CHADEMA ni Moja, Wanaotaka kufukuza wenzao wadhibitiwe haraka

CHADEMA ni Moja, Wanaotaka kufukuza wenzao wadhibitiwe haraka

Mwenyekiti wa CHADEMA @ChademaTz wa Kata ya Segerea mkoani Dar es Salaam, Kitomary Steven, amekanusha vikali madai yaliyoenezwa mtandaoni kwamba amepanga kumvua uanachama John Mrema @JonMrema , Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA.

Akizungumza na Jambo TV, Kitomary ameeleza kuwa taarifa hizo ni za uongo na hazina msingi wowote.

“Ninaomba nikanushe taarifa hizo, taarifa hizo ni ghushi. Kwanza kabisa, mimi ni Mwenyekiti wa CHADEMA wa Kata ya Segerea, huku Mrema akiwa ni mkazi wa Kata ya Bonyokwa na Mkurugenzi wetu wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, ambaye tunamheshimu sana,” amesema Kitomary.

Ameendelea kueleza kuwa haikubaliki kisheria wala kimantiki kwa ngazi ya tawi kufikia maamuzi ya kumvua uanachama Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, ambaye pia ni sehemu ya Sekretarieti ya Makao Makuu.

Awali, John Mrema alitoa madai kupitia ukurasa wake wa X kwamba viongozi wa CHADEMA, akiwemo Kitomary, walikuwa wakipanga kumvua uanachama kabla ya mkutano wake na waandishi wa habari uliotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Katika ujumbe wake, Mrema aliandika: "Nimejulishwa na mwenyekiti wa tawi langu, ameagizwa anifute uanachama kabla ya kesho ili kama nitaendelea na nia yangu ya kuzungumza na vyombo vya habari basi niwe sio mwanachama!”,

Mrema aliongeza kuwa juhudi za kumvua uanachama ni sehemu ya juhudi za kuzima maoni huru na uhuru wa kujieleza ndani ya chama.

Kitomary amefafanua kuwa Mrema alichapisha ujumbe wa kuashiria kuwa angefanya mkutano na waandishi wa habari, ambapo Kitomary alijibu ‘tweet’ hiyo kwa kumweleza kuwa mkutano huo utafuatiliwa kwa ukaribu.
Yapo yaliyomfanya akanushe, huu ujinga hautakubalika Chadema

#STRONGER TOGETHER
 
Natoa onyo kwa kikundi kinachoratibu Kufukuza wengine ndani ya CHADEMA, sitaki kuamini kwamba Katibu Mkuu na Mwenyekiti mpya mnaweza kupanga jambo hili duni na la kijinga, kemeeni jambo hili haraka sana, Uchaguzi umekwisha kwa tofauti ya kura 31 tu, kimsingi hakuna aliyeshinda bali Mshindi wa Jumla ni Chadema.

Wakati wa kampeni kila aliyetaka kuongea aliongea kila alichotaka, wamo pia waliotumia mwanya huo kutukana wenzao matusi hadi ya nguoni, lakini hakuna aliyewagusa.

Hakuna sababu yoyote ya Kijinga wala ya maana ya kuzuia John Mrema kuzungumza na Wanahabari na kutoa tathmini yake, Acheni kabisa mambo haya hayatajenga kitu chochote, Tusikilize hoja zake tuzipime na ikibidi tumjibu ikiwezekana kujibiwa.

Unaweza kukuta anaongea ili kupongeza Washindi tu, Hofu inatoka wapi na kwanini?
No stop kabisa ...Chadema inatakiwa kufanya overhaul...wote walilamba mkwanja wa Abuduli kiama
 
Huwezi kjenga chama kwa kufukuza Makamanda, Lissu hana uwezo huo na hatokuja kuwa nao
Uchaguzi umekwisha. Akileta hoja za kingese afukuzwe tu.
Lazima chama kiwe na nidhamu. Tunajua hawa machawa wa mbowe watakuja na kila aina ya hujuma kwa uongozi uliopo na sisi tunawashauri viongozi wasisite kuwafukuza wote watakaothubutu kubomoa chama.
Sisi wanachama tupo nyuma ya uongozi uliopo na tutawaunga mkono ili kukomesha uhuni utakaojitokeza.
Walizoea vya kunyonga sasa vya kuchinja hawaviwezi.
 
