Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Natoa onyo kwa kikundi kinachoratibu Kufukuza wengine ndani ya CHADEMA, sitaki kuamini kwamba Katibu Mkuu na Mwenyekiti mpya mnaweza kupanga jambo hili duni na la kijinga, kemeeni jambo hili haraka sana, Uchaguzi umekwisha kwa tofauti ya kura 31 tu, kimsingi hakuna aliyeshinda bali Mshindi wa Jumla ni Chadema.
Wakati wa kampeni kila aliyetaka kuongea aliongea kila alichotaka, wamo pia waliotumia mwanya huo kutukana wenzao matusi hadi ya nguoni, lakini hakuna aliyewagusa.
Hakuna sababu yoyote ya Kijinga wala ya maana ya kuzuia John Mrema kuzungumza na Wanahabari na kutoa tathmini yake, Acheni kabisa mambo haya hayatajenga kitu chochote, Tusikilize hoja zake tuzipime na ikibidi tumjibu ikiwezekana kujibiwa.
Unaweza kukuta anaongea ili kupongeza Washindi tu, Hofu inatoka wapi na kwanini?