CHADEMA na visingizio visivyo na mashiko baada ya kushindwa uchaguzi kabla Oktoba haijafika

CHADEMA na visingizio visivyo na mashiko baada ya kushindwa uchaguzi kabla Oktoba haijafika

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
8,746
Reaction score
5,772
Chama kikuu cha upinzani hapa nchini kwetu kinaweweseka kisiasa.

Kimekuwa hakina muelekeo na kama ni mashua inazama baharini.

Wamekuwa ni watu wa kutafuta ishu au tukio ili wajiokoe kisiasa kakini wanakwama.

Sasa hivi wamebadili gia angani kama ilivyokawaida yao wanasema eti tume ya uchaguzi sio huru. Pia wanasema eti rais alizuia mikutano ndio maana wamepoteza mvuto kwa wananchi.

Hivyo visingizio wanavyotoa havina mashiko. Sababu kwa mujibu wa katiba ya JMT ibara ya 74(7) tume ya taifa ya uchaguzi ni chombo huru. Na kinatakiwa kifanye kazi bila kuingiliwa na mtu hata kama rais ndie anaemteua mkurugenzi wa tume.

Pia hata wasimamizi wa uchaguzi huwa wanakula kiapo na kufanya kazi kama watu huru ambao hawafungamani na upande wowote. Na uzuri zaidi kila chama kinaweka wakala kwa kila ngazi ili kukiwakilisha na kuhesabu kura zake.

Kuhusu kuzuia mikutano ya siasa sio kweli kwani rais aliruhusu siasa zifanyike majimboni ili kuondoa mikanganyiko kwa watu wa sehemu moja kwenda sehemu nyingine kuleta siasa na migongano. Hii imempa fursa mh rais wa JMT kufanya mambo makubwa kwa muda mfupi maana alifanya kazi na sio siasa.

Kwa hiyo Chadema wakubali matokeo chanya aliyo yafanya Rais Magufuli na chama chake kwa muda mfupi ndio yamekiua chama chao sababu watu wameridhika na utendaji wake mkubwa wa kazi.
 
Huko mkoani Mtwara mbunge mtarajiwa amekamatwa na TAKUKURU kwa kushawishi rushwa ,huyu ni CCM yaani mnaingia ubunge kwa njia za kishetwani
 
Back
Top Bottom