Kwamba Mrema hawezi kuzungumza kwa niaba yake mwenyewe? mmeokota wapi ukubwa huo?
Tumesema akileta ujinga afukuzwe tu.
Hawa wahuni wamekichezea sana chama sasa wanaweweseka baada ya tawi kukatwa.
Chama tutakilinda na tutashiriki kukijenga sisi wenye mioyo ya kizalendo
 
Hilo ni jambo jingine na halihusu kuminywa kwa haki yake ya kujieleza
Kwani amezuiwa kujieleza? Tunamshauri tu kwamba muda wa kampeni ulishaisha.
Hatutasita kuchukua hatua kwa yeyote atakayethubutu kuhujumu chama
 
Natoa onyo kwa kikundi kinachoratibu Kufukuza wengine ndani ya CHADEMA, sitaki kuamini kwamba Katibu Mkuu na Mwenyekiti mpya mnaweza kupanga jambo hili duni na la kijinga, kemeeni jambo hili haraka sana, Uchaguzi umekwisha kwa tofauti ya kura 31 tu, kimsingi hakuna aliyeshinda bali Mshindi wa Jumla ni Chadema.

Wakati wa kampeni kila aliyetaka kuongea aliongea kila alichotaka, wamo pia waliotumia mwanya huo kutukana wenzao matusi hadi ya nguoni, lakini hakuna aliyewagusa.

Hakuna sababu yoyote ya Kijinga wala ya maana ya kuzuia John Mrema kuzungumza na Wanahabari na kutoa tathmini yake, Acheni kabisa mambo haya hayatajenga kitu chochote, Tusikilize hoja zake tuzipime na ikibidi tumjibu ikiwezekana kujibiwa.

Unaweza kukuta anaongea ili kupongeza Washindi tu, Hofu inatoka wapi na kwanini?
 
Attachments

  • v09044g40000cu8cf9fog65g717gh240.mp4
    8.8 MB
Kwani amezuiwa kujieleza? Tunamshauri tu kwamba muda wa kampeni ulishaisha.
Hatutasita kuchukua hatua kwa yeyote atakayethubutu kuhujumu chama
Wewe kama nani?
 
Natoa onyo kwa kikundi kinachoratibu Kufukuza wengine ndani ya CHADEMA, sitaki kuamini kwamba Katibu Mkuu na Mwenyekiti mpya mnaweza kupanga jambo hili duni na la kijinga, kemeeni jambo hili haraka sana, Uchaguzi umekwisha kwa tofauti ya kura 31 tu, kimsingi hakuna aliyeshinda bali Mshindi wa Jumla ni Chadema.

Wakati wa kampeni kila aliyetaka kuongea aliongea kila alichotaka, wamo pia waliotumia mwanya huo kutukana wenzao matusi hadi ya nguoni, lakini hakuna aliyewagusa.

Hakuna sababu yoyote ya Kijinga wala ya maana ya kuzuia John Mrema kuzungumza na Wanahabari na kutoa tathmini yake, Acheni kabisa mambo haya hayatajenga kitu chochote, Tusikilize hoja zake tuzipime na ikibidi tumjibu ikiwezekana kujibiwa.

Unaweza kukuta anaongea ili kupongeza Washindi tu, Hofu inatoka wapi na kwanini?
CDM tayari isha pigwa kitu kizito na CCM chalii!!
 
Kuna msemo wa wahenga wa Zamani kuwa kuna kundi la nyani lilishangilia baada ya kusikia mkulima wa mahindi amekufa wakaambiana sasa watakula mahindi kwa uhuru bila kurushiwa mawe. Hawakujua kuwa aliyefariki ndiyo alikuwa anasababisha mahindi yawepo, baada ya muda nyani nao walikufa njaa vibaya sana kwa kukosa chakula.

Stori hii ya wahenga inafanana na kitendo cha Mbowe kushangilia kufariki kwa Magufuli, asijue kuwa ndiye aliyekuwa analinda uenyekiti wake wa Chadema.

Kila mtu anajua kama Magufuli angekuwa rais wa Tanzania isingewezekana Tundu Lisu kuwa Mwenyekiti wa Chadema.

Freeman Mbowe ulishangilia wakati wengine wakilia ,leo ni zamu yako kulia huku wengine wakicheka na kushangilia.
Freeman Mbowe ni faida ipi uliyoipata kwa kushangilia kifo cha Magufuli?
Magufuli alikuwa anaulinda vipi uenyekiti wa Mbowe?

Amandla...
 
Back
Top Bottom