CHADEMA ni ngangari, usipoielewa utadhani imedhoofika kwa hama hama ya wabunge na madiwani wake

Zawadi Ngoda

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2009
Posts
4,367
Reaction score
2,407
Usipoijua historia ya CHADEMA , utadhani au kuamini kuwa chama kimekwisha kama si kufa kabisa ukifuatilia hama hama. Kama wewe ni mmoja kati ya hao wanaoamini hivyo fahamu kuwa huijui historia ya kukuwa kwa chadema. Na ninaamini kuwa wanaoamini hivyo si tu wana- CCM, bali hata baadhi ya watanzania wasioitakia mema chadema.

Kimsingi ukuaji wa CHADEMA toka ianzishwe ni chama kilichokuwa hatua baada ya hatua, kama mtoto mdogo anavyokuwa. Huanza kutambaa, kukaa, kusimama na hatimaye kutembea. Ukiangalia ukuwaji wa chama hiki toka mwanzo kilipitia hatua hizo. Jaribu kufuatilia kila chaguzi toka kizaliwe, kilikuwa kinapanda au kupata ongezeko la wabunge, madiwani na halmashauri zikiongezeka kidogo kidogo kila uchaguzi.

Uchaguzi wa mwaka 2015 hali ilibadilika baada ya chama kupata wabunge, madiwani, wenyeviti wa mitaa na hatimaye kuwa na halmashauri nyingi zaidi. Ni nini tafsiri ya matokeo ya uchaguzi huo? Hapa nisikilize vizuri sana, kwani kuna mambo mawili muhimu:
  • Kuna wanachama na wapenzi waliovutwa na ujio wa Lowasa. Hawa ni wanachama na wapenzi machale, ambao hawakufuata idiolojia ya chama bali ni mapenzi ya mtu wao. Hivyo kamwe hawawezi kuhimili mikiki mikiki ya upinzani. Wakitikiswa kidogo tu wameanguka. Chama kiliwaweka kwenye matazamio ikiwa na wengine wakiwa na nafasi katika uongozi ndani ya chama, kwani ilifahamika kuwa wako mguu pande
  • Kuna wanachama asilia. Hawa wamekuwa na chama wakiifahamu vizuri idiolojia ya chama na kuhimili mikiki mikiki wanayoipata kila siku. Wakasimama imara bila kutikisika, na kukiimarisha chama katika ngazi mbali mbali. Hawakujiunga na chama ili wachume pesa, bali wao ndio wachangiaji wakubwa kwa chama wakijua kuwa kusimama kwa chama kuna wategemea wanachama. Amini usiamini idadi hii ya wanachama bado wapo na wanaongezeka kila siku. Na hapa ndipo kwenye tegemeo la chama, na ukiijua namba hii hata siku moja hutasema kuwa chama kinakufa.
Hii inamaanisha kwamba idadi ndogo ya wabunge, madiwani na viongozi wengine waliohamia vyama vingine toka chadema ndio hao wanachama vilemba ambao kuhama kwao hakujakitikisa chama. Hawa walijiunga na chama ili waje kula, na ndio maana wanapochangishwa pesa hupiga mayowe kama wameibiwa. Huzungumzia Ruzuku- ruzuku kama vile chama kilipozaliwa siku ya kwanza kilikuwa kinapewa Ruzuku. Hivi wanajiuliza ni nani alichangia wakati chama hakina Ruzuku mpaka kikafika hapo kilipo?

Na hitimisha kwa kusema wanachama asilia ni wengi na wanaongezeka kila siku kwani CHADEMA ni wapinzani wa kweli wanaoonyesha dira ya Tanzania itakokwenda. Na kwa maana hii chama kinaweza kisipate wabunge kama wa mwaka 2015 (wabunge wa upepo), lakini wataopatikana watakuwa ngangari kuliko ya baadhi ya wa 2015. Hatutaki tena bora wabunge, tunataka wabunge bora.
 
Hata wasingeama madiwani,ki ukweli chadema imepoteza dira,miaka iliyopita niliwapa kura zangu,napenda na nina hamu hii nchi siku iongozwe na upinzani,lakini sio kwa chadema ya sasa.

Masikitiko yangu makubwa,sitapiga kura mwaka huu,sababu sina chaguzi sahihi ama niliokuwa nawategemea wote wamepoteza sifa.Chadema haiwezi amka tena chini ya Mbowe,hakika tegemeeni anguko kuu.
 
Acha kupotosha watu,mwaka 2015 mliwatapeli Cuf na Nccr mageuzi kujifanya kuunda ukawa. Waliposhutukia utapeli wenu wote wameondoka. Wabunge 17 na madiwani 270. Bado bunge likivunjwa wanaondoka kibao na wanachama kibao. Mtabaki matapeli wa kisiasa.
 
