CHADEMA ni ngangari, usipoielewa utadhani imedhoofika kwa hama hama ya wabunge na madiwani wake

CHADEMA ni ngangari, usipoielewa utadhani imedhoofika kwa hama hama ya wabunge na madiwani wake

Usipoijua historia ya CHADEMA , utadhani au kuamini kuwa chama kimekwisha kama si kufa kabisa ukifuatilia hama hama. Kama wewe ni mmoja kati ya hao wanaoamini hivyo fahamu kuwa huijui historia ya kukuwa kwa chadema. Na ninaamini kuwa wanaoamini hivyo si tu wana- CCM, bali hata baadhi ya watanzania wasioitakia mema chadema.

Kimsingi ukuaji wa CHADEMA toka ianzishwe ni chama kilichokuwa hatua baada ya hatua, kama mtoto mdogo anavyokuwa. Huanza kutambaa, kukaa, kusimama na hatimaye kutembea. Ukiangalia ukuwaji wa chama hiki toka mwanzo kilipitia hatua hizo. Jaribu kufuatilia kila chaguzi toka kizaliwe, kilikuwa kinapanda au kupata ongezeko la wabunge, madiwani na halmashauri zikiongezeka kidogo kidogo kila uchaguzi.

Uchaguzi wa mwaka 2015 hali ilibadilika baada ya chama kupata wabunge, madiwani, wenyeviti wa mitaa na hatimaye kuwa na halmashauri nyingi zaidi. Ni nini tafsiri ya matokeo ya uchaguzi huo? Hapa nisikilize vizuri sana, kwani kuna mambo mawili muhimu:
  • Kuna wanachama na wapenzi waliovutwa na ujio wa Lowasa. Hawa ni wanachama na wapenzi machale, ambao hawakufuata idiolojia ya chama bali ni mapenzi ya mtu wao. Hivyo kamwe hawawezi kuhimili mikiki mikiki ya upinzani. Wakitikiswa kidogo tu wameanguka. Chama kiliwaweka kwenye matazamio ikiwa na wengine wakiwa na nafasi katika uongozi ndani ya chama, kwani ilifahamika kuwa wako mguu pande
  • Kuna wanachama asilia. Hawa wamekuwa na chama wakiifahamu vizuri idiolojia ya chama na kuhimili mikiki mikiki wanayoipata kila siku. Wakasimama imara bila kutikisika, na kukiimarisha chama katika ngazi mbali mbali. Hawakujiunga na chama ili wachume pesa, bali wao ndio wachangiaji wakubwa kwa chama wakijua kuwa kusimama kwa chama kuna wategemea wanachama. Amini usiamini idadi hii ya wanachama bado wapo na wanaongezeka kila siku. Na hapa ndipo kwenye tegemeo la chama, na ukiijua namba hii hata siku moja hutasema kuwa chama kinakufa.
Hii inamaanisha kwamba idadi ndogo ya wabunge, madiwani na viongozi wengine waliohamia vyama vingine toka chadema ndio hao wanachama vilemba ambao kuhama kwao hakujakitikisa chama. Hawa walijiunga na chama ili waje kula, na ndio maana wanapochangishwa pesa hupiga mayowe kama wameibiwa. Huzungumzia Ruzuku- ruzuku kama vile chama kilipozaliwa siku ya kwanza kilikuwa kinapewa Ruzuku. Hivi wanajiuliza ni nani alichangia wakati chama hakina Ruzuku mpaka kikafika hapo kilipo?

Na hitimisha kwa kusema wanachama asilia ni wengi na wanaongezeka kila siku kwani CHADEMA ni wapinzani wa kweli wanaoonyesha dira ya Tanzania itakokwenda. Na kwa maana hii chama kinaweza kisipate wabunge kama wa mwaka 2015 (wabunge wa upepo), lakini wataopatikana watakuwa ngangari kuliko ya baadhi ya wa 2015. Hatutaki tena bora wabunge, tunataka wabunge bora.
Kama mtoto anazaliwa,anakua,anasoma,anaoa,huzeeka na mwishowe HUFA. So this is the death zone.
 
Na mwaka huu muwe makini sana.
Msije mkashangaa mnaambulia madiwani tu.
 
Acha kupotosha watu,mwaka 2015 mliwatapeli Cuf na Nccr mageuzi kujifanya kuunda ukawa. Waliposhutukia utapeli wenu wote wameondoka. Wabunge 17 na madiwani 270. Bado bunge likivunjwa wanaondoka kibao na wanachama kibao. Mtabaki matapeli wa kisiasa.
Walishitukiwa kuwa hawakuwa wapinzani Bali mawakala wa CCM, si umeona Leo wameanza kurudi kwao?
 
