Chadema ni lazima iteue Wabunge 19 ili kukidhi masharti ya Wafadhili. Je watakubali?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Kama itakuwa ni lazima Halima Mdee na wenzake wateme ubunge basi Chadema itabidi ipeleke wabunge wengine 19 ili kukidhi masharti ya Wafadhili wa miradi yetu

Je, Chadema watautambua rasmi uchaguzi mkuy wa 2020 kama ulikuwa huru na haki?

Je, watateua wabunge wengine 19?

Tundu Lisu ataridhia?

Mbarikiwe sana!
 
... nadhani kigugumizi ni kwamba wakiwatemesha ubunge hao 19 ita-prove officially pasi na shaka kwamba Bunge na Serikali/NEC walifoji nyaraka na kupindisha taratibu na sheria za nchi. Namna ya kuvuka kizingiti hiki ndio kizungumkuti.
 
Sema NEC.walipewa nyaraka za kufoji na wahuni kutoka Ufipa st.
 
... uko sahihi; wahuni waliojiteua wenyewe na mhuni mwingine aliyejiteua kutokea gerezani! Hao NEC ikawaje wasifanye due diligence? Bunge ikawaje lisifanye due diligence?
 
Mbowe ataanzaje kukataa? Kwa taarifa yako lineup jina la kwanza ni la Joyce mukya.
 
... uko sahihi; wahuni waliojiteua wenyewe na mhuni mwingine aliyejiteua kutokea gerezani! Hao NEC ikawaje wasifanye due diligence? Bunge ikawaje lisifanye due diligence?
Fomu zilisaimiwa na.Katibu mkuu wa Chadema
 
Kama itakuwa ni lazima Halima Mdee na wenzake wateme ubunge basi Chadema itabidi ipeleke wabunge wengine 19 ili kukidhi masharti ya Wafadhili wa miradi yetu

Je, Chadema watautambua rasmi uchaguzi mkuy wa 2020 kama ulikuwa huru na haki?

Je, watateua wabunge wengine 19?

Tundu Lisu ataridhia?

Mbarikiwe sana!
Naona wengi wenu hamjausoma mchezo uliopo.
Hangaya anasaka maridhiano.
Amemwita Mbowe Ikulu mara 2. Na Mbowe amekiri kuwa watakuwa na kikao na rais.

Kikao hicho ni moja ya maridhiano..hivyo lazima wakubaliane kuwa yaliyopita yamepita tugange yajayo.

Unafuu wa hili ni kuwa aliyevuruga uchaguzi hayupo na hawezi kurudi tena.

Hivyo Cgadema lazima wapeleke majina mapya 19 na watapokea ruzuku ya wabunge 20.

Ikiwa wataendelea kutotambua uchaguzi na kukataa kupeleka wabunge, maridhiano hayatakuwa na maana.

Concl.. watapeleka wabunge wapya...subiri muda utathibitisha hili.

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
CCM na serikali yake wawe tayari kukiri madhambi waliyofanya kwenye chaguzi za 2019 na 2020, kuomba msamaha kwa wapinzani na watanzania, kuachia huru wapinzani walio ndani kihuni, ikiwezekana kukubali kulipa fidia/kifuta machozi kwa watu walioumizwa physically na vyombo vya dola kwenye chaguzi zile.

Kisha kuiomba rasmi CHADEMA iteue viti maalum kwenda Bungeni.

Nje ya hapo, uongozi wa CHADEMA utapata tabu kuwashawishi wanachama na mashabiki kukubali matokeo ya uchaguzi wa 2020 (bila masharti) baada ya maumivu yote yale. Wataonekana “wamepozwa kiuhakika” na wanachangamkia fursa ya kupeleka “vitu maalum” vyao bungeni!
 
... nadhani kigugumizi ni kwamba wakiwatemesha ubunge hao 19 ita-prove officially pasi na shaka kwamba Bunge na Serikali/NEC walifoji nyaraka na kupindisha taratibu na sheria za nchi. Namna ya kuvuka kizingiti hiki ndio kizungumkuti.
Mkuu kitendo cha Mbowe kwenda Ikulu haikuwa bahati mbaya, haya yameongelewa.

Tulia hawezi kumpinga Samia milele hivyo tutarajie wabunge wapya.

Samia hawezi kuogopa kwani sio yeye aliyebariki utopolo huu.

Tulia hana aibu pia aliyebariki alikuwa Ndugai.

Aibu ni kwa Tume ya uchaguzi

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Sema NEC.walipewa nyaraka za kufoji na wahuni kutoka Ufipa st.
Agizo la baba yenu.
Kwani hakujua kuwa Hanje alikuwa gerezani?

Hivi nani alikuwa na uwezo wa kumtoa Hanje na kumpa mfungwa ubunge kama Hakuwa Magufuli?.

Angefanya mtu mwingine bila kumdhirikidha Magufuli angenyamaza?

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Kama itakuwa ni lazima Halima Mdee na wenzake wateme ubunge basi Chadema itabidi ipeleke wabunge wengine 19 ili kukidhi masharti ya Wafadhili wa miradi yetu

Je, Chadema watautambua rasmi uchaguzi mkuy wa 2020 kama ulikuwa huru na haki?

Je, watateua wabunge wengine 19?

Tundu Lisu ataridhia?

Mbarikiwe sana!
Kwa vile hawa wabunge wanatokana na idadi ya kura walizopata, wanaweza kusema ni sehemu ya haki yao bila kuukubali uchaguzi kuwa ulikuwa wa haki na huru. Hivyo hivyo kwa ruzuku.

Hilo la masharti ya wafadhili halihusu Chadema. Kwani huo ufadhili ni wa Chadema au Serikali?

Amandla...
 
Kwasasa serikali inapaswa iwainamie cdm ili iwasaidie kukidhi hiyo misaada
 
Back
Top Bottom