Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Marehemu Lujuna Balonzi, Wakili wa kujitegemea alifungua kesi Mahakama Kuu dhidi ya CCM na mali za wananchi walizopora na kuziita za kwake lakini kama kawaida na kama ilivyotegemewa hiyo kesi haikuweza kufika popote. Kwa katiba tuliyonayo na kwa kuzingatia mfumo tulio nao, Chadema ni busara isisumbuke kuanzisha kitega uchumi chochote kwa sasa hivi kwa sababu hapo watakuwa wanakipa CCM fimbo ya kuwachapa nayo - mizengwe.
Sababu kubwa ya serikali ya CCM kukataa wagombea binafsi ni woga wa kujitokeza kwa wafadhili wakubwa watakaomwezesha mgombea kifedha kiasi cha kutotegemea ruzuku ya serikali. Vivyo hivyo kwa vyama vya Upinzani, serikali ya CCM haiwezi kufurahi kuviona vinashamiri na kujitosheleza kifedha. Uanzishwaji wa hivyo vitega uchumi utahitaji baraka za serikali hiyo hiyo na hapa ndipo kuna hatari - refa na mchezaji kuwa upande moja.