😂😂😂😂😂
Mkuu, jibu swali vizuri bhana. Kipo katika hatua gani ya ukuaji? maana hata watoto wanakufa, vijana, watu wazima na hata wazee pia.
So kwa ulewa wangu kinaweza kufa katika stage yoyote ile.
Kwa maoni yangu, chadema inahitaji kuto dharau yanayosemwa nakuona kama wanakosea kuwakosa. hata mtoto anapokosea huwa analekebishwa. Sasa cdm wanaona tayari wameshapita kuwa watoto sasa ni wazee ambao kijana hapaswi kuwalekebisha ndio maana watapotea tu kama nccr.

Inabidi uwe na moyo mgumu sana kuwalinganisha Chadema na NCCR. Tofauti kubwa ni moja kati ya vyama hivi viwili. NCCR ilizaliwa tu na kukimbia bila kutambaa na ilipoanza darasa la kwanza chama kikaonekana kinaakili sana na kurushwa madarasa mpaka kidato cha sita na hatimaye chuo kikuu. Kiukweli NCCR ilibidi iwe iukulu baada ya uchaguzi wa mwaka 1995.

Kwa maana hiyo ilipotetemeshwa haikuwa na mawazo mbadala zaidi ya kufikiria kuwa walitakiwa kuwa ikulu. Matokeo yake wakasambaratika na kushindwa kurudia afya yake kutokana na kukosa ujasiri kwa historia ya makuzi yake.

Chadema imepitia mikiki mikiki toka awali na nyakati zote ina njia mbadala ikiwa njia namba 1 ikifeli. Rejea kuondolewa kwa Mrema NCCR. Kwa jinsi nguvu za ziada zilivyotumika kumuondoa Mbowe katika uenyekiti, kama chama kisingekuwa kimejiandaa na kujipambanua habari ilikuwa imeisha. Lakini mpaka uchaguzi mkuu ukiwa usoni kwetu, chadema inadunda tu. Hii imedhihirisha kuwa hiki chama ni ngangari kweli kweli.
 
Jazba haisaidii,ningeona kama ni hekima kutaka kufaham chama chetu pendwa kina fail wapi?matokeo yake mnakuja na ubishi na kebehi+jazba sizokua na mashiko,Chama kisichoshaurika..tunakaa pembeni tunawatazama.

Umefanya uamuzi wa busara, maana ukiona huwezi kuhimili mikiki mikiki toka Lumumba ni vyema ukae pembeni.

Napenda ieleweke kuwa ushauri si lazima ukubaliwe. Hata ushauri wako ukikataliwa, haina maana kuwa chama hakina maana. Hata ukienda Lumumba si kila ushauri wako utasikilizwa.
 
Wameanza leo? Au huu mwaka wa nne wanarudi.

Unapojisikia wakati wowote ule unarudi kwako. Hivi ulitegemea Lowasa, mzee Zero na companya yake wangeweza kukaa chadema kweli. Ilikuwa ni swala la muda du kabla hawajaamua kurudi nyumbani. Chadema walikuja kama wapita njia tu, lakini mioyo yao iko Lumumba.

Ni vyema wametoka kabla ya uchaguzi oct/2020, maana wangevujisha siri nyingi za kimkakati kupambana na chama tawala. Na wengi watafuata nyayo zao. Ni heri kwa chadema.
 
Mimi mwenyewe ni mpinzani. Ila kwa mipango wanayo panga ccm kuhusu chadema..
Hata wabunge mtawapata kwa tochi.
Mpo wengi mnaofikiri hivyo. Baada ya matokeo ndio mtaipata, pale ambapoLumumba itakuwa OUT!!!!!!!
 
2015 ulafi wa viongozi wenu kumfukuza Dr. Slaa na kumchukuwa mliemwita fisadi ndo unawatokea puani Sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Akili kama hizi lazima ziwe na hitimisho la kijinga kama hili. Nani alimfukuza Dk. Slaa na nani alimleta Lowasa Chadema? tatizo mna akili ndogo halafu mnajiingiza kwenye mijadala inayohitaji upevu. Mijitu haijui hata michezo ya kisiasa inapost ujinga ujinga JF!
 
Usipoijua historia ya CHADEMA , utadhani au kuamini kuwa chama kimekwisha kama si kufa kabisa ukifuatilia hama hama. Kama wewe ni mmoja kati ya hao wanaoamini hivyo fahamu kuwa huijui historia ya kukuwa kwa chadema. Na ninaamini kuwa wanaoamini hivyo si tu wana- CCM, bali hata baadhi ya watanzania wasioitakia mema chadema.

Kimsingi ukuaji wa CHADEMA toka ianzishwe ni chama kilichokuwa hatua baada ya hatua, kama mtoto mdogo anavyokuwa. Huanza kutambaa, kukaa, kusimama na hatimaye kutembea. Ukiangalia ukuwaji wa chama hiki toka mwanzo kilipitia hatua hizo. Jaribu kufuatilia kila chaguzi toka kizaliwe, kilikuwa kinapanda au kupata ongezeko la wabunge, madiwani na halmashauri zikiongezeka kidogo kidogo kila uchaguzi.

