CHADEMA ni mpango wa Mungu ili kupitia chama hicho Mungu aweze kuwakomboa Watanzania

CHADEMA ni mpango wa Mungu ili kupitia chama hicho Mungu aweze kuwakomboa Watanzania

Kama ilivyokuwa kwa wana wa Israel ambapo Mungu alimtumia Mussa kuwakomboa kutoka utumwani nchini Misri,ndivyo vivyo hivyo Mungu amepanga kuwatumia CHADEMA na CUF kwa kiasi fulani, ili kupitia vyama hivi,watanzania wakombolewe.

Hii ni moja ya sababu ya hawa wenzetu kukosa maarifa(mungu kwanyima) na matokeo yake mipango yao mingi iliyojaa "uovu" kila siku inafeli na ku-back fire na wao kuishia kuumbuka tu.

Hawa mabwana wanapaswa kutambua kuwa hawapambani na CHADEMA au CUF bali wanapambana na nguvu za Mungu mwenye mamlaka yote mbinguni na duniani.

Wanapaswa kutambua kwa muda mrefu wametenda mengi yasiyo mpendeza Mungu na Mungu sasa kàwachoka hivyo anawaumbua kila kukicha mpaka pale watakaposali amri.

Tambueni:
Tundu Lissu kupigwa risasi lakink aka-survive ni mpango wa Mungu(Mungu kamuokoa yeye na dereva wake ili waje waseme)

Joshua Nassari kwenda masomoni Uingereza na kupata teknolojia iliyowaumbua wanafiki leo hii ni mpango wa Mungu aliejua kabla kuwa huu uovu ungetendeka.

Bwana fulani kuwaita kina fulani "wapumbavu" huku akiwa anarekodiwa baada ya mission kufeli ni mpango wa Mungu.

Bwana fulani kuendelea kuumbuka hadharani kwa kushindwa kutoa vyeti i mpango wa Mungu na soon kila kitu kitakuwa wazi kupitia shauri alilofungua Mayor wa CHADEMA.

Hayo ni machache tu miongoni mwa mengi.

Mengi yametokea,mengi yanakuja na mengi yatatokea.

Jiulizeni ile dhana kuwa vyama vya upinzani ni vyama vya msimu imeeishia wapi siku hizi?

Huwezi kuapa kwa kutumia vitabu vitakatifu kisha ukatenda kinyume alafu ukabaki salama.
Nilidhani utani kuwa hawa jamaa huwa wanapata period bila kujali jinsia kumbe kweli na ikishawapata ni mwendo wa kubofoa tu yaani mipango yenu ya kihaini mnamshirikisha Mun gu yupi [emoji23] [emoji23] [emoji23] acheni mzaha
 
Jengeni ofisi zenu kwanza ili muaminishe Watanzania kuwa mnaweza wajengea uchumi imara..

Lowassa anashindwa kuja Ufipa sababu ya choo cha shimo..
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Mtoa uzi hapo unajitekenya na kucheka mwenyewe tu,huna lolote.Hao CDM na CUF hawatakaa wachukue nchi labda mwaka 2500
 
Jengeni ofisi zenu kwanza ili muaminishe Watanzania kuwa mnaweza wajengea uchumi imara..

Lowassa anashindwa kuja Ufipa sababu ya choo cha shimo..

Mkuu;
Inaonesha labda wewe ni mchanga saana kuingia ccm au labda unavaa miwani ya mbao kujifanya kipofu, CCM iliijenga ofisi gani mkuu?? Niambie moja tu nami nikupe mji.
Ofisi zoote za ccm ni za wananchi walijenga chini ya chama kimoja hivyo kama siasa zetu zingelikuwa za haki vyama vyote vingelipewa nafasi ya kuanza pamoja na ofisi hizo zikauzwa
 
Mkuu;
Inaonesha labda wewe ni mchanga saana kuingia ccm au labda unavaa miwani ya mbao kujifanya kipofu, CCM iliijenga ofisi gani mkuu?? Niambie moja tu nami nikupe mji.
Ofisi zoote za ccm ni za wananchi walijenga chini ya chama kimoja hivyo kama siasa zetu zingelikuwa za haki vyama vyote vingelipewa nafasi ya kuanza pamoja na ofisi hizo zikauzwa
Ile ofisi ndogo pale Lumumba, lile jengo la UVCCM.. Kile kitegauchumi pale Dodoma vilijengwa wakati wa TANU au sio?
 
Ukiamka tathmini ndoto yako kwanza, au endelea kumsubiri DJ makengeza (mkaka) akukomboe kwa kuzungusha mikono, wakati sie tunaendelea kujenga viwanda taratibu
Ni kweli mnavijenga! Tena kwa kasi ya ajabu, 4G! Viwanda vya rushwa!
 
Nimependa hii ,,Tundu Lisu kupigwa Risasi ni mpango wa Mungu" haya tumekupata, Mungu kamfyatua Tundu Lisu ili muingie Ikulu kwa raha zenu Mafia!
Umempata wewe na nani? Hukuelewa kitu bro, mara nyingine ukimya ni busara pia
 
Niseme ukweli,hakuna kitu kilichomdhalilisha na kumuumbua mkulu kana ile issue ya "Ninyi ni Wapumbavu" mpaka kesho aibu ile itamwandama.
 