Ukiona nyuzi za kujikakamua kama hizi jua kuwa kwisha habari yenu

Nyuzi kama hii inakupa mwanga wewe ndugu yangu mwenye mtazamo mfupi wa kisiasa. Nyie ndio walengwa wa POLE POLE na sera zake za kununua wabunge na propaganda za kitoto.

Fikiria kuna watanzania wengi si wanachama wa chama chochote kile, kwanini asiwafuate hao na kuwaingiza CCM. Ni mpaka ukamshawishi mbunge na diwani ndio uthibitishe kuwa unapendwa? Tafakari!!!!!!!!!!!!!!
 
Hata wasingeama madiwani,ki ukweli chadema imepoteza dira,miaka iliyopita niliwapa kura zangu,napenda na nina hamu hii nchi siku iongozwe na upinzani,lakini sio kwa chadema ya sasa.

Masikitiko yangu makubwa,sitapiga kura mwaka huu,sababu sina chaguzi sahihi ama niliokuwa nawategemea wote wamepoteza sifa.Chadema haiwezi amka tena chini ya Mbowe,hakika tegemeeni anguko kuu.

Dira chadema haijapoteza, ila unachotaka kukisema ni jinsi viongozi wake walivyolazimishwa kutumia muda wao mwingi maabusu, mahakamani na jela badala ya kuendesha chama. Hilo si kosa la chadema tena , ni la chama tawala.

Ukitaka kujua kuwa chadema hakijapoteza dira, jiulize hivi mpaka leo ni chama gani kisichoipa usingizi chama tawala. Ni chama gani cha upinzani kilicho nambari wani katika kuikosoa na kuishauri serikali. Usipoitaja chadema, ujue wewe una wivu.

Muda wa wewe kufikiria bado upo mpaka uchaguzi mkuu, kama unataka mabadiliko chagua chadema. Ukitaka wajukuu wako waendelee kupata bora elimu na kukosa ajira - chagua ccm.
 
Kwanini unadhani kuna watu wanadhani kimedhoofika?

Matamshi ya waliohama chama kwa kile kinachoitwa kuunga juhudi, hupiga kelele kuwa chadema inakufa. Hata matamshi ya spika wa wabunge akimbembeleza Lijuakali, mwisho alinena kuwa hiki chama kikirudi na wabunge angalau watatu kitakuwa kimejitahidi sana. Chadema irudi na wabunge watatu? Dhihaka.

Hao wote wanataka kuwaaminisha watanzania kuwa chadema imedhoofika, kitu ambacho hata wenyewe hawakiamini. Wenye moyo mwepesi wanaweza kuyumba, na kutojua hali halisi. Na ndio maana inabidi kufafanua mazingira hali ndani ya chama na uwezo wake.
 
Acha kupotosha watu,mwaka 2015 mliwatapeli Cuf na Nccr mageuzi kujifanya kuunda ukawa. Waliposhutukia utapeli wenu wote wameondoka. Wabunge 17 na madiwani 270. Bado bunge likivunjwa wanaondoka kibao na wanachama kibao. Mtabaki matapeli wa kisiasa.

Utapeli haukufanyika. Kwa mfano - CUF ilipata wabunge na madiwani wengi na halmashauri nyingi kuliko chaguzi zote zilizopita. NCCR - chama kilikuwa hakina mvuto sana, hata bila UKAWA kisingebadilisha sana matokeo yake.

Suala lakupoteza wabunge na madiwani nilishalieleza. Pengine niongezee tu kuwa unapofungua dirisha kupata hewa safi, hata vumbi, mbu na nzi wanaingia. Unapofagia bna kupulizia dawa, nia ni kutoa vumbi na kuua nzi na mbu. Hicho ndicho kilichofanyika chadema na kitaendelea hata baada ya kuvunja bunge. Mbu na nzi wataolijua hilo wataondoka mapema kabla ya kupulizia dawa.
 
Kitaendelea vipi? Wakati hata ruzuku hamtapata. Au mtauza Ford Ranger zilizobaki? Maana mkulu wenu kibindoni ana bil 8. Yeye anauhakika.
 
Usipoijua historia ya CHADEMA , utadhani au kuamini kuwa chama kimekwisha kama si kufa kabisa ukifuatilia hama hama. Kama wewe ni mmoja kati ya hao wanaoamini hivyo fahamu kuwa huijui historia ya kukuwa kwa chadema. Na ninaamini kuwa wanaoamini hivyo si tu wana- CCM, bali hata baadhi ya watanzania wasioitakia mema chadema.

