekujibu kule Chadema na Asha, unasema nakutaja nina posts kama 210 naomba ushahidi kuwa kila post nakutaja ktk hizo ngapi nimekutaja? kwani wewe ni nani hapa JF? au kuna classes?
 
Kifimbo

I read you loud and clear but I can guarantee you that; your actions won’t last long just be yourself and issues not JF members personally.

Mimi ndiye niliyeanzisha thread hii naomba kujua kwanini umelitoa jina langu? au kuna matusi kwenye yale maandiko yangu.
 
Kubwajinga

Nijibu pia jamani, nimeuliza swali kama uliwahi kufukuzwa CUF kutokana na tabia yako ya kuwabagua watu kutokana na dini na makabila yao.

Asha


Huu uzushi wa mimi na CUF umeutoa wapi wakati hunijui na wala mimi sikujui? Have you seen anything from my posting that is promoting or demoting CUF? Kama huna ushahidi wowote ingekuwa ustaarabu mzuri kama ungeomba msamaha ASAP.
 
Mimi ndiye niliyeanzisha thread hii naomba kujua kwanini umelitoa jina langu? au kuna matusi kwenye yale maandiko yangu.

jibu swali langu kwanza; kwanini ulinitaja nijibu na kuniweka kati ya Mnyika na Kitila? Kwanini kwa mfano hukutaka KubwaJinga, Mzee ES au Chinga kujibu?
 
Kitila na Mnyika ni watu wako wa karibu sana.

Once again, onesha ushahidi kuwa Kitila na Mnyika ni watu wangu wa karibu sana? Kwanini usiseme Mzee ES au Reverend Kishoka, au Invisible, au mtu mwingine yoyote ambaye yuko karibu na mimi? H

Onesha ukaribu wangu na Mnyika na Kitila na ueleze huo ukaribu (kama upo) umetokana na nini? go ahead..una ruhusa yangu.
 
Rudia tena swali lako liweke vizuri sijakuelewa.

of course, (ni mgumu kuelewa na mwepesi kusahau ulichokisema punde) nitakusaidia. Umesema Mnyika na Kitila ni watu wangu wa karibu sana. Onesha ushahidi kuwa ni watu wa karibu na ukaribu huo umetokana na nini (kama upo huo ukaribu)
 
nakumbuka december 2006 Bwana Mbowe alipeleka misaada kanisani-Kilimanjaro tu. lakini hajawahi kusaidia watu wa dini nyingine leo umetusaidia kuwa ni chama cha wakristu wachagga, ndio maana ANNA KOMU ilibidi awe mkristu ndio apewe ubunge.

Mwaka 2006 Vyombo mbalimbali vya habari viliandika michango ambayo Mbowe ameitoa misikitini na kwa waislamu ikiwemo milioni nne alizochangia chuo cha waislamu na kupewa cheti cha heshima na Mufti.

Ana Komu amechaguliwa kuwa Mgombea Mwenza akiwa Muislamu na baadaye akatueliwa kuwa mbunge wa Viti Maalum. Kama angekuwa si Mzanzibar pingamizi lililoweka na DP na Mtikila lingepita na Mbowe angeondolewa kwenye kugombea urais.

Asha
 

Hivi we jamani unadhani waZanzibar wote ni CUF na CCM? Hebu soma huu mjadala hapa japo utapata akili http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=12645

Na nani kakwambia kama mimi nakerwa na CUF na 'udini' wao? Hilo la udini umesewa wewe, mi najua CUF si chama cha kidini

Asha
 




It is worth recalling what was said two months ago.
 
Wakubwa na wadogo... Amani iwe kwenu!!!!!!!!!

Haya tena CHADEMA ni chama cha udikteta na mafisadi walioko pale makao makuu kama alivyosema mzee Yusuf Halimoja.

Ninaweza kabisa kuzungumzia sababu za hoja hii kuvuma na kusambazwa kwa bidii kubwa. Lakini nitafanya hivyo nitakapojiridhisha kuwa wasomaji wangu hapa hawalijui jukumu la CHADEMA bungeni wala katika majukwaa ya siasa Tanzania. Kwa ajili ya ukweli huo mimi nitazungumzia tu ulazima wa akina RA, EL, JK na wengine wengi ambao wana uhakika wa kuendelea kutawala kwa kupitia CCM, kuajiri watu na kulipa fedha nyingi kwa mission ya kupandikiza migogoro ndani ya CHADEMA.

Historia ya Tanzania inaonyesha kuwa toka miaka ya 1980 tumekuwa tukiibiwa. Na kila miaka ilivyosonga licha ya nchi kuwa na wasomi wengi, vyombo vingi ya habari, wanasiasa wengi wajuzi; ndivyo pia na kasi na ukubwa wa kuibiwa kwa rasilimali za Tanzania ilivyoongezeka.