Uchaguzi wa mwaka 2015 hali ilibadilika baada ya chama kupata wabunge, madiwani, wenyeviti wa mitaa na hatimaye kuwa na halmashauri nyingi zaidi. Ni nini tafsiri ya matokeo ya uchaguzi huo? Hapa nisikilize vizuri sana, kwani kuna mambo mawili muhimu:
  • Kuna wanachama na wapenzi waliovutwa na ujio wa Lowasa. Hawa ni wanachama na wapenzi machale, ambao hawakufuata idiolojia ya chama bali ni mapenzi ya mtu wao. Hivyo kamwe hawawezi kuhimili mikiki mikiki ya upinzani. Wakitikiswa kidogo tu wameanguka. Chama kiliwaweka kwenye matazamio ikiwa na wengine wakiwa na nafasi katika uongozi ndani ya chama, kwani ilifahamika kuwa wako mguu pande
  • Kuna wanachama asilia. Hawa wamekuwa na chama wakiifahamu vizuri idiolojia ya chama na kuhimili mikiki mikiki wanayoipata kila siku. Wakasimama imara bila kutikisika, na kukiimarisha chama katika ngazi mbali mbali. Hawakujiunga na chama ili wachume pesa, bali wao ndio wachangiaji wakubwa kwa chama wakijua kuwa kusimama kwa chama kuna wategemea wanachama. Amini usiamini idadi hii ya wanachama bado wapo na wanaongezeka kila siku. Na hapa ndipo kwenye tegemeo la chama, na ukiijua namba hii hata siku moja hutasema kuwa chama kinakufa.
Hii inamaanisha kwamba idadi ndogo ya wabunge, madiwani na viongozi wengine waliohamia vyama vingine toka chadema ndio hao wanachama vilemba ambao kuhama kwao hakujakitikisa chama. Hawa walijiunga na chama ili waje kula, na ndio maana wanapochangishwa pesa hupiga mayowe kama wameibiwa. Huzungumzia Ruzuku- ruzuku kama vile chama kilipozaliwa siku ya kwanza kilikuwa kinapewa Ruzuku. Hivi wanajiuliza ni nani alichangia wakati chama hakina Ruzuku mpaka kikafika hapo kilipo?

Na hitimisha kwa kusema wanachama asilia ni wengi na wanaongezeka kila siku kwani CHADEMA ni wapinzani wa kweli wanaoonyesha dira ya Tanzania itakokwenda. Na kwa maana hii chama kinaweza kisipate wabunge kama wa mwaka 2015 (wabunge wa upepo), lakini wataopatikana watakuwa ngangari kuliko ya baadhi ya wa 2015. Hatutaki tena bora wabunge, tunataka wabunge bora.


Yaani zamani post kama hii unakuna ina likes 70

Kwa sasa unaokoteza

Usipoteze muda mrefu kutetea wafu, hao wanaofanya kiwe ngangali ni akina nani? Chama bi watu andazi wewe!!!

Unless ni mnufaika wa 8.9b
 
Nyuzi kama hii inakupa mwanga wewe ndugu yangu mwenye mtazamo mfupi wa kisiasa. Nyie ndio walengwa wa POLE POLE na sera zake za kununua wabunge na propaganda za kitoto.

Fikiria kuna watanzania wengi si wanachama wa chama chochote kile, kwanini asiwafuate hao na kuwaingiza CCM. Ni mpaka ukamshawishi mbunge na diwani ndio uthibitishe kuwa unapendwa? Tafakari!!!!!!!!!!!!!!
Ona aibu wewe!!
 
Kitaendelea vipi? Wakati hata ruzuku hamtapata. Au mtauza Ford Ranger zilizobaki? Maana mkulu wenu kibindoni ana bil 8. Yeye anauhakika.

Ccm ndio inayotegemea ruzuku ili iwepo maana ina wanachama na washabiki wafuata maslahi. Cdm haina tatizo la kuishi kwa kutegemea ruzuku maana kina support ya watu.
 
Yaani zamani post kama hii unakuna ina likes 70

Kwa sasa unaokoteza

Usipoteze muda mrefu kutetea wafu, hao wanaofanya kiwe ngangali ni akina nani? Chama bi watu andazi wewe!!!

Unless ni mnufaika wa 8.9b

Mkuu zamani ipi, maana hata hii jf sio ya zamani.
 
Kama kawaida yetu wana cdm tuzidi kuwa na uvumilivu wa kukibeba chama chetu bila kusikiliza miruzi ya wapinzani wetu.

Ukiona kila mtu anakuongelea wewe kila siku basi jua kuwa anakuogopa

Hilo la sisi kukikubali chama wala halina mjadala. Tuko mbele kama tai.
 
Back
Top Bottom