Kimsingi ukuaji wa CHADEMA toka ianzishwe ni chama kilichokuwa hatua baada ya hatua, kama mtoto mdogo anavyokuwa. Huanza kutambaa, kukaa, kusimama na hatimaye kutembea. Ukiangalia ukuwaji wa chama hiki toka mwanzo kilipitia hatua hizo. Jaribu kufuatilia kila chaguzi toka kizaliwe, kilikuwa kinapanda au kupata ongezeko la wabunge, madiwani na halmashauri zikiongezeka kidogo kidogo kila uchaguzi.

Uchaguzi wa mwaka 2015 hali ilibadilika baada ya chama kupata wabunge, madiwani, wenyeviti wa mitaa na hatimaye kuwa na halmashauri nyingi zaidi. Ni nini tafsiri ya matokeo ya uchaguzi huo? Hapa nisikilize vizuri sana, kwani kuna mambo mawili muhimu:
  • Kuna wanachama na wapenzi waliovutwa na ujio wa Lowasa. Hawa ni wanachama na wapenzi machale, ambao hawakufuata idiolojia ya chama bali ni mapenzi ya mtu wao. Hivyo kamwe hawawezi kuhimili mikiki mikiki ya upinzani. Wakitikiswa kidogo tu wameanguka. Chama kiliwaweka kwenye matazamio ikiwa na wengine wakiwa na nafasi katika uongozi ndani ya chama, kwani ilifahamika kuwa wako mguu pande
  • Kuna wanachama asilia. Hawa wamekuwa na chama wakiifahamu vizuri idiolojia ya chama na kuhimili mikiki mikiki wanayoipata kila siku. Wakasimama imara bila kutikisika, na kukiimarisha chama katika ngazi mbali mbali. Hawakujiunga na chama ili wachume pesa, bali wao ndio wachangiaji wakubwa kwa chama wakijua kuwa kusimama kwa chama kuna wategemea wanachama. Amini usiamini idadi hii ya wanachama bado wapo na wanaongezeka kila siku. Na hapa ndipo kwenye tegemeo la chama, na ukiijua namba hii hata siku moja hutasema kuwa chama kinakufa.
Hii inamaanisha kwamba idadi ndogo ya wabunge, madiwani na viongozi wengine waliohamia vyama vingine toka chadema ndio hao wanachama vilemba ambao kuhama kwao hakujakitikisa chama. Hawa walijiunga na chama ili waje kula, na ndio maana wanapochangishwa pesa hupiga mayowe kama wameibiwa. Huzungumzia Ruzuku- ruzuku kama vile chama kilipozaliwa siku ya kwanza kilikuwa kinapewa Ruzuku. Hivi wanajiuliza ni nani alichangia wakati chama hakina Ruzuku mpaka kikafika hapo kilipo?

Na hitimisha kwa kusema wanachama asilia ni wengi na wanaongezeka kila siku kwani CHADEMA ni wapinzani wa kweli wanaoonyesha dira ya Tanzania itakokwenda. Na kwa maana hii chama kinaweza kisipate wabunge kama wa mwaka 2015 (wabunge wa upepo), lakini wataopatikana watakuwa ngangari kuliko ya baadhi ya wa 2015. Hatutaki tena bora wabunge, tunataka wabunge bora.
Hebu tuambie kwanza Mwamba kashaenda kuhojiwa na Gen Mbungo au bado anampiga vyenga?
 
Kitaendelea vipi? Wakati hata ruzuku hamtapata. Au mtauza Ford Ranger zilizobaki? Maana mkulu wenu kibindoni ana bil 8. Yeye anauhakika.

Haha, haha haaaaaa! Jiulize kwani kilipoanza wakati hakina mbunge hata mmoja kiliendelea vipi? Panua mawazo yako na ujue kuwa upinzani asili yake si jina chadema, bali ni watu wasiokubaliana na yanayoendelezwa na chama tawala, wanataka mawazo mbadala. Na hawa watu wapo tayari kutoa kilichomfukoni mwao ili kutekeleza kile wanachokiamini.

Mfano mdogo tu- Hivi Gwajima anapata ruzuku kuendeleza shughuli zake? ukipata jibu hapo, utapata kwa chadema vile vile. Nimekurahizishia hiyo quiz.
 