Hadi ilipofikia CHADEMA kwa msaada wa watanzania waliochoka kuvumilia wizi unaofanyiwa nchi yao na kutishika kuwa muda si mrefu nchi itabakia sega tupu, walitokeza hadharani na kuanza kuwavaa wazi wazi wezi wa rasilimali zetu. Iliwakilishwa Buzwagi, Ikafuata orodha ya Mafisadi, hatimaye ikawezekanishwa kashfa ya Richmonduli. Wakubwa wakajiuzulishwa, na mengine mengi yameendelea kujiri na yatakuja zaidi.
Ulitaka CHADEMA ifanye uchokozi gani zaidi ya huu. Mijitu ilizoea kula kwa kwenda mbele. Chini yao kuna watu wanasubiri wapukutishiwe makombo. Hawa ndo wanapiga kelele Oooh!!! CHADEMA ina ukabila, Eti CHADEMA inatumia vibaya fedha za ruzuku!!!!!! Na makelele mengine mengi tu!!

Hasira yao si ukabila ndani ya CHADEMA, wala si matumizi mabaya ya ruzuku.
Wanachokasirika ni jjinsi ambavyo wanavuliwa nguo na CHADEMA. wameamua kuajiri watu wa kukisambaratisha chama.

CHADEMA inapata shilingi ngapi jamani hadi tunaijadili namna hii??? Wao CHADEMA wanapewa 60,000,000/= tu kwa mwezi. Wenzao CCM wanapewa 2,000,000,000/= (shilingi bilioni mbili kwa mwezi) maana yake ni kuwa kila siku CCM inachukua 80,000,000/= kutoka katika hazina ya taifa. Kwa nini wanaochukizwa na matumizi mabaya ya ruzuku wasifuatilie hili??

Nilikuwa ninawasubiri watanzania wenye nia njema watokeze hadharani kuipongeza CHADEMA kwa kuweza kupambana na lichama kama CCM ambacho kinapata fedha nyingi kwa siku moja kuliko ambazo CHADEMA inapata kwa mwezi mzima. CHADEMA inaweza kuishikisha adabu CCM ambayo ina mabilionea wengi ambao wamevipata vijisenti vyao hivyo kwa kutumia mwavuli wa chama. CHADEMA inaibana na kuitisha CCM ambayo viongozi wake wengi wanatumia fedha za umma kukiimarisha chama. Sungura anapambana na tembo jukwaani na tembo ameridhika wazi kuwa kazidiwa. Sasa analazimika kutumia mbinu za ziada. Hiloo!!! kubwa zima hovyo*

Napeleka salamu kwa Mafisadi wanaojibidiisha sana kupandikiza migogoro CHADEMA, kwamba saa yenu ya kujitetea ni sasa. Lakini punde chaja kizazi ambacho hakitawapa ngau muda finyu wa kujitetea. Kizazi hiki hakitawapa nafasi mkidanganye na bakshishi. Hatakuwepo wa kununuliwa aanzishe migogoro CHADEMA. Na pengine aina ya siasa wakati huo haitakuwa ya vyama kama tuliyo nayo sasa.

Kama ninyi ni wevi mtaimbwa kila pahala kwa ushujaa wenu wa kuiba. Kama ninyi ni mafisadi na wala rushwa mtaimbwa hivyo hivyo kwa heshima ya uchafu wenu mlioifanyia nchi. Kutengeneza migogoro CHADEMA haitawajenga kwa muda mrefu.

Ninyi mliowekwa kuichachafya CHADEMA: tambueni mahitaji ya nchi yetu ya Tanzania. Tunahitaji wanamapinduzi wa kweli wanaoweza kupambana na ufisadi wa CCM. Tukiunyamazia tunawaacha watu wetu wengi hapa Tanzania wakiangamizwa na uharamia wa CCM. Pamoja na wajibu mliopewa na lamba lamba ambayo mmeahidiwa; hebu waacheni waliojitoa sadaka kutetea mustakabali wa masikini wazawa wa Tanzania waendelee kufanya hivyo. Oneni aibu kwa ajira mliyopewa.

Wanachama makini wa CHADEMA...... vita mbele, endeleeni kwa moto zaidi. Mamluki wanapopandikizwa kwenye chama washughulikiwe mapema kabla hawajajikita zaidi.
Karuzuku kadogo tunakopata tukatumie kwa makini kuwamaliza kabisa mafisadi.

Aluta kontinua
 

...chama mbadala!!
 
Then kuna ile issue ya WAPUKI..kuleee Kibaha

wenyewe akina Free hawataki kuizungumzia kabisa hiyo
 
Msubiri Philemon Michael aje...he gets so emotional niinvoke hii issue ya WAPUKI labda nitakutumia in PM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…