CHADEMA ni mti wenye maembe, lazima utupiwe mawe - Mbowe

That was good interview from presidential material. Siyo ubabaishaji wa kilaza wetu JK.

Naona manazi wa CCM wamejipanga msururu mrefu na mawe yao tayari kutupia mawe mti wenye maembe.
 
FMES nitakujibu very simply,kama wewe ama mchangiaji mwingine yeyote anavyoichambua habari hii,na mimi vile vile nafanya hivyo....Hapo juu nilivyoelewa mimi ni kwamba mwenyekiti huyo ameonyesha uwezo wa kuongoza kwasababu ameprove kwamba chama kina malengo ama objectives...Kama wadau wa chama wakaka chini wakaona maamuzi haya ama yale yanaendana na objectives za chama basi without hesitation watafanya hivyo mkuu.
 

Maneno mazito sana hayo Mkuu mwenye macho asome..........
 

- Mushi hakuna chama duniani ambacho hakina objectives, tatizo ni what objectives na kwa faida ya nani? na wangapi?

- Kuiminya demokrasia na katiba ndani ya chama kwa kuweka nyuma haki ya wanachama, unasema ndiyo objective ya Chadema, eti hii ni kwa faida ya nani ndani ya Chadema? Kwa sababu huwezi kusema ni ya chama kizima, Zitto hakuombwa na chama kizima ila aliombwa na wazee wachache wa chama, kinyume na katiba ya chama, unasema hii ndio objective ya Chadema as chama? Ili itusaidie nini kwenye taifa la leo na la kesho?

- Objective namba moja ya chama chochote cha siasa huwa ni kushinda uchaguzi, sasa tunailaumu CCM hapa collectivelly kwa sababu wako radhi kupindisha katiba zao wenyewe ili tu kushinda uchaguzi, na matokeo yake huhamishia upuuzi wao wa kupindisha katiba mpaka kwenye serikali kuu ama taifa, sasa hapa na Chadema nao wanakuja na objective zile zile kama za CCM zilizotufikisha taifa hapa tulipo, halafu wewe unasema Mwenyekiti wako ameonyesha objectives, vipi ndugu yangu hivi ni kweli unaelewa kinachosemwa hapa au?

Respect.

FMEs!
 

Mkuu FMES mwenyekiti wangu kivipi?
Hayo hapo chini kama ulivyotangulia kuya quote hayajanipa shida kuyaelewa...

Hapo juu kwani si kweli mkuu?Kwani kuna uhuru na demokrasia visivyokuwa na mipaka? Mipaka ni sheria na taratibu zilizowekwa...Uhuru wa kwenda popote,kusema chochote almradi usivunje sheria,sasa hapo nini kisichoeleweka mkuu?kwani hukujua demokrasia na uhuru vina mipaka inayoitwa sheria?

Swali: Maana yake nini, je, mnaweza kubadili utaratibu wa kupata mwenyekiti au viongozi wengine?
Hapo juu aliposema wanaweza kutazama kwa busara na manufaa ya chama chao na Taifa kwa siku za usoni ndio uamuzi waliouchukua unaoendana na objectives zao,sasa hapo pia kuna shida kuelewa kuwa panga pangua,piga ua maamuzi yoyote ya chama ama hata organization yoyote ni lazima yashabihiane na objectives za the so organization?
Na pia kujifunza kutoka kwa CCM haina maana kujifunza ufisadi wa CCM,hapana,pengine ni kwa namna wanavyoshughulikia issue zenye kutaka kuleta mgawanyiko. Mkuu pia ni lazima ukumbuke kuwa demokrasia ni neno ambalo ni very complex na kwa mtazamo wangu halina halina nguvu yoyote kwenye hoja hii kwasababu kama katiba ingekuwa imevunjwa,then tungeweza kusema demokrasia imeminywa...Bado sijaona kama kutoa ushauri ni kuvunja katiba endapo aliyepewa ushauri huo ameridhia.
 
Last edited:

Again...Hiyo kauli ya "Mwenyekiti wako" Haina mantiki kwasababu naona ni kama vile ulinikabidhi kadi.
CHADEMA kama organization yoyote ile ie CCM as a political party must and should adhere to their objectives.Hata katiba iko pale kusapoti namna ya kufikia objectives hizo.Kwenye kuyafikia malengo kuna ups and downs,lakini zikitumiwa vizuri zinakuwa more constructive...Politics zangu mimi ni za tofauti nilidhani ulishalifahamu hilo....Ni za common sense.Sisi kama Taifa hatuna malengo na ndio maana hata katiba yetu ni mbovu kwasababu haina guidance yoyote,na haiwezi kuwa na guidance kwasababu bado hatuna objectives ama malengo ya kitaifa.Hiyo ni issue nyingine lakini ngoja turudi kwenye hii ya chama.