Acha kupotosha watu,mwaka 2015 mliwatapeli Cuf na Nccr mageuzi kujifanya kuunda ukawa. Waliposhutukia utapeli wenu wote wameondoka. Wabunge 17 na madiwani 270. Bado bunge likivunjwa wanaondoka kibao na wanachama kibao. Mtabaki matapeli wa kisiasa.
Uchaguzi huu hawana wa kutapeli chadema sio rahisi kupata Jimbo hata moooja
 
Usipoijua historia ya CHADEMA , utadhani au kuamini kuwa chama kimekwisha kama si kufa kabisa ukifuatilia hama hama. Kama wewe ni mmoja kati ya hao wanaoamini hivyo fahamu kuwa huijui historia ya kukuwa kwa chadema. Na ninaamini kuwa wanaoamini hivyo si tu wana- CCM, bali hata baadhi ya watanzania wasioitakia mema chadema.

Kimsingi ukuaji wa CHADEMA toka ianzishwe ni chama kilichokuwa hatua baada ya hatua, kama mtoto mdogo anavyokuwa. Huanza kutambaa, kukaa, kusimama na hatimaye kutembea. Ukiangalia ukuwaji wa chama hiki toka mwanzo kilipitia hatua hizo. Jaribu kufuatilia kila chaguzi toka kizaliwe, kilikuwa kinapanda au kupata ongezeko la wabunge, madiwani na halmashauri zikiongezeka kidogo kidogo kila uchaguzi.

Uchaguzi wa mwaka 2015 hali ilibadilika baada ya chama kupata wabunge, madiwani, wenyeviti wa mitaa na hatimaye kuwa na halmashauri nyingi zaidi. Ni nini tafsiri ya matokeo ya uchaguzi huo? Hapa nisikilize vizuri sana, kwani kuna mambo mawili muhimu:
  • Kuna wanachama na wapenzi waliovutwa na ujio wa Lowasa. Hawa ni wanachama na wapenzi machale, ambao hawakufuata idiolojia ya chama bali ni mapenzi ya mtu wao. Hivyo kamwe hawawezi kuhimili mikiki mikiki ya upinzani. Wakitikiswa kidogo tu wameanguka. Chama kiliwaweka kwenye matazamio ikiwa na wengine wakiwa na nafasi katika uongozi ndani ya chama, kwani ilifahamika kuwa wako mguu pande
  • Kuna wanachama asilia. Hawa wamekuwa na chama wakiifahamu vizuri idiolojia ya chama na kuhimili mikiki mikiki wanayoipata kila siku. Wakasimama imara bila kutikisika, na kukiimarisha chama katika ngazi mbali mbali. Hawakujiunga na chama ili wachume pesa, bali wao ndio wachangiaji wakubwa kwa chama wakijua kuwa kusimama kwa chama kuna wategemea wanachama. Amini usiamini idadi hii ya wanachama bado wapo na wanaongezeka kila siku. Na hapa ndipo kwenye tegemeo la chama, na ukiijua namba hii hata siku moja hutasema kuwa chama kinakufa.
Hii inamaanisha kwamba idadi ndogo ya wabunge, madiwani na viongozi wengine waliohamia vyama vingine toka chadema ndio hao wanachama vilemba ambao kuhama kwao hakujakitikisa chama. Hawa walijiunga na chama ili waje kula, na ndio maana wanapochangishwa pesa hupiga mayowe kama wameibiwa. Huzungumzia Ruzuku- ruzuku kama vile chama kilipozaliwa siku ya kwanza kilikuwa kinapewa Ruzuku. Hivi wanajiuliza ni nani alichangia wakati chama hakina Ruzuku mpaka kikafika hapo kilipo?

Na hitimisha kwa kusema wanachama asilia ni wengi na wanaongezeka kila siku kwani CHADEMA ni wapinzani wa kweli wanaoonyesha dira ya Tanzania itakokwenda. Na kwa maana hii chama kinaweza kisipate wabunge kama wa mwaka 2015 (wabunge wa upepo), lakini wataopatikana watakuwa ngangari kuliko ya baadhi ya wa 2015. Hatutaki tena bora wabunge, tunataka wabunge bora.
2015 ulafi wa viongozi wenu kumfukuza Dr. Slaa na kumchukuwa mliemwita fisadi ndo unawatokea puani Sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata wasingeama madiwani,ki ukweli chadema imepoteza dira,miaka iliyopita niliwapa kura zangu,napenda na nina hamu hii nchi siku iongozwe na upinzani,lakini sio kwa chadema ya sasa.

Masikitiko yangu makubwa,sitapiga kura mwaka huu,sababu sina chaguzi sahihi ama niliokuwa nawategemea wote wamepoteza sifa.Chadema haiwezi amka tena chini ya Mbowe,hakika tegemeeni anguko kuu.
Lazima watakupinga tuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom