Zawadi Ngoda
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 4,367
- 2,407
Ukiona nyuzi za kujikakamua kama hizi jua kuwa kwisha habari yenu
Hata wasingeama madiwani,ki ukweli chadema imepoteza dira,miaka iliyopita niliwapa kura zangu,napenda na nina hamu hii nchi siku iongozwe na upinzani,lakini sio kwa chadema ya sasa.
Masikitiko yangu makubwa,sitapiga kura mwaka huu,sababu sina chaguzi sahihi ama niliokuwa nawategemea wote wamepoteza sifa.Chadema haiwezi amka tena chini ya Mbowe,hakika tegemeeni anguko kuu.
Kwanini unadhani kuna watu wanadhani kimedhoofika?
Acha kupotosha watu,mwaka 2015 mliwatapeli Cuf na Nccr mageuzi kujifanya kuunda ukawa. Waliposhutukia utapeli wenu wote wameondoka. Wabunge 17 na madiwani 270. Bado bunge likivunjwa wanaondoka kibao na wanachama kibao. Mtabaki matapeli wa kisiasa.
Kitaendelea vipi? Wakati hata ruzuku hamtapata. Au mtauza Ford Ranger zilizobaki? Maana mkulu wenu kibindoni ana bil 8. Yeye anauhakika.Utapeli haukufanyika. Kwa mfano - CUF ilipata wabunge na madiwani wengi na halmashauri nyingi kuliko chaguzi zote zilizopita. NCCR - chama kilikuwa hakina mvuto sana, hata bila UKAWA kisingebadilisha sana matokeo yake.
Suala lakupoteza wabunge na madiwani nilishalieleza. Pengine niongezee tu kuwa unapofungua dirisha kupata hewa safi, hata vumbi, mbu na nzi wanaingia. Unapofagia bna kupulizia dawa, nia ni kutoa vumbi na kuua nzi na mbu. Hicho ndicho kilichofanyika chadema na kitaendelea hata baada ya kuvunja bunge. Mbu na nzi wataolijua hilo wataondoka mapema kabla ya kupulizia dawa.
Hebu tuambie kwanza Mwamba kashaenda kuhojiwa na Gen Mbungo au bado anampiga vyenga?Usipoijua historia ya CHADEMA , utadhani au kuamini kuwa chama kimekwisha kama si kufa kabisa ukifuatilia hama hama. Kama wewe ni mmoja kati ya hao wanaoamini hivyo fahamu kuwa huijui historia ya kukuwa kwa chadema. Na ninaamini kuwa wanaoamini hivyo si tu wana- CCM, bali hata baadhi ya watanzania wasioitakia mema chadema.
Kimsingi ukuaji wa CHADEMA toka ianzishwe ni chama kilichokuwa hatua baada ya hatua, kama mtoto mdogo anavyokuwa. Huanza kutambaa, kukaa, kusimama na hatimaye kutembea. Ukiangalia ukuwaji wa chama hiki toka mwanzo kilipitia hatua hizo. Jaribu kufuatilia kila chaguzi toka kizaliwe, kilikuwa kinapanda au kupata ongezeko la wabunge, madiwani na halmashauri zikiongezeka kidogo kidogo kila uchaguzi.
Uchaguzi wa mwaka 2015 hali ilibadilika baada ya chama kupata wabunge, madiwani, wenyeviti wa mitaa na hatimaye kuwa na halmashauri nyingi zaidi. Ni nini tafsiri ya matokeo ya uchaguzi huo? Hapa nisikilize vizuri sana, kwani kuna mambo mawili muhimu:
Hii inamaanisha kwamba idadi ndogo ya wabunge, madiwani na viongozi wengine waliohamia vyama vingine toka chadema ndio hao wanachama vilemba ambao kuhama kwao hakujakitikisa chama. Hawa walijiunga na chama ili waje kula, na ndio maana wanapochangishwa pesa hupiga mayowe kama wameibiwa. Huzungumzia Ruzuku- ruzuku kama vile chama kilipozaliwa siku ya kwanza kilikuwa kinapewa Ruzuku. Hivi wanajiuliza ni nani alichangia wakati chama hakina Ruzuku mpaka kikafika hapo kilipo?
- Kuna wanachama na wapenzi waliovutwa na ujio wa Lowasa. Hawa ni wanachama na wapenzi machale, ambao hawakufuata idiolojia ya chama bali ni mapenzi ya mtu wao. Hivyo kamwe hawawezi kuhimili mikiki mikiki ya upinzani. Wakitikiswa kidogo tu wameanguka. Chama kiliwaweka kwenye matazamio ikiwa na wengine wakiwa na nafasi katika uongozi ndani ya chama, kwani ilifahamika kuwa wako mguu pande
- Kuna wanachama asilia. Hawa wamekuwa na chama wakiifahamu vizuri idiolojia ya chama na kuhimili mikiki mikiki wanayoipata kila siku. Wakasimama imara bila kutikisika, na kukiimarisha chama katika ngazi mbali mbali. Hawakujiunga na chama ili wachume pesa, bali wao ndio wachangiaji wakubwa kwa chama wakijua kuwa kusimama kwa chama kuna wategemea wanachama. Amini usiamini idadi hii ya wanachama bado wapo na wanaongezeka kila siku. Na hapa ndipo kwenye tegemeo la chama, na ukiijua namba hii hata siku moja hutasema kuwa chama kinakufa.