Kama nilivyoelezea hapo juu,hakuna sheria inaitwa demokrasia,demokrasia simply ni uwezo wa watu kuwachagua viongozi watakaowatumikia,ni uwezo wa watu hao kuongoza kupitia kwa viongozi,the ability to rule though any form of leadership or government....Wazee hao wa chama kwa kutoa ushauri,sidhani kama walifikia hatua ya kuwanyima wanachama demokrasia ya kuchagua kiongozi wanayemtaka....Na kama ulivyosema hapo juu,kuwa objective ya chama chochote ni kushinda uchaguzi,je utashinda vipi uchaguzi kama chama kikigawanyika kama ilivyotokea kwa vyama vingine vya upinzani vilivyoathirika na migawanyiko?Usifananishe kabisa migawaniko ya CCM yenye dola na ile ya CHADEMA.
 
 
 
 
 

- Mushi maelezo yako mengi sidhani kama yanazingatia haya juu yaliyosemwa na Mwenyekiti wa Chadema, sasa naomba ufafanue neno moja baada ya jingine katika hizi quote hapo juu, na nipo na wewe mkuu mpaka mwisho.

- Ingawa pia ninaheshimu elimu nzito sana unyaoitoa so far on this subject.

Respect.

FMEs!
 

Ni kweli mkuu maelezo hayo ya mwenyekiti wa CHADEMA jinsi yalivyo yanaweza kupelekea mtizamo wa tofauti,nadhani ilikuwa ni namna tu ya kuelezea...Hata hivyo amejitahidi kwa kiwango kikubwa kwenye hoja za mahojiano haya as a whole.
 
Ni kweli mkuu maelezo hayo ya mwenyekiti wa CHADEMA jinsi yalivyo yanaweza kupelekea mtizamo wa tofauti,nadhani ilikuwa ni namna tu ya kuelezea...Hata hivyo amejitahidi kwa kiwango kikubwa kwenye hoja za mahojiano haya as a whole.

- Sasa nimekukubali tena sana Mkuu Mushi, great debate na ninakupa Salute! Keep it up!

Respect.

FMEs!
 
Hiki alisubiriwa kufanya muda mrefu sana uliopita; politics is about timing. Impact ya majibu yake hapa kwa kweli ni minimal. Angeitisha na yeye mkutano na waandishi wa habari during prime time na kujibu hoja za JK n.k lakini kuzungumza na gazeti moja kujibu maswali muhimu sana ambayo watu wamekuwa wakiyauliza kwa muda mrefu ni kushindwa kutumia nafasi vizuri.
 
Mwanakijiji,
I think the timing was appropriate. Hii ilikuwa ni baada tu ya mkutano mkuu wa CHADEMA. Asingeweza kuyazungumzia yote aliyozungumza na kuwa na impact kama haya yangesemwa kabla ya uchaguzi mkuu, no?
 
Maembe ya mchuzi ili ufisadi upate kunoga
 
NIMEKUELEWA LEO NA UMENIDHIHIRISHIA KUWA UNAUWEZO. big up ninakuunga mkono kuanzia leo 2009/09/22
 

Katiba ya CHADEMA Inatambua uwepo wa kundi la wazee na inatamka wazi kuwa ni washauri ndani ya chama , tena imeenda mbali zaidi kwa kutambua kokasi ya wazee ndani ya chama , hivyo kusema kuwa ni kwenda kinyume na katiba ya chama inaonyesha huijui katiba ya CHADEMA.
 
Kujenga demokrasia ni ngumu, mimi nampongeza sana Mboe mpaka hapo alipofikisha CHADEMA, ndo maana alipoulizwa kuwa makosa waliyofanya ndani ya uongozi wake akukataa, alisema yapo.

Swala la kumshauri mgombea kujitoa kumwachia mwingine ni la kawaida ndani ya vyama. Hilary Clinton alishauriwa hivyo, na aligundua hivyo kuwa kuendelea na kinyanganyiro na Obama ni kuumiza Chama chake, hivyo alikubali kujiondoa kabla ya mkutano mkuu wa Democrat ili amuunge mkono Obama na kuomba wafuasi wake wamkubali Obama.
Hivyo kufanya hivyo kwa namna moja ni kujenga demokrasia kwani mgombea anabaki na uhuru wa kuamua kuendelea au kuachia.
Naitakia Mboe na CHADEMA mafanikio zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…