CHADEMA ni Moja, Wanaotaka kufukuza wenzao wadhibitiwe haraka

Kuna msemo wa wahenga wa Zamani kuwa kuna kundi la nyani lilishangilia baada ya kusikia mkulima wa mahindi amekufa wakaambiana sasa watakula mahindi kwa uhuru bila kurushiwa mawe. Hawakujua kuwa aliyefariki ndiyo alikuwa anasababisha mahindi yawepo, baada ya muda nyani nao walikufa njaa vibaya sana kwa kukosa chakula.

Stori hii ya wahenga inafanana na kitendo cha Mbowe kushangilia kufariki kwa Magufuli, asijue kuwa ndiye aliyekuwa analinda uenyekiti wake wa Chadema.

Kila mtu anajua kama Magufuli angekuwa rais wa Tanzania isingewezekana Tundu Lisu kuwa Mwenyekiti wa Chadema.

Freeman Mbowe ulishangilia wakati wengine wakilia ,leo ni zamu yako kulia huku wengine wakicheka na kushangilia.
Freeman Mbowe ni faida ipi uliyoipata kwa kushangilia kifo cha Magufuli?
 
Una hangover ya jibapa la mbowe,kubali matokeo,utajafa kibudu
 
Wakifuata ushauri wako watakuwa ni wapumbavu ni lazima watu baadhi wafukuzwe kama mbwa ndipo chadema itapona ..
 
Mbona hukutoa maoni haya wakati Mbowe akifukuza watu?
 
Kwamba Mrema hawezi kuzungumza kwa niaba yake mwenyewe? mmeokota wapi ukubwa huo?
Kama anaongelea familia yake ni sawa, Ila Kama taasisi bila utaratibu itasambaratika, yeye mwenyewe Siku akiona mtoto wake anaongea na media mambo ya familia yao lazima atakasirika, kwanini? Uongozi wa pamoja, maamuzi ya pamoja, nguvu moja
 
Hakujawahi kuwepo mwongozo wa kumuagiza Mwenyekiti wa Tawi
Hizo habari zimethibitishwa na nani?

Hata kama ni kweli, kwa nini Mrema atake press conference?

Chama kimetoka uchaguzini jana, busara ni kukaa vikao vikao vya ndani na kuwekana sawa ili kuwa wamoja.

Inaonekana Mh. Mrema hana nia njema, je ni kweli kambi ya Mbowe ilinunuliwa na CCM?
 
Kwani sio Mbowe aliemkataza Lissu kuongea na wananchi akisema hana mamlaka hayo? sasa huyu Mrema yeye katoa wapi mamlaka?
 
Kama anaongelea familia yake ni sawa, Ila Kama taasisi bila utaratibu itasambaratika, yeye mwenyewe Siku akiona mtoto wake anaongea na media mambo ya familia yao lazima atakasirika, kwanini? Uongozi wa pamoja, maamuzi ya pamoja, nguvu moja
Hata mimi simuungi mkono mleta mada, tunahitaji CHADEMA yenye umoja, sio ya kukosoana kwny media, hayo ya mwanzo yalikuwa ni kwa sababu ya uchaguzi, uchaguzi umeisha, wanatakiwa wawe wamoja.
 
Erythrocyte fatilia taarifa za kutaka kufukuzwa km za kweli maana anaentuhumu nae anataka kutoa press kukanusha,pia fatilia ile tweet yake bwana Mrema ilivyojaa chuki kwa uongozi mpya kisa,TAL na Lema walikua uhamishoni,,siku ya uchaguzi kuna tweet yake na account ni yake badae akajifanya kuikanusha kwaio ukifatilia mtiririko utaona ni mtu wa namna gani huyu bwana.
 
Huwezi kjenga chama kwa kufukuza Makamanda, Lissu hana uwezo huo na hatokuja kuwa nao
Mbona Mbowe alikuwa anawafukuza wanachama waliokengeuka na bado chama kiliendelea kuwepo ? Huu sio wakati wa kukaa na wafitini wanaoendeleza minyukano baada ya uchaguzi
 
Hii ni mwandiko wa John Mrema kabisa, mkuu umeji expose kirahisi sana why?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…