Na hitimisha kwa kusema wanachama asilia ni wengi na wanaongezeka kila siku kwani CHADEMA ni wapinzani wa kweli wanaoonyesha dira ya Tanzania itakokwenda. Na kwa maana hii chama kinaweza kisipate wabunge kama wa mwaka 2015 (wabunge wa upepo), lakini wataopatikana watakuwa ngangari kuliko ya baadhi ya wa 2015. Hatutaki tena bora wabunge, tunataka wabunge bora.
Kitaendelea vipi? Wakati hata ruzuku hamtapata. Au mtauza Ford Ranger zilizobaki? Maana mkulu wenu kibindoni ana bil 8. Yeye anauhakika.
Uchaguzi huu hawana wa kutapeli chadema sio rahisi kupata Jimbo hata mooojaAcha kupotosha watu,mwaka 2015 mliwatapeli Cuf na Nccr mageuzi kujifanya kuunda ukawa. Waliposhutukia utapeli wenu wote wameondoka. Wabunge 17 na madiwani 270. Bado bunge likivunjwa wanaondoka kibao na wanachama kibao. Mtabaki matapeli wa kisiasa.
2015 ulafi wa viongozi wenu kumfukuza Dr. Slaa na kumchukuwa mliemwita fisadi ndo unawatokea puani Sasa.Usipoijua historia ya CHADEMA , utadhani au kuamini kuwa chama kimekwisha kama si kufa kabisa ukifuatilia hama hama. Kama wewe ni mmoja kati ya hao wanaoamini hivyo fahamu kuwa huijui historia ya kukuwa kwa chadema. Na ninaamini kuwa wanaoamini hivyo si tu wana- CCM, bali hata baadhi ya watanzania wasioitakia mema chadema.
Kimsingi ukuaji wa CHADEMA toka ianzishwe ni chama kilichokuwa hatua baada ya hatua, kama mtoto mdogo anavyokuwa. Huanza kutambaa, kukaa, kusimama na hatimaye kutembea. Ukiangalia ukuwaji wa chama hiki toka mwanzo kilipitia hatua hizo. Jaribu kufuatilia kila chaguzi toka kizaliwe, kilikuwa kinapanda au kupata ongezeko la wabunge, madiwani na halmashauri zikiongezeka kidogo kidogo kila uchaguzi.
Uchaguzi wa mwaka 2015 hali ilibadilika baada ya chama kupata wabunge, madiwani, wenyeviti wa mitaa na hatimaye kuwa na halmashauri nyingi zaidi. Ni nini tafsiri ya matokeo ya uchaguzi huo? Hapa nisikilize vizuri sana, kwani kuna mambo mawili muhimu:
Hii inamaanisha kwamba idadi ndogo ya wabunge, madiwani na viongozi wengine waliohamia vyama vingine toka chadema ndio hao wanachama vilemba ambao kuhama kwao hakujakitikisa chama. Hawa walijiunga na chama ili waje kula, na ndio maana wanapochangishwa pesa hupiga mayowe kama wameibiwa. Huzungumzia Ruzuku- ruzuku kama vile chama kilipozaliwa siku ya kwanza kilikuwa kinapewa Ruzuku. Hivi wanajiuliza ni nani alichangia wakati chama hakina Ruzuku mpaka kikafika hapo kilipo?
- Kuna wanachama na wapenzi waliovutwa na ujio wa Lowasa. Hawa ni wanachama na wapenzi machale, ambao hawakufuata idiolojia ya chama bali ni mapenzi ya mtu wao. Hivyo kamwe hawawezi kuhimili mikiki mikiki ya upinzani. Wakitikiswa kidogo tu wameanguka. Chama kiliwaweka kwenye matazamio ikiwa na wengine wakiwa na nafasi katika uongozi ndani ya chama, kwani ilifahamika kuwa wako mguu pande
- Kuna wanachama asilia. Hawa wamekuwa na chama wakiifahamu vizuri idiolojia ya chama na kuhimili mikiki mikiki wanayoipata kila siku. Wakasimama imara bila kutikisika, na kukiimarisha chama katika ngazi mbali mbali. Hawakujiunga na chama ili wachume pesa, bali wao ndio wachangiaji wakubwa kwa chama wakijua kuwa kusimama kwa chama kuna wategemea wanachama. Amini usiamini idadi hii ya wanachama bado wapo na wanaongezeka kila siku. Na hapa ndipo kwenye tegemeo la chama, na ukiijua namba hii hata siku moja hutasema kuwa chama kinakufa.
Na hitimisha kwa kusema wanachama asilia ni wengi na wanaongezeka kila siku kwani CHADEMA ni wapinzani wa kweli wanaoonyesha dira ya Tanzania itakokwenda. Na kwa maana hii chama kinaweza kisipate wabunge kama wa mwaka 2015 (wabunge wa upepo), lakini wataopatikana watakuwa ngangari kuliko ya baadhi ya wa 2015. Hatutaki tena bora wabunge, tunataka wabunge bora.
Lazima watakupinga tuu.Hata wasingeama madiwani,ki ukweli chadema imepoteza dira,miaka iliyopita niliwapa kura zangu,napenda na nina hamu hii nchi siku iongozwe na upinzani,lakini sio kwa chadema ya sasa.
Masikitiko yangu makubwa,sitapiga kura mwaka huu,sababu sina chaguzi sahihi ama niliokuwa nawategemea wote wamepoteza sifa.Chadema haiwezi amka tena chini ya Mbowe,hakika tegemeeni anguko kuu.
Uchaguzi huu hawana wa kutapeli chadema sio rahisi kupata Jimbo hata moooja