Tuhuma za CHADEMA kuendeshwa kwa maslahi na kununulika hazikuanza leo.

Uteuzi na vyeo kikabila, uteuzi wa kindugu, teuzi na vyeo kimapenzi na hata kununuliwa kwa pesa tasilimu.

Viongozi karibu wote wa juu kutoka kabila moja. Lisu kumfanyia mpango marehemu dada yake kuwa mbunge. Marehemu Ndesa kumfanyia mpango binti yake Lucy Owenya kuwa mbunge. Mkuu kumpa aliyekuwa demu wake ubunge na sasa ni mzazi mwenzake. Mkuu kupewa pesa na Mzee Mkono ili asimuwekee mpinzani ili Mkono apite bila kupingwa jimboni. Mkuu kuingia dili la 'kisiasa' na Katibu Kinana kuhusu kupata unafuu wa madeni yake ya NSSF, Mkuu kupewa mzigo ili kumpa EL nafasi ya kugombea uraisi kupitia UKAWA na baadhi ya tuhuma zilizoelekezwa kwa CHADEMA na wabaya wao.

Tuhuma za hivi karibuni zinaweza kuthibitisha tuhuma za nyuma. Tuhuma hizi za CHADEMA kuweza kununuliwa hazitolewi tena na wabaya wao. Tuhuma hizi zinatolewa na wabunge wao dhidi ya waliokuwa madiwani wao. Godbless Lema na Joshua Nasari wanajaribu kuthibitisha kuwa ndani yao, miongoni mwao wanaweza kununuliwa, inategemea bei. Katika kundi lao kila mtu ana bei yake.

Tuhuma za kuuza na kununua ndani ya CHADEMA kutoka kwa viongozi wa chama hicho sio ngeni. Mheshimiwa Sugu aliwahi pia kumtuhumu makamu mwenyekiti CHADEMA Zanzibar Salum Mwalimu kuwa anachukua milioni tano tano kwa wakinadada waliokuwa wakitaka majina yao yapitishwe ubunge viti maalum.

Lema na Nasari wametufumbua macho, wametuonesha kuwa hawa watu tunaowaamini na kuwategemea kuleta tunachokiita ukombozi si watu wa kuwategemea. Ni wanafiki, matapeli wa kisiasa, wachumia tumbo, genge la walanguzi na wachuuzi. Kama wanakubali kununuliwa kwa vijisenti vidogo tu, wanauza dhamana kwa hamu zao za ngono, wanawezaje hawa wakaaminika wakapewa nchi
 
Ile ofisi ndogo pale Lumumba, lile jengo la UVCCM.. Kile kitegauchumi pale Dodoma vilijengwa wakati wa TANU au sio?

Tofautisha kujenga jengo na kulikarabati jengo. Wewe ni mtoto tu hujui mwanzo wa vitu hivyo so kaa kimya
 
AMINA! Nchi hii chini ya ccm ni laana tu
 
Tofautisha kujenga jengo na kulikarabati jengo. Wewe ni mtoto tu hujui mwanzo wa vitu hivyo so kaa kimya
Chadema hata kiwanja mnacho? Magari ya M4C yamesajiliwa kwa jina la Mbowe..
 
Hiki chama ni chama teule na ni mpango wa Mungu kwa watanzania kama ilivyokuwa Mussa kwa wana wa Israeli.

Hii ndio sababu hata ile dhana ya kusema vyama vya upinzani ni vyama vya msimu, mpaka leo hii haijatimia kwa CHADEMA, na pia ndio sababu hata matumizi ya dola dhidi ya CHADEMA hayajafua dafu hata kidogo achilia mbali biashara ya ununuzi wa mamluki wa kisiasa kwa miaka karibu mitano sasa.

Kama ambavyo Mungu alisikia kilio cha wana wa Israeli na akaamua kumteua Mussa kuwatoa utumwani nchini Misri,ndivyo hivyo Mungu yule yule kaiteua CHADEMA ili kupitia chama hiki,mtanzania akombolewe kutoka utawala wa chama kimoja uliodumu kwa zaidi ya nusu karne sasa.

Hivyo,wale wote mnaodhani mnapambana na CHADEMA,tambueni tu hampambani na CHADEMA kama ambavyo Farao alifikiri anapamban na Mussa kumbe anapambana na mwenye mamlaka mbinguni na duniani.

CHADEMA itadumu mpake pale mapenzi ya alie juu kwa watu wake yatapotimia.

No wonder mtu anamiminiwa risasi zaidi ya 16 na bado anapona huku akiwa na akili zake timamu tena zilizoimarika zaidi.

Chagua upande sahihi wakati ni sasa,usisubiri ukombozi utimie ukiwa upande ule utashindwa kusherehekea.

Habari ndio hiyo.
 
Back
Top Bottom